RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE)

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE)

June 25, 2016




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizindua Kituo kidogo cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Maguguli akisimama wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Sehemu ya wananchi na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akihutubia uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa TBA Bw. Elius Mwakalinga wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo ya ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam.. Pamoja naye ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma na binfasi.

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma leo

June 25, 2016



Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.


Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani. 
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kushoto) na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakiosha gari. 
Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kulia) akimkabidhi fedha za kuoshewa gari Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel. 
Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo.
Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa TAZARA lazinduliwa rasmi leo

Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa TAZARA lazinduliwa rasmi leo

June 25, 2016


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa. Makame Mbarawa (MB) amezindua rasmi Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) tukio lililofanyika mapema leo Juni 25.2016, Jijini Dar es Salaam.

Akisoma hutuba ya ufunguzi wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho kwa niaba ya Waziri Profesa Mbarawa, Amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa moyo mmoja katika hali ya kuifufua TAZARA kiutendaji na ufanisi kama ilivyokuwa zamani.

Akisoma hutuba hiyo, aliwapongeza viongizi wa wanaounda Mamlaka hiyo akiwemo Mhandisi Bruno Ching’andu kwa kuteuliwa kwake kuongoza Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wote.

Ambapo alisema kuwa, ni dhahiri hatua ya leo imefikiwa baada ya jitihada kubwa na hasa tukitilia maanani hali ya kifedha ambayo TAZARA inapitia katika kipindi hiki. Hivyi kuwapongeza kwa uamuzi huo kwani Mabaraza yana umuhimu mkubwa katika maeneo ya kazi na yameonyesha mafanikio makubwa kila yalipoanzishwa kwani yameweza kuongeza uhusiano mwema kati ya Manejimenti, Vyama vya Wafanyakazi na wafanyakazi kwa upande mwingine.

“Mabaraza haya ni dhana ya ushirikishwaji ikiwa na maana kuwapatia wafanyakazi fursa ya kushauri juu ya masuala ya utendaji kazi, sera za taasisi, ufanisi wa kazi, mazingira ya kazi, ustawi wa wafanyakazi katika elimu, nidhamu, vyeo, pamoja na motisha kwa wafanyakazi. Pia dhana hii ya ushirikishwaji ni kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108.

Pia ni kwa mujibu wa Sheria ya majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Pia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kifungu Na. 73 (1 - 3).

Taarifa niliyopewa ni kwamba kikao hiki cha sasa cha Baraza kitapata fursa ya kuijadili taarifa ya kazi ya Mamlaka kwa mwaka 2015/2016, kuupitia mpango kazi kwa kipindi cha 2016/2017 na pia bajeti ya mapato na matumizi ya Mamlaka kwa kipindi cha mwaka 2016/2017. Kwa maana hiyo hiki ni kikao muhimu sana kwa mustakabari wa Mamlaka ya TAZARA.

Wajumbe wote ninawaomba muwe makini sana kuelewa hayo malengo na kuweza kutafsiri kwa usahihi ili muweze kuyawakilishe hali halisi kwa wafanyakazi wenzenu kwa ili malengo yapate kutimizwa. Ninyi mtakuwa kiungo muhimu sana katikakufanikisha swala zima la kuleta matumaini mapya.

Kwa kuwa Mamlaka hii ni alama ya ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia imeendelea kuwa muhimu kwa nchi zetu. Napenda kuwakumbusha wajumbe wote kwamba wajibu wenu kwa sasa ni kuhakikisha Mamlaka inarudi katika hali yake ya zamani ilipokuwa ikijiendesha yenyewe kwa kutimiza wajibu wake wa kulipa mishahara kwa wafanyakazi,kulipa kodi Serikalini, michango ya wafanyakazi katika mufuko ya jamii ..

Na kwa njia hii pekee itayorudisha imani upya kwa wateja ambao wamejiondoa kwa kipindi sasa hali iliyopelekea hali ya Mamlaka kimapato kudhoofika.

Kwa kumalizia, napenda nitoe rai kwa uongozi wa Mamlaka na wa vyama vya Wafanyakazi kuwa mkutano huu uwe ni mwanzo muendelezo wa mikutano mingine kadri kanuni inavyoagiza ili kuongeza tija na utulivu. Mahali hapa ni fursa ya kuelezana, kukosoana na kuwekana sawa kwa manufaa ya TAZARA na Umma wote wa Tanzania na wa Zambia pamoja na nchi jirani wanaotumia reli hii kwa namna moja au nyingine.

Mwisho nawatakia mkutano wenye mafanikio na pia napenda kutangaza kwamba Baraza hili nimelizindua rasmi. Ahsanteni!
Dada Regina Tarimo Afisa uhusiani wa TAZARA-Tanzania, akiwakaribisha wajumbe wa Baraza hilo jipya kwenye mkutano maalum wa uzinduzi wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya akisoma taarifa namna ya TUCTA inavyofanya kazi na Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi.Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa.Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (mbele) akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa.Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho(wa pili kutoka kulia) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa juu wa wafanyakazi wa TAZARA. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (Katikati) akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa TAZARA. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

WATUMISHI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA NEMC WAHSIRIKI USAFI

June 25, 2016


Pichani baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza LA Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nemc..wakishiriki usafi kwa pamoja na wananchi wa Wilaya ya Temeke na kinondoni,katika kutekeleza Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi ya Usafi kitaifa..(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
TRA yazidi kuboresha timu ya kutoa elimu ya kodi, yazindua Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM

TRA yazidi kuboresha timu ya kutoa elimu ya kodi, yazindua Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM

June 25, 2016
Katika kuhakikisha kunakuwa na wasomi ambao wanakuwa na elimu kuhusu kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi (Student Tax Association) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo wanachama hao watatumika kutoka elimu kwa wananchi wengine kuhusu kodi.

Akizungumza katika uzinduzi wa jumuiya hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema malengo ya kuwa na jumuiya za kodi vyuoni ni kuwezesha jamii kupata elimu ya kutosha kuhusu kodi kupitia wanachama wa jumuiya hizo ambao watakuwa wakipatiwa mafunzo kuhusu umuhimu wa kulipa kodi lakini pia kuhudhulia midahalo mbalimbali ambayo itakuwa inazungumzia kodi.

Alisema hatua ya kuanzisha jumuiya hizo imekuja baada ya kuwa na vilabu katika shule za msingi na sekondari nchini na sasa wakaona kuna umuhimu wa kuwa na wanachama kutoka vyuo vya elimu ya juu ili wawe mabalozi wa TRA ili kusaidia utoaji wa taarifa kuhusu kodi lakini pia na wao kutambua umuhimu wa kodi ili hata baada ya masomo yao waweze kuwa walipa kodi wazuri.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).

"Tulianzisha mfumo wa vilabu mwaka 2008 ambapo tuna vilabu 195 kwa Tanzania Bara na Zanzibar na katika vilabu hivyo tuna wanachama 15,520 hivyo tukaona sasa ni muhimu kuwa na wanachama kutoka vyuoni ili nao waweze kupata elimu kuhusu kodi,

"Wanachama wa jumuiya hizi watakuwa na shughuli ya kutoa elimu kwa watu wengine ambao hawana elimu ya kodi, kuandaa wataalum wa elimu ya kodi kwa miaka ya baadae na hata walipa kodi wa baadae kwani tayari watakuwa wanafahamu umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya taifa," alisema Kayombo.
Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM (ISTA), Amon Ojode akielezea jinsi ambavyo wanafunzi wa IFM watanufaika na uwepo wa jumuiya hiyo chuoni hapo.

Nae Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM, Amon Ojode alisema kuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya kuwa na jumuiya ya kodi na zaidi ni wanafunzi ambao wanajifunza masomo yanayohusiana na kodi hivyo wanaamini watakuwa wawakilishi wazuri wa TRA.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).
Waziri wa Afya na Mambo Yote kwa Ujumla katika serikali ya wanafunzi wa IFM (IFMSO), Suleiman Kahumbu akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masalla akizungumzia kodi wakati wa uzinduzi wa jumuiya hiyo.
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya wa Wanafunzi wa Kodi IFM na wanafunzi wa chuo hicho waliohudhuria uzinduzi wa jumuiya chuoni hapo.