POLISI TANGA YAKUSANYA MILIONI 801.

January 14, 2014

Na Oscar Assenga, Tanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga Kitengo cha Usalama barabarani, limeongeza makusanyo yanayotokana na makosa mbalimbali, kutoka Sh milioni 738.2 hadi kufikia Sh milioni 801.8. Ongezeko hilo ni la kuanzia mwaka 2012 na 2013, fedha ambazo zilitokana na makosa mbalimbali ya barabarani, baada ya uimarishwaji wa doria kwenye barabara kuu na za mijini.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Isango aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alisema fedha hizo zilikusanywa kutokana na makosa 26,178 yaliyopatikana mwaka jana na makosa 24,160 yaliyopatikana mwaka juzi.

SHIRIKA LA UNDP LAMWAGA MAMILIONI KOROGWE VIJIJINI.

January 14, 2014
Korogwe SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limempatia Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu' kiasi cha shilingi milioni 253 kwa ajili ya kukabili tatizo la maji katika jimbo lake fedha ambazo zimetokana na mfuko wa maendeleo vijijini.
Akikabidhi mkataba wa fedha hizo, Ofisa Miradi Shirikishi wa UNDP, Stela Zaarh amesema fedha hizo wamezitoa kwa wilaya hiyo kama jitihada za shirika hilo kusaidiana na Serikali kutatua kero zinazowakabili wananchi vijijini hasa suala la maji, afya na elimu.

Baada ya kupokea mkataba huo ambao fedha tayari zimeshaingizwa katika akaunti ya halmashauri ya wilaya kupitia mhandisi wa maji wa wilaya, mbunge huyo alisema kwamba fedha hizo zitachimba visima virefu katika vijiji vitano kata Majengo kilichopo kata ya Mswaha-Darajani, Makuyuni,  Kikwazu, Goha na Kwetonge.

HANDENI WAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2014-2015

January 14, 2014
HALMASHAURI ya Mji wa Handeni, imepitisha mapendekezo ya bajeti yake ya mwaka 2014-2015 ya jumla ya kiasi cha sh. bilioni 7.9 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo fedha za utawala kwa watendaji.
Akisoma mapendekezo hayo katika baraza la madiwani la halmashauri ya mji huo mwishoni wa wiki, Kaimu Mwekahazina wa mji huo, Npella Kwidika amesema mapendekezo ya bajeti hiyo imezingatia mipango, sera na ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kwamba wamelenga kupata fedha hizo kwenye vyanzo vyao vya mapato na ruzuku toka Serikali Kuu.

BRAC MEMBERSCOMPLAIN OF CORRUPTION

January 14, 2014
By Paskal Mbunga, Tanga      January 14, 2014.
The Tanga Regional Manager of an institution which lends funds to small scale entrepreneurs, BRAC has said his institution will not compromise with any staff found indulging in corrupt  practices.
The Manager, Prodip Laskar was speaking to reporters today when elaborating on rumours that some of the staff in the branch offices are asking for ‘kick backs’ from clients before they are endorsed for payment of the loans.
Laskar said the allegations on named list of staff which had reached his office will be worked on immediately without delay and promised to cooperate with any source from outside who is willing to expose the corrupt staff.
There are wide spread allegations that registered members in the institution when they ask for loans, they are asked for a ten per cent commission.

BRAC TANGA YAONYA RUSHWA KWA WATENDAJI WAKE

January 14, 2014
TAASISI inayotoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Tanga,(BRAC) imewaonya wafanyakazi wake kuacha tabia ya kuchukua rushwa kutoka kwa wanachama wanaoomba mikopo kwenye taasisi hiyo.
 

Meneja wa Mkoa wa Tanga wa Taasisi ya BRAC,Prodip  Laskar aliyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake ambapo alisema tuhuma zozote za rushwa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wake zitafuatiliwa na kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria.
January 14, 2014

JINSI FAINALI YA KOMBE LA MAPINDUZI LILIVYOFANYIKA JANA.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Nahodha wa timu ya KCC ya Uganda, Kawooya Fahad, Kombe la Mapinduzi baada kumalizika kwa mchezo wa Fainali wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar jana jioni. Katika mchezo huo KCC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa katika dakika ya 7 ya mchezo. 
January 14, 2014

JAKAYA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM MJINI ZANZIBAR

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa mjini Zanzibar kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea wa nafasi uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM. Picha na Adam H. Mzee

TAIFA STARS KUIKABILI NAMIBIA FIFA DATE

January 14, 2014
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.

Stars na Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia. Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Release No. 005 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Januari 14, 2014

January 14, 2014

 30 TWIGA STARS WAITWA KUIVAA ZAMBIA
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ametaja kikosi cha wachezaji 30 wanaoingia kambini kesho (Januari 15 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya Zambia mwezi ujao.

Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek, Namibia itafanyika jijini Lusaka.

Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni Amina Ally (Lord Baden Sekondari), Amisa Athuman (Marsh Academy), Anastazia Anthony (Lord Baden Sekondari), Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar) na Belina Julius (Lord Baden Sekondari).

Donisia Daniel (Lord Baden Sekondari), Esther Chabruma (Sayari Queens), Evelyn Sekikubo (Kwimba Chuoni), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Issa (Evergreen) na Fatuma Mustapha (Sayari Queens).

Fatuma Omari (Sayari Queens), Happiness Hezron (Copa Coca-Cola Ilala), Maimuna Hamisi (U20 Tanzanite), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Real Tanzanite), Mwapewa Mtumwa (Sayari Queens), Najiat Abbas (Makongo Sekondari) na Neema Paul (U20 Tanzanite).

Pulkeria Charaji (Sayari Queens), Semeni Abeid (Real Tanzanite), Shelder Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari Queens), Theresa Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

RAMBIRAMBI MSIBA WA KANALI MMARI
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mwanzilishi wa wa timu ya Oljoro JKT, Kanali Mmari kilichotokea jana (Januari 13 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Kanali Mmari ambaye aliasisi timu hiyo na kuifikisha hadi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa baada ya kupata ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani, Januari Mosi mwaka huu.

Msiba huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani mbali kuasisi timu ya Oljoro JKT alikuwa mhamasishaji mkubwa wa mchezo huo mkoani Arusha, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mmari, klabu ya Oljoro JKT, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (ARFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina

MAOFISA TFF KUKAGUA VIWANJA 19 VYA VPL, FDL
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua maofisa wanaoanza leo (Januari 14 mwaka huu) kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Ukaguzi huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.

Viwanja vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza), Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage (Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora (Iringa).

Kumbukumbu ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani), Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui (Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), Umoja (Mtwara) na Vwawa (Mbozi).

Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.
 
RAIS MALINZI KUFUNGA SEMINA YA WAAMUZI LEO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa semina ya waamuzi na makamisha leo (Januari 4 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi zaidi ya 100 na makamishna 50 wameshiriki katika semina hiyo. Makamishna hao ni baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) wakati waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine baadaye mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL na zile za FDL.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)