URA USO KWA USO NA COASTAL UNION JUMATANO IJAYO

July 20, 2013
(Kikosi cha URA ya Uganda ambacho Jumatano kitacheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani)

Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kucheza mechi ya Kirafiki ya Kimataifa na Mabingwa wa soka Uganda URA Jumatano wiki ijayo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mkoani Tanga.

Athibtisha taarifa hizo,Mwenyekiti wa timu hiyo,Hemed Aurora "Mpiganaji"alisema ni kweli mechi hiyo ipo na kinachofanyika hivi sasa ni kufanya mazungumzo ya mwisho na uongozi wa timu hiyo ili iweze kutua mkoani hapa kwa ajili ya mchezo huo.




(Kikosi cha Coastal Union ya Tanga ambacho kitapambana na URA Jumatano wiki hii kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga)

Aurora alisema baada ya kumalizika mechi hiyo kikosi cha timu hiyo kitaondoka mkoani Tanga kuelekea Mombasa nchini Kenya kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Bandari lengo likiwa ni kukiimarisha kikosi hicho kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi kuu.

Aliongeza kuwa licha ya kucheza na Bandari lakini pia wapo kwenye mikakati ya kuzungumza na uongozi wa Yanga ili kuweza kucheza nao mechi ya majaribio siku ya Iddi Pili kwenye dimba hilo la Mkwakwani ambapo alisema anaamini mazungumzo hayo yatafanikiwa.

Mwenyekiti huyo lengo la timu hiyo msimu ujao ni kuhakikisha wanafanya vizuri ili kuweza kurudisha heshima yao ya mwaka 1988 ya kuchukua ubingwa wa Ligi hiyo na kueleza hilo linawezekana kutokana na mshikamano uliopo baina ya wapenzi,wanachama na uongozi wao.

Akizungumzia maandalizi ya mechi hiyo ,Meneja wa uwanja wa CCM Mkwakwani,Mbwana Msumari alisema kwa mara ya mwisho uwanja huo kulichezwa mechi ya kimataifa mwaka 1988 kati ya African Sports na timu kutoka nchini Swithland wakati huo African Sports ni mabingwa wa Kombe la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Msumari alisema na mwaka huo huo ,Coastal Union wakacheza na Cost De Solver ya Msumbuji ambayo ilikuwa ikishiriki mashindano ya Klabu bingwa kwa hiyo anaamini mechi hiyo itakuwa na mvuta wa aina yake kutokana na historia ya timu hiyo.

Mwisho.

COASTAL UNION WAENDELEZA DOZI YA MAZOEZI KUJIANDAA NA MSIMU MPYA.

July 20, 2013

Na Mwandishi Wetu,Tanga.
TIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”leo imeendelea na mazoezi yake katika uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa ikijiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara ambao utaanza mwezi ujao.

Mazoezi hayo ambayo yalianza majira ya saa nane mchana yalikuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi na mshabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa ambao mara nyingi hufuatilia mazoezi hayo kutoka pande zote za mkoa huu.
(KOCHA Mkuu wa Coastal Union Hemed Morroco kushoto akiteta jambo na Pius Kisambae huku Seleman Kassim Selembe akishuhudia)

Wachezaji ambao walionekana kuwakonga nyoyo mashabiki wa soka hapa wapenzi ni Haruna Moshi “Boban”,Christian Odula wa Nigeria,Jerry Santos,na wachezaji wengine chipukizi waliowasili kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na Blog hii mara baada ya kumalizika mazoezi hayo,Kocha Mkuu wa timu hiyo,Hemed Morroco alisema maandalizi ya kuelekea msimu mpya yanaendelea vizuri kwani wachezaji wana hari na nguvu mpya.

Morroco alisema mechi ya kwanza ambayo atatumia kuangalia kikosi hicho ni kati yao na URA ya Uganda mchezo unaotarajiwa kucheza Jumatano wiki hii kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani hapa.
(Mashabiki wakifuatilia mazoezi ya timu hiyo leo jioni uwanja wa Mkwakwani)

Alisema watakapomaliza mechi hiyo wataelekea Mombasa Kenya kucheza na Bandari lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho ambacho kimepania msimu ujao kuchukua kombe la Ligi kuu hapa nchini.

Mwisho.
Mhina apinga kipengele Ibara ya 117 cha Katiba.

Mhina apinga kipengele Ibara ya 117 cha Katiba.

July 20, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
ALIYEKUWA Mgombea Ubunge Jimbo la Muheza katika uchaguzi mkuu 2010 kupitia Chama cha United Demokratic Party (UDP),Mhina Peter amepinga kipengele cha ibara ya 117 cha kwanza katika rasimu ya katiba kinachoeleza sifa za mgombea ubunge,kuwa awe na umri usiopungua miaka 25 kwa sababu suala hilo linawanyima fuksa wa watanzania.

Mhina ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama  hicho Mkoa wa Tanga alisema yeye alisema mtu anaweza kugombea ubunge akiwa na miaka kuanzia 18 kwa sababu ndio umri wa kijana unapokuwa ukianzia hivyo wataweza kuwapa maendeleo wananchi wao wanaowaongoza.

Alisema suala jengine ambalo anapingana nalo kwenye kipengele 1b katika rasimu ya katiba kinachosema mtu anayetaka kugombea ubunge awe anajua kuongeza na kuandika kiswahili na kingereza akiwa tayari ameshamaliza kidato cha nne.

Aidha alisema kuna watu ambao wanafika darasa la nne na kwa sababu wanauelewa mzuri wa kuongeza wapewe nafasi katika kugombea nafasi kama hiyo ili kuweza kuwatumikia wananchi wake bila kuwepo kwa vikazo hivyo.

Alisema hata hivyo misingi ya hilo baraza lenyewe la katiba haikuzingatia elimu kwa sababu wapo watu walioingia kwenye mabaraza hayo hawakusoma kabisa zaidi ya kuwa na uelewa wa mkubwa wa kutafakari mambo.

  "Tunaweza kuzingatia misingi ya elimu kwa madaktari,wahandisi lakini kwenye suala la ubunge taaluma yake kubwa ni utendaji tu na sio vyenginevyo "Alisema Mhina.

RAMBIRAMBI MSIBA WA BERT TRAUTMANN

July 20, 2013


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kocha wa zamani wa Taifa Stars, Bert Trautmann (89) kilichotokea jana (Julai 19 mwaka huu) nchini Hispania.

Kabla ya kuwa kocha, Trautmann aliyezaliwa 1923 mjini Bremen, Ujerumani alikuwa kipa wa timu ya Manchester City ya Uingereza ambapo anakumbukwa kwa kucheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Birmingham City akiwa amevunjika shingo.

Manchester City ilishinda fainali hiyo iliyochezwa mwaka 1956 mabao 3-1. Trautmann ambaye aligongana na mshambuliaji wa Birmingham, Peter Murphy zikiwa zimesalia dakika 17 mechi hiyo kumalizika aligundua kuwa amevunjika shingo siku tatu baadaye.

Mbali ya kuwa kocha wa Taifa Stars mwanzoni mwa miaka ya 60, Trautmann pia alikuwa mkufunzi wa makocha ambapo hapa nchini aliendesha kozi mbalimbali zilizotoa makocha waliokuja kutamba baadaye.

TFF itamkumbuka Trautmann kwa mchango wake aliotoa katika maendeleo ya mpira wa miguu nchini ikiwemo wazo lake la kuanzishwa kwa Ligi Kuu (Daraja la Kwanza) ambalo alilitekeleza katikati ya miaka ya 60.

Msiba huo ni pigo kwa familia ya Trautmann, TFF na familia ya mpira wa miguu kwa ujumla nchini kutokana na mchango alioutoa kwa Tanzania hasa wakati akiwa kocha na mkufunzi wa makocha.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Trautmann, Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DFB), Chama cha Mpira wa Miguu cha Uingereza (FA) na kuwataka kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha msiba huo mzito.

Mungu aiweke roho ya marehemu Bert Trautmann mahali pema peponi. Amina
 

Kampuni ya Kokoliko Disgner itaendelea kuwabunia mavazi wabunifu nchini.

July 20, 2013

(Mmiliki wa Kampuni ya Kokoliko Disgner Mama Sophia akiwa katika pozi)

NA MWANDISHI WETU,TANGA.

Kampuni ya disgner ya Kokoliko ilinayomilikiwa na Mama Sophia Production imeelezea malengo yake ya kuendelea kuwabunia mavazi wabunifu mbalimbali hapa nchini lengo likiwa ni kutangaza utamaduni wetu wa Africa.

Sophia ambaye alibuni vazi la washiriki walioingia kwenye fainali za Miss Utalii mwaka 2013 ambalo mwaka huu lilifanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani kuanzia hatua ya mwanzo mpaka mwisho.

Alisema baada ya shindano hilo kumalizika ukumbini miss Utalii namba nne ambaye alipata nafasi ya kwenda kushiriki Mashindano ya Miss Kossovo na kufanikiwa kushika nafasi ya nne na baadaye kurejea mkoani hapa na kupokewa kushujaa na umati wa wakazi wa Tanga wakiongozwa na mama Sophia Production.

Baada ya mrembo huyo kutua mkoani hapa alifanyiwa sherehe katika Hotel ya CBA iliyopo Raskazone jijini Tanga ambayo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ambayo ilianza saa tatu usiku na usiku ambapo mrembo huyo alipata nafasi ya kuwashukuru wakazi wa Tanga akiwemo Mama Sophia Production kwa kumsapoti.



Aidha Mama Sophia anasema filamu yake mpya ya Tanga Line ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni anaimani itafanya vizuri  kwenye tasnia ambayo imejaa maadili ya kipwani na kimwambao iliyo na maadili ya kimwambao.

Filamu hiyo imeandaliwa na Kampuni maalumu ya filamu hapa nchini na kampuni ya Sophia Production na endapo kama unataka maelezo zaidi kuhusu filamu hiyo wasiliana nao 0713510530.

Mwisho.