KUMBE UNGA WA MUHOGO HUTENGENEZEA KIWASHIO MOTO CHA KIBIRITI?!!!

December 12, 2017

Uongozi wa Mkikita ukiwa na uongozi wa kiwanda cha Unga cha Ukaya, Mkuranga, Pwani, ulipotembelea kiwanda hicho ambacho wako mbioni kuingia mkataba wa kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga wa kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi wa Kiwanda, Ibrahim, Meneja wa Kiwanda, Matanga na Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange.




Na Richard Mwaikenda, Mkuranga

UNGA wa muhogo unatumika kutengenezea kishungi cha kuwashia moto katika vibiriti.

Jambo hilo lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha kusaga muhogo cha Ukaya, Mkuranga, Ibrahim mbele ya uongozi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) uliotembelea kiwanda hicho.

Alisema kuwa miongoni mwa wateja wakubwa wa unga wao ni Kiwanda cha kutengenezea vibiriti cha Kasuku kinachoutumia kwa kutengenezea kishungi cheusi cha njiti ya kibiriti kinachotumika kuwasha moto.

Uongozi wa Mkikita ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui S. Kissui na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange ulitembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuingia nao mkataba wa makubaliano ya kukitumia kusaga mihogo ya wanachama wao kupata unga utakaouzwa na katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ibrahim alisema unga pia hutumika kutengenezea dawa ya kuzuia kuhara, pombe, mafuta, chakula cha wanyama na binadamu.


Imeandaliwa na Richard Mwaikenda;Kamanda wa Matukio Blog 0715-264202

OFISI NZIMA YA MKIKITA WAHAMIA SHAMBANI VIKINDU KUPANDA MCHAICHAI

December 12, 2017

Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui S. Kissui wakibeba miche ya mchaichai wakipeleka kupanda shambani Vikindu. Shmba hilo ni la wanachama wa Mkikita. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akiwa amebeba mbolea akipeleka shambani.

Na Richard Mwaikenda
OFISI nzima ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen), umehamia shamba Vikindu kuanza kampeni ya kupanda mchaichai.

Katika kampeni hiyo ya aina yake iliwashirikisha wakurugenzi, maofisa na wafanyakazi wa mtandao huo ili kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Back to The Land.

Walipofika Block Farming hiyo ya mchaichai, waligawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wengine kazi yao ilikuwa kubeba mbegu ya mchaichai, baadhi walisombelea mbolea, kufyeka majani, kuchanganya mbolea kwenye mashimo na wengine kupanda.

Kazi hiyo ilipamba moto hasa baada ya kuhamasishwa na viongozi wakuu ambao pia walishiriki bega kwa bega kubeba mbolea, mbegu na kupanda pia. Hakuna aliyeruhusiwa kukaa bila kazi akiwemo pia mwandishi wa habari hizi, Richard Mwaikenda.

Viongozi walioshiriki kwenye kampeni hiyo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Dk. Kissui S. Kissui, Mkurugenzi Mtendaji,  Adam Ngamange, Mkurugenzi wa Utawala na Mashamba, Catherina, Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth na Mhasibu Mkuu wa mtandao huo, Mshashu na msaidizi wake Samson.

Ofisi kwa siku nzima ilibidi zifungwe kwa siku nzima, ambapo walifanya kazi ya shamba kwa siku nzima ya jana hadi majira ya saa jioni saa 12.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akishiriki kupanda mchaichai
Mkurugenzi wa Fedha wa Mkikita, Elizabeth akipanda mchaichai wakati wa kampeni hiyo
Wafanyakazi wa Mkikita wakiwa wamebeba mbolea ya kupandia mchaichai
Meneja Uhusiano wa Mkikita, Neema (kulia0 akiwa na Ofisa wa Mradi wa Kuku, Rose wakati wa shughuli ya kupanda mchaichai
Adam akibeba mbolea kupeleka shambani
Dk. Kissui akiwa amebeba miche akipeleka shambani
Eva akifanya usafi kwenye shamba tayari kupanda mchaichai
Wakichambua miche ya mchaichai
Catherina akishiriki vilivyo kwenye shamba hilo
Adam akichambua miche ya mchaichai
Meneja wa Kijaicos, Mishomari akisafisha shmba
Kazi ikiendelea
Mhasibu Mkuu, Mshahu akishiriki katika kampeni ya upandaji wa mchaichai
Ni kazi tu
Mkurugenzi wa Fedha, Elizabeth akisaidiana na Matrida
Mhasibu Mkuu msaidizi, Samson akishiriki kusafisha shamba
Hakuna kulala, Mkurugenzi wa mashamba, Catherina akiwa kazini
Sehemu ya shamba lililopandwa mchaichai
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mkikita, Dk Kissui (kulia) akiwapongeza wafanyakazi kwa moyo wao wao wa kujitolea kupanda mchaichai

RATIBA RAUNDI YA PILI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM

December 12, 2017
Baada ya droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup - ASFC), kukamilika Jumatano Desemba 06, 2017 kwenye Studio za Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichopo Tabata relini, Dar es Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa ratiba rasmi ya mechi hizo za raundi ya pili.

Kwa mujibu wa TFF, michuano hiyo imepangwa kucheza kwa siku tano ambazo ni Desemba 20, 21, 22, 23 na 24. Mchezo kati ya Simba na Green Warriors utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.

Ratiba hiyo iliyotolewa leo Desemba 12, 2017  inaonesha michezo ya Desemba 20, mwaka huu itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador na JKT Oljoro; Boma FC na Ndanda; Mvuvumwa na JKT Ruvu; Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita. 

Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.

Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.

Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.

Desemba 24, 2017 Young Africans itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI MJINI DODOMA LEO

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI MJINI DODOMA LEO

December 12, 2017
w20
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w21
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Generali John Julius Mbungo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w22
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kaongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo (kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w23
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndg. Kheri James baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w26
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w25
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Balozi Job Lusinde baada ya Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
w27
Wake wa viongozi kutoka kushoto Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mama Mary Majaliwa na Mama Bulembo wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017. 
28
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmana Kinana akiwa na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
29
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia zawadi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi aliyemaliza muda wake Alhaj Abdallah Majura Bulembo wakati wa ufunguzi wa  Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
30
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mhe. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mhe. Maalim Seif wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.
31
Wajumbe wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wazazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma leo Desemba 12, 2017.

PICHA NA IKULU

KIKAO CHA KUJADILI HALI YA USALAMA BARABARANI NCHINI CHAFANA MJINI DODOMA

December 12, 2017
Na WAMJW - Dodoma 
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji unaofuata taratibu na sheria za barabarani.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania  Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani  unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali 
Kamanda Mselemu alisema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote  ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi  wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili  na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike  na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri.
Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati  na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda  miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 ilikua 639, vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376, vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye  Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia  Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo  zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni  vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.
 Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu aliyesimama akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Mary Kessy akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 ASP Deus Sokoni wa kwanza kulia akiongea na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Wizara ya Mambo ya Ndani  Bi. Marlin Komba  anayefuata ni Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu.
 Katibu Mkuu wa Shirikishi wa vyama vya Walemu nchini Bw. Felicina Mkude aliyesimama akiongea na baadhi ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  hawapo pichani wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Baadhi  ya wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakimsikiliza kwa makini Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu hayupo pichani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Nchini SACP Fortunatus Musilimu katikati waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani  wakati wa kikao cha kujadili hali ya usalama barabarani nchini kilichofanyika leo mjini Dodoma.
KAMPUNI YA MOHAMED ENTERPRISES YASHINDA TUZO NNE ZA ATE 2017

KAMPUNI YA MOHAMED ENTERPRISES YASHINDA TUZO NNE ZA ATE 2017

December 12, 2017
  Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) imeshinda tuzo nne za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 (EYA) zinazotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), katika hafla ya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. MeTL imeshinda tuzo hizo kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Mo Assurance Limited iliyoshinda kipengele cha Tuzo ya Kampuni Ndogo, 21st Century Holding Limited imeshinda nafasi ya pili ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani na Star Oil Tanzania Limited imeshinda tuzo mbili, Tuzo ya Kampuni ya Kati na nafasi ya tatu ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Ndani. Ushindi huo wa tuzo nne, umeiwezesha MeTL Group kuwa moja ya kampuni nne ambazo zimeshinda tuzo nyingi za ATE 2017, na kuwa kampuni ya kizalendo ambayo imeshinda tuzo nyingi kuliko kampuni zingine ambazo zimeshiriki katika tuzo hizo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Royal Soap, Jackline Mbaga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya Star Oil Tanzania Limited , Ester Dotto, Meneja Mkuu wa Mo Assurance Limited, Kura Bonniface, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Hassan Dewji, Meneja Mauzo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Holding Limited, David Mziray, Ofisa wa kitengo cha Rasilimali Watu wa Mohammed Enterprises, Jessica Julius, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Textiles, Godfrey Ndimbo na Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu wa kampuni ya 21st Century Food and Packaging, Anna Zongo wakiwa na tuzo nne ambazo wameshinda kwenye tuzo za ATE 2017.
Akizungumza kuhusu ushindi huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MeTL Group, Hassan Dewji, alisema wamefurahishwa na ushindi huo, lakini pia unaonyesha jinsi gani kampuni inafanya vizuri katika soko la hapa nchini. "Tuna furaha kushiriki kwenye tuzo za ATE 2017 na tuna furaha kushinda tuzo nne, naamini tumekuwa moja ya kampuni tano ambazo zimeshinda tuzo nyingi. Nafikiri sisi ni moja ya kampuni kubwa nchini na tunaendelea kukua na kugusa maisha ya watu wengi kila siku, ushindi kama huu utuwezesha kuongeza juhudi zaidi," alisema Dewji.

RC MBEYA MHE. AMOS MAKALA AFUNGUA MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYORATIBIWA NA WCF

December 12, 2017



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mbeya

TAKRIBAN madaktari na watoa huduma za afya 100 kutoka mikoa saba ya Kanada ya Nyanda za Juu Kusini, wameanza kupatiwa mafunzo jijini Mbeya yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF).

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku tano yaliyofunguliwa rasmi Desemba 12, 2017 (jana) NA Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, alisema, mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya ili kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini ya ulemavu maradhi anayopata mfanyakazi wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi ili hatimaye madaktari hao waweze kutoa mapendekezo kuwezesha mfuko kutoa mafao ya fidia stahiki.

Kwa mujibu wa mratibu wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, mafunzo hayo yamewaleta pamoja madaktari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Katavi, Rukwa, Iringa, Njombe na Ruvuma.

Katika hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sheria, alisema Bw. Mshomba.

“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huu ni kutoa fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyepatwa na majeraha, maradhi kutokana na kutekeleza wajibu wake awapo kazini, lakini pia kuwalipa fidia wategemezi wake anapofariki katika mazingira hayo.” Alifafanua Bw. Mshomba na kuongeza, WCF ilianza kutekeleza majukumu yake Julai Mosi, 2015 na mwaka uliofuata Mfuko ulianza rasmi kupokea madai ya fidia na kulipa mafao kwa waathirika.

Wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa WCF jijini Arusha mwishoni mwa mwezi uliopita, kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, aliitaka WCF kuendelea kutoa elimu kwa wadau, ili waweze kuelewa vema shughuli za Mfuko na nia njema ya serikali ya kuanzisha mfuko huo ili mfanyakazi wa Tanzania aweze kupata fidia stahiki anapopata madhara sehemu ya kazi.

Bw, Mshomba aliishukuru Serikali na Wizara zake kwa kuunga mkono na kusaidia juhudi za WCF katika kuimarisha mifumo yake ili kutoa huduma bora kwa wadau wake.“Pia napenda nizishukuru taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili, MOI, Ocea Road Hospital, MUHAS, na OSHA kwa kuwaruhusu wataalamu wake ili tuwatumie katika kutoa mafunzo haya.” Alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, alisema, juhudi za ushirikiano wa pamoja miongoni mwa wadau yaani Serikali, Wafanyakazi, Waajiri unahitajika sana kuhakikisha tathmini endelevu ili kuimarisha mfuko. 

“Nimeambiwa mafunzo haya yataongeza uelewa katika kufanya tathmini na uchunguzi wa majeraha au maradhi anayoyapata mfanyakazi mahala pa kazi na kutoa mapendekezo stahiki kwa uamuzi wa mwisho.” Mkuu wa Mkoa pia alipongeza juhudi za WCF kwa kuendesha mafunzo hayo ambayo yatawezesha kupanua wigo wa mtandao wa watoa huduma za afya na hospitali 

“Katika mwaka wa fedha wa 2015/2016 naambiwa mlianza kutoa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya wapatao 359, katika wailaya zote za Tanzania Bara mafunzo mliyoyaendesha katika kanda nne za Pwani, kanda ya Ziwa, kanda ya Kaskazini, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na mwaka uliofuata mkatoa mafunzo kwa madaktari wapatao 145 katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza na kufanya idadi ya jumla hadi sasa ya madaktari na watoa huduma za afya ambao mmewapatia mafunzo kufikia 504, napenda kuipongeza Bodi ya Wadhamini na uongozi wa Mfuko kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alimaliza Mkuu wa Mkoa Bw. Amos Makala. 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, akihutubia wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfukom wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba ya ukaribisho kweye ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo Desemba 12, 2017. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF, yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali pa kazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makala, na Mkurugenzi wa Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Mshiriki akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Dkt. Ali Mtulia(kushoto) kutoka WCF, na wawezeshaji wakifuatilia hotuba hiyo.
Washiriki wakifuatilia hotuba kwa umakini.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge, akiwa makini kufuatilia hotuba.
Sekretariat ya WCF ikiwa kwenye majadiliano ili kuhakikisha mafunzo yanakwenda kwa ufasaha. Kutoka kushoto ni Dkt. Pascal Magesa, Bw.Vincent Steven, Bi. Laura Kunenge, na Bi.Innocencia William.
Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya (kulia na maafisa wengine wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Bw. Mshomba akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala wakati akihutubia madaktari.
Mhe. Makala, akionyesha kitu, akiwa Bw. Mshomba
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Picha ya pamoja kundi la kwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makala, (kushoto), akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (kushoto) mara baada ya kutoa hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutoka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo jana (Desemba 12, 2017). Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu au ugonjwa mahali npa kazi. Mafunzo hayo yanafanyika jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makala, (kulia), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bw. Masha Mshomba, baada ya ufunguzi rasmoi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari wanaofikia 100 kutka mikoa saba ya kanda ya nyanda za juu Kusini, kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa, jijini humo. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na WCF yanalenga kuwajengea uwezo madaktari na watoa huduma za afya kufanya tahmini ya mfanyakazi aliyepata ulemavu unaotokana na ajali au magonjwa mahala pa kazi