UPDATES MSIBA WA MAREHEMU BALOZI CISCO MTIRO, MAZISHI KUFANYIKA JUMATANO

June 05, 2017

Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

Jioni hii Bw. Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.
Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.

Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA
Waziri Mbarawa apokea Kivuko cha MV Kazi

Waziri Mbarawa apokea Kivuko cha MV Kazi

June 05, 2017
RAW1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Bw. Major Songoro (kulia)  wakati wa makabidhiano ya Kivuko cha MV. KAZI mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mtendaji Mkuu toka Wakala wa Ufundi na Umeme  (TEMESA) Dkt. Mussa  Mgwatu.
RAW2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na baadhi ya wananchi waliopanda Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa kwa Serikali toka kwa  Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
RAW3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliana Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akizungumza na mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
RAW4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akifurahia jambo na  mmoja  ya mkazi wa Kigamboni wakati wa kukabidhiwa Kivuko cha MV. KAZI kwa Serikali toka kwa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga kivuko hicho.
RAW5
Baadhi ya wananchi wakiteremka katika Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa Serikali mapema hii leo Magogoni jijini Dar es Salaam toka Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho.
………………………………………………………..
Eliphace Marwa -Maelezo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi kutoka kwa Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko hicho mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
Akizungumza na wananchi, Prof Mbarawa alisema lengo la Serikali kuongeza Kivuko hicho  ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni.
“Uwepo wa vivuko vitatu kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi na ikitokea Kivuko kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utaratibu wa kawaida”.Alisema Prof Mbarawa.
Ameongeza kuwa ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais John Magufuli  Wizara yake itaendelea kuboresha huduma za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Lindi , Kivuko cha Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani Mwanza.
Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa Mgwatu alisema Kivuko cha MV Kazi kimejengwa kulingana na viwango vinavyotakiwa Kimataifa na ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa ubebaji wa abiria na magari.
 Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170.
Kivuko hicho kimekabidhiwa leo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vitatu

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA TARIME

June 05, 2017
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua kiwanda cha kutengenezea Chaki cha Arwa kilichopo Tarime.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna chaki zinavyotengenezwa kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Arwa Bw. Tobias Raya mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho kilichopo Tarime mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Bisarwi kata ya Manga, Tarime  mkoani Mara.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 

SERIKALI YAIPATIA TADB RUZUKU YA SHILINGI BILIONI 209.5 KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO

June 05, 2017


td1
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisaini mkataba wa kuipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) fedha za kuiongezea mtaji kiasi cha shilingi bilioni 209.5. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
td2
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Eligius Mwankenja (kushoto), na Mchumi kutoka Wizara hiyo  Bw. Said Nyenge (kulia) wakiwaelekeza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga, maeneo maalumu ya kutiwa saini kwenye Mkataba wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni utakaoiwezesha Benki hiyo kutoa mikopo ya muda wa kati na mrefu kwa riba nafuu kwa wakulima wadogo wadogo, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
td3
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akibadilishana mkataba na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga mara baana ya kusainiwa mkataba wa kuiongezea mtaji Benki hiyo wenye thamani ya Sh. Bilioni 209.5 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/2021, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
td4
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu wakionesha mkataba waliokwisha usaini kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
td5
Wajumbe waliohudhuria hafla ya utiaji saini mkataba wa kuiongezea mtaji Benki ya Kilimo wenye lengo la kuunganisha maboresho ya sekta ya kilimo na mpango wa mageuzi ya viwanda wenye thamani ya Sh. 209.5 bilioni, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
td6
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akitoa ufafanuzi wa maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawamo pichani) na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam
td7
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
td8
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
td9
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania-TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akiongea na waandishi wa habari pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo (hawamo pichani).
td10
Wajumbe wa Bodi wakifuatilia kwa makini zoezi la utiaji saini mkataba wa Serikali kuipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) shilingi bilioni 209.5. kwa ajili ya kuiongezea mtaji. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TADB Bw. William Mhoja, Mkurugenzi wa Fedha na TEHAMA – TADB Bw. Severin Ndaskoi, Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha Bw. Albert Ngusaru, Mkuu wa Idara ya Utimilifu-TADB, Bw. Adam Kamanda, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Bi, Joyce Maduhu, na Mkurugenzi wa Mikopo wa TSDB, Bw. Augustino Matutu.
…………………………………………………………………………
Benny Mwaipaja, WFM- Dar es Salaam
SERIKALI imeipatia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), shilingi 209.5 bilioni kwa ajili ya kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifugo hapa nchini, leo, Jijini Dar es salaam.
Akiongea kwa niaba ya Serikali wakati wa tukio la utiaji saini mkataba wa makabidhiano ya fedha hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ambacho ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ni sehemu ya shilingi 800 bilioni ambazo Serikali inatarajia kuipatia Benki hiyo ili iweze kukuza mtaji wake.
“Ninaishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kwa kuipatia Serikali mkopo wa Dola za Marekani 93.5 milioni ambazo ni sawa na kiasi hicho cha fedha cha Sh. 209.5 bilioni kwa ajili ya kuiongezea mtaji TADB ili iweze kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu” alisema Dkt. Kazungu.
Alisema kuwa fedha hizo zitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya kilimo na mifugo ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo ili sekta hiyo iweze kuchangia zaidi katika ukuaji wa pato la Taifa kuliko ilivyo sasa.
“Mwaka jana kilimo ambacho kinategemewa na idadi kubwa ya Watanzania kilichangia wastani wa asilimia 29.1 ya Pato la Taifa lakini tunataka kupitia Benki hiyo Sekta ya kilimo iiwezeshe nchi kukua kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 7 hadi 10 katika kipindi kifupi kijacho” aliongeza Dkt. Kazungu.
Akiongea baada ya kutia saini makubaliano ya kupokea fedha hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Bw. Francis Assenga, ameishukuru Serikali kwa kuiongezea Benki yake mtaji utakaotumika kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ufugaji nyuki.
Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kitaiwezesha Benki hiyo ambayo imekwisha wafikia wakulima zaidi ya 3,700 hapa nchini, kuanza kutoa mikopo ya muda mrefu kwa wakulima wadogo na wa kati ili kuinua Sekta hiyo kwa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao yatokanayo na kilimo na mifugo.
Ameihakikishia Serikali kwamba Benki yake itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa matunda ya fedha hizo yanaonekana na kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Ras Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwakwamua wananchi wake katika lindi la umasikini.
“Riba za Mikopo ya Benki yetu ziko chini ikilinganishwa na Benki nyingine ambapo sisi tunatoza asilimia 8 hadi 12 kwa wakulima wadogo na asilimia 15 kwa wakulima wa kati wenye viwanda wakati viwango vya riba katika soko ni asilimia 18 na wakati mwingine vinafika hadi asilimia 40.” alisema Bw. Assenga wakati akijibu maswali ya wanahabari.

MZEE NDESAMBURO KUAGWA LEO UWANJA WA MAJENGO,MKOANI KILIMANJARO.

June 05, 2017
Sanduku lenye Mwili wa Marehemu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo,ukiandaliwa tayari kwa kuagwa katika uwanja wa Majengo,mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mapema leo mchana.
  Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwapungia mkono wananchi waliofika kwenye uwanja  huo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwasili atika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili wa  aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo. 
Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na dini wakiwa wamesimama mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Marehemu Phillemon Ndesamburo kuwasili uwanjani hapo



 Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa kwenye uzuni mara baada ya mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo ulipokuwa unaelekea katika viwanja vya Majengo kwa ajili ya kuagwa mwili huo. 

WAJUMBE WA BARAZA LAAWAKILISHI WAELIMISHWA KUHUSU HOMA YA INI

June 05, 2017
 Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kushajihisha wajumbe hao kuhusu kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid ambae alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo akiufungua rasmi katika Hoteli ya Ocean View (kulia) Mnadhimu wa Baraza  Ali Salim Haji na (kushoto) Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia ufunguzi wa mkutano wa kuwashahishaji kuhusu Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Mratibu wa huduma za homa ya Ini Zanzibar Dkt. Sania Shafi akiwaelezea Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hali halisi juu ya homa ya Ini katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Rashid Makame Shamsi akitoa mchango katika mkutano huo.
Meneja Kitengo Shirikishi Kifua kikuu, Ukimwi na homa ya Ini Dkt. Farhat Ahmed akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika mkutano wa kuwashajihisha kuhusu maradhi hayo katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.
MATUKIO YA PICHA KATIKA MSIBA WA MAREHEMU MZEE PHILEMON NDESAMBURO MJINI MOSHI KILIMANJARO

MATUKIO YA PICHA KATIKA MSIBA WA MAREHEMU MZEE PHILEMON NDESAMBURO MJINI MOSHI KILIMANJARO

June 05, 2017
NDESA1
Matukio mbalimbali kutoka Moshi mkoani  Kilimanjaro kwenye msiba wa Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo aliyefariki hivi karibuni mkoani humo, Marehemu Ndesamburo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa  Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini utaagwa kwenye uwanja wa Majengo kuanzia leo na kesho na kisha  kuzikwa mkoani humo haya ni matukio kadhaa ya picha za matukio yanayoendelea katika msiba huo.
NDESA2
Baadhi ya wa vijana waendesha bodaboda wakijiandaa kwa ajili ya maandamano maalum wakati mwili wa marehemu utakapokuwa akipelekwa kwenye uwanja wa Majengo.
NDESA3
Gari Maalum litakalochukuwa mwili wake.
NDESA4
Eneo la Uwanja wa Majengo ambalo ndipo shughuli za kuaga mwili zitafanyika likiwa limepambwa tayari kwa shughuli hizo.

DC MJEMA AWAONGOZA WAKAZI WA JIJI LA DAR SIKU MAZINGIRA

June 05, 2017
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akizungumza katika  maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani,yaliyofanyika viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es Salaam leo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akikabidhi cheti kwa Mwandishi wa ITV , Benjamini Mzinga kuwa mmoja wa wadau makini katika utunzaji wa Mazingira
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza katika mkutano wa kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja wa Dar es Salaam
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  akikabidhi cheti cha kuwa mtunzaji bora wa mazingira katika Manispaa ya Ilala kwa Mwanahabari mkongwe nchini kutoka shirika la utangazaji TBC, Selemani Mkufya
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjemai  kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Osterbay Zefrin Lubuva kuwa  mshindi wa Mazingira
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam na Watoto wa jeshila wokovu
Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akikagua mabanda ya taasisi mbalimbali