RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA

RAIS DK. MAGUFULI AMTEUA JENERALI MSTAAFU GEORGE WAITARA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TANAPA

October 30, 2016
waitara-anatembea
Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania  (TANAPA).
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.
Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.
WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng’ombe Makao Makuu ya TALIRI. 
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
30 Oktoba, 2016

DC NDEJEMBI AZINDUA KAMPENI YA ONDOA NJAA KONGWA (ONJAKO)

October 30, 2016
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mh Deo Ndejembi akizindua kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO)
Ofisa Kilimo Mkoa wa Dodoma Bi Aziza Mumba akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Okoa Njaa Wilayani Kongwa
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Richard Mwite
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi akisisitiza vijana Kulima na kuacha kucheza mchezo wa Pool Table wakati wa kazi

Na Peter Daffi, Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deo Ndejembi ameanzisha kampeni ya kuondoa Njaa wilaya ya Kongwa, (ONJAKO) yenye dhamira ya kuwasaidia wananchi kuondokana na hali yanjaa ambayo ni kadhia kubwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo sambamba na Taifa kwa ujumla.

Kuanzishwa kwa Kampeni ya Okoa njaa Wilaya ya Kongwa imejili wakati Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa Akizungumza na Wakuuwa Idara na vitengo, Madiwani wa Kata zote zilizopo Wilayani humo, Watendaji wa Kata, Maafisa Tarafa, Waratibu Elimu Kata, Wenyeviti wa Vijiji vyote 87 vya Wilaya ya Kongwa na watendaji wao, pamoja na wadau waalikwa na Kilimo.

Akizindua kampeni hiyo Dc Ndejembi alisema kuwa Kampeni hiyo imezinduliwa Mwezi Octoba kwa ajili ya msimu wa mwaka 2016/2017 na inatarajiwa kuwa kampeni Endelevu katika kipindi cha Miaka mitano.

Ameeleza kuwa huu ni mkakati maalumu katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ili kukabiliana na hali ya Ukame ambayo ni tatizo sugu katika maeneo mengi nchini.

Kutokana na hayo DC Ndejembi ameagiza kuwa na kilimo cha Mtama zaidi kuliko Mahindi. Kwani Wilaya ya Kongwa ina Kaya 59141, na kila kaya kama ikilima Heka mbili (2) za Mtama, Mavuno itakuwa Tani 71000, za Mtama sawa na 83% ya hitaji la chakula Wilayani Kongwa.

Katika kukabiliana na njaa mahitaji mengine mahususi yametajwa ikiwa ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa mtama toka tani 1/ Hekta mwaka 2016 hadi tani3/hekta ifikapo mwezi June 2021, Kuongeza Uzalishaji wa Muhogo mbichi toka tani 6/hekta Mwaka 2016 hadi tani 10 hekta mwaka 2029, Kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti toka tani 1.2/ hekta mwaka 2016 hadi tani 1.8/hekta mwaka 2021.

Pia Mhe Ndejembi alisema kuwa mahitaji mengine ni pamoja na Kuongeza uzalishaji wa ufuta toka tani 0.5/hekta mwaka 2016 hadi tani 1.2/hekta ifikapo june 2021, pamoja na Kuongeza pato la Mtu/watu toka Tsh 500,000/= Mwaka 2016 hadi Tsh 800,000/= June 2021.

DC Ndejembi ameagiza kufanyika utaratibu wa kuhakikisha kila kaya inalima Heka zisizopungua mbili (2) za Mtama, Mbili za Mahindi, kulingana na eneo husika wakishauriwa na maafisa ugani lakini mtama ni lazima kwa kila kaya hata kama analima mahindi.

Pia amewaagiza vijana wote wasio na kazi Wilayani Kongwa wapewe Hekari mbili kila mmoja ili waache kucheza pool table na kujihusisha na vikundi Ovu vya wizi na matumizi ya Dawa za kulevya.

Saambamba na hayo Mhe Ndejembi aamepiga marufuku kuchezwa mchezo wa Pool Table mpaka ifikapo majira ya saa 10 jioni, hivyo kwa yeyote atakaye kiuka utaratibu huo atakuwa amekiuka amri halali ya serikali.

DC MUHEZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

October 30, 2016
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2
 Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiingia kwenye vyumba vya zahanati mpya ya Zeneti kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Lwiza Mlelwa
 Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia akisisistiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kushoto kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo katikati ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi

 Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi


 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiangalia baadhi ya vyoo vya Zahanati hiyo wakati alipoitembelea kuikagua na kuona namna ujenzi wake unavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akiwaonyesha kitu diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia wakati alipoitembelea Zahanati ya Zeneti
Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi  katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti akiongea kwenye ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akielezea mipango ya Halmashauri kuhusiana na kuhakikisha huduma za Afya zinawakuwa karibu na wananchi
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zeneti wakati za ziara ya Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zeneti Kata ya Potwe wilayani humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akipitia taarifa ya ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Zeneti iliyopo Kata ya Potwe wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa nne kutoka kushoto akiwasilikiza wananchi waliokuwa wakiulioza maswali kwenye ziara hiyo
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zenethi Kata ya Potwe wilaya ni Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisikiliza kero ya mmoja wa wananchi ambaye alimfuata mara baada ya kumalizika mkutano baina yake na wananchi hao kulia ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi
 Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati waliojiwekea kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto za Afya.
Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka kijijini Maisha Plus

Waziri Mwijage azindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka kijijini Maisha Plus

October 30, 2016
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa nchini Tanzania Mhe. Charles Mwijage leo amezindua rasmi mashine ya kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Maisha Plus. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo Mhe. Mwijage alisema kitendo cha washiriki hao 16 kutoka nchi tano za Afrika Mashariki kuweza kubuni mashine ni sawa na kufaulu mitihani mikubwa ya kimaisha. Alisema mashine hiyo ni mkombozi kwa watu wote wa Afrika Mashariki kwa sababu inaweza kusaga bila kutumia umeme lakini pia inamuwezesha mtu kufanya mazoezi. 2016-10-30-PHOTO-00000145 “Hii mashine ni njia mbadala ya kumuwezesha mtu kufanya mazoezi badala ya kwenda gym kufanya mazoezi utaweza kutumia mashine hii ukiwa unasaga nafaka huku unafanya mazoezi,” alisema Mwijage. 2016-10-30-PHOTO-00000148 Alisema ni vyema kwa washiriki kutumia njia hiyo kuweza kubuni mashine nyingine zaidi ili kuweza kuongeza soko la Afrika Mashariki.
Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda. 2016-10-30-PHOTO-00000147 Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho."
Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter. Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications.

RC -PAUL MAKONDA AONGOZA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE SHULE YA SEKONDARY JITEGEMEE JKT MGULANI JIJINI DAR ES SALAAM

October 30, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
RC Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti  katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo,  Samuel Ndebeto.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Wahitimu ndani ya ukumbi.
Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

"Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.

Kessy alisema kuhitimu kidato cha nne ni hatua nyingine ya kuendelea na elimu ya juu hivyo aliwataka wahitimu hao kuondoa wasiwasi katika kipindi hiki cha kuelekea kufanya mtihani wa mwisho.

Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi Paul Makonda wanafunzi hao walisema changaoto kubwa waliyonayo na uchakavu wa miundombinu shuleni hapo kama mapaa ya vyumba vya madarasa kuezekwa kwa mabati aina ya Asbestors ambayo si mazuri kiafya pamoja na uchakavu wa sakafu ambapo Makonda aliahidi kutoa mabati 2,000 kwa ajili ya kuezekea vyumba 25.

Katika hatua nyingine Makonda amezitaka shule za sekondari za jeshi katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaunda kamati kwa ajili ya kurudisha heshima ya michezo mashuleni kama ilivyokuwa awali.


 WAZIRI MAKAMBA ASISITIZA MATUMIZI YA MAJIKO BANIFU KATIKA UKAUSHAJI WA TUMBAKU

WAZIRI MAKAMBA ASISITIZA MATUMIZI YA MAJIKO BANIFU KATIKA UKAUSHAJI WA TUMBAKU

October 30, 2016

gogo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba  akifafanua jambo kuhusu wananchi waliovamia msitu wa hifadhi ya Kijiji. Kushoto ni Bi. Veronica Nyasa mkazi wa eneo hilo ambae amesema yuko tayari kuondoka endapo atapatiwa sehemu mbadala.
gogo1
Uongozi wa Wilaya ya Kaliua wakimwonyesha Waziri Makamba magogo ya miti ya asili yanayotumiwa na wanachi katika kukaushia tumbaku kwa kutumia majiko ya kienyeji
gogo2
Pichani ni moja ya majiko ya kienyeji yanayotumia kuni/miti mingi katika kukaushia tumbaku. Waziri Makamba amewaagiza wakazi wa Kitongoji cha Mtakuja Magharibi kutumia majiko banifu ili kunusuru ukataji miti kwa wingi husnan ile ya asili
…………………………………………………………………
Na Lulu Mussa-Tabora
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira hii leo ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea Mkoani Kigoma.
Akiwa Mkoani Tabora Waziri Makamba ametembelea Wilaya ya Kaliua na kukutana na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Mazingira na Uvamizi wa Misitu unaofanywa na wananchi. Katika Kijiji cha Ufugala Wilaya ya Kaliua Waziri Makamba amefanya Mkutano wa hadhara kijijini hapo na kubaini kuwa Kitongoji hicho hakikufuata taratibu za kisheria katika kuanzishwa kwake na kimeanzishwa ndani ya Hifadhi.
Akitoa maelezo ya Awali Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abel Yeji Busalama amemueleza Waziri kuwa Kitongoji hicho kiko ndani ya Hifadhi ya Msitu wa Kijiji ambapo jumla ya Vijiji 11 viamua kutenga eneo hilo kwa ajili ya Hifadhi.
Bw. Busalama amesema kuwa wakazi hao wamekwisha amriwa kuondoka katika hifadhi hiyo na utekelezaji wake unaendelea.
Akijibu hoja zilizowasilishwa na wakazi wa eneo hilo Waziri Makamba amesema kuwa wajibu wa Serikali ni kuhakikisha kuwa Sheria, tararibu na kanuni zinafuatwa bila kukiukwa.  Waziri Makamba pia amesisitiza kuwa maamuzi ya matumizi bora ya ardhi yapo mikononi mwao. “Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mliamua kutenga eneo hili maalumu kwa hifadhi ya msitu wa kijiji na kufuata taratibu zote za kisheri katika kuusajili, maamuzi yenu ya awali yatabaki palepale mpaka mtakapofuata taratibu nyinginezo.” Makamba alisisitiza.
Aidha, Waziri Makamba ameahidi kuwasilisha suala hilo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ili kupata ufumbuzi wa kudumu. “Nitaongea na Mawaziri wenzangu na kuleta timu ya wataalumu kupitia upya mipaka ya kijiji na kuifanyia kazi” Makamba alisisitiza.
Kuhusu hifadhi ya Mazingira Waziri Makamba amewataka wakazi wa Ufulaga kuacha tabia ya kukata miti ya asili  na kusisitiza kuwa uharibifu wa mazingira unabadilisha tabia za watu. “Wana Ufulaga, binadamu wakiharibu mazingira kwa kiasi kikubwa wanaanza wizi na udokozi na wanyama wataanza kuwinda watu kwa kukosa malisho” alisema Waziri Makamba.
Waziri Makamba pia amefanya ziara katika Wilaya ya Urambo na kubaini changamoto kubwa ya uvamizi wa misitu na ukataji wa miti ya asili kwa ajili ya kuni za kukaushia tumbaku.
Waziri ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutumia Sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 2004 kifungu namba 196 (1) (a na b) kupiga marufuku ya matumizi ya majiko banifu ya kienyeji pia ukataji mkubwa wa  miti ya asili kwa ajili ya biashara ya tumbaku. Katazo hilo litawahusu  Wakulima na Vyama vya Msingi vyote vinavyojishughulisha na biashara ya tumbaku.
Waziri Makamba anaendelea na ziara yake kwa kutembelea Wilaya za Nzega na Igunga.