DKT MAHIGA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUWAANDALIA MABALOZI MCHAPALO WA MWAKA MPYA (SHERRY PARTY) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

DKT MAHIGA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KUWAANDALIA MABALOZI MCHAPALO WA MWAKA MPYA (SHERRY PARTY) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

February 08, 2016


3 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya kwa Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa maarufu kama “Sherry Party” Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 8, 2016
4 5 
Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Kimtaifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika Mchapalo wa Mwaka Mpya maarufu kama “Sherry Party” Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatatu February 8, 2016
6 
Picha ya pamoja.
MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIRY HOSPITALI MUHIMBILI

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AMTEMBELEA MUFTI MKUU WA TANZANIA SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIRY HOSPITALI MUHIMBILI

February 08, 2016

1 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe George Masaju pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi
leo Jumatatu February 8, 2016
2 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisindikizwa wakati wa kuondoka baada ya kumjulia hali Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry aliyelazwa kwa matibabu katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Pamoja naye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi
leo Jumatatu February 8, 2016
PICHA NA IKULU

MKUU WA WILAYA YA HAI,ANTHONY MTAKA ATEMBELEA KIWANDA CHA MAZIWA CHA KINA MAMA WA NRONGA WILAYANI HAI.

February 08, 2016
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiongozana na Mchungaji wa Usharika wa Nronga,Jorome Kimaro ,kulia kwake ni katibu na meneja wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga Heln Ainea alipotembelea Chma hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akiteta jambo na Katibu wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga  Helen Ainea wakati wa mkutano mkuu wa 28 wa Ushirika huo uliofanyika katika kiwanda cha zamani cha maziwa cha ushirika huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza na wanachama wa chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wakati wa mkutano mkuu wa 28 wa Ushirika huo.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga.
Baba Mchungaji wa Usharika wa Nronga,Jorome Kimaro akitoa neno wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 28 wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga.
Baadhi ya wanachama.
Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wilayani Hai,Apansia Lema akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi katika mkutano wa 28 wa chama hicho.
Baadhi ya wanachama wa chama cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wakimpongeza mgeni rasmi ,mkuu wa wilaya ya Hai,Athony Mtaka mara baada ya kutoa hotuba yake ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto zinazoukabili ushirika huo papo hapo.
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka alipotembelea kiwanda hicho.
Kiwanda cha kwanza cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga kilichopo Nronga-Machame wilayani Hai.
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimmuonesha Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka maeneo mbalimbali yanayotumika katika uandaaji wa maziwa katika kiwanda hicho.
Katibu na Meneja wa Ushirika wa Maziwa wa Nronga,Helen Ainea akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka alipotembelea kiwanda hicho
Mkuu wa wilaya ya Hai,Athony Mtaka akitizama bidhaa ya maziwa katika kiwanda cha Ushirika huo kilichopo Nronga -Machame.
Bidhaa ya Maziwa ya Chama cha Ushirika cha Nronga .
Kiwanda cha Maziwa cha Ushirika wa Maziwa cha Nronga wilayani Hai,
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo na Mwandishi wa habari James Paul alipotembelea kiwanda hicho.
DC Mtaka akiangalia mja ya mtambo unaotumika katika uandaji wa Maziwa katika kiwanda cha Ushirika wa Maziwa wa Nronga.
Sehemu ya mitambo hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

NEC YASEMA ELIMU YA MPIGA KURA HAIKUWAFIKIA BAADHI YA WANANCHI NCHINI.

February 08, 2016
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imebainisha kwamba, ukosefu wa elimu ya kutosha kwa Wapiga Kura, ulisababisha mapungufu mbalimbali kujitokeza katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25 Mwaka jana.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani (Pichani juu) aliyasema hayo jana Jijini Mwanza, katika Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.

Ramadhani alisema katika baadhi ya Kata nchini, kulitokea mapungufu kadhaa katika zoezi la kupiga kura ikiwemo Kura kuharibika kutokana na wapiga kura kuchora michoro na alaza zisizostahili katika karatasi ya kupigia kura huku baadhi yao wakiandika matusi katika karatasi hizo.

Hata hivyo Kailima alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa elimu kwa mpiga kura, lilishindwa kufanikiwa zaidi kutokana na baadhi ya Asasi za kiraia nchini kutoa elimu kinyume na mwongozi wa NEC, ambapo baadhi ya Asasi hizo zilikuwa zikitoa elimu ya mpiga kura kwa kuangazia zaidi matakwa ya wafadhiri wake.

Edwin Soko ambae ni mmoja wa Wadau kutoka Asasi zilizohudhuria katika Mkutano huo ambao umejumuisha Asasi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka jana, Asasi nyingi hazikuweza kuyafikia maeneo mengi hususani vijijini kwa ajili ya Kutoa elimu ya Mpiga kura, hii ikiwa ni kutokana na ukosefu wa fedha ambapo wameishauri Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa asasi hizo ili kutoa elimu hiyo katika chaguzi zijazo.

Kando ya Tathmini hiyo, Suala la Kuahirishwa kwa Uchaguzi Visiwani Zanzibar likajitokeza, ambapo Wanahabari walitaka kujua sababu za Uchaguzi huo kuahirishwa, na hapo ndipo Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC akatumia tena fursa hiyo kufafanua kwamba Uchaguzi Visiwani Zanzibar uliahirishwa na Tume ya Uchaguzi Visiwani humo ZEC kutokana na tume hiyo kubaini kasoro kadhaa katika karatasi zake za wapiga kura, kasoro ambazo hata hivyo hazikujitokeza katika karatasi zilizokuwa zikisimamiwa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC ikizingatiwa kwamba ZEC na NEC ni tume mbili tofauti zisizoingiliana katika majukumu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akifungua Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wanahabari na Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Geita.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Kagera.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mwanza.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Shinyanga.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mara.
Kutoka Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju (Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC), Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Simiyu.

TANZANIA KUENDELEZA UTAFITI WA BIOTEKNOLOJIA

February 08, 2016

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Uvuvi, Dk. Florens Turuka (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Wema wa siku tatu wa watafiti kutoka nchi za Afrika wa kutathimini utendaji kazi wa Wema kwa mwaka uliopitaKushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Uharishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Dk. Denis Kyetere na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda.
Mkurugenzi wa Ushirikiano Mradi wa Wema, Kampuni ya Monsanto, Mark Edge (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa Mkuu wa Programu, Taasisi ya Bill and Melinda Gates Dk.Lawrence Kent (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mradi wa Wema, Shirika la Kimataifa la Uhaurishaji wa Teknolojia za Kilimo (AATF), Sylvester Oikeh akizungumza katika mkutano huo.
Mtafiti wa Mahindi, Shirika la Kimataifa la utafiti wa ngano na mahindi (CIMMYT), Yoseph Beyene akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja Mfumo na Uzalishaji wa Mbegu (AATF), Gospel Omanya akitoa mada katika mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Watafiti na washiriki wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu za utafiti.
Watafiti na washiriki wakiwa Busy na nyaraka.
Watafiti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florens Turuka amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza utafiti wa bioteknojia pamoja na kutekeleza mradi wa WEMA kwa hatua. Mradi huo unajishughulisha na utafiti wa mbegu za mahindi nchini.


Turuka ameyasema hayo kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, wakati akifungua mkutano wa nane wa mradi wa mahindi  yanayostahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa WEMA, leo asubuhi jijini Dar es salaam. Mkutano huo wasiku tatu umewaleta pamoja watafiti kutoka nchi za Afrika, kutathimini utendaji kazi wa mradi kwa mwaka uliopita.


Alisema awamu ya utafiti wa njia ya kawaida wa mahindi imekamilika na aina  sita mpya za mahindi zimepatikana na kuwa hivi sasa kwa kufuata kanuni za usalama wa viumbe, itaanza utafiti wa mahindi kwa njia ya  uhandisi jeni.


"Sera na kanuni zipo, tutafanya utafiti wa GMO na matokeo ya utafiti yatatoa mwongozo wa dira yetu ya kilimo" alisema Dk. Turuka.


Katika hatua nyingine Dk. Turuka amewataka watafiti wa mbegu za mahindi nchini kuhakikisha mbegu bora walizozifanyia utafiti zinawafikia wakulima kwa wakati.


"Serikali inafurahishwa na mradi huu wa WEMA kwani unamsaidia mkulima kupata mbegu bora ambazo zinahimili ukame na haziwezi kushambuliwa na magonjwa" alisema Dk.Turuka.


Alisema kwa kutumia mbegu bora zilizotokana na utafiti huo mkulima anaweza kupata tani 8.5 za mahindi kwa ekari moja na kusisitiza kuwa mbegu hizo zisipo mfikia mkulima kwa wakati mradi huo utakuwa haujaisaidia serikali.


Dk. Turuka alisema serikali inaangalia kwa karibu sheria na kanuni za kuwapa uwanja mpana watafiti bila ya kuharibu mazingira na kuhatarisha maisha ya wananchi wakati wa kufanya tafiti zao.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda alisema tafiti hizo za mbegu zinatoa nafasi kwa wakulima kupata mbegu bora na kuwa utafiti huo uliofanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka nchi mbalimbali umeonesha mafanikio makubwa.


Mratibu wa mradi huo wa WEMA, Dk.Alois Kullaya alisema mradi huo ulianza mwaka 2008 na kuwa wamekuwa wakitumia mbinu za kisasa kupata mbegu bora.


Alisema Tanzania na nchi nyingine tayari zimepasisha mbegu 59 ambapo kwa hapa nchini zipo mbegu sita tu ambazo zinazalishwa.



Aliongeza kuwa kwa nchi ya Afrika Kusini wao tayari wameidhinisha matumizi ya mbegu za GMO.