NAIBU WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI,TEKNOLOJIA NA UFUNDI ENG. STELLA MANYANYA APONGEZA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI(NACTE)WAKATI WA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA BARAZA HILO

February 10, 2016

Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.Wapili toka kushoto Mkurugenzi Msaidizi  wa Wizara hiyo Eng.Enock Kayani na  Mratibu wa maktaba ya Nacte, Clara Kihombo. 
 Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam kujua maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,katika Mratibu wa maktaba hiyo, Clara Kihombo.
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) jijini Dar es Salaam kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.
 Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(katikati) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam, kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi  wa Wizara hiyo Eng.Enock Kayani.
 Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(wapili kulia)akimsikiliza Vicent Jacob Mtaalam wa Mtandao wa Udhibiti wa Utoaji wa vyeti vya Satifiketi na Diploma kwa Baraza la Taifa na Ufundi(Nacte) wakati alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam, kujionea maendeleo ya utendaji wa baraza hilo.Watatu toka kulia Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera.
 Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi  na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya(kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwera(kulia)Wakati alipotembelea chumba cha maktaba ya kutunzia nyaraka alipofanya ziara maalumu ya kikazi,Makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam kujua maendeleo ya utendaji wa baraza hilo,Wapili kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi  Wizara hiyo Eng.Enock Kayani.
KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

February 10, 2016

4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania  Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar.
1 
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.
5
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika  katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,

2
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika  sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,3  
Baadhi ya majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi  katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
6
Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman  Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.
7
Kikundi cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,{Picha na Ikulu.]
Siku 100 za Rais John Magufuli, Wagonjwa Muhimbili Wapata Dawa kwa Asilimia 96

Siku 100 za Rais John Magufuli, Wagonjwa Muhimbili Wapata Dawa kwa Asilimia 96

February 10, 2016

muh1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
muh2
Waandishi wa habari  na Madaktari wakifuatilia mkutano huo leo.
muh3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Museru akisisitiza jambo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hospitali hiyo.
muh4
Kaimu Mkurungenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Museru akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwenye mkutano huo.
………………………………………………………………………………………………………………….
 Wagonjwa anaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi sasa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa yaliopo hospitali hapa.
Mafanikio hayo yamekuja baada ya uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa.
“Wagonjwa wanaokosa dawa kwenye maduka yetu, hospitali inanunua haraka ili mgonjwa apate dawa kwa wakati. Kwa sasa ukosekanaji wa dawa hospitalini umepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kuimarisha utendaji ndani ya hospitali,” amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.
Hayo yamesemwa leo na Profesa Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Profesa Museru amesema kwamba Katika muda wa kipindi cha miezi miwili Disemba 2015 na Januari 2016, hospitali imefanikiwa kulipa wafanyakazi malimbikizo ya madai yao ambayo walikuwa wakiidai hospitali hiyo kwa kipindi kirefu.
Malipo hayo ni malipo ya on call, malipo ya wauguzi ya usiku, malipo ya posho mbalimbali hasa kwa madaktari pamoja na kada nyingine za afya ambazo zinashughulika moja kwa moja na wagonjwa.
Amesema kwamba kutolipwa kwa malipo hayo kulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa na kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kukosekana kwa tija katika utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.
Katika hatua nyingine, Profesa Museru amesema kwamba mapato kwenye hospitali hiyo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 baada ya Disemba hospitali hiyo kuzalisha Shilingi bilioni 3.3 kutoka wastani wa shilingi 2.7 zilizokusanywa miezi mitano (Julai 2015 hadi Novemba 2015)
“Mwezi  Disemba mwaka jana  tulizalisha shilingi bilioni 3.3 na Januari 2016 tulizalisha shilingi bilioni 4.3,” amesema mkurugenzi huyo.
Akizungumzia mashine za CT-Scan na MRI, Profesa Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli ilinunulia Hospitali hiyo mashine mpya ya CT-Scan yenye uwezo wa 126 slices.
“Uwapo wa mashine hii mpya umeongeza uwezo kwa kiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwa wakati mmoja. Sasa tunaweza  kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde sita. Awali  tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakini sasa tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa 24.
“Baada ya kuwapo kwa mashine hizi mbili za CT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwa vipimo vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hii mpya ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye nguvu kubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamu zaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kama moyo, utumbo, ubongo na hivyo kupata majibu sahihi ya chunguzi na uhakika zaidi. Mashine hii mpya tangu ilipofungwa Novemba 26, 2015 hadi Februari 9, 2016 imepima wagonjwa 863,” amesema Profesa Museru.
Amesema kwamba baada ya mashine ya MRI kutengenezwa wagonjwa zaidi ya 2,200 wamepimwa na kwamba baada ya mashine ya CT-SCAN kutengenezwa wagonjwa zaidi 1,000 wamepatiwa vipimo.
Benki ya Dunia kutengeneza miundo mbinu imara Temeke

Benki ya Dunia kutengeneza miundo mbinu imara Temeke

February 10, 2016

msu 

Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO

Serikali kushirikiana na Benki ya Dunia inategemea kuanza ukarabati wa Miundo Mbinu mibovu hususani  ya mitaro inayosababisha maafa wilayani Temeke kuanzia mwezi Mei mwaka huu.
 Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Wilaya ya Tem
eke Joyce Msumba alipokua akiongea Ofisini kwake kuhusu maafa yaliyotokea maeneo ya Sokota,Shule ya Sekondari ya Kibasila na Mtaa wa Butiama  ambayo yalisababishwa na ubovu wa miundo mbinu hiyo.
Hili limetokea baada ya uchunguzi uliofanyika jana ambapo Mhandisi wa Wilaya, Bwana Afya pamoja na Afisa Habari wa Wilaya walifika eneo la tukio na kuona hali halisi.
‘’Ni kweli maafa hayo yametokea na sababu hasa ni miundo mbinu ya mitaro ambayo ilielekezwa katika maeneo ya makazi ya watu,kwahiyo inapotokea mvua kubwa maji hayaendi yanapostahili na badala yake yanaingia katika nyumba za watu’’Alisema Msumba.
Aliongeza kuwa ukarabati huo wa mitaro ni mradi ulio chini ya Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Aidha, Joyce Msumba amesema kuwa endapo mvua kubwa zitanyesha kabla ya mradi kuanza watatumia njia ya kuyanyonya maji kwa pampu na kuyapeleka sehemu husika ili kuzuia maafa yasiendelee kutokea.
Mradi huu unalenga kuhamisha njia za mitaro kutoka kwenye maeneo ya makazi na kuielekeza Bahari ya Hindi ili maji yanayopita katika mitaro hiyo yaende moja kwa moja baharin
MWIGULU ATUA MVOMERO KUJIONEA HALI HALISI ,ZAIDI YA MBUZI 70 WAKATWAKATWA MAPANGA

MWIGULU ATUA MVOMERO KUJIONEA HALI HALISI ,ZAIDI YA MBUZI 70 WAKATWAKATWA MAPANGA

February 10, 2016

Mh:Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi  Ndg,Mwigulu Lameck Nchemba akiwasili kata ya Hembeti,Kijiji cha Dihinda mapema hii leo kuangalia madhara na kuchukua hatua dhidi ya uhusiano mbaya uliopo kati ya wakulima na wafugaji uliopelekea kuuawa kwa mbuzi Zaidi ya 70 kwa kukatwakatwa mapanga wilayani Mvomero.

Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa kata ya Hembeti wilaya ya Mvomero wakati wa hatua za awali za kutafuta suluhu ya kuondokana na mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyosababisha Mbuzi zaidi ya 70 kukatwa katwa usiku wa kuamkia tar 9/02/2016 katika kitongoji cha Dihinda.
Katika Mkutano huo,Mwigulu pamoja na wananchi wamekubaliana tar 21/02/2016 kutafanyika mkutano mkubwa utakao husanisha wakulima na wafugaji ilikuweka mipaka ya kutenganisha eneo la kufigia na kilimo.
Wakati huohuo wote walioshiriki kwenye tukio la kukata kata mifugo wameshaanza kukatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,Mwigulu amesisitiza kuwa si vyema kujenga tabia ya visasi baina ya wakulima na wafugaji.Serikali imeshajipanga kuanza kugawa maeneo kwaajili ya jamii hizi mbili katika sehemu mbalimbali za nchi,hivyo basi wananchi wa Mvomero na sehemu zingine wawe wavumilivu wakati huu serikali ikianza kugawa maeneo upya kwaajili ya hifadhi,kilimo na malisho ya mifugo.
Mh:Mwigulu Nchemba akipokea baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkuu wa polisi (RPC) Mkoa wa Morogoro kuhusiana na tukio la mapigano ya wakulima na wafugaji eneo la Mvomero.
Mama mjane akilia mbele ya mifugo yake iliyouawa kwa kukatwakatwa mapanga.
Mwigulu Nchemba akishuhudia madhara yaliyotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji kitongoji cha Dihinda uliopelekea mbuzi hawa kukatwakatwa.

Serikali yasisitiza kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi nchini

February 10, 2016

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye (kulia) wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Serikali imesema dhamira yake ya kujenga uchumi wa viwanda nchini imejengwa kupitia maeneo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kutumia malighafi zipatikana nchini ikiwemo mzao ya misitu, kilimo, uvuvi na madini ili kuwahudumia wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam.

Dkt. Mpango aliyaeleza maeneo hayo ya vipaumbele ambayo yataanza kutekelezwa katika bajeti hiyo ni pamoja na kuvirudisha viwanda vilivyobinafsishwa na kutafuta wabia ambao wanaweza kufanyakazi iliyodhamiriwa.

Maeneo mengine ni miradi mikubwa ya kielelezo ambalo wataalam wanalifanyiakazi ili kuweza kupata matokeo makubwa, akitolea mfano Dkt. Mpango alisemas kuwa yapo maeneo maalum ya kibiashara yakiwemo Bagamoyo, Kigoma na Mtwara kutokana na maliasili iliyopo hapo.

Zaidi ya hayo, Dkt. Mpango aliongeza kuwa ujenzi wa kiwanda cha chuma kwa kutumia malighafi inayozalishwa kwa kutumia chuma kutoka Liganga na Mchuchuma itakuwa ni msingi wa viwanda mama ikizingatiwa “Hakuna ujenzi usiohitaji chuma”.

Katika suala la ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa, Dkt. Mpango alisema kuwa mradi huo ni muhimu kwa lengo la kusukuma mbele sekta ya usafirishaji ndani na nje ya nchi ikwemo nchi za Rwanda, Burundi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mataifa mengine.

Mafanikio ya ujenzi wa viwanda nchini yanawezekana kwa kwa kuwa Serikali imedhamiria kushirikiana na serkta binafsi kwa kuwa maendeleo ya viwanda yanapaswa kuendana na maendeleo ya watu kwa kuwapatia ajira, elimu inayoendana na mahitaji ya viwanda ili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.

Aidha, ili kujenga uwezo wa kuwa na viwanda nchini, Serikali imejipanga kukusanya kodi ambayo ndiyo msingi wa kuwa na uchumi imara utakaosaidia nchi kujiendesha ambapo wafanyabiashara wote nchini wanapaswa kujisajili na kupewa namba ya usajili (TIN) huduma ambayo inapatikana nchi nzima kupitia ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika mkutana huo, Dkt. Mpango amewaasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara yao ili kuwa na kumbukumbu ambazo zinatoa taarifa sahihi na kuhimiza wafanyabiashara wenye mashine za kielekroniki (EFD) waendelee kuzitumia wanapouza bidhaa zao na kuwaptia risiti wateja wao, kwa wale wasio na mashine hizo, Serikali inaendelea kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli la kuwapatia mashine hizo.

Vile vile, Dkt. Mpango ametoa namba za simu za ofisi za TRA kitengo cha Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na Idara ya Mambo ya Ndani TRA juu ya maadili ya watumishi wa mamlaka hiyo nchi nzima kwa namba 0689122515 na kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0689122516.

Aidha, Dkt. Mpango amewaonya wafanyabiashara ambao sio waaminifu waache kufanyabiashara za magendo ambapo ameainisha baadhi ya maeneo yanayotumiwa ni pamoja na mwambao wa bahari ya Hindi maeneo ya Mbweni, ziwa Victoria na ziwa Tanganyika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati na Sera TPSF Felix Mosha  amesema kuwa Sekta binafsi itaendelea kushirikiana na Serikali katika mpango wa kukuza uchumi wa nchi na kumhakikishia  Waziri wa Fedha na Mipango kuwa watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi na kuhamasisha wafanyabiashara wote nchini wanakwenda pamoja na Sera ya “Hapa Kazi Tu”

RC MAHIZA AWAPA MAELEKEZO WAKURUGENZI KUHUSU MAELEKEZO YA KUTUMIA FEDHA KWENYE MPANGO WA ELIMU BURE

February 10, 2016
MKUU WA MKOA WA TANGA,MWANTUMU MAHIZA AKIZUNGUMZA NA WADAU WA ELIMU KWENYE KIKAO CHA PAMOJA BAINA YAO NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NA MAAFISA ELIMU NA WALIMU WAKUU.





WAKURUGENZI NA MAAFISA ELIMU WA SHULE ZA SEKONDARI NA MSINGI WAKILA KIAPO CHA KUTUMIA FEDHA ZINAOPELEKWA KWENYE MAENEO YAO KWA MATUMIZI YALIYOKUSSDIWA NA SIO VYENGINEVYO




KOMBE LA SHIRIKISHO RAUNDI YA 16

KOMBE LA SHIRIKISHO RAUNDI YA 16

February 10, 2016
Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16 bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.
Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.
Ijumaa tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumamosi, Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex - Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Februari 28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Raundi hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Young Africans watawakaribisha JKT Mlale katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.

BELLA KUPAGAWISHA TANGA USIKU WA VALENTINE DAY "RED IN WHITR PARTY JUMAMOSI HII

February 10, 2016

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AZUNGUMZIA TUKIO LA KUSHAMBULIWA HELKOPTA YA DORIA ILIYOPELEKEA KIFO CHA RUBANI WAKE.

February 10, 2016

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 09/02/2016 katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu ya Wizara hiyo kuzungungumzia tukio la hivi karibuni (tarehe 29 Januari 2016) la kushambuliwa kwa helkopta ya doria na kuuawa Rubani Rogers Gowel Raia wa Uingereza. Katikati ni Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Wizara hiyo Maja Gen. Gaudence Milanzi. SOMA TAARIFA KAMILI HAPO CHINI (SCROL DOWN FOR MORE DETAILS)
 Mkutano na Waandishi wa Habari ukiwa unaendelea.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, INSPEKTA Jenerali (IGP), Ernest Mangu, kulia akifafanua moja ya jambo katika Mkutano huo. Kulia ni Waziri wa  Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
 Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Maliasili walioshiriki mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keraryo. 
Waandishi wa habari wakichukua matukio ya mkutano huo na baadhi ya washiriki wakifuatilia.
(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)