UPATIKANAJI WA DAWA KWENYE VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA WAFIKIA ASILIMIA 80

June 20, 2017
 Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga akifungua mafunzo ya  mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri mjini Tanga kulia ni Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga
Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika mjini hapa  ambapo
alisema asilimia 70 wakina mama wajawazito wamejiunga na mradi wa tumaini la mama kwa ajili ya kupata matibabu
 Mwezeshaji wa mafunzo wa Tumaini la Mama,Ally Omari akisisitiza jambo wakati  akitoa somo kwenye mafunzo hayo


Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa Tumaini la Mama Tanzania Irine Meaki akielezea masuala mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Jiji. 
 Baadhi ya wauguzi  wanaohudumia wakina anama wajawazito wakimsikiliza mgeni rasmi wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.



Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
 Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo

UPATIKANAJI wa dawa kwenye vituo vya Afya kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga umeelezwa kufikia asilimia 80 kwa wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu wakiwemo wanaohudumiwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.

Alisema upatikanaji huo wa dawa umesaidia kuweza kuwadumia wakina mama wajawazito ambao wamekuwa wakijitokeza kupata huduma za matibabu na vifaa tiba pamoja na wategemezi wao.

Aidha alisema jambo hilo limeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kuondokana na vifo vya wakina mama wajawazito ambavyo vilikuwa vikijitokeze kutokana na kukosa huduma muhimu za matibabu wakati wanapojifungua.

Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo watoa huduma wanapaswa kuweka mipango mizuri ya kuwahudumia wakina mama wajawazito wakati wanapofika kwenye vituo vyao vya afya ili waweze kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali walizokuwa nazo.

“Mradi huu una zaidi ya miaka minne nyie kama watoa huduma mnauzoefu mkubwa hivyo kupitia mafunzo hayo jaribuni kushirikiana na wawezeshaji kuhusu changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wake “Alisema.

Aidha pia aliwataka watoa huduma wafanye uhamasishaji mkubwa kwa wakina mama wajawazito waliopo kwenye maeneo yao kwa lengo la kuongeza wigo mpana wa kuwaandikisha kwenye mradi huo ambao ni muhimu kwao.

Akichangia wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo,Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani Mkinga Elizaberth Dickson alisema moja kati ya changamoto kubwa zilizopo hivi sasa ni ucheleweshwaji wa kadi za bima ya afya kwa wakina mama wajawazito jambo ambalo linakwamisha huduma kwa baadhi yao wanapohitaji
matibabu.

“Lakini nisema upatikanaji wa kadi za mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wakina mama wajawazito na wategemezi kwa wakati zitarahisisha upatinaji wa huduma za matibabu katika vituo mbalimbali vya afya ndani na nje ya mkoa”Alisema

Katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakina mama wengi mkoani Tanga, Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo aliwataka watoa huduma kuihamasisha jamii kuona umuhimu wa kuajiandikisha katika vituo vya afya wakati wa ujauzito kupitia mradi huo

“Kwani kujiandikisha huko wanaweza kupata fursa muhimu ya kupitia mradi wa tumaini la mama kwa kupata huduma za matibabu wao na wategemezi wao kwenye vituo vya afya “Alisema.

Aidha alisema kwa mkoa wa Tanga tayari wamekwisha kuandikisha wakina mama wajawazito asilimia 70 ambao wananufaika kupitia mpango huo ambao una lengo la kupambana na vifo wakati wanapojifungua.
RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAHA MKOA WA PWANI

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAHA MKOA WA PWANI

June 20, 2017
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Bondeni Mjini Kibaha kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Pwani.
1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu
Mkoani humo.
2
Mmoja wa Wananchi akionesha hisia zake wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kibaha Maili moja katika Viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwananchi Azilongwa Buhali alipokuwa akimuelezea shida yake mara baada ya kuhutubia wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
5
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano huo.
6
Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
7
Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mjini Kibaha. PICHA NA IKULU

Dk. Kigwangalla “Nasimama na Rais wangu”, afunguka mapambano ya rasilimali za Taifa

June 20, 2017
Kupitia ukurasa wa kijamii wa twitter wa Mbunge wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ameweka wazi kuwa daima ataendelea kupambana dhidi ya rasilimali za umma, kwani amekuwa mwanaharakati kwa muda mrefu. “Tuliopinga wizi wa madini yetu tulibezwa, tulikamatwa kama wezi; tuliswekwa ndani, tulionekana wasaliti. Leo kiko wapi? #NasimamaNaRaisWangu" aliandika Dk. Kigwangalla huku watu mbalimbali wakitoa maoni yao. Kwa mujibu wa Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, suala la kupambana na rasilimali za Taifa alilianza miaka mingi kwani miongoni mwa matukio makubwa ni la 2013, ambapo alijitolea kupambana kudai haki tukio lililopelekea kutiwa nguvuni na Jeshi la Polisi. Mtandao huu ulipowasiliana na Dk. Kigwangalla ambaye yupo Bungeni Mjini Dodoma, alibainisha kuwa, katika kupigania maslai Taifa ataendelea kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli mwanzo mwisho kwani ni moja ya matunda ya nchi yoyote ile Duniani, kiongozi Mkuu lazima alinde na kupigania rasilimali za nchi, hivyo akiwa Mtanzania na kiongozi mwenye dhamana anaunga juhudi hizo bila kuchola. "Tulipambana na tunaendelea kupambana. 2013/4 Nilipambana na kudai haki kwa wachimbaji wadogowadogo na wale waliokuwa wakitunyonya katika migodi yetu, ikiwemo mgidi wa Resolute uliojulikana kama Nzega Golden Pride Project. Tulipambana tulibezwa na hata kulala mahabusu kwa kupambana na rasilimali zetu, leo hii tumepata kiongozi mkuu mwenye uchungu na taifa ili, lazima tumuunge mkono" alieleza Dk. Kigwangalla kwa njia ya simu na mtandao huu. Tazama VIDEO la tukio lingine la Dk. Kigwangalla alivyosimamia masuala ya risilimali Bungeni:
Ujumbe wake huo..
Baadhi ya maoni ya watu
Dk. Kigwangalla akiwa ametiwa nguvuni wakati wa kusimamia haki ulinzi wa migodi jimboni kwake, Nzega, Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEMBELEA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE KUHIMIZA UWAJIBIKAJI

June 20, 2017
 Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazohusu  menejimenti ya  Rasilimaliwatu serikalini kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi za  Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka.
 Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakizungumza masuala ya kiutumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2017.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Bi. Amina Kiwanuka akieleza utekelezaji wa masuala ya kiutumishi katika eneo lake la   kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma waliomtembelea ofisini kwake leo alasiri kuhimiza uwajibikaji ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
 Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bw. Abdullfariq Mkata (wa pili kulia) akitoa taarifa  ya kiutendaji ya Idara yake kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma walipoitembelea Halmashauri hiyo leo kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais,Menenimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kiutumishi  kwa Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka ofisini kwa mkurugenzi huyo leo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Amina Kiwanuka akisikiliza kwa makini.

NGULI WA TIMU ZA TAIFA ZA WANAWAKE DUNIANI KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KATIKA KRETA YA MLIMA KILIMANJARO

June 20, 2017
Baadhi ya wapagazi Zaidi ya 300 wakijiandaa kwa ajili ya safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro katika Lango la Lemosho kusindikiza ugeni wa kund la wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali nchini .
Wachezaji wa timu za taifa kutoka mataifa mbalimbali nchini ,wakishuka katika gari mara baada ya kuwasili katika lango la Lemosho kwa ajili ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuweka historia ya kucheza mchezo a kirafiki eneo la Kreta katika kilele cha Uhuru.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ,Twiga Stras ambaye kwa sasa anakipiga timu ya IFA Academy ya nchini Dubai,Rajvi Ladha akifurahia jambo na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Geofrey Tengeneza.
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania ,Twiga Stars ,Rajvi Ladha akiandika jambo muda mfupi baada ya kuzungumza na wanahabari juu ya mchezo huo ,
Wachezaji wa timu za Volcano fc na Gracier fc wakikamilisha taratibu kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakao pigwa June 26 mwaka huu katika kilele cha Uhuru.
Afisa Uhusiano Mkuu wa TTB ,Geofrey Tengeneza akipata taswira ya pamoja na wachezaji hao.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini,TTB Geofrey Tengeneza akieleza jambo kwa wachezaji hao muda mfupi kabla ya kuanza safafri ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mwakilishi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Willy Lyimo akizungumza na wachezaji hao kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza safari ya kupanda Mlima Kilimanjao.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.


MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA HAI ASHIKILIWA NA POLISI KWA SAA TANO BAADA YA KUMALIZA KIKAO CHA BARAZA

June 20, 2017
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Hela Mchomvu (Kulia) akiingia katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa ajili kuongoza kikao cha baraza hilo.Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai,Hela Mchomvu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Yahana Sintoo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya Madiwani wanaounda baraza la Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao cha baraza hilo.
Diwani Harry Masakia akisoma kanuni za kudumu za Halmashauri wakati wa kikao cha baraza hilo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akitoka nje ya ukumbi wa mikutno mara baada a kuhairisha kikao cha baraza hilo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,akizungumza na askari Polisi waliokuwa nje ya ukumbi wakimsubiri kwa ajili ya kumfikisha kituo cha Polisi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu akiongozana na askari Polisi wakati akilekea ofsiini kwake.
Askari Polisi wakiomngojea Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Helga Mchomvu nje ya ofisi yake .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai ,Helga Mchomvu akieleka kito cha Polisi huku  akisindikizwa ana askari Polisi.
Mwenyekiti wa Halmahauri ya wilaya ya Hai ,Helga Mchomvu akiingia kituo cha Polisi Bomang'ombe.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.