MWENYEKITI CCM WILAYA YA TANGA AWAAGIZA WATENDAJI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWA UKARIBU.

November 04, 2013
Na Amina Omari,Mzizima.
Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi Wilaya ya TangaKassim Mbuguni amewaagiza watendaji wa mitaa,vitongoji na kata kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo kwa ukaribu katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho  na kama wakishidwa waachei ngazi.

Agizo hilo alilitoa wakati wa uzinduzi wa shina la Vijana wa nguvu

kazi wa  Chama Cha Mapinduzi UVCCM kata ya  Mzizima mwishoni mwa wiki ambapo alisema kuwa haiwezekani kuwa na watendaji ambao hawasimami wa kutekekeleza ilani ya chama.

Alisema kuwa ifike mahali ni lazima tuwe na watendaji ambao

tunaendanao kwenye maamuzi yetu sio kuwa na ambao wanatupinga na kurudisha nyuma maendeleo pamoja na kasi katika kuwasogezea huduma wananchi.

“Salamu nazitoa kwa watendaji ambao watashindwa kusimamia na

kutekeleza miradi wajitoe wenyewe,Ni aibu kwa mtendaji wa mtaa
kushindwa kusimamia mradi mdogo wa darasa moja la shule halafu
unajiita mtendaji hutufai katika mbio zetu za kuleta maendeleo jitoe
mapema kabla hatujakutoa kwa nguvu”Mbuguni.

Pia aliwashauri watendaji hao kuacha kukaa ofisi pekee na kusubiri

taarifa kwenye makaratasi bali wahakikishe wanashuka hadi katika ngazi za chini za wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi wa haraka .

Aliongeza kuwa sifa ya kiongozi bora aliyechaguliwa na wananchi ni
kuhakikisha anawasikiliza na kuwatatulia kero zao wanazokabilianazo waliomchangua na sio kusubi maamuzi kutoka ngazi za juu pekee.

“Nawapa taarifa nitaanza kupita kuanzia ngazi za mitaa,kata na

vitongoji katika Jiji hili na  kukagua maendeleo na changamoto
zilizopo Na jinsi zilivyotatuliwa na viongozi wa serikali nitakapo
baini mapungufu hatabaki mtu nitamtoa kwa aibu “alisisitiza Mbuguni.


Katika Hatua nyingine alimuagiza Diwani wa Kata hiyo Daniel Mgaza
  kuhakikisha na maliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji na umeme katika kata hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ili wananchi hao wasiendelea kuteseka na kero hizo.

Alisema kuwa diwani ni ndio msimamiaji sera na ndiuo aetetea wananchi
katika kata yake hivyo tatizo la maji na umeme kuikabili kata hiyo tena ipo mjini ni jambo la aibu hivyo ni vemna ahakikishea ameimaliza mapema kero hiyo.

PICHA ZA UZINDUZI WA SHINA LA VIJANA WA NGUVU KAZI UVCCM

November 04, 2013



HAPA WAKICHEZA NA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA TANGA,KASSIMU MBUGUNI BAADA YA UZINDUZI WA SHINDANO HILO.

KATIBU ITIKADI UENEZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA TANGA,LUPAKISYO KAPANGE AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI HUO LEO


MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA TANGA,KASSIM MBUGUNI KATIKATI WAKATI WA UZINDUZI WA SHINA HILO LA UVCCM KATA YA MZIZIMA JIJINI TANGA KULIA NI KATIBU ITIKADI UENEZI WILAYA YA TANGA,LUPAKISYO KAPANGE

RPC MKOA WA KASKAZINI AIPONGEZA TIMU YA POLISI PEMBA

RPC MKOA WA KASKAZINI AIPONGEZA TIMU YA POLISI PEMBA

November 04, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba .04/11/2013.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed Shekhan amewapongeza wachezaji wa timu ya Polisi inayoshiriki ligi kuu Visiwani hapa kwa kuonyesha nidhamu na kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kuchukua alama sita kutoka Kisiwani Pemba .

Akizungumza na msafara wa timu hiyo huko Ofisini kwake Wete , Kamanda Shekhan amewataka wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuongeza juhudi za mazoezi ili kuiwezesha timu kuchukua moja ya nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi na kuiwakilisha Nchi kwenye michuano ya Kimataifa . 

Amesema kuwa bila ya kuwepo na ushirikiano wa dhati  kati ya wachezaji na viongozi pamoja na   kuthaminiana kwa kila mmoja  wawapo nje na ndani ya uwanja mafanikio hayawezi kupatikana .

" Ni jambo la kujivunia kwamba timu umekuja Pemba na kuondoka na alama zote sita , nawaombeni muendelee kushirikiana , kuthaminana na kupendana ndani na nje ya uwanja ili muweze kuiletea mafanikio timu na jeshi la Polisi Visiwani hapa " alieleza Shekhan .

Naye msemaji wa timu hiyo Ramadhan Khamis Ramadhaman amesema kuwa ushindi walioupata kwa mechi za Pemba  umetokana na ushirikiano walionao wachezajio pamoja na Benchi zima la uongozi ambapo kila upande ulitimiza wajibu wake kama ilivyotakiwa .

"Unajua mafanikio haya yametokana na sisi kuwa na ushirikiano , ambapo wachehzaji walitekeleza majukumu yao kama walivyoelekezwa na viongozi nao waliwajibika kwa mujibu na kazi zao " alifamaisha .

Aidha Nahodha wa timu Adam Juma amesema kuwa lengo lao ni kutwa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar , na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono ili waweze kutimiza azma yao hiyo .

"Lengo ni kuwa mabingwa , tumewahi kutwa ubingwa  wa ligi kuu  Zanzibar na tunajua utamu wa ubingwa , sisi wachezaji tumewasha moto na kwa sasa sifikirii kama kuna timu utauzima , tunataka kurejesha heshima na hadhi ya timu yetu " alijinadi Adam .

Ikiwa kisiwani Pemba Timu ya Polisi imecheza michezo miwili ambapo iliifunga timu ya Kizimgbani Unioted mabao 3-1 kabla ya kuifunga timu ya Jamhuri ambayo inahemea chumba cha wagonjwa mahtuti kwa jumla ya mabao 2-1. na kuifanya timu ya Polis kufikisha alama 19 .