Rais Dkt.Magufuli afanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato

Rais Dkt.Magufuli afanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato

January 09, 2017

chato chato-2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na  kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.
chato-3 chato-4 chato-5
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.
…………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 9 Januari, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Msingi Chato,ambapo ndipo aliposoma kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo.
Rais Dkt Magufuli ameahidi kujenga madarasa matatu na ofisi moja ya walimu katika Shule hiyo kufuatia ombi la Walimu kuwa shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Aidha Dkt.Magufuli amewaasa wanafunzi kutilia mkazo masomo ili waweze kufaulu na kuwataka walimu kuhakikisha wanatumia vyema fedha zinazotolewa na Serikali kila mwezi katika kutoa elimu bila malipo na pasiwe na wanafunzi hewa kama ilivyo kwa baadhi ya shule ambazo zimegundulika kuwa na wanafunzi hewa katika uhakiki uliofanywa na serikali.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chato, Bwana Mwita Chacha amemshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa msaada aliowapatia katika kukabiliana na uhaba wa madarasa uliokuwa unaikumba shule hiyo, pia kuitembelea Shule yao jambo ambalo limewatia moyo walimu na wanafunzi shuleni hapo.
Rais Magufuli pia ametembelea eneo la Stand ya zamani na kuzungumza na baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo hilo na kutoa msaada kwa kikundi cha wasafisha viatu ili kuongeza mtaji wa biashara yao.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato, Geita.
9 Januari, 2017

WATAKAOZIDISHA NAULIABIRI KUKIONA-SUMATRA TANGA.

January 09, 2017
MAMLAKA ya Usimamizi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Tanga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wameanza operesheni maalumu kwa madereva wanaozidisha abiria na nauli kwenye mabasi yanayotoka  mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kaskazini.

Hatua inafuatia idadi kubwa ya abiria ambao wanatoka mikoa hiyo kurejea mkoani Tanga na maeneo mengine hivyo baadhi ya mabasi wanapandisha nauli kiholea na kuzidisha abiria.

Hayo yalisemwa na Ofisa Sumatra Mkoani Tanga, Dkt Walukani
Luhamba (Pichani Juu) wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema waliamua operesheni hiyo ili kuweza kudhibiti masuala hayo ambayo yamekuwa yakiwapa wakati mgumu wananchi wanaotumia vyombo hivyo kwa ajili ya matumizi yao.

Operesheni hiyo inafanyika kwenye maeneo ya Mombo,Korogwe, Mkata na Segera ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuweza kuikomesha kwa madereva wenye tabia kama hiyo.

Dkt Walukani alisema katika kuhakikisha wanazibiti operesheni hiyo hivi sasa wanamshikilia dereva wa basi la Hood Issa Kayela (30) linalofanya safari zake kutoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kosa la kuzidisha abiria zaidi ya idadi aliyotakiwa kubeba.

Alilitaja basi hilo lilikuwa na namba za usajili T.779 AVL Scania aina ya Torino lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Mbeya ambapo baada ya kumkamata walimpelekwa mahakamani na baada ya kufika huko akukosa dhamana amerudishwa mahabusu na baade ya wiki mbili anatarajiwa kupandishwa kizimbani.

Akizungumza hatua inayofuata,Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo kukaa kwenye kituo hicho kutokana na kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.

“Ukiangalia basi hilo la hood lilikuwa linapaswa kupakia abiria 51 lakini lilipokamatwa eneo la mkata wilayani Handeni  lilikuwa na abiri 80 jambo ambalo ni hatari sana “Alisema.

 “Kutokana na hali hiyo dereva wa basi hilo alipelekwa mahakamani na alikosa dhamani na hivi sasa anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Mkata kwa ajili ya kufikishwa mahakamani na ikithibitisha ana kosa basi atalazimika kwenda Jela mwaka mmoja au miwili hii itakuwa fundisho kwa madereva wengine wenye tabia kama hii “Alisema.

Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo alikaa kwenye kituo hicho baada ya kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.

Naye kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani   Tanga, Nassoro Sisiwayah alisema operesheni hiyo itakuwa endelevu kwa kufanyika kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ikiwemo Mombo, Korogwe, Mkata na Segera lengo kubwa kuhakikisha sheria za usafirishaji zinafuatwa.

Alisema katika operesheni hiyo wanazibiti nauli kwenye mabasi y mikoani ambayo hivi sasa kwa asilimia kubwa watu wengi wanarudi kutoka mikoa ya kaskazini ambapo ulanguzi wa nauli umekuwa ukitumika.

SIMBA YAJIPELEKA MIKONONI MWA YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI,JUMANNE SAA MBILI USIKU ZANZIBAR KUTIKISIKA

SIMBA YAJIPELEKA MIKONONI MWA YANGA NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI,JUMANNE SAA MBILI USIKU ZANZIBAR KUTIKISIKA

January 09, 2017
ngoma-vs-juuko
Na.Alex Mathias.
Ushindi wa tatu wa Simba katika Michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar yameifanya ifikishe jumla ya pointi 10 na kuongoza kundi A na sasa itakutana na watani wao jadi Yanga Mchezo wa Nusu Fainali itakayopigwa siku ya Jumanne kwenye uwanja wa Amaan baada ya kuwatandika Jang’ombe boys magoli 2-0.
Simba waliuanza mchezo kwa kasi ya 4G huku Shiva Kichuya akiwatesa mabeki wa Jang’ombe boys na katika dakika ya 11 Laudit Mavugo aliwanyanyua mashabiki waliokuwa wamefurika akimalizia kazi nzuri ya Kichuya na mashabiki kulipuka shangwe kwa kusema kuwa tunaitaka Yanga Nusu fainali.
Hadi mwamuzi Mfaume Nassoro anapuliza kipyenga cha Mapumziko Simba walikuwa mbele kwa ushindi wa bao hilo moja la mshambuliaji Raia wa Burundi ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kushindwa kuonesha kiwango cha hali ya juu kwa mashabiki wa Simba.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko hata hivyo Simba waliendelea kuumiliki mchezo huo na kuweza kupata bao la pili dakika ya 53 kupitia kwa Laudit Mavugo aliyeachia bonge la shuti na kujaa moja kwa moja golini huku shangwe za mashabiki wa Simba zikisema kiama kwa Yanga siku ya Jumanne ya Januari 10.
Hadi dakika 90 za mwamuzi Mfaume Nassoro ubao ulikuwa ukisomeka Simba 2-0 dhidi ya Jang’ombe boys iliyokuwa chini ya Mchezaji wa zamani wa Yanga Abdi Kassim na kuwafanya Jang’ombe wayaage mashindano hayo wakiwa na pointi zao 6.
Kwa matokeo hayo Simba itacheza na Yanga siku ya Jumanne saa mbili usiku mchezo wa Nusu Fainali  ambao unategemewa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na historia ya ikumbukwe mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1.
Yanga wanaingia Nusu Fainali na kumbukumbu ya kuunganisha kifurushi cha 4G toka kwa matajiri wa jij la Dar es salaam timu ya Azam FC ambao waliwadhalilisha kwa kipigo cha magoli 4-0 na tayari kamati ya mashindano imetaja viingilio vya mechi hiyo huku kiingilio cha chini kabisa ni cha sh elfu tatu na cha juu elfu kumi.
Mchezo wa pili utachezwa saa mbili na robo kati ya Taifa Jang’ombe dhidi ya Mabingwa watetezi URA toka Uganda na mshindi wa hapa atakutana na Azam FC Nusu Fainali ya kombe la Mapinduzi.
MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA AMRI KUHUSU KUPOKEA, KUINGIZA, KUIHAMISHA, KUSAFIRISHA NA KUPITISHA MIFUGO NDANI YA MKOA WA RUKWA

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA AMRI KUHUSU KUPOKEA, KUINGIZA, KUIHAMISHA, KUSAFIRISHA NA KUPITISHA MIFUGO NDANI YA MKOA WA RUKWA

January 09, 2017
musoma
Mkuu wa mko wa Rukwa kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakuu wa Wilaya kutokubali kupokea mifugo kutoka katika wilaya nyingine bila ya mifugo hiyo kuipa kibali maalum cha kuhamia katika wilaya zao.
Ameyasema hayo katika amri halali namba 1/2017 kuhusu kupokea, kuingiza, kuihamisha, kusafirisha na kupitisha mifugo ndani ya mkoa wa rukwa kwa mamlaka aliyopewa na kifungu cha 7 cha sheria Nambari 19 ya mwaka 1997 ya Tawala za Mikoa Sura Namba 97 mapitio ya mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia na kutekeleza maagizo ya waraka wa Rais Na. 1 wa mwaka 2002 unaokataza kabisa usafirihaji kiholela wa mifugo.
“Mifugo isihamishwe kutoka katika Kijiji, Wilaya ama Mkoa kabla ya kupata kibali cha Kijiji, Wilaya ama Mkoa inakopelekwa. Hivyo Kijiji, Wilaya na Mkoa itatoa kwanza idhini ya kupokea mifugo hiyo ndipo kibali cha kusafirisha mifugo kitolewe,” Zelote Stephen alisema.
Zelote Stephen alisisitiza kuwa Vijiji, Wilaya na Mkoa usitoe vibali vya kupokea mifugo kabla ya kujiridhisha kwamba wanayo maeneo ya kutosha ya malisho ya mifugo, yaliyopimwa na kuthibitishwa na wataalamu kama yanafaa kwa malisho na maji ya kutosha na majosho ya kuoshea mifugo.
Vile vile Mkuu wa Mkoa aliwaagiga maafisa mifugo kuanzia ngazi ya Kijiji, Wilaya na Mkoa kusisimamia na kuhakikisha hakuna mifugo inayosafirishwa kutoka Kijiji, Wilaya na Mkoa kwenda Mkoa mwingine au kuingia katika Kijiji, Wilaya au Mkoa bila ya kupimwa na kuchanjwa chanjo lengo likiwa ni kuthibiti uenezaji wa magonjwa ya mifugo nchini.
“Kabla ya kutoa vibali vya kusafirisha mifugo, madaktari wa mifugo wa Wilaya ama wawakilishi wao wahakikishe kwamba mifugo inaogeshwa na kuchanjwa dawa za kuzuia magonjwa husika kabla ya kuiruhusu mifugo hiyo kusafirishwa ili kuzuia uenezaji wa magonjwa ya mifugo,” Zelote Stephen alifafanua.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewatahadharisha maafisa mifugo ambao sio waaminifu wanaotumia njia ya kuingiza mifugo kwenye wilaya kwa njia ya biashara za minada na matokeo yake mifugo hiyo kubaki eneo husika bila ya kufuata taratibu zozote.
Amri hii itafanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe 9 January, 2017 hadi tarehe 31 Desemba, 2017.

MVUA YAWAATHIRI WANANCHI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

January 09, 2017
 Mkazi wa Kijiji cha Ndubi kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Julius Mwambola (kulia), akionyesha migomba iliyoangushwa kutokana na mvua iliyonyesha wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni mke wake Nabwike Swebe.

VIDEO: VITUKO VYA USWAHILINI AVAA DERA LA MKEWE BAADA YA KUPIGIWA SIMU YA HELA!

January 09, 2017
Uswahilini ni sehemu ambayo inaongoza kwa vituko, ugomvi na maneno ya shombo. Wahenga  walisema kuishi kwingi ndio kuona mengi,  Haraka Haraka haina baraka  hii misemo inamaanaisha ukiishi sehemu tofauti tofauti utaona vitu vingi na kujifunza pia. Haraka haraka haina baraka hii imebeba maana ya kwamba ukienda haraka unaweza kukosea au kusahau kitu muhimu.
Tumia dakika zako chache kuitazma short video, ya uswahilini iliyo chezwa na Vicent Petro (Mr.Kilaka) Husina, Moses & Ziada Mgwassa (Zaydar). Endelea kusapport sanaa ya Tanzania tunaamini bila wewe hatuwezi fika popote thanks. Kwa maelezo na taarifa yeyote wasiliana nasi kwenye 0658161950.