IMEWEKWA saa 1:15 Mchana.
Na Oscar Assenga, Tanga.
MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva mkoa wa Tanga, Lucas Silas “Dr.Leader”ametamba
wimbo wake wa “Mganga” aliouachia hivi karibuni kufanya vizuri kutokana na
vionjo vikali ambavyo amevitumia kwenye wimbo huo.
Akizungumza blog hii, Dr.Leader ambaye ni msanii mahiri kutunga
nyimbi zenye mahadhi ya kipwani alisema katika wimbo huo anaelezea jinsi watu
wanaopenda kutamani wake za watu kwa hiyo alienda kwa mganga kumshtaki.
Alisema baada ya wimbo huo kuendelea kupigwa katika vituo
mbalimbali vya radio hapa nchini lakini pia anatarajia kutoa video ya wimbo huo
ambayo itatoka baada ya mwezi wa ramadhani na itakuwa imesheheni vitu
mbalimbali.
Dr.Leader alisema mpango wake ni kutoa single moja moja
kutokana na utoaji wake unakuwa ukilipa sana kuliko kusubiri kutoa album ambazo
mara nyingi hushindwa kupata fedha nzuri kutokana na kupata mapato kiduchu.
Alisema wanaiomba serikali iangalie hatimiliki za wasanii ili
waweze kufaidika na kazi zao ikiwemo kuwasaidia wasanii chipukizi kama zilivyo
nchi nyengine duniani kutokana na kuwa na utaratibu mzuri wa kazi zao
Hata hivyo,Dr.Leader alitoa wito kwa wasanii wakubwa kuacha
kuwabagua chipukizi kufanya nao kazi badala yake washirikiane pamoja lengo
likiwa ni kusukuma gurudumu la maendeleo ya mziki huo hapa nchini.
Mwisho.