MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB BANK DKT CHARLES KIMEI ATUNUKIWA TUZO NA AFRICAN LEADERSHIP, NEW YORK NCHINI MAREKANI

September 23, 2016
 
Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014  katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akifuatilia hafla ya utoaji tuzo kwa viongozi wa Afrika iliyofanyika siku ya Alhamisi Sepemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis New York. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akielezea mafanikio na utendaji wa benki ya CRDB na jinsi gani inavyowawezesha wawekezaji wazawa kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu katika kusaidia kuinua uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei akitunukiwa tuzo na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 kushoto ni Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akisalimiana na Rais wa Malawi Mhe. Prof. Arthur Peter Mutharika mara tu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei kupokea tuzo iliyotolewa na African Leadership siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 katika hotel ya St. Regis, New York. kulia ni fisrt lady Mke wa Rais wa malawi.
 Picha ya pamoja.
 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa fedha wa benki ya CRDB, Bwn. Frederick  Nshekanabo, Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt Charles Kimei alipokua akifanyiwa mahaojiano mara tu baada ya kupokea tuzo kutoka African Leadership katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016.

 Mkurugenzi wa masoko, utafiti na huduma kwa wateja, Bi. Tully Esther Mwambapa akifuatilia sherehe ya Tuzo kutoka kwa African Leadership iliyofanyika katika hotel ya St. Regis, New York siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016. Kulia ni Rais wa Burkina Faso, Mhe. Roch Marc Christian Kabore.


Hapa ni siku Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, alipomkabidhi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya nne  Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo katika sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014

Utafiti: Misitu na mazingira vikisimamiwa ipasavyo vitaboresha maisha ya wananchi vijijini

September 23, 2016
Dr. Nicole Cross-Camp ambaye ni Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha East Anglia cha nchini Uingereza chini ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation) akitoa mada kuhusiana na matokeo ya utafiti kuhusu changamoto wanazozipata wanakijiji katika utunzaji wa misitu kwa wadau kutoka Wizara mbalimbali pamoja na Sekta binafsi.
Maneja Mradi, Lasima Nzao akiwasilisha matokeo ya utafiti uliopo chini ya mradi wa ESPA (Ecosystem Services for Poverty Alleviation). Mkutano huo ulifanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Mistu na Mazingira kutoka Serikalini, Taasisi na Mashirika binafsi walikutana na watafiti hao ili kujadili matokeo hayo ya utafiti na kuweza kuchanganua mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana na changamoto na faida zinazotokana na usimamizi wa misitu kwa wanajamii wanazozungukwa na hifadi ya misitu hapa Tanzania.

Akizungumza na Lasima Nzao na Dr Nicole Gross-Camp walisema kuwa utafiti huo uliofanyika katika vijiji nane vya wilaya mbili, halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini na wilaya ya Kilwa kuanzia Septemba 2014 na kumalizika september 2016 na ulikuwa "unaangalia mchango wa misitu inayosimamiwa na Jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maisha kwa wanakijiji husika". 

Utafiti unaonyesha  kuwa mistu na mazingira ikisimamiwa  ipasavyo inaweza kuboresha maisha ya wananchi walio vijijini kwa kuwa wanajamii wanapenda mfumo wa misitu ya jamii japokua bado kuna changamoto nyingi katika usimamizi wa misitu kwa wanajamii hasa misitu inayosimamiwa na Jamii.

Utafiti huo ulidhaminiwa na ESPA, UKAID, NERC na ESRC na ulifanywa na mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha East Anglia UEA nchini Uingereza Dr Nicole Gross-Camp akishirikiana na mtafiti kijana wa kitanzania, Lasima Nzao ambaye pia alikua meneja wa mradi wa Utafiti huo.
Mtafiti na Mshauri wa masuala ya Misitu, Kihana Lukumbuzya akichangia mada baada ya wataalamu kuwasilisha utafiti uliofanyika katika vijiji nane ndani ya wilaya mbili.
Mshauri wa masuala ya Misitu na Mabadiliko ya Tabianchi, Faustine Ninga akichangia mada kuhusu  utafiti uliofanyika katika wilaya mbili kuhusu mchango wa jamii (CBFM) katika kuboresha hali ya maishaya wanajamii.
 Gabriel Marite Ole Tuke
Msimamizi wa Maliasili kutoka Mkoani Dodoma, Sanford Kway akichangia mada
Picha ya pamoja
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA

Tigo yatoa simu 800 zenye thamani ya 120m kusaidia zoezi la kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa ya Njomba na Iringa.

September 23, 2016


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr Rehema Nchimbi mara baada ya kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, uzinduzi huo ulifanyika jana mjini Iringa.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.


Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akikabidhi cheti cha kuzaliwa kwa motto Christina Muyinga, mara baada ya kuzindua uandikishaji na utoaji wav yeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi hilo umefanyika jana mjini Iringa, zoezi hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Simuza mkononi ya Tigo ambayo imeipatipatia serikali simu 800 ili kufanikisha zoezi hilo linalofanywa kwa pamoja na RITA, Unicef, VSO na SIDA.

 Baadhi ya wakazi wa Iringa wakiwa katika foleni ya kusubiri kujiandikisha ili kupata vyeti vya kuzaliwa kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi hilo umefanyika jana mjini Iringa, zoezi hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Simuza mkononi ya Tigo ambayo imeipatipatia serikali simu 800 ili kufanikisha zoezi hilo linalofanywa kwa pamoja na RITA, Unicef, VSO na SIDA.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mkoa wa Iringa na viongozi wa  tigo  katika makabidhiano ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika jana mjini Iringa. 

WAZIRI MUHONGO AAGIZA UTAFITI WA KINA TETEMEKO KAGERA.

September 23, 2016


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ili kujadiliana kuhusiana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akielezea jambo wakati wa kikao na wataalamu wanaofanya utafiti wa tetemeko Mkoani Kagera (hawapo pichani).
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim  Mruma ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu wanaofanya utafiti wa tetemeko mkoani Kagera akionesha kitovu cha tetemeko hilo katika kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro kilomita 88 kutoka Bukoba mjini kupitia barabara ya Bukoba-Kyaka-Minziro.
 Baadhi ya nyumba katika kijiji cha Kampanji kilichopo Mpakani mwa Tanzania na Uganda ambazo zilibomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akikagua eneo lililokumbwa na Tetemeko na kusababisha mpasuko kwenye ardhi katika kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro ndani ya Kitongoji cha Bilongo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa ziara ya kukagua shughuli za utafiti wa tetemeko zinazofanywa na timu wataalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa GST, Profesa Abdulkarim Mruma ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu hao.

Wataalam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)  na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanaofanya utafiti wa tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba, mwaka huu mkoani Kagera, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanafanya utafiti wa kina ili kubaini namna ambavyo miamba ya maeneo husika ilivyo na vilevile kuandaa ramani mpya ya miamba katika maeneo yatakayotafitiwa.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kukagua shughuli za utafiti wa tetemeko zinazoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo.

Alisema kuwa, utafiti huo utachukua muda mrefu kwani hautafanyika mkoani Kagera pekee bali utafanyika pia  katika Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Dodoma na baadaye nchi nzima.
Katika ziara hiyo, Waziri Muhongo aliwaagiza wataalam hao kuhakikisha wanatoa mafunzo ya awali kwa umma hususan kwenye maeneo yaliyoathiriwa zaidi na tetemeko ili waelewe nini wanapaswa kufanya endapo tetemeko litatokea.

Aliagiza elimu hiyo ianze kutolewa siku ya Jumamosi, tarehe 24/9/2016 Saa 4 Asubuhi, huku wakiandaa ratiba ya mafunzo hayo kwa maeneo mengine na kuandaa vipeperushi vyenye maelezo ya kutosha  kuhusu Tetemeko la Ardhi kwa ajili ya kuwasambazia wananchi.

Aidha, Profesa Muhongo aliwaagiza wataalam hao, kuepuka kutoa kauli zinazokinzana  ili kuepusha kuwachanganya na kuwaletea hofu wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo na kueleza kuwa Msemaji Mkuu wa wataalam hao wanaofanya utafiti husika ni Mtendaji Mkuu wa GST, ambaye yupo mkoani humo akishirikiana na wataalam kufanya utafiti.

Mbali na hilo, Profesa Muhongo aliagiza kuwa, ujengwe mnara maalum katika eneo ambalo tetemeko hilo lilianzia huko katika kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro, kilomita 88 kutoka Bukoba mjini ili iwe kumbukumbu ya baadaye.

"Eneo hili mliwekee alama, muandike siku na muda ambao tetemeko lilitokea," aliagiza Profesa Muhongo.

Katika ziara hiyo,  Waziri Muhongo pia amekagua miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambayo iliathiriwa na tetemeko la ardhi, ili kubaini hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa lengo la kuiboresha na baadaye leo hii atakutana na Kamati ya Maafa ili kuweka mikakati ya kusimamia Shughuli za maafa na namna bora ya kuwaelimisha wananchi jinsi ya kujihami kabla na baada ya Tetemeko.

KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI

September 23, 2016



Na  Mwandishi Maalum, New York

Shirika lisilo la  Kiserikali    la Speak  Up for Afrika    limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake  kwa  makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu hususani wanawake na watoto.
Utoaji wa  Tuzo hiyo  ya  uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na   hafla ya  miaka mitano ya kuanzishwa kwa  Taasisi ya Speak up  Afrika. Hafla  hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New York   ilikuwa  pia  ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji   wa shughuli za  Taasisi hiyo.
Mchango ambao umetambuliwa na  Speak Up  Afrika,   taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi  kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni  katika maeneo ya  upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi za afya hususani afya ya mama na mtoto,  udhibiti wa  ugonjwa  wa malaria kupitia kampeni  ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa vyandarua  vyenye viatilifu, kampeni ya  lishe bora, na  kampeni ya   chanjo kwa watoto.
Pamoja  na  kutambua  juhudi za   Rais Mstaafu  Kikwete katika  kuyasemea maeneo hayo,  Taasisi hiyo kupitia  Mkurugenzi wake  Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua  kama kiongozi ambaye    amekuwa mstari wa mbele  wa kulisema Bara la Afrika kila  mara alipopata  fursa  ya  kufanya hivyo wakati akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais kikwete ameelezwa katika hafla hiyo iliyowashirikisha  wadau wa kada mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za kijamii ambazo  au wameshindwa kuzipata kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea  Tuzo hiyo, Rais  Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya watoto wote  waafrika ambao ndio  waliomfanya asimame   mbele ya wageni waalik
“ Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu  baada ya kustaafu kusukuma mbele agenda ya  kuboresha maisha yanu. Ninafanya hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama  ya mtoto yeyote yule wa  kiafrika, nimeyaishi maisha  wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika  hamu na kiu yao ya kuwa  na maisha bora na afya njema”. Akasema Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza kuwa  ,  mafaniko ambayo ameyapata katika  juhudi hizo  za kufikisha huduma za msingi  za kijamii kwa makundi  yenye mahitaji  yametokana na mambo mawili makubwa moja ni   aina ya uongozi  alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili  uhamasishaji uliofanyika katika  kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na    kampeni yao ya  malaria haikubaliki.
“ Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya   bila uungugwaji mkono na  ushirikiano  wa karibu nilioupata  na ninaoupata kutoka taasisi za kimataifa  ikiwamo hii ya  Speak Up  Afrika. Ndio maana  kwa mfano,  tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa   theluthi mbilli,  tumefanikisha  upatikanaji wa chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na  malaria kwa   nusu.” Akaeleza Kikwete na kushangiliwa  tena.
Akasema, anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali  kama akina Ray Chambers kupitia kampeni ya  hakuna tena malaria, Taasisi ya  Bili na Melinda Gates na Gavi Vaccination   Alliance ambayo anashirikiano  nayo kwa karibu katika  kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais  Mstaafu amewahakikishia   watendaji wa Speak  Up Afrika kwamba  ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu  kutokana  kile alichosema amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
 Akawasihi  wadau mbalimbali  kuichangia taasisi hiyo  kwa kile alichosema, inafanya kazi kubwa  ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale zinapotakiwa lakini  pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.
Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii ni  pamoja na   Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa Afya  wa Senegal, Bibi Toyin  Saraki,  mwanzilishi wa Taasisi ya  Wellbeing  Afrika ambayo  pia imekuwa ikitoa  elimu na misaada kwa wanawake na watoto pamoja na elimu  kwa wakunga na kutambua kazi nzuri, kubwa na ngumu  ya kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua.  Na  Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa  Taasisi ya  Wari.
Taasisi ya  Speak  Up  Afrika  imeanzishwa  na wanawake na inaongozwa na wanawake. Ni taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani  ya kipindi cha miaka mitano tangu  kuanzishwa kwake.