WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

WAZIRI JAFO ATAKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KILWA KUKAMILIKA KWA WAKATI.

September 18, 2024


IMG-20240918-WA0013-1536x1024-1-1024x683Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Na.Mwandisi Wetu.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo amewashauri wananchi wa wilaya ya Kilwa kushikamana na kusimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa wilayani humo ikamilike kwa wakati na iendane na gharama halisi ili kutimiza Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha wananchi hao wananufaika na miradi hiyo.


Dkt.Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara Maalum Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

Waziri Jafo ameliagiza Shirika la Umeme (TANESCO ) kuhakikisha mradi wa nyumba za walimu (Two in One) zilizopo Kata ya Somanga zinapata umeme na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhakikisha wanajenga barabara nzuri ndani ya miezi miwili ili kuweka mazingira bora ya kuishi na kufanya kazi kwa ufanisi kwa Walimu hao.


"Naielekeza Mamlaka ya Maji Kilwa Masoko (KIMUWASA) inayosimamia Mradi wa maji katika vijiji vya Mavuji, Nangurukuru, Singino, Kivinje, Mpara na Masoko uliopo Wilayani Kilwa kusimamia Mradi huo kukamilifu na kuandaa Mpango unaonesha Mradi huo utakamilika lini na kuwasilisha katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi ndani ya Wiki mbili (2) ili kuhakikisha Mradi huo unaleta manufaa yanayotarajiwa kwa Wananchi wa Kilwa."amesisitiza Dkt.Jafo

Aidha, Dkt Jafo amebainisha kuwa ujenzi wa Mradi wa Bandari ya Uvuvi unaolenga kurahisisha upatikanaji wa Samaki, Soko na kukuza biashara uchumi kwa ujumla pamoja ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo, Kipimimbi unaendelea kwa kasi , unaendana na gharama iliyopangwa na hivyo kufikia malengo yanayotarajiwa na Wananchi wa Kilwa.

Akiongea na Wananchi wa Kipimindi Wilayani Kilwa Dkt Jafo amewapongeza wananchi wa Wilaya hiyo kwa kutumia Mfumo wa stakabadhi gharani hususani katika mazao ya ufuta na mbaazi na kupata mafanikio makubwa katika kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi kwa bei inayoridhisha na kuchangia katika kukuza biashara na kuongeza pato la Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo inayolenga kuleta manufaa makubwa kwa Wananchi wa Mkoa huo na kuwaomba kutumia fursa za miradi hiyo ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

IMG-20240918-WA0005-1024x682

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Lindi kwa jaili ya kufanya ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

IMG-20240917-WA0032-1-1024x682 IMG-20240917-WA0035-1-1024x682 IMG-20240917-WA0036-1-1024x682

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Kilwa, Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Somanga iliyopo Kata ya Somanga, alipotembelea Shule hiyo kujionea Mradi wa ujenzi wa nyumba za Walimu (two in one) wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".



IMG-20240918-WA0011-1024x682 IMG-20240918-WA0013-1024x682

IMG-20240918-WA0009-1024x682

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakitembelea mradi wa bandari ya Uvuvi uliopo Kilwa Masoko wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

IMG-20240918-WA0016-1024x682 IMG-20240918-WA0019-1024x682

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akiwa na viongozi wakikagua ujenzi wa Mradi wa Maji mavuji,Nangurukuru,Singino,Kivinje,Mpara ,Masoko uliopo wilayani Kilwa wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

IMG-20240918-WA0018-1024x682



IMG-20240918-WA0024-1024x682IMG-20240918-WA0026-1024x682

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi wa Kipimindi wilayani Kilwa baada ya kutembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Njinjo Mkoani humo wakati wa ziara Maalum Mkoani humo yenye lengo la kukagua utekekelezaji wa Miradi ya maendeleo chini ya kauli mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone".

RAIS MSTAAFU DKT KIKWETE YUKO BOSTON KUTOA MAFUNZO KWA MAWAZIRI WA AFYA NA ELIMU TOKA NCHI ZINAZOENDELEA KUPITIA MPANGO WA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA HAVARD, MAREKANI

September 18, 2024

 

Mheshimiwa Rais Mstaafu wa Jmhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho, yuko mjini Boston, Marekani ambapo anashiriki katika kutoa mafunzo kwa Mawaziri wa Afya na Elimu kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Harvard  (Harvard Ministerial Leadership Program)  inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.


 Mheshimiwa Dkt. Kikwete ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanoshiriki kutoa mafunzo hayo.


Akiwa Boston, Mheshimiwa Dkt. Kikwete amekutana na baadhi ya wanafunzi Watanzania wanaosoma hatua mbalimbali za elimu hapo katika Chuo Kikuu cha Harvard.

BENKI YA NMB YAPIGA JEKI ZAHANATI YA KIJIJI CHA IVILIKINGE WILAYA YA MAKETE

September 18, 2024

 Na Mwandishi wetu, Makete.


Benki ya NMB imekabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda na mashuka katika Zahanati ya Kijiji cha Ivilikinge wilyani Makete mkoani Njombe vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Willy Mponzi alisema benki hiyo kila mwaka imekuwa na utamaduni wa kutenga asilimia moja ya pato lake baada ya makato ya kodi kwa lengo la kurudisha kwa jamii.

“Msaada huu ambao leo tumekabidhi Makete pia tumekuwa tunakabidhi katika sehemu mbalimbali katika nchi yetu na huu msaada umehusisha vifaa tiba,” amesema Mponzi.

Alisema awali wakati zahanati hiyo inaanza ujenzi, benki hiyo pia ilichangia bati zenye thamani ya milioni nane.

Aidha alisema kuwa, kwa miaka kadhaa sasa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu ambayo inahusisha madawati, vifaa vya kuezekea lakini kwenye vituo vya afya wametoa vitanda, magodolo na vifaa vyengine vya matibabu.

"Na pia benki ya NMB tumekuwa tukisaidia nchi yetu kwa majanga mbalimbali, tunatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka," amesema Mponzi.

Naye Katibu wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA), Award Mpandila aliishukuru NMB kwa msaada huo na kuwaomba kuendelea kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya NMB na wananchi.

Kwa Upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana aliishukuru benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi na kuwataka kuendelea kushirikiana ili kuleta tija kwa taifa.

Awali Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Ivilikinge, Hassan Yusuph alisema mara baada ya wananchi kuibua mradi wa ujenzi zahanati benki ya NMB iliwasaidia bati yenye thamani ya shilingi milioni nane.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Makete, Juma Sweda aliiomba benki ya NMB kuwaunga mkono pia kwenye ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa zahanati hiyo.