COASTAL UNION YAFANYA KWELI,YAICHAPA SIMBA KIMOJA TU.

July 28, 2013
KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOIBAMIZA SIMBA BAO 1-0 LEO KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI.

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOANZA KWENYE MCHEZO WA LEO NA COASTAL UNION

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU AKISALIMIANA NA WACHEZAJI WA SIMBA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO.

KOCHA MSAIDIZI WA SIMBA JAMHURI KIWELU "JULIO"AKITANIANA NA MWENYEKITI WA KLABU YA COASTAL UNION ,HEMED AURORA "MPIGANAJI "KABLA YA KUANZA KWA MCHEZO HUO.
KIKOSI CHA SIMBA NA COASTAL UNION WAKISALIMIANA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO.

MWAMUZI WA MECHI YA LEO MKONO AKIWA NA MANAHOZA WA TIMU ZOTE MBILI KALBA YA KUANZA MECHI HIYO LEO.

SIMBA WAKIPIGA DUA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO LEO AMBAPO COASTAL UNION ILISHINDA BAO 1-0.

KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIPIGA DUA KABLA YA KUANZA MECHI HIYO YA LEO

KOCHA MKUU WA TIMU YA SIMBA ,ABDALLAH KING KIBADENI MWENYE MIWANI KUSHOTO AKIFUATIWA NA KOCHA MSAIDIZI WA TIMU HIYO,JAMHURI KIWELU "JULIO

PROMOTA BONGA NAYE PIA AKIKUWEPO KWENYE MECHI HIYO KAMA ANAVYOONEKANA HAPO

MWENYEKITI WA UVCCM WILAYA YA TANGA,MH.SALIMU PEREMBO MWENYE TISHETI NYEKUNDU YA COASTAL UNION  AKIFURAHIA JAMBO LEO KWENYE MECHI YA SIMBA NA COASTAL UNION

MENEJA WA COASTAL UNION,AKIDA MACHAI MWENYE TISHETI NYEKUNDU AKIWA NA MASHABIKI WENGINE WA TIMU HIYO WAKIUFUATILIA MCHEZO HUO

MASHABIKI WA SOKA MKOANI TANGA WAKIUFUTILIA MCHEZO HUO WA LEO.

MAMBO YALIYOIFANYA SIMBA KUFUNGWA NA COASTAL UNION.

July 28, 2013
Na Mwandishi Wetu,Tanga.
 

KAMA ulibahatika kuutazama mchezo wa kirafiki kati ya Coastal Union na Simba kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga utagundua yapo mambo mengi sana yaliyowafanya Simba kufungwa mechi ya Leo.

Suala la kwanza ambalo liliifanya Simba SC ifungwe ni wachezaji wake kucheza kwa kujiamini sana na kushindwa kucheza mpira wa kutulia badala yake walikuwa wakipata mpira walikuwa wakifikira kupiga mbele  bila bila kutumia njia za kufika mbele.

Katika mchezo huo ambao ulianza kwa kasi ya mashambulizi kwa kila timu zilishuhudiwa dakika 45 za kwanza zikimalizika na timu kutoka uwanjani hapo zikiwa nguvu sawa ya kutokufungana kutokana na upinzani ulioonyeshwa na timu hizo.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote zikiingia uwanjani hapo zikiwa na hari na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake ambapo Simba waliwatoa Vicent Mabusela,

Abdullahim Humud,Sino Augustino na Ramadhani Chombo Ridondo na kuwaingiza Miraji Adam,William Lucian,Christopher Edward,Zahoro Pazi na Twaha Ibrahim.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo Simba waliweza kuongeza nguv ya mashambulizi langoni mwa Coastal Union bila mafanikio yoyote huku baadhi ya wachezaji wake wakipiga mipira ya pembeni, kutokana na shambulizi hilo Coastal Union waliweza kucheza kwa umakini mkubwa.

Umakini huo uliweza kuwafanya Coastal Union kupata bao lao kwenye dakika ya 53 kupitia Crispian Udulla ambaye aliweza kutumia uzembe wa mabeki wa Simba kupachika wavuni bao hilo na kuwafanya mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kulipuka kwa shangwe uwanja mzima.

Lakini suala lengine ambalo lilionekana kuwapa shida sana Simba ni kucheza mpira bila kufahamu kuwa wanacheza na timu ambayo imejithatiti kikamilifu kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kutokana na usajili walioufanya ili waweze kutimiza dhamira yao ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara.

Kikosi cha Simba kiliwakilishwa na mlinda mlango Abel Dhaira,Nassoro Masoud Chollo,Issa Rashid,Rahim Juma,Vicent Mabusela,Jonas Mkude,Said Ndemla,Abdullahim Humudu,Sino Augustino,Ramadhani Singano,Ramadhan Chombo Ridondo.


Coastal Union iliwakilishwa na Shaban Kado,Mbwana Bakari, Othumani Omary,Juma Nyosso,Marcus Ndahele,Jerry Santo,Uhuru Seleman,Crispian Udulla,Keneth Masumbuko,Haruna Moshi na Danny Lyanga.

Mwisho.