WIZARA YA MAMBO YA NJE YAMUAGA BALOZI WA INDIA ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI
Balozi
wa India nchini Tanzania anayemaliza muda wake wa kazi, Mhe.Debnath
Shaw akitoa hotuba yake ya kuaga mbele ya wageni waalikwa wakiwemo
baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakiongozwa na
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Simba Yahya wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyofanyika
katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Julai, 2015.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Simba Yahya (kushoto) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo hapa nchini ambaye pia ni mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi
zao hapa nchini, Mhe.Juma Halfan Mpango wakifuatilia hotuba
ya Mhe.Debnath Shaw (hayupo pichani).
Balozi
wa China hapa nchini, Mhe.LU Youqing (kulia) pamoja na Afisa Mambo ya
Nje, Bi.Eliet Magogo (katikati) pamoja na mmoja wa wageni waalikwa
wakisikiliza hotuba.
Mabalozi pamoja na Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifurahia hotuba ya Balozi huyo wa India hapa nchini.
Balozi Yahya kwa pamoja na Balozi Shaw wakitakiana afya njema
Mshereheshaji akiendelea kusherehesha wakati wa hafla hiyo.
Balozi
Yahya akiwaongoza Balozi Shaw (kulia) na Balozi Mpango kupata chakula
wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchan akumuaga Balozi Shaw.
Balozi Yahya akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Shaw na Balozi Mpango
Picha ya Pamoja.
Balozi Simba akibadilishana mawazo na Balozi Debnath Shaw mara baada ya hafla hiyo.
Balozi Simba akiagana na Balozi Juma Mpango baada ya hafla hiyo Picha na Reuben Mchome
Shirika la Umoja wa Mataifa kukabiliana na biashara, YA matumizi za dawa za kulevya ZANZIBAR
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA ECG NA AL KAN KUTOKA MISRI, IKULU DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Wafanyabiashara wa ECG na Al Kan kutoka nchini Misri, wakati walipofika
Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015 kwa
mazungumzo.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na Wafanyabiashara wa ECG AL Kan kutoka nchini Misri, baada ya
kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.
JESHI LA POLISI LANOLEWA JUU YA HAKI ZA BINADAMU KIPINDI CHA UCHAGUZI
aji
Mstaafu Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Semina ya Siku mbili
kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu nchini ili kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika
kulinda haki za binadamu kipindi cha uchaguzi. Semina hiyo imefanyika
huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.
…………………………………………………..
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Jeshi la Polisi nchini limeshauriwa kuzisoma kwa kina na kuzielewa vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi kabla ya kuzitekeleza.
Kufanya hivyo kutalipelekea Jeshi
hilo kuepuka lawama na kufanya wajibu wao kikamilifu ili kuufanya
Uchaguzi unaokuja uwe katika hali ya uhuru, haki na amani.
Wito huo umetolewa na Jaji Mstaafu
Thomas Mihayo alipokuwa akitoa Mada katika Warsha ya Siku mbili kwa
Maafisa wa Jeshi la Polisi iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki
za Binadamu nchini huko Ukumbi wa Hotel ya Grand mjini Zanzibar.
Amesema Jeshi hilo linawajibu wa
kuhakikisha Sheria za nchi zinafuatwa lakini jambo la msingi ni
kuzielewa Sheria hizo kabla ya kuzitekeleza.
Jaji Mihayo amesema inashangaza
kuona kuwa Tanzania inaelekea katika kipindi cha uchaguzi Mkuu wakati
Maafisa na Makamanda hawazielewi vyema Sheria na kanuni za Uchaguzi
unaokuja.
Hivyo amewaomba Maafisa
Wawaelimishe Makamanda wenzao juu ya Sheria na kanuni za uchaguzi ili
wakati utakapofika watende haki na Wajibu wao bila ya upendeleo.
“Polisi kazi yenu nikuhakikisha
Sheria zinafuatwa lakini zitafutwa vipi wakati wenyewe hamzijui..Jambo
la msingu ni kuzisoma na kuzielewa kwanza ndio mufanye juhudi za
kutekelezwa” alisema Mihayo.
Amefahamisha kuwa Jeshi hilo
linapaswa kufuata Sheria za nchi bila kufuata matakwa ya Watawala na
kwamba Watawala hao watabadilika kulingana na uchaguzi lakini Wananchi
wataendelea kuwepo.
“Jeshi la Pilisi linawajibika kwa
Wananchi na si Viongozi wa Serikali hivyo nakuombeni mzijue Sheria na
muwe wakwanza kuzitekeleza” Alishauri Jaji Mihayo.
Kwa upande wake Kamishna wa Jeshi
la Polisi Zanzibar Hamdan Makame ameshukuru Mtandao wa Watetezi wa haki
za Binadamu kwa kuendesha Semina hiyo katika kipindi muafaka cha
harakati za uchaguzi mkuu.
Amesema kila mtu ni mlinzi wa haki
za binadamu katika kila sehemu anayofanyia kazi nakwamba jambo muhimu
ni kuhakikisha Haki zinalindwa hasa ikizingatiwa kuwa suala la haki za
binadamu ni lakimataifa.
Kwa upande wake Makamu mwenyekiti
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Harusi Mpatani
ameliomba Jeshi hilo kuhakikisha linawalinda Wananchi wote ikiwemo
Watetezi wa haki za binadamu.
Semina hiyo ya siku mbili
iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini ni
mwendelezo wa kulijengea uwezo Jeshi la Polisi katika kulinda haki za
binadamu ili kuufanya uchaguzi unaokuja uwe huru,haki na Salama.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA UONGOZI WA SUMATRA, TRA, TABOA, RC-DSM NA WAZIRI WA FEDHA IKULU KWA MAZUNGUMZO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Baadhi
ya Viongozi wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) TRA,
SUMATRA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa Fedha, wakati
walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 29, 2015.
Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya viongozi wa SUMATRA, TRA, na Wamiliki wa Mabasi
Tanzania TABOA, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Fedha, baada
ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu
jijini Dar es Salaam,leo Julai, 29, 2015.
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny
Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu
ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na
Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe 28 Julai
2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima
yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai
2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiutambulisha ujumbe wake kwa Waziri Mkuu wa
Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai, 2015
katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni
alipowasili kwenye jumba la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015
na kukutana na kufanya mazungumzo na Gavana Mkuu wa Australia
Mheshimiwa Peter Cosgrove aliyesimama nyuma yake pamoja na Mama Salma
Kikwete na Mke wa Gavana huyo Mama Cosgrove.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa chakula cha mchana kwenye jumba
la serikali jijini Sydney tarehe 28 Julai 2015 baada ya kukutana na
kufanya mazungumzo na Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter
Cosgrove.
PICHA NA IKULU
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE, AUSTRALIA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na
viongozi wa chuo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipata picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe.
Nuatali Nelmes kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
Mstahiki Meya wa jiji la Newcastle Mhe. Nuatali Nelmes na viongozi wa
chuo wakipata maelezo kabla ya kuanza kwa msafara wa kwenda jukwaa kuu
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika msafara wa kwenda jukwaa kuu kutunukiwa shahada ya heshima
ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo
tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa na viogozi wa chuo jukwaa kuu wakisimama wakati nyimbo za Taifa za
Tanzania na Australia zikipigwa wakati wa kuanza kwa sherehe za
kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws
honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans
chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo
hicho.
Wasanii wa kabila la Wakakulang wakicheza ngoma za asili yao katika kunogesha sherehe za kihistorua ambapo Rais Kikwete amekuwa ni Mkuu wa Nchi wa kwanza kupokea digrii hiyo ya heshima kutoka katika Chuo hicho.
PICHA NA IKULU
Jaji Mutungi Ajiandikisha Katika Daftari la Kudumu La Wapigakura
Mhe. Jaji Francis S.K. Mutungi akiwa na kitambulisho chake mara baada ya kujiandikisha mapema Leo katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge Jijini Dar es salaam.
Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi fomu ambazo zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha
Alama za vidole zikichukuliwa na Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho.
Mhe.Jaji Francis Mutungi akipokea kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw.Ernest Moses Selelya.
CAPTIONS.do
Mwandikishaji Msaidizi Bi. Maida Ally Yusufu akimsainisha Jaji Mutungi fomu ambazo zimebeba taarifa zake kwa ajili ya kujiandikisha Leo katika kituo cha
Alama za vidole zikichukuliwa na Mwandikishaji Bw. Ernest Moses Selelya mara baada ya kukamilisha taratibu za ujazaji wa fomu ya utambulisho.
Mhe.Jaji Francis Mutungi akipokea kitambulisho cha mpiga kura kutoka kwa Mwandikishaji Bw.Ernest Moses Selelya.
Subscribe to:
Posts (Atom)