ZIARA YA BODI KATIKA MRADI WA MAJI NZUGUNI, DODOMA

August 04, 2023

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (wanne kushoto) akiwa na wajumbe wa bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)

MAFUNDI kutoka kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakiendelea na kazi ya kumwaga zege katika ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika Mradi wa maji wa Nzuguni jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)
MAFUNDI kutoka kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakiendelea na kazi ya kumwaga zege katika ujenzi wa tanki la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika Mradi wa maji wa Nzuguni jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (kulia) akiwa na wajumbe wa bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkandarasi Noel Lukuwi kutoka Kampuni ya Kandarasi ya Help Desk wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Balozi Job Masima (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo ya ramani kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph wakati bodi na menejimenti ya Mamlaka hiyo ilipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa maji Nzuguni jijini Dodoma jana. (Picha na Mpigapicha Wetu)



 

DK.KIJAJI ATAKA WENYE VIWANDA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA

August 04, 2023

 WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amevitaka viwanda vyote nchini kutengeneza  bidhaa zenye ubora  kwa gharama nafuu  ili ziweze kuingia katika soko  Eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA)

Ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji  wa maziwa  na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo. 

 "Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wafanyabiashara na wawekezaji  wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa, " amesema.

Pia amesema Serikali ya Dkt Samia nikuona wafugaji wanabadilika kutoka katika ufugaji wa kienyeji kwenda  katika uwekezaji  wa kisasa  ili  kukidhi mahitaji ya soko.

Aidha amepongeza kiwanda hicho kwa ajira walizotoa hapa nchini na ametaka  ajirasizizo za moja kwa moja  ziongezeke.