WAZIRI MAKAMBA AKATAZA UCHEPUSHAJI WA VYANZA VYA MAJI

October 22, 2016





 Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika. 



Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo vya dola.

 Na Lulu Mussa,Songwe

Wakazi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.
Akiwa katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia kutumika mamlaka ya Dola. "Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya Maji na kuwabembeleza watoke" Makamba alilisitiza.
Waziri Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira Nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.
Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.

KAMPENI YA KUPIGA VITA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI YA BINTI WA KITAA YAFANYIKA TABATA JIJINI DAR

October 22, 2016
Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto  wao.
Furahini Michael akiulizwa swali na Bwana Steven Mfuko kuhusu athari za mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo.
 Mkazi wa Tabata kwa Cecy ambapo kampeni ya Binti wa kitaa ilifanyika Bi.Sheira Mheni akielezea jinsi watoto hususani wa kike wenye umri kati ya Miaka 12-17 walivyoharibika kutokana na mabadikiko ya Teknolijia ambapo imewapekea kufahamu mambo ya wakubwa wakiwa watoto na hatimaye kupata matamanio na kufanya kama walivyo ona katika Mitandao ya kijamii na Runinga jambo linalowasababishia Mimba za Utotoni
 Mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo zimefanywa na  Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa  vinavyosaidia kutatua tatizo hilo.
 Mmoja wa Mabinti ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anatoa ushuhuda wa kuachishwa shule,na hapa alipo hasomi na kampeni ya Binti wa kitaa kupitia wadau watafanya jambo kwa Binti huyu
Mwanaharakati Kijana Victoria Mwanziva akijibu swali na kuelezea kwa kina tafsiri ya Jinsia
 Mwezeshaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Steven Mfuko akiwahoji baadhi ya Maswali watoto hawa wenye umri wa miaka 12 kama wanajua maswala mbalimbali kuhusu wao na kusema kwamba hawafahamu, na kuomba wapewe elimu juu ya mabadiko yao ya mwili ili kuepuka Mimba za utotoni
 Bi. Mwama Ajabu akielezea namna Simu zilivyoweza kuwaharibu watoto wa kike na kuongeza kuwa wazazi hawana muda nao ndio mana hizo simu zimawaharibu sana, na mara nyingi hufanya mawasiliano kisiri mida ya usiku wakati watu wamelala na kibaya zaidi watoto hao hupendelea zaidi kufatilia mitandao ambayo sio mizuri, ameshauri wazazi mwenzake kuwa lazima wawe karibu na mabinti zao.
 Baadhi ya wahusika wa Binti Kitaa wakiongea na Bodaboda waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa
 Anna akizungumzia Jinsi Binti wa Kitaa inavyofanya kazi
 Hii Timu  ya Binti wa kitaa Wakimsikiliza Mtoto aliyeachishwa Shule na Mzazi wake
 Baadhi ya wahusika wa Binti wa Kitaa wakiwa katika eneo la tukio
 Baadhi ya watu wakiwa katika Mdahalo huo
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania akielezea kwa kina juu ya kampeni ya Binti wa Kitaa
 Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo akiendela kutoa Mwongozo


Mwakilishi wa  Sunshine Group akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Binti wa Kitaa
Mwakilishi kutoka GW Health World Limited akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Binti wa Kitaa
 Bwana Steven Mfuko akitoa Elimu juu ya Mimba za Utotoni na Kuolewa wakiwa chini ya Miaka 18
 Watu mbalimbali wakiwa katika kampeni hiyo
 Kulia ni Binti akitoa ushuhuda wa yeye kupata mimba wakati akiwa na miaka 16 na kusema hiyo ilisababishwa na familia yake
Aliyemwakilisha Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata  Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa  kusababisha Mimba nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili kupiga vita swala hilo
Bwana nidhamu wa Madereva wa Bodaboda kituo cha Cecy Bwana Atupele akieleza namna elimu ya maswala ya Jinsia ilivyo wasaidia wao kuunga mkono kupambana na mimba za utotoni ambapo wamejiwekea utaratibu wa adhabu kali kwa yeyote atakayempa mimba binti mwenye umri wa chini ya miaka 18
Mambinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa
Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akielezea namna mimba za utotoni zinavyo athiri maisha ya Binti na pia kusababisha matatizo ya kiafya na kumsababisha akose mambo mengi na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampeni ya Binti wa Kitaa kupinga swala hilo
Mwakilishi kutoka TBC FM akielezea majukumu yao ya kuhakikisha kila mtu anapata habari na taarifa pia elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni pamoja na ndoa
Bwana Makundi kuroka Radio France RFI akielezea namna baadhi ya Nchi zenye machafuko zinavyo wanyanyasa mabinti wadogo wenye chini ya umri wa miaka 18 kwa kuwaoa, kufanya nao ngono pia kuwahusisha katika mashambulizi mbalimbali, Pia alieleza kuwa vyombo vya Habari vina jukumu kubwa sana la kuhakikisha jamii inapata taarifa na elimu juu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni
Kila sehemu ambapo Kampeni ya Binti wa Kitaa inapita huwa panaachwa alama inayo onesha kuwa kuna kitu kilifanyika hapa Meneja wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James (kushoto) akiwa na mtoto ambaye aliachishwa shule na Baba yake , hapa anakabidhiwa rasmi kwa wawakilishi wa Sunshine Group Ltd pamoja na GW Health limited kwa ajili ya kusomeshwa ili amalizie masomo yake
Picha ya pamoja 
Picha zote na Fredy Njeje

SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200.

October 22, 2016
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akipokea madawati 200 kutoka kwa Meneja wa Shamba la Miti Lunguza, yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Abdallah Mchomvu katika halfa iliyofanyika leo

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo.
RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUFI 500

RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUFI 500

October 22, 2016
mchi1
Mhandisi wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
mchi2
Maneja Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
mchi3
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.
mchi4
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya  Muriet.
mchi5
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha kupitia Tiket ya Ccm Catherine Magige(kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa kampuni ya Ujenzi iliyotoa msaada kwa ajili ya kuwezesha huduma za kijamii Mkoani Arusha.
mchi6
Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Kundi la Walemavu kupitia Tiket ya Ccm Amina Mollel(kwanza kushoto) pia alitoa shukrani zake kwa kwa Kampuni iliyotoa msaada.
mchi7
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia (pili kulia) akishkuru kwa msaada wa Mabati 100 na Mifuko ya saruji 100 aliyopewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Terrat.
mchi8
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500.
mchi9
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mhe. Catherine Magige baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500 toka kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sakina Tengeru na barabara ya Mchepuko.
…………………………………………….
Nteghenjwa Hosseah – Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.
Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100  kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.
Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.
Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina  – Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.
“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.
Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati 100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet Jijini Arusha. Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.
Katika  makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na  wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM JANA

October 22, 2016







 Taaswira ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu