TIMU ZA DAR ZAJITOKEZA KWA WINGI USHIRIKI MICHUANO YA KIKAPU

TIMU ZA DAR ZAJITOKEZA KWA WINGI USHIRIKI MICHUANO YA KIKAPU

May 15, 2017
20170513_141607
Kiongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Weusi Basketball Club ya jijini Dar es Salaam, Mntambo Mngeja (kulia) akipata maelekezo ya juu ya kujiandikisha kutoka kwa mratibu ya michuano ya Sprite Bball Kings, Basilisa Biseko wakati wa zoezi la uandikishaji wa timu mbalimbali kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo. Uandikishaji ulifanyika Tegeta Complex jijini Dar es Salaam huku timu zaidi ya 20 zikijitokeza kujiandikisha. Michuani ya Sprite Bball Kings inaendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa udhamini wakampuni ya Coca-Cola.
Na Mwandishi Wetu, Dar.
Ikiwa ni siku ya kwanza kwa timu mbali mbali za michuani ya kikapu ya Bball Kings, zaidi ya timu 20 zimejitokeza kujiandikisha mwishoni mwa wiki hii wakati wa zoezi la uandikishaji linaloendelea jijini Dar es Salaam.
Michuani ya mchezo wa kikapu ya Bball Kings inayoendeshwa na kituo cha Televisheni na Radio cha East Africa (EATV/Radio) kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji chake cha Sprite siku ya jumamosi imeshuhudia wawakilishi wa timu mbalimbali wakijitokeza na kujaza fomu za ushiriki, huku wawakilishi wa timu hizo wakijigamba kujidhatiti kikamilifu kuchukua ubingwa wa mwaka huu.
Kati ya timu zilizojitokeza ni pamoja na Cavarious, Lycans, Tegeta Camp, Lord Baden, K-Warriors, DMI, St Joseph na MJ Junior.
Nyingine ni Oilers, TMT, Mchenga, Bahari Beach, Street Boys, Street Warriors, Chanika Legends, God With Us, Weusi Basketball Club, Junior Basketball Club na Celestial Basketball Team.
Akizungumza wakati wa uandikishaji wa timu shiriki, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa wa EATV, Roy Mbowe alisema mwitikio wa timu mbalimbali umejaa hamasa kubwa na wa kuridhisha, huku kila timu iliyojitokeza ikiwa na wachezaji wasiozidi 10.
“Mashindano hayo yanahusu vijana wenye umri wa kuanzia miaka 16 na watapaswa kuunda timu ya wachezaji 10 ambao watachuana na timu nyingine zitakazokuwa zimejiandikisha, huku tukitoa fursa katika wachezaji hao 10, timu inaweza kuwa na wachezaji wasiozidi watatu kutoka katika timu kubwa za Ligi Darasa la Kwanza za za kikapu za hapa nchini,’’alisema Mbowe.
Michuano ya Sprite Bball Kings itaendeshwa kwa njia ya mtoano katika hatua ya kwanza ili kupata timu 16 zitakazoingia hatua ya pili na kutaja zawadi kwa timu itakayotwaa ubingwa itakuwa ni Sh.milioni 10 wakati mshindi wa pili atapata Sh.milioni tatu huku pia kukiwa na zawadi ya Sh milioni mbili kwa mchezaji bora (MVP).
Mashindano hayo yatakayoshirikisha wachezaji kutoka mikoa yote nchini, yanatarajiwa kuanza mwezi huu na kumalizika Julai mwanzoni.
MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 25, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 15, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 25, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 15, 2017

May 15, 2017
NGE2
Baadhi ya wabunge wakiwa Bungeni leo
NGE3
Naibu Waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Suleiman Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 15, 2017
NGE4
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Prof Sospeter Muhongo akizungumza jambo na Mbunge wa Nkasi Mhe.Ally Kessy katika  kikao cha Ishirini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 13, 2017.
NGE5
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 15, 2017
NGE6
Naibu Waziri  wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 15, 2017
NGE7
Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Prof Sospeter Muhongo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 15, 2017
NGE8
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe katika  kikao cha Ishirini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 13, 2017.
NGE9
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 15, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA TANGA ALHAJI MUSSA MBARUKU ATEMBELEA KUONA ATHARI ZA MAFURIKO ENEO LA NEEMA DARAJANI

May 15, 2017
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akiteta jambo na mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga eneo la Neema mara baada ya kukutana njiani wakati mbunge huyo alipokwenda kukagua kujionea athari zilizotokana na mvua kubwa iliyonyesha kulia ni Diwani wa Kata ya Mnyanjani (CUF) Thobias Haule
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akisisitiza jambo wakati alipotembelea eneo la Neema kujionea athari za uharibifu wa barabara ya Tanga hadi Pangani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kusababisha barabara hiyo kutokupitika
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku wa kwanza kulia akiangalia athari za miundombinu ya barabara ya Tanga hadi Pangani katika eneo la Neema ambako alikwenda kuangalia namna ilivyoharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitazama
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea kujionea athari za barabara hiyo
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akisalimiana na wananchi wa Tangasisi
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akipata maelekezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Bacc Technicla co.Ltd ya Mkoani Dodoma , Husein Bakeme kuhusu namna wanayofanya kuondoa adha hiyo
 Creda likiendelea kufanya kazi ya kurekebisha barabara ya Tanga -Pangani eneo la Neema ambalo lilikuwa halipitiki kutokana na kuharibika vibaya na kusababisha magari kushindwa kupita
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akitembelea eneo la Neema
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Masiwani kushoto wakati walipotembelea eneo la Neema kujionea athari za barabara kutokana na mvua zilizonyesha
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia akiwa na diwani wa Kata ya Masiwani Said Alei wakati akitembelea eneo la Neema ambalo limeathirika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha mkoani Tanga
 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisalimiana na wananchi wa Jimbo lake
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akiteta jambo na wapiga kura wake mara baada ya kutembelea eneo la Neema ambalo limeathirika kwa miundombinu ya barabara kuharibika kutokana na mvua kubwa zilizonyesha jijini Tanga
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI YAWABANA WATUMIAJI WA STIKA ZA BIMA BANDIA

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI YAWABANA WATUMIAJI WA STIKA ZA BIMA BANDIA

May 15, 2017
unnamed
ASKARI wa usalama barabarani wilayani Kibaha mkoani Pwani wakisikiliza elimu juu ya matumizi ya mfumo wa kubaini stika bandia kwa magari mbalimbali,mfumo ulianzishwa na mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
A
kamishna wa mamlaka ya usimamizi wa bima nchini,dr.Baghayo Saqware ,wa kwanza kulia akieleza jambo kwa askari wa usalama barabarani eneo la Mailmoja Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)
A 2
Jopo la wajumbe kutoka mamlaka ya usimamizi wa bima nchini wakihakiki stika za bima katika moja ya lori eneo la mizani Mailmoja Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)
…………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA),imeanza kampeni endelevu ya kuhakiki magari yenye stika za bima bandia ili kuondoa wimbi la stika hizo ambalo hulisababishia serikali kukosa mapato.
WALIMU WA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) NA VYUO BINAFSI VYA AFYA WAANDALIWA MAFUNZO YA MAADILI

WALIMU WA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) NA VYUO BINAFSI VYA AFYA WAANDALIWA MAFUNZO YA MAADILI

May 15, 2017
unnamed
Kaimu Naibu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Bi. Amina Abdulkadir akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman kufungua warsha ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli hiyo na viongozi wa wauguzi wa Hospitali za Serikali na Binafsi huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
A
Waziri wa Afya Harusi Saidi Suleiman akisisitiza maadili kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya afya wakati akifungua warsha ya siku nne ya maadili na utafiti kwa walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi katika skuli hiyo iliopo Mbweni.
A 1
Baadhi ya washiriki wa warsha ya maadili na utafiti  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo inayofanyika Skuli ya afya na Sayansi za tiba Mbweni.
A 2
 Mkuu wa Idara ya Uuguzi Mwanaisha Juma Fakih  akisoma malengo makuu ya warsha hiyo inayowashirikisha walimu wa Skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi wa hospitali za serikali na hospitali binafasi Mbweni.
A 3
Kaimu Mkuu wa Skuli ya afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Salum Seif akitoa neno la shukrani baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo katika skuli hiyo iliyopo Mbweni.
A 4
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya (wa kati kati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya maadili na utafiti inayofanyika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.
………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi Said Suleiman ameiagiza Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kufanya tafiti kujua chanzo cha mmongonyoko wa maadili kwa wafanyakazi wa afya wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.
Alishauri baada ya kupata majibu ya tafiti hizo kuishauri serikali hatua ya kuchukuliwa ili kuinusuru hadhi ya taaluma ya afya ambayo inajengeka katika misingi ya ukarimu na kutoa huduma bila upendeleo.
 Naibu Waziri ametoa maagizo hayo alipokuwa akifungua warsha ya siku nne juu ya Maadili na Utafiti kwa wakufunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na viongozi wa wauguzi wa Hospitali binafsi na Serikali  katika skuli hiyo  iliopo Mbweni.
Alisema watendaji wa Hospitali na vituo vya afya na hasa vya Serikali baadhi yao wanakiuka maadili ya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha mbaya
Alisema tatizo la unyanyasaji wagonjwa limekuwa kubwa zaidi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo ni tegemeo kubwa la wananchi wa Zanaizbar.
Aliongeza kuwa jambo la kusikitisha ni kuwa wafanyakazi wa hospitali za serikali ambao wamekuwa wakilaumiwa kwa kukiuka maadili wanapokuwa katika vituo binafsi wanakuwa ni mfano wa kuigwa kwa tabia njema.
Hata hivyo Bi. Harusi aliwataka walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba kuwa mfano bora wa maadili na kuimarisha somo hilo kwa wanafunzi wao ili kurudisha hadhi ya taaluma ya afya na wananchi waendelee kuwaamini.
Kaimu mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba Dkt. Salum Seif alisema somo la maadli ni moja kati ya masomo yanayopewa kipaumbele katika skuli hiyo lakini kupata elimu ni jamabo moja na kuitumia elimu uliyonayo ni jambo jengine.  
 Alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa watakuwa waangalifu na kuongeza udadisi katika sulala la maadili kwa wanafunzi wanaomba kujiunga na Skuli hiyo na atakaeonekana hawezi kukidhi kigenzo watamuacha.
Alisema tatizo kubwa linalochangia ukosefu wa maadili Zanzibar ni watu kuoneana muhali kutokana na kujuana sana na kupelekea kuzifumbia macho sheria zilizopo.
RAIS DKT. MAGUFULI AIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU CDA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS DKT. MAGUFULI AIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU CDA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

May 15, 2017
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilikiza viongozi mbalimbali waliokuwa wakichangia mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi kuhusu uamuzi wake wa kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Z
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kusaini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 5
Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakifatilia kwa makini Hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutia saini Amri ya Rais (Presidential Order) kuifuta   Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDADodoma ,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Waziri wa Katiba na Sheria akisoma Rasimu ya Amri ya Rais (Presidential Order) kabla ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuisaini ili kuifuta, Ikulu jijini Dar es Salaam.
A
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ardhi William Lukuvi wakifatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza mara baada ya kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 1
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika kikao hicho.
A 2
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika kikao hicho.
A 3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Waziri wa Ardhi William Lukuvi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma Adam Kimbisa mara baada ya kuifuta Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA,tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
A 5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa CDA Eng. Paskasi Muragili mara baada ya kuifuta mamlaka hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU