MALINZI AMPIGA STOP KIPA WA JKT RUVU KUCHEZA LIGI HADI AWASILISHE VIPIMO TFF

September 27, 2014

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
 RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameizuia klabu ya JKT Ruvu ya Pwani kumtumia kipa Jackson Abraham Chove hadi hapo itakapowasilisha vipimo kwamba hana madhara kichwani baada ya kuumia katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanania Bara mwishoni mwa wiki. Chove au Mandanda, alipata dhoruba kichwani katika mechi dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kupoteza fahamu kwa zaidi ya dakika ya 10, Jumamosi timu hizo zikitoka 0-0- lakini tayari amekwishaanza mazoezi kwa ajili ya mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Jumapili. Akizungumza mchana wa leo wakati wa kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya soka vya wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara, Malinzi amesema amefanya hivyo kufuata mwongozo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). “FIFA inasema mchezaji akipata pigo la kichwani mchezoni, anatakiwa apimwe na kuthibitishwa hajapata maumivu ya hatari, ndipo aruhusiwe kuendelea kucheza, ili kuepuka kuhatarisha usalama wake,” amesema Malinzi.
Papa Mandanda; Kipa Jackson Chove amezuiwa kucheza hadi hapo atakapowasilisha vipimo TFF 
“Sasa nami nimeagiza yule kipa wa JKT Ruvu aliyeumia kichwani kwenye mechi na JKT asiruhusiwe kucheza, hadi klabu yake itakapowasilisha ripoti ya vipimo vyake TFF na kuthibitishwa na TASMA (Chama cha Madaktari wa Michezo Tanzania) kwamba yuko salama ndipo ataruhusiwa kucheza,”aliongeza Malinzi.
Kwa upande wake, Meneja wa JKT Ruvu, Sajini Taji Constantine Masanja amesema kwamba hawajapata taarifa ya maandishi kutoka TFF, hivyo wanashindwa waanzie wapi kutekeleza hilo.
“Huyu mchezaji kweli aliumia kwenye mchezo huo, lakini hayakuwa maumivu makubwa amepimwa na kuonekana yuko fiti na tayari ameanza mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao,”amesema.
Hafla ya kufunga mafunzo hayo imefanyika leo asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mtanzania Henry Tandau.

SIMBA WANAWEZA KUIFUNGA POLISI MORO LEO….LAKINI WASIINGIE KICHWA-KICHWA

September 27, 2014


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SIMBA SC inawakosa wachezaji wanne muhimu katika mechi yake ya pili, ligi kuu soka Tanzania bara inayopigwa leo jioni dimba la Taifa, Dar es salaam dhidi ya Maafande wa Polisi Morogoro.
Wachezaji hao ambao kocha Patrick Phiri atawakosa ni kipa namba moja, Ivo Philip Mapunda, beki wa kushoto, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Winga hatari Haroun Chanongo na Mshambuliaji Paul Kiongera , wote ni majeruhi.
Mechi ya ufunguzi wikiendi iliyopita ambayo Simba ililazimishwa sare ya 2-2 na Wagosi wa Kaya, Coastal Union katika uwanja huo wa Taifa, Issa Rashid pekee ndiye hakucheza kati ya wachezaji hao wanne.
Ivo alisimama langoni na alifanya jitihada kubwa kuisaidia timu yake ipate ushindi, lakini hakufanikiwa kufuatia kuruhusu nyavu zake kuguswa mara mbili.

EVELYN BAASA NDIYE MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014

September 27, 2014


 
Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.
 Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangzwa kwa matokeo hayo.
 Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014
Father Kidevu, Arusha
Mlimbwende Evelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na kutwaa taji la  Miss Photogenic 2014.

Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.

Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika mapema mwezi ujao.

Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wadau wa masuala ya urembo  wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Majaji waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habarileo, Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa Itifaki Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la Redd's Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa.
Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole Sarakikya, Lilian Timothy na Lilian Kamazima.

Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model katika shindano litakalofanyika Triple A jijini Arusha.

KINANA ZIARANI WILAYANI KOROGWE MKOANI TANGA

September 27, 2014

 Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni,kulia ni Mbunge wa Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani ,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya siku moja katika wilaya ya Korogwe Vijijini ambapo licha ya kukagua miradi mbali mbali ya ujenzi wa maabara na ofisi za CCM alipata nafasi ya kuwahutubia wananchi na kuwasikiliza  .

  Katibu  Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Ueneziwakinunua matunda kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara Mombo.


 Diwani wa kata ya Mombo akishangiia baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kutamka wazi kuwa katika kuhakikisha wanapata halmashauri ya mji mdogo.
 Mama akiwa amembeba mwana ili awaone viongozi wake vizuri kwenye uwanja wa mikutano Mombo ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alihutubia.
 Wananchi wakiwa wamekaa kwa shauku ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahan Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapungia watu wakati wa kuwasili kwenye uwanja wa mikutano mjini Mombo akiwa pamoja  na Katibu wa NEC Itikadi Nape Nnauye
 Katibu Mkuu akiwapugia watu waliojazana kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mombo
 Umati wa wakazi wa Mombo uliojitokeza kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mombo ambapo aliwaambia wananchi hao wanachofanya wapinzani ni biashara, kwani kwao kuandamanisha watu ni mtaji mzuri wa kuwaingizia pesa kutoka nje.

 Umati wa watu ukimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Aisha Kigoda pamoja na Mjumbe wa NEC wa Wilaya ya Korogwe Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tanga Dk. Edmund Mdolwa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mombo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mombo.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Kinana mjini Mbombo
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa kwenye kiti tayari kupokea zawadi kutoka kwa wamasai wanaoishi Mombo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi kutoka kwa wamasai wa Mombo.
 Katibu wa CCM Ndugu Abdulrahman akipeana mkono wa shukrani kwa kiongozi wa wamasai wa Mbombo Samng'o Maikaambaye [ia ni mwenyekiti wa Tawi la Chang'ombe ,Mombo.

DKT BILALI AZINDUA Kivuko Kipya cha MV Tegemeo jijini Mwanza

September 27, 2014


 Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kivuko hicho kipya cha MV Tegemeo.
 Kivuko kipya na chakisasa cha MV Tegemeo kama kinavyoonekana, kimetengenezwa kama mfano wa Meli kutokana na huduma zake.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akimuonesha Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal jinsi kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakavyofanya kazi.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Marceline Magesa akimuonesha Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal baadhi ya sehemu ndani ya Kivuko hicho kipya.
 Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal  akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutoka kukagua sehemu ya kuendeshea kivuko hicho
 Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia ngoma iliyokuwa ikichezwa ndani ya kivuko hicho kipya.
 Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kushoto akifurahia jambo na  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Dkt Charles Tizeba  kabla ya uzinduzi wa Kivuko cha MV Tegemeo.
 Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kulia akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiwa njiani ndani ya Kivuko cha MV Misungwi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za ufunguzi wa kivuko kipya cha MV Tegemeo.
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akimsikiliza Mbunge wa Buchosa na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba  wakati wa  Uzinduzi. 
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kivuko kipya cha MV Tegemeo kitakachotoa huduma kati ya Kahunda hadi kisiwa cha Maisome katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza. Wengine walioshikilia utepe ni pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mbunge wa Buchosa Dkt Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Ujenzi