MO Dewji Foundation kushirikiana na Tulia Trust kujenga vyoo katika Hospitali ya Rungwe

MO Dewji Foundation kushirikiana na Tulia Trust kujenga vyoo katika Hospitali ya Rungwe

March 11, 2017
  Katika kuendeleza huduma zake kwa jamii, Taasisi ya MO Dewji imeungana kwa pamoja na Taasisi ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson kujenga vyoo katika Hospitali ya Rungwe iliyopo mkoani Mbeya. Akizungumza kuhusu ushirikiano huo katika mashindano ya kukimbia ya Tulia Marathon, Mratibu Miradi wa Taasisi wa MO Dewji, Catherine Decker amesema taasisi yao imeamua kushirikiana na Dk. Tulia ili kusaidia kuboresha sekta ya afya ya nchini ambayo kwa sasa bado inakabiliwa na changamoto nyingi. Catherine alisema Taasisi ya MO Dewji imejikita zaidi katika kusaidia sekta ya elimu, afya na huduma za kijamii na hivyo ushirikiano na Tulia Trust ni mzuri kwao na umekuja ikiwa ni miezi miwili imepita tangu walipotoa msaada mwingine katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya SekouToure iliyopo Mwanza na kama taasisi wana miradi nyingi wamepanga kuifanya ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano.
Mratibu Miradi wa Taasisi wa MO Dewji, Catherine Decker akizungumza kuhusu ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Tulia Trust kujenga vyoo katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rungwe.
“Huduma za afya ya uzazi zimekua ni changamoto katika sekta ya afya nchini, hivyo taasisi yetu imekusudia kutoa misaada ili kuziboresha na sasa safari yetu imetuleta mkoani Mbeya, ambapo tuna muunga mkono Mheshimiwa Naibu Spika kuchimba vyoo katika hospitali ya Rungwe kwenye wodi za kina mama wajawazito, “Wanawake ni msingi wa maendeleo katika jamii zetu, tafiti zinaonyesha kuwa kufanya kazi na wanawake, kunawapa nafasi ya kuongeza kipato chao, kwani ni njia bora katika kuchangia maendeleo chanya kwa jamii,” alisema Catherine na kuongeza. “Lakini ili tuwaheshimu wanawake tunapaswa kuhakikisha kuwa wanapata huduma za afya ya uzazi, ikiwemo vifaa bora pamoja na mazingira safi ili kuboresha usalama wa afya zao. Kwa kufanya hivi itachangia kuboresha sekta ya afya katika jamii zetu, jambo ambalo tuna litazamia kama taasisi.” Kwa upande wa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dk. Tulia Ackson aliishukuru Taasisi ya Mo Dewji kwa udhamini huo ambao umeambatana na mashindano ya kukimbia ya Tulia Marathon na malengo ya kuanzisha mashindano hayo ni kukusanya pesa ili kusaidia kuboresha sekta ya elimu na afya.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania na mwanzilishi wa Taasisi ya Tulia Trust, Dk. Tulia Ackson akizungumza kuhusu ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Tulia Trust kujenga vyoo katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Rungwe.
“Tulikuwa na malengo maalumu ila kikubwa ni kuimarisha afya na elimu, hospitali ya Rungwe kwa sasa wodi ya kina mama ina choo kimoja na sisi kama Tulia Trust kwa kushirikiana na wadhamini wetu [Mo Dewji Foundation] tumepata fedha ambazo tutajenga vyoo kwa ajili ya hiyo wodi ya kina mama na mabafu pia, “Na hicho ndicho kinachotofautisha marathon hii ya kwetu na hizo zingine, hii tulikuwa na mpango maalumu wa kukusanya fedha ili tuweze kuboresha miundombinu ya elimu na afya na huu ni mwanzo tu mwakani tutafanya mambo mengi zaidi,” alisema Dk. Tulia. -- RABI HUME Journalist - MO Blog 0769241355 / 0676231455
SHYROSE AWASILISHA MUSWADA BINAFSI KUSAIDIA WENYE ULEMAVU

SHYROSE AWASILISHA MUSWADA BINAFSI KUSAIDIA WENYE ULEMAVU

March 11, 2017
Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda. Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania. Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu. Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino. Mheshimiwa Shyrose Bhanji"Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii, " anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill 2017. Mwanamuziki mahiri nchini Chege Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika: “Hongera sana Mbunge wetu wa Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.  
Kipande cha nakala ya muswada huo. -- Zainul A. Mzige, Managing Director, Mzige Media Limited, www.thebeauty.co.tz +255714940992.

MASHINDANO YA MABALOZI WA MTOTO MFANYAKAZI WA NYUMBANI YAFANA JIJINI MWANZA

March 11, 2017

     Mgeni rasmi, Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza, Kizito               Wambura (kulia), akikabidhi kombe kwa washindi wa                             mashindano hayo yaliyofanyika leo katika viunga vya                                         shule ya msingi Nyamagana.
                                                                       #BMGHabari
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamagana wameibuka washindi kwenye mashindano elimishi kwa klabu za mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani dhidi ya wakubwa zao kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma, zote za Jijini Mwanza.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) ya Jijini Mwanza, yalijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo maigizo, ngonjera pamoja na mashairi yenye jumbe za kuainisha aina za ukatili wanaokumbana nao watoto wafanyakazi wa majumbani ikiwemo vipigo, utumikishwaji na fursa ya kukosa elimu, na kuiasa jamii kuachana na vitendo hivyo.

"Ukiona mtoto anatendewa ukatili wa aina yoyote, paza sauti (toa taarifa) sehemu mbalimbali ikiwemo WoteSawa, polisi kupitia kitengo cha dawati la jinsia, kwa Mwenyekiti wa Mtaa ama Mtendaji wa Kata". Amesisitiza mgeni rasmi, Wambura.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya WoteSawa, Angel Benedicto, amebainisha kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kutumikishwa kwa kuajiriwa ili kutembeza bidhaa mtaani kwa ujira mdogo, kunyimwa fursa ya kusoma pamoja na vipigo kutoka kwa baadhi ya waajiri hivyo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu katika jamii ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.

"Lengo ni kupunguza ukatili wa watoto majumbani, kulinda haki za watoto, kuibua vipaji ikiwemo uchoraji na uigizaji ili kuvitumia katika kufikisha elimu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto". Imefafanua sehemu ya risala ya klabu za wanafunzi mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya msingi Nyamagana na Nyakurunduma sekondari, iliyosomwa na Neema Christopher. 
Shule ya msingi Nyamagana wakifurahia ushindi wao ambapo igizo wamepata asilimia 93 dhidi ya 92 za Nyamagana sekondari, Shairi Nyamagana wamepata asilimia 74 dhidi ya 85 za Nyakurunduma huku Ngonjera Nyamagana wakipata asilimia 91 dhidi ya 77 za Nyakurunduma. Ushindi wa jumla, shule ya Msingi Nyamagana wamepata asilimia 86 dhidi ya 85 za Nyakurunduma sekondari.
Mabalozi kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma wakipokea kombe baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo
Pia mabalozi wote wamepatiwa vyeti kwa kujitoa kuwa mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Mabalozi wakipokea vyeti
Mabalozi kutoka shule ya msingi Nyamagana wakionesha makali yao katika ngonjera na mashairi
Mabalozi kutoka Nyakurunduma sekondari wakighani mashairi na ngonjera
Afisa Ustawi wa jamii Jijini Mwanza, Davis Justine (katikari) akitoa matokeo ya mashindano hayo kwa niaba ya majaji wengine
Mkurugenzi wa WoteSawa, Angel Benedicto, akizungumza wakati wa mashindano hayo
Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha, akizungumza kwenye mashindano hayo
Taasisi ya WoteSawa imechora mchhoro huu katika shule ya Msingi Nyamagana, ukiwa na jumbe mbalimbali ikiwemo "Mpe elimu siyo kumuajiri kazi za nyumbani" ikiwa ni mwendelezo wa kufikisha elimu juu ya mapambano dhidi ya ukatili wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani.
Mgeni rasmi akizungumza jambo kwenye mashindano hayo na kuzindua pia mchoro huo
Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya sekondari Nyakunduruma Jijini Mwanza wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya shule ya msingi Nyamagana Jijini Mwanza wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
Mabalozi wote wakiwa kwenye picha ya pamoja

INUKA KUTOA ELIMU ZA MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA KWA MIKOA MINNE NCHINI

March 11, 2017
Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania (INUKA) inatarajiwa kutumia kiasi cha milioni 20 kwa ajili ya kutoa elimu kwenye mikoa minne iliyopo hapa nchini lengo kubwa kuielimisha jamii juu ya madhara ya dawa ya kulevya ili waweze kubadilika na kuachana nayo.

Hatua ya Taasisi hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya kuhakikisha vita ya dawa za kulevya hapa nchini inakwisha ili vijana waweze kuepukana na matumizi hayo ambayo yanaathari kubwa kwa maendeleo ya uchumi wao na jamii
zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa  na Mratibu wa Inuka Kanda ya Ziwa, Gaudance Msuya wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani hapa ambapo alisema elimu hiyo itakuwa chachu ya kuibadili jamii kuachana na matumizi hayo ambayo yamekuwa na athari kubwa.

Alisema licha ya hivyo lakini pia itasaidia kuipa jamii uelewa ambao utawawezesha kupiga vita matumizi ya madawa hayo ambayo yameathiri nguvu kuvwa ya vijana kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aliitaja mikoa ambayo inatarajiwa kunufaika na elimu hiyo kuwa ni Tanga, Iringa, Ruvuma na Lindi ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha vijana wanaondokana na matumizi ya dawa hizo.

“Tatizo la dawa kuvelya limekuwa kubwa sana kwenye jamii hivyo sisi kama Taasisi tumeona ni bora tuunge mkono kulitokomeza kwa kutoa elimu kwa jamii na watumishi wa serikali “Alisema.

Aidha alisema lengo kubwa ni kuhakikisha jamii inaelimisha kuhusu madhara ya matumizi hayo ili waweze kuachana nayo kama sio kwisha ili vijana waweze kuepuka kuyatumia.

“Lakini pia tunaomba makatibu tawala wa mikoa na wilaya tunapofika tushirikiane kwa pamoja kwenye vita hii kubwa ambayo inaathiri nguvu kazi za vijana wengi “Alisema.

 Hata hivyo alisema kupitia elimu hiyo inaweza kuwasaidia vijana kubadilika ikiwemo kuachana nayo pia kutumia muda mwingi kujikita kwenye shughuli za kimaendeleo badala ya kushinda vijiweni.

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AFUNGUA RASMI MKUTANO WA KAMATI KUU DODOMA

March 11, 2017
 Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akipokewa na Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana alipowasili Makao Makuu ya CCM, mjiniDodoma leo kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Maguguli akiwana Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kushoto) kwenye chumba cha mapumziko kabla ya kuanza kikaocha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulraman Kinana akishauriana jambo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kulia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idi
 Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiwa na viongozi wengine wa Chama wakati wakisubiri kuingia ukumbini kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM,leo mjini Dodoma
 Baadhi ya Maofisa wa Chama wakiwa ukumbini wakati wa kikao hicho
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira na William Lukuvi wakipitia makabrasha kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo
 Wajumbe wa Sekretarieti wakiwa ukumbi kusubiri kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
 Wajumbe wa Kamati Kuu Jason Rweikiza (kushoto) na Alhaji Adan Kimbisa wakibadlishana mawazokabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kuanza mjini Dodoma leo
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Hussein Mwinyi na Jerry Silaa, wakibadilishana ma wazokabla ya kikao hicho kuanza
 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Alhaj Abdallah Bulembo na Shamsi Vuai Nahodha wakibadilishana mawazo kabla ya kikao hicho kuanza leo mjini Dodoma. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini
 Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara PhilipMangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulidikabla ya kuanza kikao hicho. Katikati ni Spika wa Bunge Job Ndugai 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa utangulizi kumpa nafasi Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk JohnMagufulikufungua na kuongoza kikaocha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kushoto ni Dk. Shein na Kulia ni Mangula.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Seif Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai 
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Dk John Magufuli akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli na viongozi wenzake wa meza kuu, wakifurahia jambo wakati wa kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

“RC SHIGELLA AITAKA TEMESA KUMPATIA ORODHA YA WADAI SUGU”

March 11, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisisitiza jambo wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara (Road Boad) ambapo alisisitiza umuhimu wa wabunge wa mkoa wa Tanga kutumia nafasi zao kusaidia kuelezea changamoto zinazozikabili barabara zetu ili zipewe msukumo
Meneja wakala wa barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Alfred Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu

Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina akitolea ufafunzi baada ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa kikao hicho

 Wajumbe wakifuatilia hoja zilizoainishwa kwenye makabrasa kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda Mtondoo
 Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia jambo kwenye kabrasha lake wakati kikao hicho kikiendelea
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji katika wakati wa kikao hicho
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto,Kazimbaya Makwega akiperuzi kabrasa kwenye kikao hicho
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Musa Mbaruku na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema) Yosepher Komba
 Mbunge wa Jimbo la Mkinga(CCM) Dustan Kitandula kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Rashid Gembe
 Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini kikao hicho
 kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akifuatilia kikao hicho
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatilia kwa umakini kikao hicho
 Mwandishi Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji la TBC Mkoani Tanga,Bertha Mwambela akiandaa taarifa za kikao hicho
WAKALA wa Ufundi na Umeme Mkoani Tanga (Temesa) wameagizwa kuwasilisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu wa taasisi mbalimbali za serikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwemo kuharakisha ulipwaji wake.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani hapa ambapo alisema wao kama serikali ya mkoa hawapo tayari kuona wakala huyo akishindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na juhudi zao kurudishwa nyuma kimaendeleo.

Katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio makubwa yenye tija alimtaka Meneja wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMEMSA) Mkoa Tanga, Mhandisi Margareth Gina kumpelekea idadi ya wadaiwa sugu na taasisi hiyo ili kuweza kuangalia namna ya kuweza kupata malipo yao.

Hatua hiyo inafuatia taarifa ya Meneja wa Temesa Mkoa kuonyesha zipo taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa fedha nyingi bila kuwepo jitihada zozote za ulipwaji wa madeni hayo huku tasisi hizo zikiendelea kupatiwa huduma na taasisi hiyo ya Serikali.

Alisema ifike wakati kwa taasisi zote za umma zinazopata huduma kutoka kwa wakala huo wa ufundi na umeme wahakikishe wanalipa madeni yao kwa wakati kabla majina hayo ya wadaiwa hao sugu hayaja wekwa hadharani.

Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa majina ya wadaiwa wote sugu
yaorodhoshwe bila ya kuoneana aibu na taasisi za Serikali ambazo inadaiwa kuwa ndio vinara wakubwa wa kudaiwa ili kuweza kuangalia namna ya kupunguza madeni hayo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa wakala huyo.

Awali akizungumza katika kikao hicho,Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina alisema temesa imekuwa ikitoa huduma bora kwa taasisi za Serikali kutokana na kuwepo na wataalamu wengi waliobobea katika fani mbalimbali huku wakishindwa kufikia malengo kutokana na kutolipwa
na wateja wao.

Mhandisi Gina alisema ipo orodha kubwa ya majina ya wadaiwa sugu ambapo ipo haja ya kuyaweka hadharani kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza na kufanya hivyo kunaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kuweza na kukusanya madeni hayo.

“Zipo taasisi za serikali zanadaiwa hadi milioni 100 na orodha yote ya wadaiwa sugu ninayo na naweza kuyataja ila naona itakuwa kufedheheshana tu mbele ya kikao hiki”Alisema

Aidha alisema taasisi za Serikali kwa asilimia kubwa zimekuwa miongoni mwa wateja wanaoikwamisha temesa kuendelea na ufanisi wa shughuli zake jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzina wa haraka kukomesha tabia hiyo iliyozoeleka.

Kwa upande wake, katibu Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Saidi alisema hakuna sababu ya kuficha wanaodaiwa lazima waorodheshwe na walipe madeni yao kwa wakati ili temesa iweze kuendelea na majukumu yake.