RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA DADA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

December 22, 2015
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji mke wa Rais Mtaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada yake kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete akimlaki Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipohudhuria katika mazishi ya shangazi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Sitti Mwinyi katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Khadija Mwinyi katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Mama Janet Magufuli katika mazishi ya  dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Salma Kikwete akimpoke Mama Janet Magufuli katika mazishi ya wifi  yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Rais John Pombe Joseph Magufuli akipokewa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete Marehemu Tausi Khalfani Kikwete,  kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015. Kushoto ni Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete  Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mama Janet Magufuli (kulia) akiwa na wafiwa kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akitoa hutba wakati wa mazishi 
 Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akiongoza swala 
 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa  mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21
 Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini
 Ni wakati wa dua baada ya mazishi
Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi. PICHA NA IKULU

WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS DOKTA MAGUFULI KUPAMBANA NA UFISADI-DR.WALUKANI

December 22, 2015
Mhitimu wa Shahada ya Udaktari na
Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi akizungumza wakati wa mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho


 DR.WALUKANI  LUHAMBA AKIPONGEZWA NA FAMILIA YAKE MARA BAADA YA KUHITIMU  SHAHADA YA UDAKTARI NA UZAMIVU WA FALSAFA KATIKA MASWALA YA UONGOZI KUTOKA CHUO CHA NEW LIFE BIBLE COLLEGE AND SEMINARY US CHENYE TAWI LAKE KATA YA MLANDIZI MKOANI PWANI KATIKATI NI MKEWE

WAHITIMU wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kumsaidia Rais John Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi uliokithiri kwa kuhakikisha hawajihusishi na masuala hayo katika maisha yao ikiwemo kutumia taalumu walizozipata kujipatia maendeleo wao na jamii zinazowazunguka.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mhitimu wa Shahada ya Udaktari na
Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi
mkoani hapa Walukani Luhamba mara baada ya kutunikiwa cheti cha kuhitimu kwenye mafalali iliyofanyika mjini hapa.
 

Alisema kuwa wahitimu hao wanaweza kutumia vizuri taaluma zao
walizozipata kuhakikisha wanazitumikia jamii zao ikiwemo kuwa wabuni katika kujipatia vipato halali ambavyo vinaweza kuwasaidia kwenye kukabiliana na maisha badala ya kusubiriwa kuajiriwa.

 

Dokta Luhamba  alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua wao wanafursa kubwa ya kuibadilisha jamii ili waweze kuondokana na masuala ya jamii tegemezi badala yake watumia nafasi walizonazo katika kujiletea maendeleo.
 

 “Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana ambazo zinaweza kutumika vizuri katika kuhakikisha wanajiletea maendeleo hivyo viongozi waliopewa dhamana na wananchi waangalie alama za nyakati na wafanya kazi kwa uadilifu mkubwa kama serikali ya sasa inavyofanya shughuli zake chini ya Rais Dr. Magufuli “Alisema Luhamba
 

Aidha aliwataka kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi zao kwa uadilifu na hekima kubwa ili kuchochea kazi ya ukuaji wa uchumi kwao na nchi kwa ujumla sambamba na kusaidia serikali kukabiliana na wabadhirifu wa mali za umma.
 

   “Lakini pia tuhakikisha tunakuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwa na kumuombea Rais wetu Magufuli ili mungu aweze kumtia nguvu za kuweza kutekeleza kazi zake nzuri alizozianza kwa ueledi mkubwa na ufanisi katika kulipatia maendeleo Taifa letu “Alisema Walukani.
 

Katika mahafali hayo zadi ya  wahitimu 30 walitunukiwa vyeti na mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Proffesa John Adamson Mwakilema lakini kwa upande wa Shahada ya Udaktari na Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi walikuwa wahitimu wawili akiwemo Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) Mkoa,Dr.Walukani Luhamba.
 

Proffesa Mwakilima aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika jamii zao kwa kutumia vizuri taaluma walizozipata katika kuinua uchumi wao na wananchi wanaowazunguka.

MSWADA WA SHERIA YA WAZEE KUWASILISHWA BUNGENI-WAZIRI UMMY

December 22, 2015

Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano maalumu na wazee wa Jiji la Tanga leo
Serikali inatarajia kuwasilisha  mswada wa sheria katika bunge la Mwezi wa tisa  kwa ajili ya kuundwa kwa sheria ya wazee ili kuhakikisha sera ya wazee inafanyakazi ipasavyo hapa nchini .
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Alhaj Abdulla Lutavi akitoa neno kwenye mkutano huo

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri  wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea katika mkutano maaluma na wazee wa Jiji la Tanga leo


 Alisema kuwa Mswada huo utakapofikishwa bungeni na wabunge kuuridhia itasaidia kusimamia ufanyaji kazi wa sera ya wazee ambayo ilikuwa imetungwa siku nyingi lakini ilikuwa haifanyiwakazi kwa kukosa muongozo.

“Licha ya serikali kujitahidi kupunguza changamoto za wazee lakinia tunajua kuwa bado  matatizo mengi ya wazee ambayo yanahitaji ufumbuzi na usimamizi wa kisheria hivyo kwa jitihada hizo zitawezesha kumaliza changamoto hizo”alisema Waziri Mwalimu.

Moja kati ya wazee wa mkoa wa Tanga,Alhaji Kassim Kisauji akiuliza swali kwenye mkutano huo
Aidha aliziagiza Halimashauri zote nchini kuhakikisha zinawatambua wazee walioko katika maeneo yao hususani wale waliofikia umri wa miaka 60 na kuendelea.

“Niwaombe katika utambuzi huo muhakikishe unawaainisha wazee wanaojiweza na wale wanaojiweza ilikuhakikisha mnawatengeneza utaratibu maaluma wa kupata mahitaji yao muhimu kama ilivyoainishwa kwenye sera”alisisitiza

Baadhi ya wazee wa mkoa wa Tanga wakifuatilia matokeo mbalimbali kwenye mkutano huo na Waziri Ummy
Hata hivyo Waziri Mwalimu alisema kuwa moja ya mikakati ya wizara yake ni kuhakikisha wamewasajili wazee wapatao laki mbili na kuwaingiza kwenye mpango wa matibabu bure .

Alisema kuwa licha ya idadai hiyo kuwa ni ndogo lakini anaamini mpango huo ukipata usiamamizi mzuri unaweza kuwasaidia wazee kupata huduma bora za matibabu katika ngazi zote za wilaya hadi rufaa.

 
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa asasi ya wazee mkoa wa Tanga TARINGO Fredorin Mbunda aliiomba serikali iangalie uwezekano wa kuongeza kiwango cha fedha za pesheni kwa wazee ili iendane na hali halisi ya mazingira ya sasa.
 

Alisema kuwa peshen iliyopo inawasaidia kupata milo miwili tu kwa siku hali ambayo inasababisha wazee wengi kuishi katika maisha ya tabu na duni kwa kiasi kikubwa.

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

December 22, 2015


‪#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
1.MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
2.PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
3.MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
4.NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
5. BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
6.KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
7.MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.CHANZO CRI SWAHILI
Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili

Pilipili kali 

Brokali

Nyanya 
‪#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo: 1.MAFUTA YA SAMAKI Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja. 2.PILIPILI KALI Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa. 3.MBEGU ZA MABOGA Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa. 4.NYANYA Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili. 5. BROKOLI Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee. 6.KARANGA Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini. 7.MAYAI Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.CHANZO CRI SWAHILI

UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI WA VIJIJI NI DHANA KUU YA KUTATUA KERO ZINAZOWAKABILI WANANCHI WANAO WAONGOZA.

December 22, 2015



Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo yao yaliyofanyika wilayani hapo. 

“Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,”  Hayo ni maneno ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Loliondo.
Alisema hayo kwa lengo la kufafanua dhana ya uwajibikaji kwa viongozi kama njia muhimu ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini katika wilaya yake. Ni dhahiri kwamba viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maeneo husika.  Kuna nafuu kwa watendaji wa kata na vijiji,  ambao ni waajiriwa wa serikali na hupewa kazi kutokana  na miongozo, lakini siyo kwa wenyeviti wa vijiji na madiwani, wakati mwingine hata wabunge.


Akielezea changamoto hiyo wakati wa mafunzo ya wenyeviti wa vijiji kupitia mradi wa Chukua Hatua yaliyofanyika Septemba mwaka huu na shirika mdau la CABUIPA, mwenyekiti wa kijiji cha Nyakafulu kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Salum Said amesema:  “Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki, hakika sikufahamu vya kutosha kuhusu majukumu yangu mapya kama kiongozi. Na hii ni changamoto kubwa kwa wenyeviti wa vijiji karibu vyote vya wilaya yetu.” 


Yeye ni mmoja kati ya wenyeviti 200 wanaopatiwa mafunzo katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Simiyu. Wakati wananchi wakiwezeshwa kuwasimamia viongozi wao, viongozi hawakuwa wakiwezeshwa kutimiza majukumu yao kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi wao.  Hivyo kuna haja ya kutoa mafunzo kwa viongozi hao ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowachagua, ilikuwa lazima. 
Wanakijiji wa Kijiji cha Uchunga wilayani Kishapu wakiendelea na mkutano pamoja na viongozi wa kijiji na wazee Maarufu
Akielezea umuhimu wa kuwawezesha wenyeviti wa vijiji  wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wenyeviti na watendaji wa kata Julai 2015, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Jane Mutagurwa alisema “Kwa muda mrefu wenyeviti mmekuwa mkilalamika kusahaulika kwenye programu zetu za mafunzo, fursa ndio hii imekuja. Tunafahamu kwamba wenyeviti wetu mnakutana na changamoto nyingi za kiutendaji zinazotokana na uwelewa mdogo katika majukumu yenu, hasa kwa wale wanaoingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivyo mtumie mafunzo haya vizuri.” 


Pamoja na umuhimu wa mafunzo hayo kwa viongozi wa ngazi  ya kijiji na kata, bado imekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali kuwawezesha wenyeviti kujua majukumu yao. Na hii inatokana bajeti kuwa na vipaumbele vingine ambavyo halmashauri huwa wamejiwekea katika  kutimiza majukumu yao."


Kwa upande wa Ngorongoro, mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Arusha anaeleza:“Tangu tulipofanya uchaguzi mwaka jana hatujawahi kutoa mafunzo kwa wenyeviti. Kwa hiyo tunaunga mkono mafunzo haya yanayotolewa na PALISEP yatasaidia sana kwenye kuwawezesha viongozi hawa na watendaji wetu,”  Kutokana na hali hii, wenyeviti wamekuwa na changamoto za kuelewa mipaka ya majukumu yao, hivyo muda mwingine hujikuta kwenye mzozo na watendaji wa vijiji vyao.  Mwenyekiti anawajibika kwa mwananchi aliyemchagua, wakati mtendaji anawajibika kwa mkurugenzi aliyemwajiri. Kutokana na tofauti hizo, mafunzo ya sasa ya wenyeviti na watendaji yanaendeshwa kwa pamoja kuwafanya waelewe mipaka yao ya kiutendaji, hivyo kuboresha utendaji wao.


Afisa Programu wa CABUIPA, Michael Ikila anafafanua: “Tunawafundisha vitu sita muhimu; taratibu za uendeshaji serikali za mitaa, majukumu na haki za  wenyeviti wa vijiji, uwajibikaji na utawala bora,  mamlaka za vijiji, masuala ya fedha, ikiwamo uandaaji wa  bajeti na mawasiliano mazuri baina ya viongozi wa  vijiji.”  Mada hizi ni kwa mujibu wa mwongozo wa wizara ya Tawala za Mikoa and Serikali za Mitaa (TAMISEMI).  Majukumu mengine ya wenyeviti hawa ni pamoja na  kuhamasisha shughuli za maendeleo, utawala na  kuhakikisha usalama wa watu katika maeneo yao kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji.
Viongozi wa Kijiji cha Negezi wakiwa pamoja na wanakijiji kujadili mambo mbalimbali ya eneo lao.
Kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro, hii ni mara ya kwanza kwa wenyeviti kufundishwa majukumu yao. Mwanzoni mafunzo haya yaliwalenga madiwani ambao kimsingi hawakuyapenda kwa sababu ya kutokuwapo kwa posho. Hivyo mafunzo yao yakaamishiwa kwa wenyeviti wa vijiji ambao walipokea mwaliko kwa furaha pasipo kudai posho. “Mafunzo haya yatatusaidia kuboresha mahusiano na utendaji wetu. Mara kadhaa unakuta wenyeviti wanaingilia mipaka yetu ya kazi, hivyo kuathiri uhamasishaji wa shughuli za maendeleo. Na hii hutokea pale mwenyekiti mpya anapotaka kuwaonyesha wapigakura wake kwamba mwenzake aliyepita hakufanya kazi,” anaelezea mmoja wa watendaji wa kijiji aliyehudhuria mafunzo hayo.


Pamoja na changamoto hizo, bado washiriki ambao ni wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wamekiri kwamba mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kumaliza tofauti zinazojitokeza baina yao. Lakini si hivyo tu, viongozi wa wilaya wameonyesha kuunga mkono mafunzo hayo kwa kuwa yanasaidia kuhamasisha wananchi kutimiza majukumu yao. Lakini pia viongozi hao walionyesha umuhimu wa kufikia wajumbe wengi zaidi ya halmashauri za serikali ya kijiji. Kwa mfano, wakati akizungumza na wakufunzi kwenye ofisi yake, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, alisema: Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ina jumla ya vijiji 117 vyenye wajumbe 2,925. 

Katika mazingira hayo, mkurugenzi alitoa ombi maalumu la kusaidiwa kuwawezesha wakufunzi 25 wa wilaya watakaotoa mafunzo kwa wajumbe wa halmashauri za vijiji hivyo. Gharama za wakufunzi hawa kuwafikia wajumbe wengine zitakuwa ni za serikali.  Na huu ni ushirikiano unaotakiwa baina ya sekta ya umma na binafsi kwa kuwa ni jukumu letu sote kwa mustakabali wa maendeleo yetu.
  Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com
KIGWANGWALLA ATEMBELEA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA KUSINI

KIGWANGWALLA ATEMBELEA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA KUSINI

December 22, 2015
01
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) alipotembelea eneo la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini, mkoani Mtwara.
02
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimuuliza swali Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) wakiwa eneo la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini, mkoani Mtwara.
IMG_9637
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (kushoto) inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini inayojengwa eneo la Mikindani mkoani Mtwara.
03
05
Muonekano wa moja ya majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma inayojengwa eneo la Mikindani mkoani Mtwara.(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO).
Na Mwandishi wetu, Mtwara
UJENZI wa hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini, unaofanyika mkoani Mtwara sasa upo katika majengo ya wagonjwa wa nje (OPD).
Ujenzi huo ulioanza mwaka 2009 kwa kusafishwa kwa eneo na kujengwa kwa uzio wa kilomita 2.7 mwaka 2011 kwa gharama ya shilingi milioni 840 na kuanza kujengwa kwa majengo ya OPD mwaka 2013 umelenga kuwezesha mikoa ya Kusini kuwa na hospitali kubwa yenye hadhi ya kisasa.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi kwa Naibu Waziri katika wWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara alisema kwamba ujenzi wa mapokezi umetarajiwa kutumia shbilioni 4.8 na hadi sasa wametumia bilioni 1.8
Mganga huyo alisema mradi mzima unatarajiwa kujengwa kwa bilioni 78.
Alisema kuchelewa kuendelea japo sasa wana ghorofa 2 zilizoezekwa na wanapiga ripu kunatokana na upatikanaji wa fedha kutoka serikali kuu.
Alisema hospitali hiyo ni muhimu sana kukamilika kutokana na kukua kwa uchumi wa Mtwara na mikoa jirani na pia kuwapo kwa uhitaji kwa mikoa ya kaskazini mwa nchi jirani.
Naye Naibu Waziri Kigwangwalla alisema kwamba ni matumaini yake kuwa hospitali hiyo itakamilika mapema na kubakiza changamoto za matumizi ya wananchi kutoka nchi jirani ambao kwa sasa wanafaidika sana na hospitali ya Ligula.
Alisema wataalamu wanatakiwa kuangalia hali hiyo ili kuwepo na matumizi sahihi ya miundombinu hiyo iliyolenga kufaidisha wananchi wa Tanzania.
Aidha akiwa Mtwara Naibu Waziri huyo aliendelea kusisitiza watumishi wote kuwajibika na kuwahi maeneo yao ya kazi.
Alisema watumishi wa umma wanaofikia laki nne wamepata nafasi adimu ya kuutumikia umma wa watu takribani milioni 50 na hivyo ni lazima waheshimu watanzania kwa kuwatumikia ipasavyo.
Alisema wao waliomba nafasi ya kuhudumia watanzania kwa hiyo ni lazima wawahudumie watanzania na kila mmoja katika kitengo chake ni lazima kuhakikisha watumishi wanafanya kile walichoahidi katika mikataba yao.

WARAGHABISHI WA KIJIJI CHA OLOLOSOKWANI WILAYA YA LOLIONDO WAPIGWA MSASA NA PALISEP

December 22, 2015

Mraghbishi Kootu Tome (wa pili kushoto) akiwa na mtendaji wa kijiji Rabie Lebuna (mwenye shati la njano) na Mwenyekiti wa Kijiji, Kerry Dukonya (wa pili toka kulia).



Na Kisuma Mapunda,Loliondo

Sasa ni dhahiri waraghbishi wanatambua majukumu na haki zao ndani ya jamii. Uelewa wao umewapa fursa ya kuchukua hatua na kusimamia kile wanachoamini kwa manufaa ya wanajamii wanaowatumikia.
Watu hawa wamekuwa mhimili muhimu wa kuleta mabadiliko katika maeneo wanayoishi. Lakini inapendeza zaidi kuona waraghbishi hao wakijawa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wao kwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kama ilivyo kwenye Kijiji cha Ololosokwani, kilichopo katika tarafa ya Loliondo, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.
Kijiji hiki kina jumla  ya kaya 1,520 zinazoundwa na vitongoji vinne vya kijiji, ambavyo ni Sero, Ololosokwani, Mairowa A na B. Baadhi ya wanaounda kaya hizo ni pamoja na waraghbishi wanaofanya kazi na mradi wa Chukua Hatua, akiwamo Kootu Tomu, mama wa watoto sita kutoka kitongoji cha Mairowa.
Tomu ni mmoja wa waraghbishi wa kwanza kuanza kufanya  kazi na mradi wa Chukua Hatua wakiwa na jukumu la  kufuatilia ahadi za wagombea wakati wa uchaguzi wa mwaka  2010. Ni katika uraghbishi huu wa kufuatilia ahadi zilizokuwa zinatolewa na wagombea, ndipo alipojifunza taratibu na kanuni za kuwa kiongozi bora.
Miaka mitano baadaye, alijitokeza katika kinyang’anyiro cha kuomba kuchaguliwa na wanachama wenzake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kura ya ndani ya maoni. Na baada ya hapo alipata fursa ya kupeperusha bendera ya chama chake na kuchaguliwa katika uchaguzi uliofanyika mwezi Disemba mwaka 2014.
Akielezea jinsi ilivyokuwa Kootu Tomu anasema:
“Nilifahamu jukumu lililokuwa mbele yangu katika kusimamia haki kwenye migogoro ya ardhi katika eneo letu. Hivyo, katika uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa niliomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kijiji kupitia CCM na nilichaguliwa. Sasa naweza kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa akinamama kupitia fursa hii ya uongozi niliyopata,”
Ndani ya halmashauri ya serikali ya kijiji cha Ololosokwani, mraghbishi huyu amechaguliwa kuwa mmoja kati ya wajumbe 9 wanaounda kamati ya elimu. Akiwa kama mjumbe wa kamati hiyo, anafafanua majukumu yake:
“Moja ya jukumu la kamati yetu ni kusimamia upatikanaji wa ada kwa wanafunzi. Kijiji chetu kinapata fedha kutoka idara ya wanyama pori, ambazo ndiyo hutumika kulipia ada za watoto kwenye kijiji chetu.”
Katika kijiji cha Ololosokwani, kila mtoto anapata fursa ya kupata elimu kwa kulipiwa gharama stahiki kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi kiwango cha shahada ya uzamili.
Serikali ya kijiji hiki imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha walengwa wanapata huduma husika na kuhakikisha wanatoa taarifa za kweli.
Akifafanua utaratibu huo, mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani, Kerry Dukonya anasema:
“Jambo la kwanza ni mwanafunzi kutafuta shule na baada ya kupata atatakiwa kuleta fomu na barua ya kukubaliwa kujiunga na shule husika kama kielelezo. Barua hiyo ndio inayotoa maelezo ya ada na mahitaji mengine ya shule.  Ndipo hapo kamati inafuatilia na kuhakiki taarifa, kabla ya kupitishwa na halmashauri ya serikali ya kijiji.”
Waraghbishi wamekuwa msaada mkubwa katika kutimiza majukumu ya serikali kwa kuwa mstari wa mbele katika harakati za kuhimiza wananchi kutambua haki na majukumu yao katika kijiji. Na viongozi wa kijiji wanakiri kwamba waraghbishi wamekuwa wakishawishi wananchi kuchukua hatua mbalimbali, ikiwamo kuwawajibisha viongozi wazembe.

Akifafanua hali hiyo na jinsi viongozi wanavyojisikia iwapo uraghbishi utagusia masilahi yao hasa linapokuja suala la kuwawajibisha, mwenyekiti wa kijiji anasema:
“Sisi kama viongozi, tunamruhusu Kootu kwenda popote na akinamama hawa wamekuwa mstari wa mbele kutukosoa na kutukumbusha majukumu yetu. Hii ni njia mojawapo ya kuruhusu haki itendeke. Hivyo ni haki ya wananchi kujua mapato na matumizi ya serikali yao ambayo sisi kama viongozi  tunayasimamia.”
Kama mwanamke ndani ya halmashauri ya serikali ya kijiji, amepatiwa jukumu maalumu la kuhakikisha wanawake na wasichana wanashiriki katika shughuli za maendeleo.  Akifafanua jambo hilo, mwenyekiti wa Ololosokwani, Kerry alisema:
“Tungependa kuona anakuwa kielelezo cha mwanaharakati mwanamke kutokana na nafasi yake kama mjumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Lakini pia wanawake wamekuwa ni kundi la pembezoni, ikiwamo walemavu. Mraghbishi huyu atakuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wenzake kutambua umuhimu wa elimu.”
Mraghbishi Kootu Tome (kushoto) akigawa nakala za Riwaya za Chukua Hatua kwa baadhi wa wananchi wa kijiji cha Ololosokwani ikiwa kama sehemu yake ya uraghbishi. (Picha na Kisuma Mapunda)

Mraghbishi Tome, kwa kutumia mbinu za kiuraghbishi, anahakikisha watoto wa kike wanakwenda shule. Katika hili, anaeleza anaeleza mikakati yake:
“Kama mraghbishi, nimepata fursa ya kukutana na akinamama na kuhakikisha watoto wa kike wanapata nafasi za kusoma. Lakini siku zote nimekuwa nikiwataka kuwasiliana na walimu ili watambue changamoto zinazowakabili watoto wao wa kike, hasa kwa wale ambao wapo mashuleni tayari,”
Kwa upande wake, mtendaji wa kijiji Rabia Legula anasema:
“Ninapozungumzia mraghbishi, namaanisha wale wanaohamasisha wananchi kudai haki zao za msingi, ikiwamo kuwawajibisha viongozi. Si hivyo tu, waraghbishi wamekuwa mstari wa mbele kunisaidia masuala yanayohusu wanawake. Kupitia ujuzi wao na kama wanawake waraghbishi tunatoa kipaumbele kwa wanawake.”
Katika jamii ya kimasai ambayo bado wanawake hawajapata nafasi ya kutosha, uwepo wa waraghbishi wanawake umekuwa chachu nzuri ya kuwawezesha wenzao kuongea katika mikutano ya hadhara.
“Tunapenda waraghbishi waendelee kuhamasisha akinamama kuongelea masuala yao katika mikutano ya vijiji. Kwa kutumia nafasi yangu ya utendaji, nitahakikisha natoa fursa kwa waraghbishi hawa kuzungumza kwa uwazi mambo ya  wanawake.”
Kama mjumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji, mraghbishi amekuwa na jukumu la kuhakikisha  wananchi wanahudhuria mikutano ya kijiji.
“Huwa nawahamasisha akinamama wenzangu kuhudhuria mikutano ya kijiji kila tunapokutana kwenye vikundi vyetu vya ushirikiano,” anasema.



 Mkurugenzi Mtendaji wa PALISEP, Roberth Kamakia,akielezea jambo katika mkutano uliokutanisha waraghabishi toka mikoa ya Arusha ,Simiyu na Shinyanga uliofanyika hivi karibuni 

Awamu ya pili ya mradi wa Chukua Hatua, unalenga kuwawezesha waraghbishi wa zamani kufundisha waraghbishi wapya waliochaguliwa na serikali za kijiji, kama anavyoelezea Mkurugenzi Mtendaji wa PALISEP, Roberth Kamakia,

“Tuliwaandikia barua serikali za vijiji tukiwaomba watuchagulie watu wanaofaa kuwa waraghbishi. Tuliwapa sifa za watu hao na mwongozo wa jinsi ya kuwachagua.
Baada ya waraghbishi hao kuchaguliwa, waliandaliwa kwa ajili ya mafunzo ya pamoja ikijumuisha wale wa zamani na wapya. Na baada ya hapo waraghbishi wa zamani walikuwa na jukumu la kuwafundisha wenzao jinsi ya kufanya uraghbishi.
Katika mafunzo hayo, walikumbushwa maana ya uraghbishi na sifa za uraghbishi. Ndipo wale waraghbishi wa zamani, akiwamo Kootu walipopewa jukumu la kufundisha wenzao kwa kutumia uzoefu waliopata wa uraghbishi.
Akielezea jinsi wao waraghbishi wa zamani wanalivyofundisha waraghibishi wapya wanaotoka vitongoji vya Ololosokwani na Njoroi, Kootu anasema:
“Tulikaa pamoja PALISEP na kuwafundisha waraghbishi wapya. Kwa upande wangu, nilifundisha maana ya uraghbishi na kutoa maana ya mtu anayeitwa mraghbishi Kazi yake ni kuwahamasisha wananchi. Mraghbishi anatakiwa awe na sikio kubwa la kusikiliza, mdomo mdogo wa kuongelea na macho makubwa ya kuangalia,” anasema.  
Kootu si mraghbishi pekee aliye kwenye halmashauri ya serikali ya Kijiji cha Ololosokwani, mraghbishi mwingine ni Noorkishili Naing’isa ni mjumbe wa halmashauri na  kamati ya fedha. Ni dhahiri waraghbishi wanawake wameendelea kuwa chachu ya maendeleo kutokana na utendaji wao mzuri kwenye serikali za kijiji. Hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha harakati hizi za uraghbishi ndani ya halmashauri za vijiji vyetu zinaungwa mkono.


                           CHANZO ; MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG 


photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"