ORYX YAKABIDHI MITUNGI YA GESI NA MAJIKO YAKE 700 KISARAWE,KUFUNGA MFUMO WA GESI MINAKI SEKONDARI

January 28, 2024

 Na Mwandishi Wetu, Kisarawe


KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo wamekabidhi mitungi 700 ya gesi pamoja na majiko yake kwa walimu 500 pamoja na Baba na Mama Lishe 200 yenye thamani ya zaidi ya Sh.milioni 50 katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani huku kampuni hiyo ikiahidi kufunga mfumo wa gesi katika Shule ya Sekondari Minaki ili waanze kutumia nishati safi ya kupikia badala ya kutumia kuni na mkaa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi hiyo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari Wilaya ya Kisarawe Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema anamshukuru Waziri Jafo, kwa kumpatia nafasi ya kupeleka nishati safi ya kupikia kwa walimu pamoja na Baba na Mama lishe wilayani Kisarawe.

“Oryx Gas tunaamini kwamba ukipika kwa kutumia gesi, inaleta maendeleo mengi kwa jamii yetu. Kupika kwa gesi ya Oryx ni kulinda mazingira kwa kuacha kukata miti. Zaidi ya yote ni kulinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.

“Wanawake wanatumia muda mchache kupika hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula, na wanaume pia watajiongezea marks ukiwazadia wamama mitungi ya gesi.Kwa kutumia gesi ya Oryx, Watoto wanakua na muda mwingi zaidi kusoma na sio kwenda kutafuta kuni.”

Amesisitiza kuwa kuanzia Julai mwaka 2021 wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali waliyopokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

Araman amesema kupitia mipango hiyo Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa ambayo si tu mbaya kwa afya bali pia ni hatari kwa mazingira yetu huku akitumia nafasi hiyo kueleza pia Oryx Gas inatekeleza juhudi za kueneza matumizi ya nishati safi kwa Watanzania wengi ipasavyo ambayo ni ndoto kubwa ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

Pia amesema Oryx Gas inatekeleza agizo la Serikali kwa kuhakikisha taasisi zenye watu zaidi ya 100 kutumia nishati safi kwa kutengeza mifumo salama ya gesi kwa kutumia tenki kubwa ambapo mifumo hiyo inaweza tumika shuleni, kambi za jeshi, vyuo vya polisi, magereza na katika kampuni za uzalishaji.

“ Hii inasaidia kupunguza matumizi ya mafuta machafu kwenye mifumo ya uzalishaji. Oryx Gas Tanzania inajipongeza kwa kujulikana kua kampuni kinara katika usambazaji wa gesi ya kupikia majumbani kwa Watanzania kwa sasa. Sisi Oryx Gas Tanzania tutaendelea kuwekeza zaidi katika kuratibu kubadilisha na kueneza nishati safi kutumika na Watanzania kwa kutumia gesi ya Oryx kwa manufaa yetu wote.”

Pia amehimiza wananchi kutumia gesi ya LPG katika shughuli zao mbalimbali ili kuleta maendeleo katika nchi ya Tanzania na kwa ajili ya kuboresha Maisha yetu kiujumla huku akitumia nafasi hiyo kueleza Waziri Jafo amekuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa waalimu na jamii kiujumla kwa kuunga mkono katika mpango huo wa matumizi ya nishati safi wilayani Kisarawe.

Akizungumzia kuhusu kufunga mfumo wa nishati safi ya kupikia katika Shule ya sekondari ya Minaki , Aramn amesema watafunga mfumo huo ili shule hiyo kuondokana na kutumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia na kwamba Orxy itafunga mfumo wenye uwezo wa kubeba ujazo wa tani moja ya gesi na ametoa ahadi hiyo baada ya Waziri Jafo kutoa ombi kwa kampuni hiyo kufunga mfumo huo katika shule hiyo ambayo yeye amesoma kidato cha tano na sita.

Kwa upande wake Waziri Jafo ametumia nafasi hiyo kuishukuru Oryx kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa vitendo huku akieleza kuwa tayari Serikali imeshatoa maelekezo kuanzia mwaka huu wa 2023 taasisi , mashirka na maeneo ambayo yana watu kuanzia 100 kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo nishati ya gesi.

Akizungumzia zaidi Waziri Jafo amesema mbali ya kugawa mitungi ya gesi kwa walimu 500 bado ataendelea kuzungumza na wadau ili apate mitungi mingine kwani lengo lake ni kuhakikisha walimu wote 1300 walioko katika wilaya hiyo wawe wamepata mitungi ya gesi.

“Idadi ya walimu waliko Kisarawe ni 1300 hivyo baada ya kugawa majiko 500 yatahitajika tena majiko 800 ya gesi lakini hili suala tutaendelea kuwafikia wadau .lengo langu kila mwalimu wa Kisarawe awe na gesi. Pia nimemuomba Mkurugenzi wa Oryx atufungie mfumo wa gesi katika sekondari yetu ya Minaki na amekubali na huu ni mwanzo tu kwani nataka kuona shule zote za Kisarawe tunafunga mfumo huo ili kuondakana na matumizi ya kuni na mkaa,”amesema Waziri Jafo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo(katikati) na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman(kushoto) wakimkabidhi mtungi wa Oryx Mwalimu wa Shule ya Msingi Kitonga Mango iliyopo wilayani Kisarawe mkoani Pwani Mkegani Mkuya ( kulia) wakati wa hafla ya ugawaji mitungi ya gesi na majiko yake kwa walimu 500  wa Wilaya hiyo, lengo likiwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya oryx 700 ambayo imekabidhiwa kwa walimu 500 pamoja na Baba na Mama Lishe 200 katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (wa tatu kushoto) akimkabidhi mtungi wa gesi ya Oryx Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Seleman Jafo  ikiwa ni sehemu ya mitungi 700 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuigawa kwa walimu 500 pamoja na baba na mama lishe 200 katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani
Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Araman (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Salemani Jafo wakati wa hafla ya kukabidhi  mitungi ya gesi ya Oryx 700 yakiwa na na majiko yake kwa walimu pamoja na baba na mama lishe katika Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo(kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman wakijadiliana jambo wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya oryx pamoja na majiko yake kwa walimu , baba lishe na mama lishe wilayani Kisarawe
Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi salama ya mtungi wa gesi kabla ya kukabidhiwa kwa walimu pamoja na baba na mama lishe wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza matumizi sahihi ya gesi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa mtumiaji




WAZIRI MAKAMBA ATETA NA MKURUGENZI MKUU IOM

January 28, 2024


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji (IOM) Bi. Amy Pope jijini Roma, Italia

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Makamba ameipongeza IOM kwa kazi inazofanya nchini katika masuala ya Uhamiaji na amemuhakikishia Bi. Pope kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanya kazi na Shirika hilo kwa ukaribu zaidi.

Mhe. Waziri Makamba amesema Shirika hilo limekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya wakimbizi, majanga ya asili na kwamba ni matumaini yake kuwa Tanzania na IOM zitaendelea kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.

Waziri Makamba ameipongeza IOM kwa kuendelea na zoezi la kuwarejesha nyumbani raia wa Ethiopia waliokuwa katika magereza mbalimbali nchini na kuongeza kuwa kitendo hicho kimesaidia Tanzania kukabiliana na changamoto ya msongamano wa watu katika magereza yake.

Kwa upande wake, Bi. Pope ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa jinsi inavyoshirikiana na Shirika la IOM katika kutekeleza majukumu yake na kuahidi kuwa na mpango maalum wa kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha majukumu yake. Aliongeza kuwa Shirika hilo litahakikisha kuwa wahamiaji wanapata haki zao za msingi na kuwa katika mazingira salama nchini.





WANACHAMA WAFURAHISHWA NA HUDUMA YA PSSSF KIGANJANI MOBILE APP

January 28, 2024

 NA KVIS BLOG/KHALFAN SAID, MNAZI MMOJA

WANACHAMA wengi wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, wamefurahishwa na huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App.

Huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App, inamuwezesha mwanachama kupata taarifa zote zinazohusiana na uanachama wake akiwa mahali popote kupitia simu yake ya kiganjani, Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta wa Mfuko huo Bw.Gideon Mwashihongo amesema leo Januari 28, 2024, wakati akitoa elimu ya matumizi ya huduma mtandao.

Bw. Kizza Sostenes, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya Temeke, ameupongeza Mfuko huo kwa kutoa huduma zake kidijitali.

“Nimefaidika sana baada ya kufika hapa, nimeelekezwa jinsi ya kutumia huduma ya PSSSF Kiganjani na nimeijaribu ni huduma nzuri na rahisi kutumia.” Amesema Bw. Sostenes.

Mwanachama mwingine Bi. Lightness G. Msuya, yeye amesema huduma ya PSSSF Kiganjani Mobile App, inasaidia kuokoa muda, kwani yeye kama mtumishi, inamsaidia kupata taarifa za Mfuko akiwa mahali popote.

Kwangu mimi huduma hii inanipunguzia gharama za usafiri kufuata huduma kwenye ofisi za PSSSF, kuanzia sasa silazimiki kwenda PSSSF, baada ya kujiunga kwenye huduma hii, kwani simu yangu inatosha.” Amesema Mwnachama mwingine wa PSSSF, Bw. Kudura Said Kondo, mtumishi wa Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ushiriki wa Mfuko kwenye maonesho hayo, Bw. Kikula Suleiman, kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria PSSSF Makao Makuu amesema, PSSSF kama taasisi iliyoundwa kisheria ni mdau mkubwa wa Mahakama na watumishi wa mahakama na taasisi nyingine za umma ni wanachama wa Mfuko huo, hivyo ushiriki wa Mfuko kwenye Maonesho ni fursa nzuri ya kutoa huduma na elimu kwa wanachama.

“Katika jitihada za kuhakikisha wanachama wanapata huduma bora na rafiki tumeamua kujikita kutoa elimu ya huduma za PSSSF kiganjani Mobile App, PSSSF ulipo Mtandaoni Member Portal.” Amesema na kuongeza, kwa kutumia huduma hiyo tunaamini inatoa uhuru sio tu kwa wanachama lakini pia kwa waajiri kuweza kulipia michango na kujihudumia wenyewe, yaani self-service.” Amefafanua Bw. Suleiman.

Maonesho hayo ya siku saba yaliyobeba kauli mbiu “Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai” yamezinduliwa rasmi Januari 27 2024, na yatafikia kilele Januari 30, 2024.



Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (katikati), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa wanachama wa PSSSF waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kupitia PSSSF Kiganjani mwanachama anaweza kupata huduma zote zitolewazo na Mfuko bila kulazimika kufika ofisi za PSSS


Bw. Kikula Suleiman (aliyesimama), kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria PSSSF Makao Makuu, akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwenye banda la Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka Kanda ya Dar es Salaam kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2024.


Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bi. Lihhtness G. Msuya, kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.
Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Gideon Mwashihongo (kulia), akitoa elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani Mobile App, kwa mwanachama wa PSSSF, Bw. Kudura Said Kondo kwenye banda la PSSSF, Januari 28, 2024.



Bw. Kizza Sostenes (kulia), Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba, Wilaya ya Temeke, akihudumiwa na Bi. Hellen Mollel, Afisa Mafao PSSSF.







AWESO AFANYA MABADILIKO YA WATENDAJI MAJI RUFIJI, AMUONDOA KWENYE NAFASI YAKE MKURUGENZI UTETE.

January 28, 2024
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefanya mabadiliko ya Kiuongozi katika Mamlaka ya Maji Utete kwa kumuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo bwana Christopher Mwigune akiwa wilayani Rufiji alipofanya kikao maalum cha kuongea na Watumishi wa Sekta ya Maji wilaya ya Rufiji na wilaya jirani za mkoa wa Pwani.

Awali pia Waziri Aweso alifanya mabadiliko ya kiutendaji eneo la Maji Vijijini (RUWASA) kwa mabadiliko ya Meneja wa Wilaya hivyo;

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso amemtambulisha rasmi kwa uongozi wa serikali ya Mkoa na Wilaya Meneja mpya wa wilaya wa Maji Vijijini (RUWASA) Eng Alkam Omari Sabuni na kumuelekeza pia Kukamimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Utete katika kipindi hiki cha Mpito ambacho ataifanya mabadiliko makubwa mamlaka hiyo na kuiunda upya.

UTT AMIS YAWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI

January 28, 2024

 KAMPUNI ya Uwekezaji ya UTT AMIS imetoa elimu kwa wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa jijini ikiwa ni hatua ya kuwasaidia kuelimisha umma kuhusu Uwekezaji.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini hapa, ofisa mwandamizi kutoka kampuni hiyo, Rahimu Mwanga, amesema mafunzo hiyo yamekusudia kuwajengea uwezo kuhusu kuelimisha umma juu ya mifuko ya Uwekezaji wa pamoja.

"Tuna mifuko Sita ya Uwekezaji na tumekuwepo kwenye soko kwa takriban miaka 20 sasa na mifuko hii imekuwa ikifanya vizuri sokoni," amesema Mwanga.

Mwanga amesema mifuko hiyo ni pamoja na mfuko wa watoto, Umoja, Kujikimu, na Ukwasi, wekeza maisha na kwamba mpaka sasa wana zaidi ya wateja 300,000 huru rasilimali zao zikifikia thamani ya Sh1.9 trilioni.

Akieleza baadhi manufaa ya kuwekeza katika mifuko hiyo, Mwanga amesema wazazi na walezi wanaweza kutumia mfuko wa watoto kuwawekezea watoto wao ambao kiwango chake Cha Uwekezaji ni kidogo.

"Kuna watu Wana mahitaji ya kukuza mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, kama vile biashara, kununua ardhi na kujenga, vyote hivi vinahitaji fedha, na fedha ya mkupuo inakuwa ni ngumu, kwa hiyo wanaweza kuanza kuwekeza kidogo na wakakuza mitaji kupitia mitaji yao," amesema.

Mwanga ameongeza kuwa kupitia mifuko ya hati fungani na mfuko wa kujikimu ambayo ni mifuko inayotoa magawio ya mara kwa mara, inalenga wawekezaji ambao wamepata hela za mkupuo kama wastaafu ambapoa inatoa gawio la mara kwa mara.

"Moja ya changamoto ya wastaafu ni namna nzuri ya kutumia mafao yao, kwahiyo kwa kupitia mfuko wa hati fungani wanaweza kuwekeza na kupata gawio kila mwezi au Kila baada ya miezi Sita," amefafanua.