WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA UTURUKI NA CUBA

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA UTURUKI NA CUBA

February 09, 2016
 
IMG-20160209-WA0010

Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

IMG-20160209-WA0011

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akirekodi mambo muhimu kwenye 'diary' yake wakati wa mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

IMG-20160209-WA0012

Balozi wa Uturuki nchini, Bi. Yasemin Fralp akifurahi jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki.

IMG-20160209-WA0009

UJUE MTUNGI WA FAYA ULIOJAZWA NA ULIOTUPU/AMBAO GESI IMEKWISHA

February 09, 2016
Mtungi uliojaa kwa kuzima Moto
Mtungi uliotupu kwa maana ya kwamba mshale wake umerudi kushoto kama unao kwenye gari lako,ofisini au nyumbani ujue hilo ni kopo tu hautakusaidia chochote kuzima moto. Sana sana utautumia kuwadanganya askari na wakaguzi wasiojua tu. Kwa ufupi unajidanganywa wewe mwenyewe.
Mtungi ulioactive kwaajili ya kuzima moto mshale wake utakuwa kwenye green (kijani). Ikiwa mshale utakuwa kulia mwa alama ya kijani mtungi huu umejazwa kupita kiasi na ni hatari.Imeandaliwa na RSA na Dj Sek Blog

Huu ni mtungi ambao hauna ujazo wowote na hauwezi kuzima moto kwa namna yoyote ile


DJ SEK BLOG P.O.BOX Dar es salaam IT DEPARTMENT +255713966552,+255788462579 Web:www.dj-sek.blogspot.com

MWANAHARAKATI KHADIJA LIGANGA ANUIA KUKUSANYA PEDI KWA AJILI YA MABINTI WANAOSOMA.

February 09, 2016
Kutokana na Wasichana wengi walio Mashuleni kulazimika kukosa Masomo yao katika Kipindi cha hedhi, Mwanaharakati wa Kutetea haki za Wanawake na Wasichana nchini Khadija Liganga, amelazimika kuanzisha kampeni ya kukusanya pedi 3,000 ndani ya mwezi huu ili kuwasaidia wahitaji.

Akizungumza jana katika Kipindi cha Passion Break Fast kinachorushwa na Radio Passion Fm ya Jijini Mwanza, Liganga alibainisha kwamba ameamua kukusanya pedi hizo kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuziwasilisha katika Shule 10 za Msingi na Sekondari zilizo katika Mikoa ya Mwanza na Mara hii ikiwa ni maalumu kwa ajili ya wasichana wanafunzi ambao hawana uwezo wa kumudu kununua pedi hizo.

“Tarehe Moja mwezi wa Kwanza mwaka huu, wanawake tulikutana Jijini Mwanza chini ya mpango tuliouita Women Round Table kwa ajili ya kupanga mikakati mbalimbali ya kimaendeleo kwa mwaka huu 2016. Moja ya mikakati niliyoipanga ni pamoja kuanzisha mradi uitwao Binti Box ambao umelenga kusaidia uchangiaji na upatikanaji wa pedi kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji mashuleni pamoja na kuwapa elimu ya namna ya kujiweka katika hali ya usafi wawapo katika kipindi cha hedhi”. Alisema Liganga na kuongeza kuwa mpango huo utakuwa endelevu.

Kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wasichana katika maeneo mbalimbali nchini kukosa masomo yao katika kipindi cha hedhi huku baadhi yao wakilazimika kuacha shule kutokana na aibu wanayokumbana nayo wawapo shuleni hii ikiwa ni kutokana na kukosa elimu ya kutosha pindi waingiapo katika kipindi cha hedhi.

Unaweza kuungana na mwanaharaki huyo kwa kuchangia pedi ambapo anapatikana kwa nambari 0713 093 801 hiyo ikiwa ni kwa wale walio mbali na Jijini Mwanza ama waweza kutembelea ofisi za Dida Vitenge Wear zilizopo Nganza Sekondari barabara ya kwenda Chuo Kikuu cha SAUT jirani na ghorofa upande wa kushoto hapo.
SERA YA ELIMU YATAJWA KUCHANGIA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

SERA YA ELIMU YATAJWA KUCHANGIA TATIZO LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA

February 09, 2016
Katika kuadhimisha miaka 50 ya mahusiano na ushirikiano baina ya Uswisi na Tanzania, ubalozi wa Uswisi nchini umefanya mdahalo wa wazi kuhusu ajira kwa vijana ulioshirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili kubadilishana mawazo jinsi wao wanavyofanya ili kupambana na tatizo la ajira.
Mdahalo huo ambao ulifanyika katika hoteli ya Coral Beach, jijini Dar es Salaam ulijadili mambo mbalimbali ambayo yanasababisha kuwepo kwa ajira chache lakini pia uwezo wa vijana wa kuingia katika soko la ushindani la ajira.
Aidha mdahalo huo uliweza kujadili kuhusu changamoto iliyopo ya ajira kwa vijana na kuependekeza njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linaonekana kukua kwa jinsi siku zinavyokwenda.
Wakizungumza na Mo Dewji Blog baada ya kumalizika kwa mdahalo huo wadau mbalimbali ambalo walihudhuria walisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana linaanzia katika aina ya sera ambazo serikali inazitumia katika sekta ya elimu kushindwa kufanya kazi katika soko la ajira la sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema kuwa ili serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana inatakiwa kuhakikisha inaimarisha uchumi wa nchi lakini ambao unatoa nafasi za ajira zaidi.
Alisema mbali na kuimarisha uchumi pia inatakiwa kuwatengenezea wananchi wake mazingira mazuri ambayo yatawashawishi kujiajiri bila kutegemea ajira ya serikali au makampuni binafsi ambayo kwa sasa ndiyo yanaonekana kutoa nafasi nyingi za ajira.
“Vijana wengi kwa sasa wakimaliza vyuo wanajiajiri na hata kama wanauza barabarani korosho huko nako ni kujiajiri … serikali inatakiwa kuimarisha uchumi wa nchi na sio kukuza tu lakini ukue na utoe fursa za ajira kwa wazawa,” alisema Eyakuze.
Aidha aliwataka vijana kuacha tabia ya kutegemea ajira za serikali na sekta binafsi kwani ushindani katika soko la ajira ni mkubwa na kama wanakuwa hawajajiandaa kwa kiasi kinachohitajika sasa katika soko la ajira basi inaweza kuwa ngumu kwao kupata nafasi.
Nae Amabalis Batamula kutoka Femina alisema sera ambazo zinatumika nchini hazitekelezwi kama zinavyopangwa na serikali na pia hazina faida kwa soko la ajira la sasa kutokana na kubadilika kwa jinsi miaka inavyozidi kwenda.
Alisema ni jambo la ajabu baadhi ya sera za elimu ni kuendelea kutumika hadi sasa licha ya soko la ajira kubadilika na hivyo kuhitaji sera mpya ambazo zinakwenda na wakati lakini pia kuwashauri vijana wanaohitimu kuacha kuishi kwa mazoea na badala yake wawe wakijiajiri ili kuepuka tatizo la ukosefu wa ajira.
Katika taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), inaonyesha kuwa zaidi ya vijana 800,000 humaliza chuo kila mwaka na wanaokadiriwa kupata ajira rasmi ni 40,000 pekee hivyo kuonyesha ni jinsi gani kuna upungufu mkubwa wa ajira nchini.
IMG_2472
Balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely Mattli akitoa neno la ufunguzi katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijana
IMG_2469 Wachangia mada katika mdaharo huru kuhusu ajira kwa vijanaIMG_2480 Baadhi ya washiriki waliohudhuria mdahalo huo703 Mmoja wa washambuzi wa mada akielezea jambo katika mdahalo huru kuhusu ajira kwa vijanaIMG_2572 Washiriki wa mdahalo wakiwa katika makundi kujadili mada zilizotolewa[/caption]
Unaweza kusikiliza hapa baadhi ya washiriki waliozungumza na Mo Dewji Blog

ELIMU BORA ITOKANE NA WALIMU BORA - MELISA

February 09, 2016

Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa Kwanza Maganga Lorry wa shule ya msingi Mbaaseny ,katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa tuzo za Walimu Bora ,,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo
Kushoto ni Afisa Elimu wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akikabidhi tuzo za Walimu Bora kwa mshindi wa 5 Mwalimu Clara Ernest wa shule ya Msingi Tuvaila ,
katikati ni Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
washindi wa tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tommorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo
Na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali  la The Foundation for Tomorrow  (TFFT) ,Melissa Queyquen ameyasema hayo jana wakati wa utoaji wa tuzo za walimu bora wa shule za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu katika maendeleo ya elimu nchini na ustawi bora wa jamii .

Melisa alisema kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu waliyonayo watu wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu ifikirie kuboresha mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda kufundisha ,vifaa vya kufindishia pamoja na stahiki zao.

Bila Walimu Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na vyeti vya kutambua mchango wao ,washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa cheti na shilingi la kitano,na washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha taslimu” Alisema Melisa

Afisa Elimu wa Shule za Msingi  Wilaya ya Meru  Tumsifu Mushi  amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia jamii,taifa na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito unaostahili.

Kwa upande wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari  na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.

“Kazi ya ualimu unapaswa uwe unapenda watoto  unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim
-- Gadiel E.W. U (Gadiola Emanuel) IT/ PR /Photojournalist and Blogger -Based in Arusha, Tanzania. Mob :+255 715 643 633 E-mail: gadiola25@gmail.com WEB: www.wazalendo25.blogspot.com : www.arushapublicity.blogspot.com :www.northernshotstz.blogspot.com

ASILIMIA 15 YA WANAWAKE NCHINI WAMEGUNDULIKA KUWA WAMEKEKETWA - DK. KIGWANGALA

February 09, 2016

Na Jumbe Ismaill, Singida

NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto amesema asilimia 15 ya wanawake wamegundulika kuwa wamekeketwa na kwamba takwimu hizo zinaonyesha pia kuwa ukeketaji huo umekithiri katika mikoa minane hapa nchini.

Naibu Waziri huyo,Dk.Hamisi Kigwangala ametoa takwimu hizo alipokuwa akifunga kongamano la siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji dhidi ya watoto wa kike na wanawake lililofanyika mjini hapa.

Alifafanua naibu waziri huyo kuwa takwimu hizo zinaonyesha kwamba ukeketaji huo umekithiri katika mikoa ya Manyara,Dodoma,Arusha,Singida pamoja na mkoa wa Mara na kwamba ukubwa wa tatizo hilo katika mikoa hiyo linatokana na imani na mila potofu.

“Kwa mujibu wa utafiti wa kidemografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey) wa mwaka 2010 unaonyesha kuwa asilimia 15 ya wanawake wamekeketwa na kwamba takwimu hizo zinaonyesha ukeketaji umekithiri katika mikoa ya Manyara asilimia 71”alisema.

Aliitaja mikoa na asilimia zake kuwa ni mkoa wa Dodoma asilimia 64,Arusha asilimia 59,Singida asilimia 51 na Mara asilimia 40 huku akiweka bayana kuwa takwimu hizo zinaonyesha pia ukubwa wa tatizzo la ukeketaji katika mikoa ya Dar-es-Salaam,Morogoro na Pwani kutokana na watu wa makabila mbali mbali kuhamia katika mikoa hiyo.

“Serikali inapinga,kulaani na kukemea tabia ya kuendelezwa kwa vitendo hivi vya ukatili unaomdhalilisha mtoto wa kike kwani unamsababishia madhara makubwa kiafya,kielimu, kisaikolojia na kimaendeleo”alisisitiza Dk.Kigwangala.

Katika kuhakikisha kuwa suala la udhalilishaji kwa wanawake na watoto wa kike linazuiwa na kutokomezwa kabisa nchini,Dk.Kigwangala alibainisha kuwa serikali imesaini na kuridhia mikataba ya kimataifa na kikanda,maazimio na makubaliano mbali mbali yanayohusu haki na maendeleo ya watoto na wanawake.

Hata hivyo Naibu waziri huyo aliitaja baadhi ya mikataba hiyo kuwa ni pamoja na mkataba wa kimataifa wa Haki za mtoto wa mwaka 1989,Mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake wa mwaka 1989,mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Haki za watu wa mwaka 1982 na itifaki yake ya nyongeza inayohusu wanawake wa Afrika wa mwaka 2003 inayopinga mila zenye kuleta madhara kwa binadamu kama vile ukeketaji.

Akitoa salamu za shukurani mara baada ya hotuba ya mgeni huyo,Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,Edda Sanga aliweka wazi kwamba suala la harakati za ukeketaji ni harakati ambazo zimeweza kuleta machungu mengi katika jamii,jambo ambalo linahitaji msukumu mkubwa wa serikali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo licha ya machungu yanayotokana na vitendo vya ukeketaji kunakosababisha vilio vya watu kutoka sehemu mbalimbali,lakini vilio peke yake havitasaidia chochote na kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuchukua hatua za kuhakikisha mila na desturi zilizopitwa na wakati zinatoweka kabisa nchini.

“Mheshimiwa Naibu waziri tulilia hapa machozi jana lakini kama unavyojua mheshimiwa waziri machozi hayatoshi ni lazima tuchukua hatua na hatua ndizo hizo ambazo umetuahidi hapa,jamani naomba tumpigie makofi mheshimiwa waziri”alisisitiza Sanga.
baadhi ya wanaharakati wa mapambano dhidi ya kupinga vitndo vya ukeketaji kutoka katika mikoa mitano ya Tanzania Bara waliohudhuria kongamano la siku mbili lililofaanyika mjini Singida.
ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’

ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’

February 09, 2016

uw1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw4 uw5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia  au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
uw7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa  Wadau wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw8
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola   (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.

WAFANYABIASHARA WAASWA KULIPA KODI.

February 09, 2016


WAFANYABIASHARA waasa kulipa kodi  kwa kuto kulipa kodi ni kinyume cha sheria kwani huleta kuleta msukumo kwa Mamlaka ya Mapato kukusanya wa mapato ya serikali ili fedha hizo zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakati akizungumza na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam leo.

Pia amesema kuwa   wafanyabiashara wanatakiwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano katika ukusanyaji mapato ili kujenga mazingira bora ya wafanyabiashara.

Mpango amewaomba wafanyabiashara kutumia mashine za EFD ili kuongeza mapamo ya serikali wanampango wa kununua Mashine za EFD ili kuwapa wananchi ambao hawajaanza kuzitumia kwaajili ya kukusanya mapato ya serikali.

 Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango akizungumza na wafanyabiashara leo katika ofisi za wizara ya Fesha jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Salum Shamte.
Kutoka kulia ni Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, katika ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile wakiwa kwenye mkutano wa waziri wa Fedha na Mipango leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Salum Shamte akizungumza na wafanyabiashara  waliokusanyika leo katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF), Felix Mosha  na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) wakiwa kwenye mkutano wa wafanyabiashara leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafabiashara wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa sekta ya Kilimo Sinari Sinari akizungumzia kuhusiana na sekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo. 
Mkurugugenzi wa Bravo Logistics, Angelina Ngalula akizungumza na wafanyabiashara katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na usafilishaji wa mizigo kwa kutumia magari na jinsi adha ya usafari katika sekta ya usafirishaji hapa nchini.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

TIGO YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA CHAMA CHA WAANDISHI DODOMA

February 09, 2016

Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha (Kushoto) akikabidhi vifaa mbalimbali vifaa vya mawasiliano na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni nane kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) Habel Chidawali, ili kufanikisha bonanza la wanahabari la kufunga mwaka 2015 lililopangwa kufanyika baadaye mwezi huu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) Habel Chidawali, akitoa shukrani  mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vifaa vya mawasiliano na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni nane na Meneja mawasiliano wa Tigo John Wanyancha  ili kufanikisha bonanza la wanahabari la kufunga mwaka 2015 lililopangwa kufanyika baadaye mwezi huu  wanaoshuhudia ni makamu mwenyekiti wa CPC Rachel Chibwete (kushoto) na katibu wa CPC bw .Bilison vedastus