NOOIJ ANAWEZA TUPIWA VIRAGO VYAKE JUMAPILI,

May 21, 2015
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
HATIMA ya Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuendelea na kazi au kupigwa chini, inatarajiwa kujulikana Jumapili (Mei 24, 2015).
Siku hiyo, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Rais wake, Jamal Malinzi inatarajiwa kukutana kujadili mwenendo, maandalizi na maendeleo ya timu za taifa.
Kikao hicho kinaitishwa siku moja baada ya Taifa Stars kutolewa Kombe la COSAFA kufuatia kufungwa mabao 2-0 jana na Madagascar katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace mjini Rusternburg, Afrika Kusini.
Safari imeiva; Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij anaweza kutupiwa virago Jumapili

Huo ni mchezo wa pili mfululizo timu hiyo kufungwa, baada ya awali kulala 1-0 mbele ya Swaziland Jumatatu na sasa itakamilisha ratiba Ijumaa kwa kumenyana na Lesotho kabla ya kurejea nyumbani.
Kikao hicho kinatarajiwa kuibuka na tamko la kumfuta kazi Nooij, kutokana idadi kubwa ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
Mholanzi huyo ameiongoza Stars katika mechi ya 15 jana tangu awasili mwishoni mwa Aprili kuchukua mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen ikifungwa sita, sare sita na kushinda tatu.
TFF ilihadaika na wasifu mzuri wa Nooij aliyetua Tanzania akitokea klabu ya St George ya Ethiopia Aprili mwaka jana na kumpa Mkataba mnono. 
Wasifu wa Nooij unasema amewahi kuwa mwalimu maalum katika programu za maendeleo ya soka katika Chama cha Soka Uholanzi (DFA) na pia amewahi kufundisha timu ya EVC 1913 ya Marekani na baadaye Kazakhstan.
Alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Burkina Faso katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2003 na mwaka 2004 alikuwa kocha wa muda wa klabu ya FC Volendam ya Uholanzi.
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa Msumbiji na akaiwezesha kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza Mambas wanashiriki AFCON baada ya msoto wa miaka 12. 
Hata hivyo, katika fainali hizo, Msumbiji ilishika mkia katika kundi lake baada ya kuambulia sare moja na kufungwa mechi mbili. Baada ya kukosa tiketi ya AFCON 2012, Nooij akajiuzulu Septemba mwaka 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani, Gert Engels.
Aprili 19 mwaka 2012, aliajiriwa na klabu ya Santos ya Afrika Kusini, ambako hata hivyo alifukuzwa Desemba 18, mwaka 2012 na kuhamia St George ya Ethiopia kabla ya kuja Tanzania Aprili mwaka jana.

KAMPUNI YA BONITE BOTTLERS YAMWAGA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MOSHI VIJIJINI

May 21, 2015

 
Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers
,Joyce Sengoda akiwasalimia wananchi katika vijiji vya Mikocheni
,Kilungu na Chemchem vilivyofikwa na mafuriko hivi karibuni wakati
uongozi wa kampuni hiyo ulipofika kwa ajili ya kutoa
msaada.
Meneja Masoko na mauzo na wa kampuni ya
Bonite Bottlers Ltd Christopher Loiruk akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika
vijiji hivyo.
Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya
Bonite,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa sukari kilo 750 kwa
mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi
walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi
chemi.
Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite
Bottlers Ltd ,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa maji zikiwa ni
katoni 500 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga kwa ajili
ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya
Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.
Meneja muajiri wa Bonite Bottlers ,Joyce
Sengoda akikabidhi ndoo za mafuta kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus
Makunga ambazo zimetolewa 30 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko
katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemchem.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga
akipokea msaada wa sabuni kutoka kwa meneja masoko na mauzo wa kampuni
ya Bonite Bottlers,Christopher Loiruk kwa ajili ya waathirika wa
mafuriko yaliyotokea wilaya ya Moshi vijijini.

BALOZI WA PSPF FLAVIANA MATATA ATOA ELIMU YA FURSA MBALIMBALI ZINAZOPATIKANA KATIKA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF KWA WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI JIJINI MWANZA.

May 21, 2015



  Baloziwa PSPF, Bi. Flaviana Matata akitoa elimu kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya
elimu ya juu (hawapo pichani) jijini Mwanza
 Afisa
Mfawidhi Ofisi ya PSPF Mwanza, Bw. Salim Salim, akisalimiana na Balozi wa PSPF,
Bi. Flaviana Matata, kabla ya kuanza semina ya siku moja kwa wanafunzi wa vyuo
mbalimbali vya elimu ya juu jijini Mwanza.

Baadhi
ya wanafunzi wakisoma vipeperushi vyenye taarifa kuhusu Mfuko wa PSPF wakati wa
semina juu ya Mfuko huo iliyotolewa na Balozi wa PSPF, Bi. Flaviana Matata hivi
karibuni.
Mmoja
wa wanafunzi waliohudhuria semina juu ya Mfuko huo iliyotolewa na Balozi wa
PSPF, Bi. Flaviana Matata hivi karibuni akiuliza swali ili kapata ufafanuzi.
 
  Balozi
wa PSPF, Bi. Flaviana Matata (mstari wa mbele katikati), katika picha ya pamoja
na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wa elimu ya juu jijini Mwanza baada ya kuotoa
elimu kwa wanafunzi hao juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa
mwanachama wa PSPF.

STARS YAPOTEZA MCHEZO WA PILI

STARS YAPOTEZA MCHEZO WA PILI

May 21, 2015

Wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars wakiwa katikati ya msitu wa wachezaji wa timu ya Madagascar katika mchezo wao wa jana ambapo ilifungwa magoli 2-0.  st3 
Kikosi cha timu ya Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo huo kuanza. st4 
Timu zikiingia uwanjani.
…………………………………………………………………………..
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) jana imepoteza mchezo wa pili mfululizo katika michuano ya kombe la Cosafa, baada ya kufungwa mabao 2 – 0 na Madagascar, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Royal Bafokeng jijini Rustenburg.
Kwa Taifa Stars kupoteza mchezo huo, moja kwa moja inakua imeaga michuano katika hatua ya makundi,kutokana na kubakisha mchezo mmoja tu wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho utakaochezwa kesho ijumaa katika uwanja wa Moruleng.
Katika mchezo huo wa jana, Taifa Stars ilishindwa kuonyesha makali yake mbele ya timu ya Madagascar na kupelekea kufungwa mabao 2 katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Sehemu ya ushambuliaji ya Taifa Stars haikua na madhara yoyote langoni mwa Madagascar, huku sehemu ya ulinzi iLijikuta na wakati mgumu muda wote kuzuia hatara za washambuliaji wa Madagascar.
Mara baada ya mchezo huo, kocha wa Stars Mart Noij alisema amesikitishwa na matokeo hayo, kwamba hakutegemea kupoteza mchezo dhidi ya Madagascar.
“Timu yangu haikucheza vizuri, haikuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga , huku wapinzani awetu wakitumia nafasi mbili walizozipata kupata mabao mawili katia mchezo huo” alisema Nooij.
Mpaka sasa kundi B la linaongozwa na Madagscar yenye ponti 6 sawa na Swaziland yenye pointi 6 pia zikiwa na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, na mchezo wa mwisho utakaowakutanisha kesho ndio utakaoamua nani atatinga hatua ya robo fainali.
Kufuatia Taifa Stars kupoteza michezo yote miwili, inaungana na Lesotho kutoka kundi B kuaga michuano hiyo, huku kundi A timu za Mauritius na Shelisheli zikiwa zimeshaaga michuano hiyo pia.
Stars inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kesho iumaa usiku mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Lesotho utakochezwa kesho jioni.

Wanawake waliopona Fistula CCBRT waamua kujiajiri

May 21, 2015

Baadhi ya wanawake wa kituo cha “Mabinti” kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, chini ya Hospitali ya CCBRT wakiwa darasani kujifunza elimu ya ushanoaji wa aina mbalimbali za vitu baada ya kutibiwa na kupona Fistula kupitia mradi wa matibabu unaofadhiliwa na Vodacom Foundation. Kituo hicho kinawawezesha mabinti hao kupata elimu ya kazi za mikono ili waweze kujikimu kimaisha pindi wanaporudi makwao.
Mmoja wasichana wa kituo cha “Mabinti” aliyepata kutibiwa Fistula na kupona katika Hospitali ya CCBRT Cherry David ( kulia) akiwaonesha maofisa wa Vodacom Foundation moja ya mkoba alioushana wakati walipotembelea katika kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuangalia maendeleo ya wanawake hao baada ya matibabu. Kituo hicho kinawawezesha mabinti hao kupata elimu ya kazi za mikono ili waweze kujikimu kimaisha pindi wanaporudi makwao.
Tatu Hussen wa kituo cha “Mabinti” aliyepata kutibiwa Fistula na kupona katika Hospitali ya CCBRT akionesha umahiri wa kutengeneza urembo kwenye kitambaa (screen printing) wakati maafisa wa Vodacom Foundation ambao ndio wadhamini wa mradi wa matibabu ya Fistula kupitia CCBRT walipotembelea kituo hicho kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuangalia maendeleo ya wanawake hao baada ya matibabu. Kushoto ni Mwalimu wa kituo hicho David Mkinga, Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza na Afisa wa Mawasiliano Abigail Ambweni (kulia). Kituo hicho kinawawezesha mabinti hao kupata elimu ya kazi za mikono ili waweze kujikimu kimaisha pindi wanaporudi makwao.
Mratibu wa Kituo cha Mabinti Center kilichopo chini ya Hospitali ya CCBRT Bi. Katia Geurts akiwaelezea maafisa wa Vodacom Foundation shughuli zinazofanywa na kituo hicho wakati walipotembelea kituo hicho kuangalia maendeleo ya wanawake hao baada ya matibabu. Mabinti hao wanapata elimu ya kazi za mikono mara baada ya kupona Fistula baada ya matibabu katika Hospitali ya CCBRT ili waweze kujikimu kimaisha wakati wanaporudi makwao.

Wanawake waliougua na  kutibiwa na hatimaye kupona maradhi ya fistula katika Hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam wameamua kujikita katika sanaa ya kazi za mikono kwa lengo la kujiajiri sambamba na kujikwamua na wimbi la umasikini.

Takribani wanawake wapatao 62, chini ya mpango madhubuti ulioratibiwa na hospitali ya CCBRT, wamekuwa wakihitimu mafunzo mbalimbali ya kazi za mikono zikiwemo sanaa za ushonaji wa batiki, nguo za aina tofauti, utengenezaji wa mabegi, kofia, na  ususi katika Kituo kinachoendeshwa na hospitali hiyo kijulikanacho kama ‘Mabinti Centre’ tangu mwaka 2007.

Mratibu wa Kituo hicho, Katia Geurts aliueleza ujumbe wa wafadhili kutoka Taasisi ya Vodacom Foundation waliotembelea kituo hapo kuwa  kituo  kinatoa mafunzo mahususi kwa wakinamama waliopona baada ya kusumbuliwa na fistula.

“Wengi wao wanatoka katika familia duni, hivyo mafunzo haya wanayoyapata baada ya kumaliza matibabu ya Fistula yanakwenda kuwasaidia kujiajiri wao wenyewe warudipo makwao jambo linalowasaidia kupunguza ukali wa maisha,” alisema Geurts.

Aliongeza kuwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo kituo hicho huwapatia vyeti vya uhitimu vinavyotambulika, sanjari na vitendea kazi vinavyoendana na stadi stahiki aliyohitimu mwanafunzi kwa minajiri ya kuwarahisishia upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha yao.

 Mkufunzi wa Kituo hicho ambaye awali alikuwa mmoja wa waathirika wa fistula hospitalini hapo, Tatu Hussen Jane Rugalabamu, alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu aanze kufundisha wenzake kituoni hapo amebaini kuna idadi kubwa ya wanawake wenye matatizo ya fistula ndani ya jamii lakini waume zao wamekuwa wakiwaficha kwa dhana ya kuficha aibu.

“Kuna haja kubwa ya kuelimisha akinababa wawaruhusu wake zao wenye matatizo waje kutibiwa. Fistula kwani inatibika na wala sio tatizo la kulogwa kama wengi wanavyodhani, sisi sote hapa kwenye kituo cha mabinti tulikuwa na maradhi hayo na sasa tumepona kabisa wanawake jitokezeni,” alisema Rugalabamu.

Kwa upande wake Mkuu wa Vodacom  Foundation,Renatus Rwehikiza,  baada ya kukagua shughuli mbalimbali za mafunzo zinazoendelea kituoni hapo, alisema kwa niaba ya wafanyakazi wa Vodacom na Vodafone duniani kote, wataendelea kuwasaidia akinamama wote wanaopatwa na maradhi ya Fistula hatua kwa hatua, sambamba na kuhakikisha wanazidisha kasi katika kampeni inayoendelea dhidi ya maradhi hayo.

“Tutaendelea kuwa karibu zaidi na waathirika wa Fistula kuanzia hatua ya kuwasafirisha kutoka vijijini na mikoani kwa kuwatumia fedha kupitia huduma yetu ya M-Pesa, pia tutakuwa pamoja wakati wote wa matibabu na baada ya kupona tutawaunga mkono kwenye mafunzo kama haya ili kuwaletea ustawi ulio bora kwa maisha bora kwa ajili yao na familia zao,” alisema Rwehikiza.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TATU, NCHINI CHINA, AKUTANA NA MWENYEJI WAKE MAKAKU WA RAIS WA CHINA

May 21, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati alipowasili kwenye Ukumbi Maalum kwa watu wa China. 'Peoples Great Hall', jijini Beijing China kwa ajili ya mazungumzo rasmi, alipoalikwa kwenye chakula cha jioni na Makamu wa Rais wa China baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo. jana Mei 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Serikali ya China, wakati alipowasili kwenye ukumbu Maalum wa watu wa China, 'Peoples Great Hall' kwa ajili ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, jana Mei 20, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisindikizwa na mwenyeji wake, Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Kushoto ni mkarimani wa Makamu wa Rais wa China.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, baada ya mazungumzo yao kwenye Ukumbi Maalum wa Watu wa China, jijini Beijing China. Makamu wa Rais Dkt. Bilal, amemaliza ziara yake ya siku tatu nchini China. Picha na OMR