DKT. MPANGO NA BALOZI WA KUWAIT WAZUNGUMZA KUHUSU UJENZI BARABARA YA MOROGORO- DODOMA

DKT. MPANGO NA BALOZI WA KUWAIT WAZUNGUMZA KUHUSU UJENZI BARABARA YA MOROGORO- DODOMA

March 23, 2018





Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani) kuhusu ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.



Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (Kulia) na Afisa mwandamizi kutoka Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) kuhusu ufadhili wa ujenzi wa barabara za Mkato za kuingia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma.



Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini Dodoma.



Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Bw. Edwin Makamba na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Hangi Laban, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri huyo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani), Mjini Dodoma.



Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.



Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Selikarini Wizara ya Fedha na Mipango

…………………

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Dodoma, Machi 23, 2018: Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.

Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.

Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.

Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.

Dkt. Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77,

Mradi mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TUMIENI TOVUTI KUTANGAZA MAENDELEO YA WANANCHI

SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TUMIENI TOVUTI KUTANGAZA MAENDELEO YA WANANCHI

March 23, 2018

1.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali wakati wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
2.
Baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatiliano mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
3.
Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Atley Kuni akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikali wakati wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa tovuti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa yaliyofungwa leo Ijumaa Machi 23, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
(NA MPIGAPICHA WETU
………………….
Na Mwandishi Wetu,
MAELEZO
MOROGORO
23.3.2018
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, wametakiwa kuongeza kasi ya matumizi ya  mitandao ya kijamii ikiwemo tovuti ili kuleta mageuzi yaliyokusudiwa na Serikali katika kutangaza shughuli za maendeleo ya wananchi.
Hayo yamesemwa leo (Ijumaa Machi 23, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini yaliyohusu mwongozo wa uendeshaji wa  Tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus alisema Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa pamoja waliandaa mwongozo huo ili kuhakikisha kuwa tovuti za Mikoa na Halmashauri zinakuwa nyenzo muhimu ya taarifa za Serikali.
“Mafunzo mliyoyapata ni vyema mkahakikishe kuwa tovuti zenu zinaweza kusaidia maendeleo ya wananchi kwa kutangaza shughuli za maendeleo pamoja na kuzingatia thamani ya fedha zilizotolewa na wadau wetu wa maendeleo kwa kuleta mabadiliko ya mwonekano wa tovuti zetu” alisema Thadeus.
Aidha alisema kupitia mafunzo yaliyotolewa kuhusu mwongozo huo, ni matarajio ya Serikali kuwa tovuti zote za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakuwa zimesheni habari zilizoandikwa kwa usahihi pamoja na kuwekwa taarifa za mara kwa mara hatua itayowezesha wananchi wengi Zaidi kuweza kuzitembelea na kupata huduma zinazostahili.
Alisema Ofisi yake ipo tayari kufanyia kazi na Maafisa Habari na Mawasilino waliopo katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa iwapo kutajitokeza changamoto yoyote inayohusu usimamizi, uendeshaji na uboreshaji wa maudhui ikiwemo mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji wa tovuti hizo.
Thadeus alisema Idara ya Habari (MAELEZO) itahakikisha kuwa inafanya mawasiliano ya mara kwa mara na Watendaji Wakuu wa Mikoa na Halmashauri za Wilaya ili kuhakikisha kuwa Maafisa Habari na Mawasiliano ambao ndio watendaji  wa tovuti hizo wanapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Wakuu mbalimbali wa Idara na Vitengo katika Mikoa na Halmashauri zote nchini.
Kwa upande wake, Afisa Habari kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Atley Kuni alisema malengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa tovuti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa zinakuwa kiunganishi baina ya Serikali na wananchi kwa kuhakikisha zinatangaza taarifa mbalimbali za mafanikio ya Serikali katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Tumepanga tuwe na jarida maalum litakalokuwa na habari mbalimbali za mafanikio ya miradi ya maendeleo, ambazo zitakuwa zikiandikwa na Maafisa Habari na Mawasiliano waliopo katika Mikoa na Halmashauri ambazo zitakuwa zikiakisi maendeleo yaliyoweza kupatikana mara baada ya kuanzishwa kwa tovuti hizi” alisema Kuni.
Aidha aliongeza kuwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa hawana budi kuongeza ubunifu ili kuhakikisha kuwa tovuti hizo pia zinaweza kuwa chanzo kikuu cha mapato katikas maeneo yao ya kazi.

NAIBU KATIBU MKUU UWT EVA KIHWELE AMEVUNA WANACHAMA WAPYA ZAIDI 300 KATIKA TARAFA YA MAZOMBE MKOANI IRINGA

March 23, 2018
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa 
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiwapatia kadi wanachama wapya wa umoja wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa

 Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa wakiwasindikiza wanachama wapya kula kiapo cha kukitumikia chama hicho
 Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwaonge na wananchi pamoja na wanachama wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa.

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

NAIBU katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele amevuna wanachama wapya zaidi ya mia tatu (300) katika tarafa ya Mazombe wilayani Kilolo mkoani Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.

Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo naibu katibu mkuu bara Eva Kihwele alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa tarafa ya Mazombe ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa katibu huyo.

Kihwele alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia  mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.

“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisema Kihwele


Aidha Kihwele aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.

“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisema Kihwele

Kihwele alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.

“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Kihwele

Kihwele alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.

“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Kihwele

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.

“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Twelve

Naye Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer amewataka wanawake kote nchini kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za ujasiriliamali ili kuachana na utegemezi.

Laizer alisema kuwa baadhi ya wanawake hasa wa vijiji wamekuwa wakipata msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kipato licha ya kushiriki shuhuli za uzalishaji mali ngazi ya familia lakini wengi wao wamekuwa hawashirikishwi katika matumizi ya kipato walichokitolea jasho. 

Laizer alisema kuwa kuna mifuko maalumu ya kuwaisidia wanawake hasa wa hali ya chini kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi ili kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuachana na utegemezi hivyo msaada walioupata utawafanya wapige hatua kubwa zaidi.

Laizer alisema kuwa kumsaidia mwanamke wa hali ya chini kwa kumuwezesha kimtaji ni kukomboa jamii kwani mama huyo ataweza kuhuduma familia yake bila ya kuwa tegemezi.

SHEHENA YA BIDHAA YAKAMATWA WILAYANI MUHEZA

March 23, 2018
 Sehemu ya Shehena ya sukari iliyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga
 Sehemu ya Mafuta ya kula yaliyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga wakati wa operesheni yao
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe kulia akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya sukari iliyokamatwa
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe akiwaonyesha shehena ya sukari iliyokamtwa waandishi wa habari ambao hawapo pichani
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe akionyesha pia baadhi ya vitu vilivyokamatwa

JESHI la Polisi Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato wam ekamata shehena ya bidhaa kwenye kisiwa cha Karange karibu nabandari bubu ya Kigombe wilayani Muheza huku watu watano wakishikiliwakwa kuhusika kuingiza bidhaa hizo.

Bidhaa hizo zilikuwa zikiingizwa kwa kutumia usafiri wa majahazi  ni sukari na mafuta zimekamatwa kufutia operesheni ambazo Jeshi la Polisi wanaloendelea nalo kwa nchi kavu na majini kuhakikisha wanazibiti biashara haramu ya magendo kuingia mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Edward Bukombe alithibitisha kukamatwa kwa shehena hiyo juzi na watu hao ambao wanadaiwa kuhusika na usafirishaji wa magendo kwa njia ya bahari.

 Alisema ukamataji wa bidhaa hizo unatokana na operesheni za nchi kavu na baharini zinazoendelea kupitia jeshi hilo ili kudhibiti wimbi la uingizwaji wa bidhaa za magendo zinazoingizwa mkoani hapa kupitia bandari bubu.

Kamanda Bukombe alisema kuwa majahazi hayo yalikuwa yamesheheni mifuko 300 ya sukari,madumu 200 ya mafuta ya kula na vitambaa vya kushonea nguo za wakina nama maarufu kama majora vikiwa vinatokea katika visiwa vya Zanzibar na Pemba.

Alisema jeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kufanya operesheni zake ili kuhakikisha wafanya biashara wote wanatumia bandari zilizorasimishwa kwa ajili ya kuingizia bidhaa zao kihalali na kuzilipia kodi.

“Tunamashaka na watu hawa na hata hizi bidhaa zenyewe maana kama kweli hazina mashaka kwa nini wanaziingiza kwa njia ya panya zinaweza kuwa hazina ubora au watu hawa wanakwepa kodi sisi tutapambana nao tu”Alisema.

Bukombe alisema hatua ya kukamata ni ya awali na kukabidhi bidhaa hizo kwa mamlaka ya chakula na dawa ili wathibitishe ubora na mamlaka ya mapato Tanzania watatoa maamuzi ya bidhaa hizo na vyombo vilivyo bebea.

Alisema watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi mkali na hakutaja majina yao mapema kwa ajili ya swala la kiupelelezi na kusema baada ya kukabidhi taarifa kamili katika mamlaka husika taariza itatolewa kwa hatma ya bidhaa hizo na vyombo.

Akizungumzia ukamataji huo mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kigombewilayani Muheza Athumani Mbwambo alisema ipo haja kwa serikali kuangalia upya suala la kodi ili kuepusha wafanyabiashara kuendelea kutumia njia za panya  na kujikuta wakiingia mikononi mwa Polisi na kupoteza mitaji yao.

Alisema pamoja na ukamataji huo lakini serikali iweka mpango mzuri wa kuzirasimisha bandari bubu za asilimia ikiwemo ya Kigombe ili kuwawezesha wafanyabiashara wanaoitumia kulipa kodi.

“Lakini pia nafikiria Serikali inaowajibu wa kuangalia upya kodi
wanazotoza inawezekana zikawa kubwa kuliko mitaji yao na kupelekea wafanyabiashara kukwepa kutumia njia halali”Alisema.

Mwisho.

SERIKALI KUWEKEZA HALI YA HEWA-PROF. MBARAWA

SERIKALI KUWEKEZA HALI YA HEWA-PROF. MBARAWA

March 23, 2018





Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo wakati wa Siku ya Maadhimisho ya Hali ya Hewa Duniani, mkoani Dodoma, kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Atashasta Nditiye, wa pili Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agness Kijazi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), Hamza Johari.

………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kuwezesha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati na usahihi kwa manufaa ya taifa.

Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mjini Dodoma leo wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Hali ya hewa, na kusisitiza kuwa kwa sasa TMA imeongeza imani kwa wananchi kwani imekuwa ikitoa utabiri wa kuaminika kwa sababu ya kuwa vifaa vingi na vya kisasa vya utoaji taarifa.

“Nipende kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwezesha TMA na kuhakikisha kuwa inatoa utabiri ambao ni sahihi na wa uhakika kwani kuwepo kwa utabiri sahihi kutawezesha vyombo husika kuchukua hatua mapema kabla ya madhara makubwa kutokea” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuepuka kuchafua maeneo ya bahari ili kuepusha athari zinazoepukika zikiwemo uharibifu wa miundombinu ya uchukuzi.

“Niwaombe wananchi wote watunze mazingira kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu katika maeneo mbalimbali yasiyotakiwa kulimwa au kujengwa, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa kwa kutoa fedha kununua vifaa mbalimbali ambavyo vimewezesha mamlaka hiyo kutoa utabiri uliosahihi kwa zaidi ya asilimia 70.

Dkt Kijazi ameongeza kuwa kwa sasa taarifa za hali ya hewa hasa kwenye usafiri wa anga zimeimarika ambapo hutolewa kila baada ya nusu saa na kuwawezesha watumiaji wa usafiri huo kupata taarifa kabla ya kuanza safari zao.

“Kwa sasa utabiri wa usafiri wa anga ni wa uhakika mpaka asilimia 90 na hutolewa kila baada ya nusu saa na marubani hupata taarifa hizo kwa wakati kabla ya kuanza safari zao, amesema Dkt. Kijazi.

Siku ya Hali ya Hewa duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi ambapo mwaka huu yanaongozwa na kauli mbinu isemayo “JIWEKE TAYARI NA ZINGATIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA”.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

SHIRIKA LA AGPAHI LAKABIDHI MASHINE YA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE KWA WILAYANI MUHEZA

March 23, 2018




Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa kushoto akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Muheza MwanashaTumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake(cryotherapy machine) kushoto anayeshuhudia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa akimpongezwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Dkt Asha Mahita



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGPAHI, Dr.Sekela Mwakyusa katikati akiwasikiliza kwa umakini Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Dkt Asha Mahita na kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala

SHIRIKA la AGPAHI linalojihusisha na masuala ya ukimwi katika kutambua mchango wa sekta ya afya katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza limemkabidhi mkuu wa wilaya ya Muheza Mwanaasha Tumbo mashine ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake( cryotherapy machine).

Mashine hiyo mkuu wa wilaya ya Muheza alikabidhiwa juzi na mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika warsha ya siku mbili ya wadau wa sekta ya ukimwi kutoka taasisi binafsi na serikali iliyofanyika katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga juzi.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo hiyo Dr.Sekela Mwakyusa alisema kuwa katika kutambua mchango wa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mkuu huyo wa wilaya ya Muheza katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza waliamua kumzawadia mashine hiyo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika vifaa tiba.

"Sisi AGPAHI leo tunakukabidhi mashine hii ya kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kama sehemu ya mchango wetu katika harakati za ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza" alisema Mwakyusa.

Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya alilishukuru shirika hilo hiyo kwa kumzawadia kifaa hicho muhimu ambapo kwa kuanza atakikabidhi katika hospitali Teule ya Muheza( Muheza DDH) ili ianze kazi.

Hata hivyo aliwashukuru shirika la AGPAHI kwa kunipatia kifaa hiki muhimu kwa wakina mama,nikisema kikae mpaka hospitali ikamilike kitaharibika hivyo nitawakabidhi hospitali Teule ya Muheza ili waanze kukitumia" alisema.

Kwa kuanzia mkuu huyo wa wilaya alimuomba mganga mkuu wa mkoa kupanga siku maalum ya upimaji wa saratani ya kizazi wilayani Muheza ili wakinamama wote wa mkoa wa Tanga wapate huduma hiyo.

MRADI WA MAHINDI BORA WAZINDULIWA MOROGORO

March 23, 2018




Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin, akimuonyesha Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, moja ya picha katika Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini, katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji hicho. Mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro na Chuo hicho Kikuu cha Kilimo cha China. Nyuma yao ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro.



Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, akisalimiana na Profesa Wu Jiu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.



Wasanii akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.



Balozi wa Tanzania hapa nchini Wang Ke akisaini kitabu ca wageni alipowasili kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba moani Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa mkoa huo Regina Chonjo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro



Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe (mwenye gauni la bluu) na Regina Chonjo wakiselebuka muziki na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho mkoani Morogoro.



Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.



Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro.



Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani humo.



Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.



Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji hicho cha Mtego wa Simba.



Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, akipongezwa na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo baada ya hotuba yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya gairo Siriel Mchembe



Benjamin Amos akizungumza wati wa uzinduzi wa kwanza wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China. uzinduzi huo ulienda pamoja na uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba Mikese mkoani Morogoro.



Waliosoma katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha China waakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya uzinduzi wa Jumuiya ya Waliosoma katika Chuo hicho



Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo na Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (kulia) wakijiandaa kufungua mabango yenye maelezo, wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.



Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.



Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke, wakifungua bango lenye maelezo wakati wa uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.



Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro Clinfford Tandari na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakifurahi baada ya kufanya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.



Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China Profesa Sun Qixin (kushoto ) na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Morogoro Regina Chonjo wakionyeshana bango lenye maelezo baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Mafunzo cha kupunguza Umasikini kijijini katika Kijiji cha Mtego wa Simba, Mikese mkoani.



Balozi wa China hapa nchini Wang Ke (katikati) akiwa na viongozi mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Cha China na Viongozi wa mkoani Morogoro baada ya uzinduzi wa Mradi wa pamoja wa Tanzania na China wa kuongeza kuzalishaji wa tija wa zao la mahindi, uliofanyika jana katika kijiji cha Mtego wa Simba mkoani Morogoro. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO