METL KILIMO YAMKABIDHI SARUJI MIFUKO 200 MBUNGE WA JIMBO LA KOROGWE VIJIJINI MAJI MAREFU

August 29, 2017
KAMPUNI ya METL Kilimo imetoa msaada wa mifuko 200 ya Saruji kwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani almaarufu Profesa Majimarefu lengo likiwa kumwezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii hatua ambayo itaweza kusaidia kuboresha miundombinu
kwa sekta mbalimbali.

Makabidhiano ya msaada huo yamefanyika juzi wilayani Korogwe kati yamwakilishi wa kampuni ya METL Kilimo,Mtegwa Katuga ambaye ni Meneja ufundi na Mbunge Stephen Ngonyani hatua ambayo imeonekana kuwa ni
sehemu ya mchango wa wadau kuharakisha shughuli za kimaendeleo kwa
jamii.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo wa tani kumi za Saruji,mbunge Ngonyani alisema Saruji hiyo imekuja kipindi muafaka na itasaidia kukamilisha miradi iliyoanza kutekelezwa kwenye jimbo lake huku akitanabaisha kuwa kipaumbele cha ugawaji saruji hiyo ni kwa wale
walioanza kutekeleza miradi.

Mbunge Maji marefu wakati akiwasilisha shukrani zake baada ya kupoea msaada huo wa saruji alisema,anaishukuru kampuni ya METL Kilimokupitia Rais wake Mohammed Dewji kwa kumpatia msaada huo ambao utakaosaidia kusukuma jitihada za maendeleo katika jimbo la Korogwe
vijijini.

“Kwa kweli sikutarajia kupata msaada huu kwa wakati huu,Mungu ambariki huyu rafiki yangu Moo..kweli nilimuomba kwa kumueleza shida yangu akasema atanipa na bila kujua ni lini, leo napigiwa simu kuambiwa nije kupokea Saruji hapa kama mnavyoona Lorry linateremsha”alisema mbunge Maji marefu.

Mbali na kueleza kuwa kipaumbele cha saruji hiyo kitakuwa kwa wananchiwaliopo maeneo ambayo yameanza kutekeleza miradi hususani ile ya sekta ya elimu lakini pia Majimarefu alisema kwamba miradi mingine ikiwemo ile ya afya itaangaliwa sanjari na mwananchi mmojammoja pale itakapobidi atasaidiwa..

Hata hivyo mbunge huyo alitanabaisha kwamba pindi Saruji hiyo
itakapoanza kugawanywa kwenye miradi ya ujenzi atahakikisha inatumika kama ilivyokusudiwa hatua ambayo itawezesha tija kupatikana na hivyo wananchi kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye maeneo yao.

Naye mwakilishi wa Rais wa METL Mtega Katuga alisema msaada huo ni sehemu ya kampuni katika kusaidia huduma za jamii hatua itakayosaidia kuleta ustawi kwa umma wa watanzania walio wengi.

Katuga alisema licha ya METL Kilimo kutoa msaada huo kupitia mashamba yaliopo yake ya Korogwe huo hautakuwa mwisho kwao kuisaidia jamii huku akiahidi kuendelea kufanya hivyo kila watakapokuwa wakihitjika kusaidia huku akitanabaisha kuwa utaratibu huo unasaidia kuimarisha
mahusiano.

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ASISITIZA UKUSANYAJI WA MAPATO YA ARDHI NA MAJENGO

August 29, 2017
 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Geita na akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo Nyuma yake ni mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga 
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akisaini kwenye kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mbongwe. Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe Mathar Mkupasi akisoma taarifa ya ardhi na maendeleo ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanatokana na ardhi pamoja majengo yaliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya Hiyo. Watumishi wa halmashauri ya Mboongwe pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama wakifuatilia kikao cha Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe Elias Kayandabila akionesha mchoro na ramani ya nyumba ambazo zinatarajia kujengwa na shirika la Nyumba la Taifa. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe Elias Kayandabila akikabidhi ramani kwa meneja wa shirika la Nyumba Mwanza, Simiyu na Geita Mhandisi Benedict Kilimba . Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akikagua mafaili kwenye ofisi za Ardhi za Wilaya hiyo. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akiangalia ramani ya Kijiji cha Bukandwe ambacho kipo kwenye Wilaya ya Mbongwe Mkoani Geita.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

August 29, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi. PICHA NA IKULU
MAJINA 8 YAPITA MCHUJO WA AWALI UONGOZI TPLB

MAJINA 8 YAPITA MCHUJO WA AWALI UONGOZI TPLB

August 29, 2017
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Waliopitishwa ni kuwania uenyekiti wa Management Committee ni Clement Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan Crysostoms ameiptishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti. 

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake.

Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.

Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika.

Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.

Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.
TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI DAR

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI DAR

August 29, 2017
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.

Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba.

Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
TFF YATOA NGAO MPYA YA JAMII

TFF YATOA NGAO MPYA YA JAMII

August 29, 2017
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu.
Siku hiyo mara baada ya mchezo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa mpira wa miguu.

TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine ambayo sasa imetolewa leo Jumanne Agosti 29, mwaka huu na itakabidhiwa kwa Simba kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom  dhidi ya Azam FC jijini Dar es Salaam.