BENKI YA NBC YATOA MSAADA KWA WALEMAVU WA NGOZI

October 12, 2015


 Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mussa Jallow (wa tatu kushoto), akikabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha, Pwani jana. Wengine ni baadhi ya wanachama wa TAS na maofisa wa NBC.
 Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa tatu kushoto) akikabidhi pikipiki kwa mmoja wawakilishi wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha, Pwani jana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Mwenyekiti wa TAS Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani.
  Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara( NBC) Alina Maria Kimaryo (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanachama wa Chama cha Albino (TAS) Mkoa wa Pwani  katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha mkoani Pwani jana.
 Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya NBC, Andrew Lyimo (wa pili kulia), akikabidhi baadhi ya misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao ni wanachama wa Chama cha Albino Tanzania (TAS) katika Mkoa wa Pwani. Katika hafla hiyo iliyofanyika Kibaha jana, NBC ilikabidhi msaada wa pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta maalumu ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Wanaoshuhudia ni baadhi ya wanachama wa TAS na maofisa wa NBC.
 Meneja Mahusiano ya Biashara wa NBC, Emanuel Mseti (wa tatu Kushoto) akimkabidhi mlemavu wa ngozi, Mwalimu Matimbwa, boksi lenye miwani katika hafla ambayo NBC ilikabidhi pikipiki tatu, kofia, miwani na mafuta ya ngozi ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuisaidia jamii katika kukuza uchumi na pia kujali afya zao. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Kibaha mkoani Pwani jana. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa wa NBC na wanachama wa TAS.
 Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo (katikati), akizungumza na mmoja wa walewavu wa ngozi wakati NBC ikikabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu wa wanachama wa Chama cha wenye ulemavu wa ngozi (albino) wa Mkoani wa Pwani. Pamoja na misaada mingine NBC ilikabidhi mafuta maalumu ya ngozi, kofia na miwani vitu vinavyowasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya zinazotokana na hali ya hewa.

MAGUFULI AFANYA KAMPENI ZAKE WILAYA YA NACHINGWEA,RUANGWA,MTAMA NA LINDI MJINI,AMFAGILIA DIAMOND

October 12, 2015


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kweny mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi,
Katika mkutano huo wa hadhara Dkt.John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali atakayounda baada ya kuchaguliwa na Watanzania Oktoba 25 mwaka huu, itahakikisha inawatumikia huku akiweka wazi kuwa yeye  hakuwa na mchezo kwani dhamira yake ni kutatua shida za wananchi kwa spidi kubwa.

Amesema anatambua shida ambazo watanzania zinawakabili na hivyo uamuzi wake wa kuomba nafasi hiyo ni kuhakikisha anakabiliana nazo huku akisisitiza serikali yake,Mawaziri atakaoteua wajiandae kufanya kazi na atakayeona hawezi ni bora akajiweka pembeni mapema kabla ya kuapishwa ama akakataa uteuzi.
Dkt Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya wali0jinyakulia tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best Inspirational Song of The Year.

Wakati huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.

Dkt Magufuli amefanya kampeni zake katika jimbo la Nachingwea,Ruangwa,jimbo la Mtama na Lindi mjini huku akisimamishwa na wanachi mara kadhaa kila alikokuwa anapita.
Sehemu ya umati wa kazi wa mji wa Lindi Mjini wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura ya kuwania nafasi ya Urais.PICHA NA MICHUZI JR-LINDI
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akimuombea kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi jioni ya leo.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia mkutano wa kampeni a Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Lindi.

Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimuombea kura kwa wananchi Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtama,Ndugu Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mjumbea wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Mh Bernad Membe akiwahutubia wananchi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi mpili pili,mkoani Lindi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majaliwa,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi mara bada ya kumkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM.
Mmoja wa wafuasi wa chama cha CHADEMA akizungumza mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Ruangwa mara baada ya kurejesha kadi ya chama chake kwa Mgombea Urasi wa CCM Dkt Magufuli,ambapo wanachama wapatao 150 wa vyama mbalimbali pinzani walirejsha kadi zao.
Wananchi wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jimbo la Mtama,mkoani Lindi kwenye mkutano wa kampeni
Wananchi wa jimbo la Mtama wakifuatilia sera za mgombea wa Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema loe mchana kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa jimbo la Mtama wakifuatila mkutano kampeni wa mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Wananchi wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtamba,Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo wakati wa kumuombea kura mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,ili aibuke mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Wakazi wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtama,Ndugu Nape Nnauye wakifuatilia jambo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingin Mpili pili,Lindi mjini.
Baadhi ya Wananchi wa Mjini Lindi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,Mzee Ali Mtoba akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,ahutubie wananchi na kumwaga sera zake ikiwemo na kuwaomba kura wakazi wa Lindi,za kuwania nafasi ya Urais katika uwamu ya tano,kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoka 25 mwaka huu.
Wakazi wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,
Wakazi wa mji wa Lindi mjini wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,

Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Wananchi waliokuwa wemefunga barabara wakati akitokea wilaya ya Nachingwea kuelekea wilaya ya Ruangwa kuwahuubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majariwa,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi.
MSAJILI -AWAASA viongozi wa vyama vya siasa KUHUSU AMANI

MSAJILI -AWAASA viongozi wa vyama vya siasa KUHUSU AMANI

October 12, 2015

2
Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akizungumza na waandishi wa habari  Jumatatu Oktoba 12, 2015  kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
Picha zote na Magreth Kinabo-Maelezo.
3
Msanii Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
4
Mwanamziki wa nyimbo za injili nchini, Christina Shusho akizungumza na waandishi wa habari  kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam kuhusiana na masuala ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
6
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
………………………………………………………………….
Na Magreth Kinabo-maelezo
Ofisi ya Msajili wa Vyama  Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa  vyama  vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa amani hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada  ya uchaguzi huo.
Hayo yamesemwa  leo na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam.
“Dhamana  ya nchi iko mikononi mwenu,ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa la Tanzania ama  utaliingiza taifa katika vurugu na mfarakano,” alisema Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi alisema katika kipindi cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii yakiwemo baadhi ya makundi ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama siasa.
“Makundi hayo yanadiriki kutoa maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana, hata kujeruhi makundi mengine, ambayo siyo ya upande wao. Hali  iiachwe mara moja ili kuiweka nchi yetu Tanzania  katika hali ya amani na kuiepusha kuingia kwenye vurugu, mfarakano na machafuko yasiyokuwa na  ulazima.
“Dumisheni amani na kamwe  tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na uvunjifu wa amani, kumbukeni  kuna maisha baada ya uchaguzi na amani ya nchi yetu ni fahari  yetu sote,alisema  Mutungi.
Aliongeza ni vyema Watanzania, wakatambua kwamba utofauti wa itikadiya vyama ndio ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na kufanya siasa za kiustaarabu.Hivyo  kutovumiliana kwa utofauti wetu wa itikadi za kisiasa kunaweza kulata madhara makubwa kwa jamii itakatopelekea idadi kubwa ya Watanzania kupata athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi,njaa na maradhi.  
Aidha ofisi hiyo imetoa rai kwa waandishi wa habari watumie kalamu zao vysema kuhubiri amani  na kuepuka kuandika habari za uchochezi, bali wawasaidie wananchi kupata taarifa sahihi zitakazowasaidia kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi wao.
Kwa upande wao mabalozi wa amani, ambao ni Mrisho Mpoto na Christina Shusho walisema kwa nyakati tofauti kuwa wamejitolea kuhubiri amani kupitia fani yao  ili nchi yetu iendelee kuwa na amani.
Akizungumzia suala hilo, Mpoto aliwapa changamoto waandishi wa habari wajiulize kuwa wana mchango  gani  katika nchi yao ili kuhakikisha inakuwa na amani. Hivyo wanapoandika habari yoyote wakumbuke  kwamba kuna watoto, yatima, walemavu na wajane, isije ikawa ni chanzo cha kuvuruga  amani.
Naye Shusho alisema kwamba yeye si mfuasi wa chama chochote,bali balozi wa kuhubiri amani.
Ofisi hiyo imetoa kauli hiyo, kwa kuwa ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba.
Siku Nane zatolewa kuhakiki taarifa kituo cha kupigia kura

Siku Nane zatolewa kuhakiki taarifa kituo cha kupigia kura

October 12, 2015

index 
Na Anitha Jonas-Maelezo Dar es salaam
………………………………………………….
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  yawaasa  wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika Oktoba 12, 2015  jijini Dar es Salaam,
Jaji Lubuva amesema kuwa lengo la mkutano huo ni  kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.
“Tume imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura  anapata haki ya kupiga  kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu wenye ulemavu  wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume katika majukwaa  wakati wa kampeni  pia amewasaa wanasiasa hao  kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.
“Katika kuelekea uchaguzi  Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo Tanzania Bara ni vituo 63,525 na Zanzibar  ni vituo 1,580 kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema Bw.Ramadhan.
Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.
KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI , VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEA MABANDA MAONYESHO YA WIKI YA VIJANA MJINI DODOMA.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI , VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO ATEMBELEA MABANDA MAONYESHO YA WIKI YA VIJANA MJINI DODOMA.

October 12, 2015

1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (katikati) akiangalia baadhi ya picha mbalimbali wakati alipotembelea banda la Mwalimu Nyerere Foundation 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma.
2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (kushoto) akiangalia moja ya vitabu wakati alipotembelea banda la Mwalimu Nyerere Foundation 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma.
3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga akiangalia mikanda ya DVD zinazomuhusu Mwalimu Nyerere wakati alipotembelea banda la Mwalimu Nyerere Foundation 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma.
4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akiangalia vitabu wakati alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma. Kushoto ni Maafisa Vijana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
5
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akiangalia baadhi ya kazi za sanaa za ufundi wakati alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma. Kushoto ni Afisa Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo, Bwana Mussa Nyoni.
6
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akiangalia baadhi ya kazi zinazofanywa na Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, wakati alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Bi. Joyce Fissoo.
7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga (mwenye batiki nyekundu) akipewa maelekezo ya namna ya kutumia Kamera ya kisasa ya kutengenezea filamu wakati alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni  na Michezo 12 Oktoba, 2015 katika Maonyesho ya Wiki ya Vijana na Kilelecha Mbio za Mwenge mjini Dodoma.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA
Uhusiano wa Tanzania na China wazidi kuimarika

Uhusiano wa Tanzania na China wazidi kuimarika

October 12, 2015

index 
Na Beatrice Lyimo-Maelezo Dar es Salaam.
…………………………………………………
SERIKALI imesema itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na Jamhuri ya Watu wa China kwa kuimarisha  fursa mbalimbali za kijamii ikiwemo nyanja ya  kiutamaduni.
Hayo yamesemwa Jumatatu (Oktoba 12, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene wakati wa halfa ya uzinduzi wa chaneli mpya ya filamu ya China –Africa Movies itakayoonyeshwa kupitia kituo cha televisheni cha Easy Television kilichopo nchini.
Bw. Mwambene amesema kuwa uwepo wa chaneli hiyo utasaidia wazalishaji wa Tanzania kuonekana na kujulikana kimataifa na kuweza kujiongezea kipato na fursa kwa waandaaji hao.
“Chaneli hii itawapa fursa kwa pande zote mbili kwani filamu ya Tanzania itaonyeshwa china na kutafsiriwa kwa lugha yao na kwa upande wa Tanzania filamu za china zitaonyeshwa hapa Tanzania na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili”
Aidha Mwambene alisema  Chaneli ya China –Africa movies, licha ya kuwa  daraja la kujifunza tamaduni za kichina  pia itatoa fursa kwa Watanzania kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za biashara na kufungua milango kwa Watanzania kufahamu hatua mbalimbali za maendeleo ya kiuchumi na  kiutamaduni.
Mwambene ameitaka  Idara ya filamu nchini China kuitembelea Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni kwani ina kitengo kinachohusika na filamu za ndani.
Kwa upande wake Waziri wa Radio, Televisheni na usimamizi wa filamu wa Jimbo la Henan, China  Bi. Song Fengxian  alisema Serikali ya China itaongeza ubunifu kwa watazamaji wa pande zote mbili na kuwashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha uzinduzi wa filamu hiyo.  
Naye mwakilishi wa Kituo cha EASY TV Bi. Sophia Selis alisema kuwa katika kuendeleza urafiki baina ya Tanzania na China, kituo cha Easy Television imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha, kujifunza na kubadilishana utamaduni kulingana na wakati.
“Tunarusha program zetu kwa kutumia lugha mbalimbali ikiwemo kiingereza, kichina, kiarabu, kihindi na Kiswahili ili kukidhi tija za watazamaji wetu wa mataifa mbalimbali kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotoa picha zenye ubora” alisema Bi. Selis.
Easy television inarusha jumla ya chaneli 33 vya televisheni ikiwemo filamu, muziki, burudani, michezo, matukio, habari, vipindi vya watoto.

MAMA SAMIA AFUNIKA JIMBO LA GEITA MJINI

October 12, 2015

Maelfu ya wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita Jumatatu Oktoba 12, 2015.
 
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita, Oktoba 12, 2015.
 William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita .
 Mkuu wa mkoa wa Geita, akimtuza, William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi
ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya
kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho
kutoka CCM, wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni
uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia
Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hiko mkoani Geita.
Baadhi ya wanachama waliokuwa wa Chadema wakisubiri kuhamia CCM, kumfuata William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita. jumla ya vijana 61, walijiunga CCM
Mgombea Ubunge jimbo la Geita mjini, Costantine Kanyasu, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika jimbo hilo mkoani Geita.
Mgombea Ubunge jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku maarufu kwa jina la King Msukuma, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanywa na Mama Samia katika jimbo la Geita Mjini mkoani Geita.
Msanii wa Bongo Movie anayeko katika kundi la Nimestuka, akionyesha machejo yake katika mkutano wa kampeni uliofanywa leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita.
Vijana wanaounda kundi la kampeni la Nimestuka, wakishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva anayeko katika kundi la Nimestuka, Juma Kiroboro maarufu kwa jina la Juma Nature, akishambulia jukwaa akiwa na Ispekta Haruna wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akiwapongeza Juma nature na Inspekta Haruna baada ya kutumbuiza katika mkutano wa kampeni aliofanya katika jimbo la Geita mkoani Geita leo
Kiongozi wa kundi la kampeni la Mama sema na Mwanao, Steve Nyerere akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Geita mkoani Geita leo
Msanii wa Bongo Movie ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Majanga, akitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita, Oktoba 12, 2015.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO