MANISPAA YA ILALA YATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI 25 KWA KUTOHUDUMIA IPASAVYO DAMPO LA PUGU KINYAMWEZI.

July 07, 2017

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akiwa ameambatana na Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita (kushoto) wakati wa ziara ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi ambap ameipiga faini ya milioni 25 Manispaa ya Ilala kwa uchafu wa mazingira kwa wakazi wa Pugu. 

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akionyesha jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati wa ziara yake aliyoifanya mapema hii leo jijini Dar es salaam ya kukagua uchafuzi wa mazingira katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Wilaya ya ILala.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizumgumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo aliyoifanya katika Dampo la Pugu Kinyamwezi lililopo Ilala jijini Dar es salaam.  
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina (kulia) akibadiishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema(katikati), Sophia Mjema na kushoto ni Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita wakati wa ziara ya ukaguzi wa uchafuzi wa mazingira uliofanyia katika dampo la Pugu KInyamwezi jijini Dar es salaam.  

NA EVELYN MKOKOI
Kufuatia ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, iliyofanyika Jijini Dar es Salam leo katika Manispaa ya ilala, iliyohusisha ukaguzi wa Dampo la Pugu Kinyamwezi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkaguzi wa Mazingira wa kanda ya Mashariki Bw. Jaffari Chimgege imeitoza faini Manispaa  ya jiji ya Dar es Salaam kiasi cha shilingi Milioni 25.

Faini hiyo inatokana na kosa la uchafuzi wa Mazingira wa kutohudumia Dampo hilo ipasavyo na kupelekea harufu mbaya, vumbi na maji yenye sumu kali na kuhatarisha afya ya wakazi wa maeneo jirani viumbe hai na mzingira kwa ujumla.
 
Kufuatia malalamiko ya wakazi wa mtaa wa Viwege uliyopo katika kata ya Majoe yaliyowasilishwa na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bi Amina Rashid yaliyoeleza kuwa na changamoto mbali mbali katika dampo hilo zikiwemo za vumbi na maji yenye kemikali kwenda katika maeneo ya makazi.

 Naibu Waziri Mpina, ameitaka Halmashauri ya jiji kuja na mpango mkakati utakaoweza kuupunguzia mzigo dampo la Pugu ambalo kwa sasa linatumika kupokea takataka zote za Halmashauri za jiji la Dar es Salaam na kuonekana kulemewa na mpango huo uwezeshe kila manispaa kuwa na dampo lake.

Aidha Mpina alibaini kuwepo kwa madhaifu makubwa katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kuondosha taka katika manispaa za jiji na kuutaka uongozi wa jiji Hususan Mkurugenzi wa Jiji kufuatilia madeni hayo kikamilifu.

Pamoja na kutoa deadline ya uwasilishwaji wa fedha hizo “ni vyema ghahama za uondoshwaji wa taka zikatokana na taka zenyewe na siyo kutoa fedha za kuhudumia taka kutoka katika vyanzo vingine vya mapato. Alisisitiza Mpina.”

Mpina pia aliitaka manispaa ya jiji  kutafuta namna bora ya kuondosha taka sumu na kuelekeza taka zote za matairi katika jiji la Dar es Salaam zitafutiwe sehemu tofauti na namna pekee ya kuzitekekeza.

Akionekana kuongea kwa hasira na msisitizo Naibu Waziri Mpina alisema,   “ Hakuna kitu nisichopenda katika utendaji wangu kama kuona taasisi za serikali zikiwa za kwanza katika suala zima la uchafuzi wa mazingira na faini hiyo jiji mtailipa ndani ya siku 14 lakini pia kuhakikisha mnarekebisha  matobo yote yanayolalamikiwa kupitisha maji na kupeleka katika makazi ya wananchi.

Lakini pia hilo litaendana  pamoja na kujenga mifereji ya maji ya mvua, na maji ya sumu yaende katika mkondo sahihi wa maji hatarishi na bila kusahau kuruhsu maji hayo baada ya kujiridhisha na vipimo vinavyotakiwa.

Awali akitoa taarifa ya hali ya mazingira  na usimamizi wa taka katika Dampo  la Pugu Kinyamwezi , Mkuu wa Idara ya usimamizi taka wa jiji la hilo Bw. Shedrack Maximillian alimueleza Mpina kuwa jiji linakabiliana na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja dampo kupata moto, dampo kutokuwa la kisasa na maji yenye sumu kwenda katika makazi ya wananchi.

Hata hivyo Manispaa ya ilala imetenga kiasi cha fedha shilingi Bilioni moja za kitanzania kwa mwaka wa fedha ulioisha pamoja na kuzungumza na wadau wa maendeleo ikiwa ni mkakati madhubuti wa kuweza kuboresha Dampo hilo kinalotumika kwa kiasi kikubwa na manispaa zote za jiji la Dar es Salaam.


MAMA JANETH MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA

MAMA JANETH MAGUFULI AZUNGUMZA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI KWA WAZEE WASIOJIWEZA 400 CHATO MKOANI GEITA

July 07, 2017
unnamed
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bi. Winfrida Lawrent(65) kutoka Kata ya Kasenga kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Kilo 4000 Maharage, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
1
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mwakilishi wa Wazee 400 kutoka Wilaya ya Chato Bw. AnatoryBisate  (64) kabla ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali ikiwemo Kilo 10,000 za Mchele, Kilo 10,000 za Unga wa mahindi, Maharage kilo 4000, Mafuta, Sabuni pamoja na Sukari.
2
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakabidhi kwa pamoja mafuta waakilishi wa Wazee kutoka kata ya Kasenga AnatoryBisate  (64) kulia pamoja na Bi. Winfrida Lawrent(65) kushoto mara baada ya kuzungumza na wazee 400 katika Ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
3
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiimba pamoja na wanakwaya wa Mwagazege mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mshikamano SACCOS Chato mkoani Geita.
4
Mama Janeth Magufuli akiwasili katika eneo la mkutano mara baada ya kupokewa  na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga Chato mkoani Geita.
5
Mama Janeth Magufuli akiwa na viongozi wengine wa mkoa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga  wakwanza kushoto wakati wa dua kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi  ya 400.
6
Mama Janeth Magufuli akifurahi pamoja Naibu Waziri wa nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wakati Kwaya ya Mwakazege ya kutoka Chato ilipokuwa ikitumbuiza kabla ya kuzungumza wazee wasiojiweza zaidi ya 400.
7
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Wazee wasiojiweza zaidi ya 400 kutoka Wilaya ya Chato katika Ukumbi wa Mshikamano Saccos.
8 9
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa, Wilaya na Chama waliojumuika na Waakilishi wa wazee wasiojiweza zaidi ya 400 Chato mkoani Geita.
10
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
11
Wazee wakishangilia wakati wa hotuba ya mgeni rasmi.
PICHA NA IKULU

BEI YA DAWA ZA SERIKALI YASHUKA NCHINI

July 07, 2017
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.

TANZIA: KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, HASSAN SHEBUGE AFARIKI DUNIA

July 07, 2017
Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagala Majimatutu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaama iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.

IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA