Na Mwandishi Wetu,Tanga.
MFUMKO
wa bei ya kiungo (Nazi) na vyakula kama Ndizi ya mkono wa Tembo jijini
Tanga, umepanda maradufu katika masoko mbalimbali hususani katika
kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Uchunguzi
uliofanywa na Blog hii katika baadhi ya masoko ya Ngamiani, Mgandini na soko la
Makorora unaonyesha kwamba wafanyabiashara wengi wamepandisha bei za
nafaka hususan nazi na ndizi ya mkono wa Tembo.
Bei
hizo zimeonekana kupanda haraka kwa kipindi cha mwezi huu mtukufu wa
ramadhani ambapo awali bei ya ndizi ya mkono wa Tembo kikonyo kimoja
kilikuwa Sh300 hadi 400, lakini sasa imefika sh800 kwa kila kikonyo
kimoja, nazi ilikuwa kati ya Sh300 hadi Sh400 na sasa imepanda na
kufikia Sh700 hadi Sh1000 kwa kila moja.
Wakizungumza
suala la kupanda kwa bei ya Nazi na ndizi ya mkono wa Tembo baadhi ya
wafanyabiashara hao wamesema licha ya kuwa huu ni mwezi mtukufu wa
ramadhani, lakini kinachochangia pia ni kutokana na halisi ya usafiri na
miundombinu ya barabara ambako bidhaa hizo zinakotoka.
“Nikweli
kuwa kipindi hiki cha mwezi huu mtukufu wa ramadhani watu wengi wa
dhehebu la dini ya kiislamu wanashirki kufunga na hata wengine pesa
wanazonunulia futari zinawashinda kutokana na kipato wanachopata
hakitoshelezi lakini siyo sisi wafanyabiashara ndiyo tunajipandishia bei
hapana bali hata huko tunakokwenda kununua wakulima nao wametupandishia
bei,” amesema mfanyabiashara wa Nazi na Ndizi ya mkono wa Tembo
aliyejitambulisha kwa jina la Josephat.
Aidha wamesema
kuwa bei hiyo ya Ndizi ya mkono wa Tembo na kiungo hicho (Nazi) inaweza
kupanda maradufu tena kutokana na hali ngumu ya usafirishaji kutokana
na kutopatikana kutoka kwa wakulima mashambani.
(Mwisho).