RAIS DK.MWINYI APOKEA POLE KUTOKA KWA MAKAMU BARA KINANA

RAIS DK.MWINYI APOKEA POLE KUTOKA KWA MAKAMU BARA KINANA

March 12, 2024

 


Mak Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Comrade Abdulrahman Omar Kinana kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Mwenyekiti wa CCM Taifa Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja . 

TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KUTOKOMEZA MATENDE NA MABUSHA

TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KUTOKOMEZA MATENDE NA MABUSHA

March 12, 2024

Na Sophia Kingimali

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema nchi imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha inatokomeza magonjwa ya matende na Busha kwa kuokoa watu milioni 31.2 waliokuwa na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa huo.

Alizungumza na waandishi wa Habari leo Machi 12,2024 jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa katika kutokimeza ugonjwa huo nchini hususani mkoa wa Dar es salaam.

Amesema awali maambumizi makubwa ya ugonjwa huo yalikuwa katika Halmashauri 119 ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wameza kudhibiti ugonjwa huo katika Halmashauri 112 kati 119 na kubakiwa na Halmashauri 7.


Amesema katika mkoa wa Dar es salaam Halmashauri zote yaani ya manispaa ya Kigamboni na Ubungo,Temeke na Halmashauri ya jiji hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huo baada ya kusitisha umezeshaji wa kingatiba na kubaki na kata 10 za Halmashauri ya Kinondoni ambazo zinamaambukiza mapya kwa asilimia 2.3.

“Kutokana na matokeo haya wizara ya Afya inapenda kutoa taarifa rsmi kwa wananchi wa mkoa huu tunasitisha kampeni za uwezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa lakini pia nitoe rai kwa wananchi kuchukua taadhari kwa kufanya usafi na kuua mazakia wa mbu”,!amesema Ummy.

Amesema zoezi la umezeshaji kingatiba utafanywa kwa kata 10 za manispaa ya Kinondoni ambazo ni Tandale,Kijitonyama,Mwananyamala,Kigogo,Mzimuni,Magomeni,Ndugumbi,Hananasif,Kinondoni na Makumbusho.

Aidha Waziri Ummy ametoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kushiriki kampeni hiyo ya kingatiba zitakazoendelea kufanyika kwenye maeneo yao ili kuweza kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.

Sambamba na hayo Waziri Ummy amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa yaliyokuwa ayapewi kipaumbele.

“Kupitia mkutano wa ‘Reaching the last mile’uliofanyika mwezi Desemba 2023 huko Dubai Rais aliahidi kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani milioni tatu karika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2024 ili kufanikisha kutokomeza magonjwa haya hususani Matende na Mabusha.”amesema.

Akitaja Halmashauri zenye maambukizi mapya hivi sasa ni Pangani,Mafia,Kinondoni,Kilwa,Lindi Manispaa,Mtama na Mtwara Mikinfani ambako kuna jumla ya wakazi 1,203,359.    

WAZIRI JAFO AWASILISHA TAARIFA YA MIRADI KWENYE KAMATI YA BUNGE

March 12, 2024

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema miradi mbalimbali ya mazingira imechangia kuwajengea wananchi uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Hifadhi Endelevu ya Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa (SLM-Nyasa) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira katika kikao kilichofanyika leo Machi 12, 2024 jijini Dodoma.

Dkt. Jafo amesema kuwa kutokana na wananchi kuendelea kupata elimu ya mazingira, wameendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za upandaji wa miti hatua iliyochangia kupatikana kwa mvua katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mheshimiwa Mwenyekiti kupitia Kamati yako mmefanya kazi kubwa sana kwani mmetupa maelekezo ambayo tumeyafanyia kazi hasa katika eneo la kuwaelimisha wananchi kuhusu kuhifadhi mazingira na matunda yake tunayaona, wananchi wengi wameendelea kupanda miti kwa wingi,” amesema.

Dkt. Jafo amesema kuwa kutokana na uharibifu wa mazingira katika bonde la Ziwa Nyasa unaotokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu, Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza Mradi wa SLM-Nyasa kuwajengea uwezo wananchi hao kutumia mbinu bora za kuhifadhi ardhi.

Ameongeza kuwa kupitia mradi huo wananchi wanaojengewa uwezo wanaweza kuboresha maisha yao kwa kuwa na njia mbadala ya kujipatia kipato na kuachana na vitendo vya ukataji wa miti ovyo au uvuvi usio endelevu.

Halikadhalika, Waziri Dkt. Jafo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais inatekeleza Mradi wa SLR ili kuimarisha usimamizi jumuishi wa mazingira na urejeshwaji wa mazingira yaliyoharibiwa ili kujenga uhimilivu wa mifumo ikolojia.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya Iringa pamoja na Mradi wa Hifadhi Endelevu ya Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa (SLM-Nyasa) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kilichofanyika leo Machi 12, 2024 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga (kushoto) akiongoza kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa Urejeshwaji wa Mazingira na Hifadhi ya Bayoanuai Tanzania (SLR) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya Iringa pamoja na Mradi wa Hifadhi Endelevu ya Ardhi katika Bonde la Ziwa Nyasa (SLM-Nyasa) unaotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kilichofanyika leo Machi 12, 2024 jijini Dodoma.

DKT. NCHEMBA AITAKA IAA KUSIMAMIA KWA WELEDI UJENZI WA KAMPASI YAKE JIJINI DODOMA

DKT. NCHEMBA AITAKA IAA KUSIMAMIA KWA WELEDI UJENZI WA KAMPASI YAKE JIJINI DODOMA

March 12, 2024


SHARE


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akikata utepe katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kukalisha wanafunzi 4,500 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli, Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akiweka saruji kuashiria Uzinduzi wa Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Hafla hiyo ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli, Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo, Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha anayemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Fredrick Mwakibinga, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha anayemwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Lusius Mwenda.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi ya 4,500 kwa wakati mmoja.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Mwamini Tulli, akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) kutoa hotuba yake, wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, ambapo Mwenyekiti huyo ameishukuru Wizara ya Fedha kwa kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka, akizungumza wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma, ambapo amesema kuwa Ujenzi huo unaoendelea unafanywa kwa kutumia mapato yake ya ndani kupitia wataalam wa ndani yaani ‘Force Account’.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, baada ya kuweka Jiwe la Msingi, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi ya 4,500 kwa wakati mmoja.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), akizungumza na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (katikati) wakati akikagua ujenzi unaoendelea wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, baada ya kuweka Jiwe la Msingi, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma. Jengo hilo la ghorofa Sita lenye ukubwa wa takribani Sqm 6600, litakuwa na uwezo wa kukalisha wanafunzi ya 4500 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (watatu kulia walioketi), Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli (watatu kushoto walioketi), Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto walioketi), Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha anayemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Fredrick Mwakibinga (wapili kulia walioketi) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma, Bi. Sakina Mbughi (wa kwanza kulia walioketi), na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka, wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo hicho baada ya hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati walioketi), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (watatu kulia walioketi), Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho, Dkt. Mwamini Tulli (watatu kushoto walioketi), Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa kwanza kushoto walioketi), Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma kutoka Wizara ya Fedha anayemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Fredrick Mwakibinga (wapili kulia walioketi) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Dodoma, Bi. Sakina Mbughi (wa kwanza kulia walioketi), na Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka, wakiwa katika Picha ya pamoja na Timu ya wataalam wa ujenzi wa jengo hilo baada ya hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.
…………………..
Na. Joseph Mahumi na Saidina Msangi, WF, Dodoma.

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameuagiza uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kusimamia kwa ukaribu ujenzi miundombinu yake inayoendelea kujengwa ili ikidhi viwango vya ubora na kuonesha thamani halisi ya fedha.

Alisema hayo wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Taaluma la Chuo cha Uhasibu Arusha katika Kampasi ya Dodoma, linalojengwa eneo la Njedengwa wilaya ya Dodoma, Jijini Dodoma.

Alisema ni muhimu kuzingatia usimamizi mzuri katika ujenzi wa majengo mengine ya hosteli, utawala, madarasa pamoja na kumbi za mihadhara yanayoendelea kujengwa katika Kampasi za Arusha na Babati, ili watekeleze miradi hiyo kwa kuzingatia viwango vya ubora, sheria, taratibu na miongozo ya matumizi ya fedha za umma na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili iweze kutoa huduma kwa Watanzania.

‘‘Miongoni mwa malengo Endelevu ya milenia kufikia mwaka 2030 ni kila nchi kutoa Elimu bora kwa watu wake. Ninawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika utekelezaji wa malengo ya milenia katika Sekta ya elimu,’’ alisema Dkt. Nchemba.

Aidha alisema kuwa matarajio ya Serikali kupitia ujenzi wa miundombinu ya elimu kama madarasa, kumbi za mihadhara, maktaba, maabara za kompyuta unaoendelea katika Kampasi ya Dodoma na Kampasi za Arusha, Babati utakuwa chachu katika kutoa elimu bora kwa Watanzania.

‘‘Ninaamini miundombinu hiyo itawawezesha kuwaandaa wataalam mahiri kwenye fani za Uhasibu, Fedha, Benki, Uchumi, TEHAMA, Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Utalii, Masoko na maeneo mengine wataokakidhi mahitaji ya soko la ajira, wakiwa na ujuzi na maarifa ya kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumii’’ alisema Dkt. Nchemba.

Aidha, alitoa rai kwa Chuo hicho kuendelea kubuni kozi mbalimbali ambazo zitawasaidia Watanzania kuelimika na kujikwamua kiuchumi pamoja na kufanya tafiti zitakazoleta tija kwa Taifa ambazo matokeo yake yataisaidia serikali, jamii na wadau wengine kuzitumia kama dira katika kufanya maamuzi mbalimbali yenye mchango katika ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa Wizara ya Fedha itaendelea kushirikiana na Chuo cha Uhasibu Arusha katika kuhakikisha kinatekeleza majukumu ya msingi kama Taasisi ya Elimu ya Juu ambayo ni kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Mwamini Tulli, aliipongeza Serikali kwa kuendelea kuunga mkono Chuo hicho katika ujenzi wa miundombinu ya elimu kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ambapo katika kipindi cha miaka miwili shilingi bilioni tatu (03) zilipokelewa kwa ajili ya ujenzi unaoendelea katika Kampasi ya Arusha na Kampasi ya Babati.

Aliahidi kuwa Chuo kitaendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo na kuhakikisha kuwa zinafanya kazi iliyokusudiwa pamoja na kuhakikisha kwamba Chuo chao kinatoa wahitimu wenye weledi na ujuzi unaohitajika katika kuleta maendeleo ya taifa.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Eliamani Sedoyeka aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya fedha za mradi wa HEET ambao Chuo hicho kimetengewa kiasi cha Sh. bilioni 48 ambazo zinatarajiwa kuendelea kuboresha Chuo katika nyanja mbalimbali.

Alisema Kwa kutambua kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi, Chuo cha Uhasibu Arusha kupitia Kampasi ya Dodoma kitaendelea kutoa mafunzo ya shahada ya uzamili kwa mwaka mmoja kwa kufundisha darasani vipindi vya jioni kwa njia ya darasani na mtandao kwa pamoja , pia kinatarajia kuanza kutoa masomo ya jioni kwa baadhi ya kozi za stashahada (diploma).

Chuo cha Uhasibu Arusha kinaendelea na ujenzi wa jengo la Taaluma litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,500 kwa wakati mmoja, kwa kutumia mapato yake ya ndani kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account) na linatarajiwa kukamilika mwezi Julai na litaanza kutumika mwezi Oktoba, 2024.

SIKU YA MISITU NA UPANDAJI MITI KITAIFA KUFANYIKA WILAYANI SAME

March 12, 2024

 Na Mwandishi Wetu


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Misitu na Upandaji miti duniani ambayo kitaifa itafanyika Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Same machi 21 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akiwa wilayani Same kwenye ziara ya kukagua eneo litakalofanyika maadhimisho hayo pamoja na kukagua miradi ya maendeleo atakayotembelea Dkt. Mpango akiwa Wilayani humo.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakazi wa Same na maeneo ya jirani kutumia vizuri nafasi ya kuwepo tukio kubwa la kitaifa la maadhimisho ya siku ya Misitu na Upandaji Miti kushiriki kikamilifu ikiwemo kwa kupanda miti sehemu ya kuunga mkono kampeni za kitaifa za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kwaupande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameziomba kamati za maandalizi kufika kwa wakati eneo la tukio ili kushirikiana kwa pamoja na watendaji wengine wa Wilaya na Halmashauri sskuhakikisha maandalizi yanakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.

Maadhimisho hayo yataanza rasmi Machi 18 kwa kufanya shughuri mbali mbali ndani ya Wilaya ikiwemo utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi pamoja na miti inayopaswa kupanda kwenye maeneo yao kulingana na mazingira yake.





UTENDAJI BORA WA KAZI WENYE TIJA KWA KUZINGATIA WELEDI UTAIWEZESHA SERIKALI KUPATA MAPATO

March 12, 2024

 Na Janeth Raphael - MichuziTv- Dodoma


Naibu Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu Deogratius Ndejembi amesema ili kuwepo na matokeo bora ya kiutendaji kazi katika kutoa huduma bora kwa wananchi lazima tija na maslahi viwe na uwiano.

Naibu Waziri Ndejembi ameyasema hayo leo Machi 12,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI cha kupitisha bajeti na mpango kazi kwa mwaka 2024/25.

“Hivyo ieleweke kuwa utendaji bora wa kazi na wenye tija kwa kuzingatia weledi na uwajibikaji utaiwezesha Serikali kuongeza mapato na hivyo kuwezesha kuongeza vile vile utoaji wa maslahi bora,”amesema.

Amesema kuwa madhumuni ya baraza la wafanyakazi ni kutoa fursa kwa watumishi kupitia kwa wawakilishi wao kujadiliana juu ya masuala mbalimbali ya msingi yanayohusu tija na ufanisi kwa upande mmoja na maslahi yao kama watumishi kwa upande mwingine.

“Baraza la wafanyakazi linaongeza ushiriki wa wafanyakazi katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za taasisi kama ilivyo fafanuliwa katika sheria ya majadiliano ya pamoja katika utumishi wa umma sura namba 105,”amesema.

Aidha amewasisitiza kuwa mikutano ya mabaraza ya wafanyakazi itumike katika kujadili malengo na mipango ya taasisi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi na kuongeza kuwa mabaraza hayo yanatakiwa kujadili utendaji kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji kazi zaidi.

“Hapa nisisitize sana kuna umuhimu wa kila mtumishi katika kila taasisi kufahamu malengo ya taasisi ( Vision and Mission) ili tuweze kwenda pamoja na tusihiahi kama headless chicken kuku ukimkata kichwa anaruka ruka hujui Mission na Vision inakwenda wapi kwahiyo ni muhimu sana kujadili hayo katika mabaraza haya,”amesisitiza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amesema baraza la wafanyakazi liliundwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2003 kama yanavyoundwa mabaraza mengine katika uwajibikaji na ndiyo linalounganisha kati ya wafanyakazi na wakuu wa idara wengine na kuwafanya kutimiza wajibu wao katika utendaji wa kazi.

Amesema moja kati ya ajenda zitakazojadiliwa katika kikao cha baraza hilo ni kuhusiana na bajeti itakayoenda kusomwa bungeni mwezi ujao pamoja na kupanga mpango kazi utakao wasaidia kufikia malengo yao.