DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO

January 26, 2018
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.

Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

RAIS WA FIFA KUSHUHUDIA FAINAL YA NDONDO SUPER CUP

January 26, 2018

Baada ya kufanyika michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup kwa mafanikio katika mikoa ya Mwanza na Mbeya sasa yaongeza wigo kwa mabingwa wa mikoa.
leo jijini Mbeya kamati ya mashindano hayo imetangaza rasmi uwepo wa mashindano ya Ndondo Super Cup itakayofanyika jijini Dar es salaam mwezi februari kwa kushirikisha mabingwa wa mikoa ilipofanyika Sports Xtra Ndondo Cup.
Mwenyekiti wa kamata ya Ndondo Cup Shaffih Dauda amewaambia waandishi wa habari kuwa uwepo wa mashindano hayo ni hitimisho la msimu wa Ndondo Cup 2017 kabla ya kuzinduliwa msimu mpya mwezi wa tatu.
"Mashindano hayo yatashirikisha timu nne na kutakua na michezo minne itakayofanyika tarehe 17, 18, 20, na 21 mwezi februari jiji Dar es salaam" amesema Dauda.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Ndondo Super Cup Gipson George amesema hili ni jambo lingine kubwa kutoka Clouds Media kama support ya wanamichezo wa Tanzania na ulimwenguni kote kwa ujumla hususani ujio wa viongozi wa FIFA nchini.
"Hakuna asiyejua Rais wa FIFA atakuwepo hapa, hii ni heshima kubwa tuliyopewa Duniani lazima na sisi tuwaoneshe kuthamini ujio wao"
"Shaffih Dauda amewasiliana na TFF kuona namna ya kushirikiana kutusaidia kuwezesha kumpata rais wa FIFA kuja kwenye fainali ya Ndondo Super Cup ndio maana tumepanga iwe tarehe 21" amesema Gipson.
Gipson ameongeza kuwa mashindano hayo yanaendana na agenda ya Rais wa sasa wa FIFA ya kurudi chini kabisa (grassroot) mpira unapochezwa na watu wa kawaida wenye vipaji vya hali ya juu.
Msafara wa FIFA ukiongozwa na Rais Infantino unatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 na siku inayofuata watakua katika mkutano utakaofanyika hapa nchini.
Kutangazwa kwa michuano hiyo mikubwa kwa timu za mtaani jijini Mbeya ni heshima kwa chama cha soka cha mkoa huo MREFA ambapo mwenyekiti wake Elias Mwanjala amesema hiyo ni bahati ya kipekee waliyopata kwenda kukutana na Rais wa FIFA.
"Ndondo imefanyika miaka minne lakini sisi tumepata nafasi ya kukutana na rais wa FIFA ni bahati iliyoje, lakini kikubwa ni wana mbeya kuungana kufanikisha jambo hili kwani sio la chama cha soka bali ni jambo la mkoa na nyie Clouds mtusaidie kupata wadhamini" amesema Mwanjala.
Timu zitakazoshiriki Ndondo Super Cup ni mabingwa wa Mwanza timu ya Mnadani Fc, Mabingwa wa Mbeya Itezi United na mabingwa wa Dar es salaam timu ya Misosi Fc huku Goms United iliyocheza fainal msimu uliopita na misosi imeongezwa kama heshima ya mkoa wa Dar es salaam kuwa mwasisi wa mashindano hayo.
Mbali na kutangazwa kwa mashindano hayo Clouds Media imetoa zawadi ya fedha kwa washindi wa mashindano ya Sports Xtra Ndondo Cup Mbeya yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Mabingwa Itezi Fc wamepata milion tatu, washindi wa pili Terminal fc milion mbili, na washindi wa tatu Tukuyu Star milion moja.
Gasper Samwel Mwaipasi wa Tukuyu Star ameibuka mfungaji bora kwa kufunga goli tano, Frank Anthonwa Itezi United amechaguliwa kuwa kipa bora na  beki wa kushoto wa Itezi United Salum Idrisa Chau ametajwa kuwa mchezaji bora

RAIS MSTAAFU KIKWETE AFURAHIA SOMO LA MKIKITA KUHUSU KILIMO BORA CHA PAPAI

January 26, 2018
 Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete akifurahi kuona papai alililopelekewa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Livinggreen) walipokwenda kumpa elimu kuhusu kilimo bora cha zao hilo nyumbani kwake Msoga, Chalinze mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange.
 Dk. Kikwete akishukuru kwa mafunzo hayo yaliyotolewa na Mwanachama wa Mkikita  Mtaalamu wa Kilimo cha Papai kutoka Kampuni ya Awino Farm, Ezra Machogu. Kulia ni Adam NGAMANGE


Na Richard Mwaikenda, Msoga,
.RAIS mstaafu Dk.Jakaya Kikwete amefurahishwa na elimu ya kilimo cha kisasa cha Papai chenye 
gharama nafuu aliyopatiwa na Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita/Living green)

Elimu hiyo ilitolewa hivi karibuni nyumbani  kwake Msoga, Chalinze, mkoani Pwani na Ezra Machogu  Mtaalamu wa Kilimo wa Kampuni ya Awino Farm ambayo ni mwanachama wa Mkikita.

Kikwete alifurahi kuambiwa kwamba kampuni hiyo inaweza kuzalisha papai lenye ubora kwa 
kutumia teknolojia ya kisasa yenye gharama nafuu hivyo kumfanya mkulima apate faida kubwa 
wakati wa mauzo.

Ezra anasema kuwa unaweza kupunguza gharama kwa kuacha kuchimba mashimo badala yake 
unalima shamba mara tatu kwa kutumia trekta, hivyo kuufanya udongo kuwa tifutifu kitendo 
kitakacho kurahisishia kupanda miche ya papai bila matatizo.

Anasema ukitumia njia hiyo itakuondolea gharama ya kuchimba mashimo 1200 katika heka 
moja ambayo jumla ni sh. mil. 6 ikiwa kila shimo itakuwa sh. 500 wakati kulima mara tatu 
heka moja kwa trekta ni sh. 150,000.

Ezra anamweleza Dk. Kikwete kuwa unaweza pia kupunguza gharama ya mbolea kwa kila shimo 
kuweka majagi mawili badala ya debe moja.

Pia alimweleza kuwa katika umwagiliaji papai halihitaji maji mengi, hivyo unaweza kutumia 
lita 10,000 kwa siku kumi badala ya siku nne.

Alisema kuwa pia wamejipanga kimasoko kwa kuutumia mtandao wa Mkikita ambao tayari una 
watalaam wa masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na watalaamu wa kufungasha (Packaging) 
bidhaa kwa teknolojia ya kisasa.

Baada ya kuridhika na maelezo hayo, Rais mstaafu, alifurahi na kuishukuru Mkikita kwa 
kumpelekea watalaam hao kutoka Kampuni ya Awino Farm.

Ezra alizidi kumfurahisha, Dk. Kikwete kuwa kwa heka moja akiuza papai anaweza kupata hadi 
sh. mil. 80,000,000 kwa mchanganuo ufuatao; 

Heka moja inaweza kupandwa mipapai 1000 hadi 1200 na kwamba mpapai mmoja unaweza kuzaa 
papai 100 hadi 1300 na endapo kila papai lenye uzito wa kilo 2 likiuzwa kwa bei ya jumla sh. 
800 ukizidisha na wastani wa papai 100 kila mche halafu zidisha kwa miche 1000 tu unapata 
kiasi hicho cha fedha kwa msimu wa kwanza.

Pia alimueleza kuwa uzuri wa miche ya papai huishi miaka mitatu ambapo kila wiki utakuwa 
unavuna na kuuza, hivyo kukupatia faida kubwa tofauti na mazao mengine ambayo ukivuna mara 
moja tu.

"Laiti kama ungekuwa mchungaji, padri au sheikh anayehubiri kutafuta waumini, basi bila 
shaka mimi mmenipata nimekuwa muumini wenu." Alisema Dk. Kikwete huku akicheka kwa furaha.

"Kubwa mlilonifurahisha ni jinsi mlivyopunguza kwa kiasi kikubwa gharama ya kuzalisha papai 
na faida kubwa nitakayoipata, nipo tayari kutoa heka 10 za kuanzia."Aliahidi Dk. Kikwete 
ambaye alisema kazi ya kilimo anaipenda na kwamba iko kwenye damu yake. 

Ujumbe huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita Adam Ngamange, ambaye akabla y yote alimshukuru Dk. Kikwete kwa kuwaalika na kumuomba ajiunge na mtandao, jambo ambalo 
alilikubali.

Ujumbe alioongozana nao ni Ezra Machogu, Martine  Wamaya wa Kampuni ya Awino Farm, 
Khalid Tamim, Hassan Tamim na Ali Said ambao ni Wawekezaji wa zao la muhogo,  Mkurugenzi  
Betl Worldwide Ltd, Murtaza Bharmal ambaye ni mtaalamu wa masoko na uongezaji thamani mazao na Richard Mwaikenda ambaye ni Mshauri wa Habari wa mtandao huo.
 Meneja  Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikwete, Justine (kushoto) akiwa na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino, Martine Wamaya (kulia) na Mtalaamu wa kilimo cha Papai,  Ezra Machogu walipokuwa wakitoka kuchuma papai kutoka kwenye shamba darasa la Kampuni ya Awino eneo la Msata tayari kumpelekea Rais mstaafu, Dk. Kikwete. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk. Kikwete akisalimiana na Adam Ngamange wa Mkikita
 Dk. Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Awino Farm, Wamaya.
 Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra
 Dk. Kikwete akisalimiana na wanachama wa Mkikita wawekezaji katika shamba la Muhogo. Kushoto ni Khalid Tamim na Hassan Tamim.
 Meneja wa Kilimo wa Mashamba ya Dk. Kikiwete, Justine akiutambulisha ujumbe wa Mkikita nyumbani kwa Kikwete, Msoga
 Ngamange akielezea mbele ya Dk Kikwete kuhusu utendaji wa mtandao huo
 Mtaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra (kulia) akitoa elimu kwa Dk. Kikwete kuhusu kilimo bora cha zao hilo kwa gharama nafuu
 Ngamange akimkabihi Dk. Kikwete mafuta yaliyotengenezwa kwa kutumia mchaichai
 Dk. JK akinusa mafuta hayo ya mchaichai

 Dk. Kikwete akifungua kasha la mchaichai
 Mtaalamu wa Masoko na Ufungashaji wa bidhaa mshirika wa Mkikita, Murtaza Bharmal (kulia) akitoa maelezo jinsi anavyoweza kutafuta masoko kirahisi kwa kutengeneza makasha mazuri ya kuhifadhia bidhaa ili kuongeza thamani.
 J akiwa na ujumbe wa Mkikita pamoja maofisa wasaidizi wake
 Dk. Kikiwete akizungumza Ngamange (kulia) pamona na Murtaza
 JK akiagana na kiongozi wa ujumbe wa Mkikita, Ngamange baada ya ziara yao kumalizika
JK akiagana na mwandishi wa habari wa Azam TV, Octor

Kamishna Mkuu mstaafu Mwasalla atoa msaada wa sare Girl Guides

January 26, 2018
 Kamishna Mkuu wa zamani wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Faithjoy Mwasalla (kushoto), akikabidhi msaada wa sare na fulana kwa chama hicho katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni; Girl Guides Asha Ramadhan, Rhoda Idd, Mariam Nuru, Salma China, Kiongozi wa Girl Guides, Rehema Kijazi, Kiongoizi wa Girl Guides Temeke, Leonida Komba na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Na Richard Mwaikenda, Msasani.

Kamishna Mkuu wa zamani wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), Faithjoy Mwasalla ametoa msaada wa sare na fulana kwa chama hicho.

Hafla hiyo ilifanyika leo katika Makao Makuu ya TGGA, Msasani Dar es Salaam, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Grace Shaba na maofisa wengine.

Msaada huo aliukabidhi kwa Girl Guides kutoka shule za Wilaya ya Temeke, walioongozwa na Kiongozi wa TGGA wa wilaya hiyo, Leonida Komba.

"Sisi Tgga tunaamini katika kujitolea hivyo nikiona wenzangu wanastawi nafurahi sana, ndiyo maana nimetoa msaada huu ili Girl Guides wapendeze na waendelee vizuri wawe viongozi wazuri wa kesho, kwani anayekulia malezi ya girl Guides anakuwa na maisha mazuri yenye nidhamu." Amesema Mwasalla huku akipigiwa makofi.

Pia Girl Guides waliopokea msaada huo kwa niaba ya wenzao, walishukuru sana kupata msaada huo na kwamba wamejifunza suala la kujitolea pamoja na mshikamano na umoja uliomo ndani ya chama chao na kuahidi kuendeleza mambo hayo muhimu.

Kiongozi wa Girl Guides Wilaya ya Temeke, Leonida Komba naye kwa niaba ya viongozi wa TGGA Manispaa ya wilaya hiyo alitoa shukrani kwa Mwasalla ambaye ni mmoja wa waasisi wa chama hicho, kwa kutoa msaada huo na kumtakia aendelee na moyo huo wa kizalendo ambao ni watu wachache wanao, aliomba Mungu amjalie na ambariki sana.

Naye Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba, alimshukuru Mwasalla kwa Moyo aliouonesha wa kujitolea kwa kutoa msaada huo hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho vijana wengi hawana uwezo wa kununua sare,na kwamba msaada huu ameutoa wakati muafaka. 







 Girl Guides wakimshukuru Mwasalla kwa kuwapatia msaada huo.
 Mwasalla akipongezwa na Kiongozi wa Girl Guides Temeke, Leonida Komba.
 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akizungumza na Guides wakati wa hafla hiyo
 Mwasalla akionesha moja ya sare hizo 

 Girl Guides wakibeba msaada huo
Girl Guides wakiwa wamevaa baadhi ya sare walizopewa msaada.
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUIKARABATI NYUMBA YA NYERERE MAGOMENI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUIKARABATI NYUMBA YA NYERERE MAGOMENI

January 26, 2018
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla (MB) mapema leo Januari 26,2018,amefanya ziara maalum katika Makumbusho ya Kumbukizi ya Nyumba ya Mwl Nyerere iliyopo Magomeni Mtaa wa Ifunda Namba 62, ambayo aliishi hapo miaka ya 1950's Dk. Kigwangalla ameweza kujionea mambo mbalimbali ndani ya makumbusho hayo huku pia akipokea maoni ya namna ya kufanyiwa maboresho ya kituo hicho ikiwemo ufinyu wa eneo la ofisi na maegesho ya wageni wanaotembelea hapo. "Nimefika hapa leo kujionea Kituo hichi ambacho ni kielelezo kikubwa cha Mwasisi wa Taifa letu. Hapa pana hazina kubwa na kituo hiki kina mambo mengi sana ya kumuenzi Baba wa Taifa. Kwa hali tuliookuta kwa kweli tutakaa na timu yangu kuona tunafanya maboresho makubwa kabisa ili kiwe kama maeneo mengine yenye Wahasisi wa Mataifa yao, tumeona kama eneo alilozaliwa Mzee Mandela kule Afrika Kusini, nyumba yake imehifadhiwa vizuri na imekuwa na wageni wengi. Kwa hapa kwetu na sisi tutakaa na wenzetu kutatua changamoto hizi. Hapa tutajenga Maktaba ambapo watu watakuja kusoma vitabu vya Mwasisi wetu na kuona mambo aliyokuwa akifanya. Lakini pia tutaonana na Viongozi wa Halmashauri ya Kinondoni kuona namna ya kupaboresha mahala hapa ikiwemo miundombinu ya Barabara ya kuingia na kutoka eneo ili" alieleza Dk. Kigwangalla. Pia aliongeza kuwa, kituo hicho kipo katika hali mbaya kikikabiriwa na changamoto licha ya kuwa ni kituo muhimu sana hapa nchini. hivyo amewahakikishia wahifadhi wa Makumbusho hayo mipango iliyopo ni pamoja na kukifanyia marekebisho kutengeneza choo, kupaka rangi pamoja na kufanyia ukarabati mkubwa vionyeshi vya kumbukumbu nzima ya Baba wa Taifa. Aidha, amesema kuwa, lengo kwa sasa ni kuifanya nyumba hiyo iwe kama nyumba halisi ailivyokuwa akiishi mwenyewe Baba wa Taifa kwani ndani bado kuna vitu halisi alivyokuwa akivitumia Mwasisi mwenyewe huku pia mikakati ni pamoja na kununua hata nyumba za jirani ili kuongeza eneo na kuongezwa baadhi ya ofisi na pawe na hadhi kama Mwasisi mwenyewe" alieleza Dk.Kigwangalla. "Kiukweli nimefika hapa kushuhudia makumbusho haya ambayo kiuhalisia hapa ni hazina kubwa sana ya kumbukumbu ya Taifa letu hasa katika harakati za kupigania Uhuru pia zilianzia hapa katika nyumba hii. Pia tutaboresha zaidi kwa kuweka studio maalumu ambayo pia tutaboresha CD zote za Baba wa Taifa zitakuwa zikioneshwa humo ikiwemo zile za Hotuba. Awali Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho hayo, Bi. Neema Mbwana alieleza changamoto zinazoikabili kituo hicho pamoja na kuomba kuboreshwa kwa vitu muhimu ikiwemo Ukarabati wa nyumba nzima, ikiwemo, paa na kupaka rangi. Aidha, waliomba kuboreshewa vionyeshwa ikiwemo kujengea vioo katika kuta za vionyeshwa, kuzitengeneza picha katika fremu kitalaamu. Mhifadhi huyo aliendelea kusema kuwa, kwa umuhimu wa vitabu ambavyo hakuna nakala zake halisi ambavyo ni mali za Baba wa Taifa, walimuomba Waziri awachapishie tena nakaza zaidi ili ziweze kutumika kwa miaka mingi zaidi kwani vilivyopo vimezidi kuchakaa. Mbali na kutembelea Makumbusho hayo ya Nyumba ya Baba wa Taifa hiyo ya Magomeni, Dk. Kigwangalla pia aliweza kutembelea soko kubwa la Vinyago lililopo Mwenge na kujionea wachngaji vinyago hao ambao ni kiungo muhimu cha Utalii hapa nchini hata hivyo alikutana na kero juu ya Watalii kusumbuliwa Viwanja vya ndege kwa bidhaa zao hizo za vinyago.
Muhifadhi Mkuu wa Makumbusho nyumba ya Nyerere iliyopo Magomeni Jijini Dar es Salaam,Bi. Neema Mbwana akisoma taarifa za kituo hicho kwa Waziri Dk Kigwangalla alipotembelea kituoni hapo mapema leo Januari 26,2018.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha Wageni alipowasili kituoni hapo
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Kigwangalla akitambulishwa wafanyakazi wa kituo hicho
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya vitabu vya Mwalimu Nyerere ambavyo vimehifadhiwa nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akitazama baadhi ya picha mbalimbali za Baba wa Taifa ambazo zipo nyumbani hapo
Mhifadhi Mkuu wa Neema Mbwana akimuonesha Dk. Kigwangalla moja ya makochi aliyokuwa akiyatumia Baba wa Taifa wakati akiishi hapo
Dk. Kigwanglla akiangalia moja ya chungu cha shaba alichokuwa akitumia Mwalimu Nyerere katika nyumba yake hiyo ya Magomeni
Dk. kigwangalla akiangalia moja ya pasi ya mkaa aliyokuwa akitumia Baba wa Taifa wakati akiishi nyumbani hapo
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vitanda vilivyokuwa vikitumiwa na watoto wa Baba wa Taifa wakati akikaa hapo. (Chumba cha watoto wa Baba wa Taifa walitumia)
Dk. Kigwangalla akiangalia kitanda alichokuwa akikitumia Baba wa Taifa wakati akiishi kwenye nyumba hiyo
Mhifadhi Neema Mbwana akimuonesha Waziri Dk. Kigwangalla nyuma ya nyumba hiyo na eneo lilivyo
Eneo la nyuma ya nyumba hiyo kama linavyoonekana
Akiwa katika Eneo la Vinyago Mwenge, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kushuhudia baadhi ya bidhaa hizo ambazo pia zimekuwa ni kielelezo kikubwa cha watalii
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago cha Umoja abacho kinaelezea taswira mbalimbali ikiwemo hali ya uhifadhi wa hifhadhi za Taifa katika nyanja za Ulinzi wa wanyama
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya vinyao vyenye umbo tofauti ambavyo vimekuwa vikitumika sana katika maofisi za Serikali na mashirika ikiwemo Balozi
Dk.Kigwangalla akiwa anatembelea baadhi ya mabanda ya wachongaji vinyago hao
Dk.Kigwangalla akiangalia moja ya kinyago kikubwa chenye taswira ya Kimbunga
Mkurugenzi wa Mipango na matumizi endelevu ya misitu na nyuki nchini, Mohamed Kilongo (kulia) akimwelezea jambo Waziri Dk.Kigwangalla namna wanavyoshughulikia suala la Wachongaji vinyago hao haswa katika vibali vya miti
Dk.Kigwangalla akimsikiliza kwa makini mmoja wa wachonga vinyago ambao walilalamikia hali ya kutozwa kwa gharama kubwa katika viwanja vya ndege hasa kwa wageni ambao asilimia kubwa ni watalii
Dk.Kigwangalla akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wachonga Vinyago Mwenge kukaa pamoja ili kuona watakavyoelewana namna ya kumiliki eneo hilo huku akiahidi kushughulikia suala la bidhaa zao zinazotozwa ushuru mkubwa viwanja vya ndege vya hapa nchini
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla akiangalia moja ya michoro ya picha katika eneo la Tingatinga lililopo Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
Dk. Kigwangalla akiangalia moja wachoraji wakongwe wa Umoja wa michoro ya Tingatinga alipotembelea kujionea michoro hiyo eneo la Oyster bay Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE