RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BI JAMIE COOPER

February 02, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bi. Jamie Cooper ambaye ni Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Big Win Philanthropy, Ikulu Chamwino, Dodoma tarehe 2 Februari, 2024.

 




MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MKUTANO WA DHARURA WA SADC

February 02, 2024

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa dharura wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao.


Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Angola, Joao Manuel Lourenco ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, ulikuwa na ajenda moja tu ya kujadili kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika ukanda wa SADC.

Akizungumza kutoka ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma leo (Ijumaa, Februari 02, 2024), Waziri Mkuu Majaliwa amesema Tanzania inapendekeza kuwa ni vema Kanda ya SADC ikachukua hatua jumuishi kwa kuhusisha sekta zote mtambuka ikiwemo sekta za maji na mipango miji ili kuleta suluhisho la kudumu la kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine ya mlipuko.

“Hii ni kwa kuzingatia kuwa jamii kwa ujumla na kila mwananchi ana jukumu la kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha anazingatia kanuni za usafi (WASH) kwa manufaa binafsi, jamii na ukanda mzima.”

“Tunashauri nguvu kubwa ielekezwe katika kuboresha mifumo na upatikanaji wa maji safi na salama katika jamii zetu ili kuwa na matokeo chanya katika kudhibiti mlipuko huu.”

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu; Waziri wa Maji, Jumaa Aweso pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Mapema, akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa SADC, Rais Lourenco alisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuimarisha mawasiliano baina ya wataalamu wake ili kusaidiana kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo hasa kwenye maeneo ya mipakani.

Aidha, alisisitiza viongozi wa nchi wanachama waweke kipaumbele kwenye teknolojia mpya na tafiti ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. “Ni lazima tuhakikishe mifumo yetu ya afya inaweza kukabili na changamoto hizi za magonjwa ya mlipuko.”

Marais walioshiriki mkutano huo ni Phillipe Nyusi (Msumbiji), Lazarus Chikwera (Malawi), Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Haikande Hichelema (Zambia) Felix Tshisekedi (DRC). Wengine ni wawakilishi wa Wakuu wa Nchi kutoka Afrika Kusini, Lesotho, Eswatini, Seychelles na Madagascar.

DKT HUSSEIN :ACHENI KUTUMIA MITISHAMBA KUTIBU MACHO

February 02, 2024

 


Daktari Bingwa wa Macho katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo Dkt Hussein Abbas Tayebji amewataka wananchi wanaotumia njia ya kienyeji kutibu macho ikiwemo kutumia mkojo na maji ya chumvi kuweka kwenye macho kama tiba kuacha kufanya hivyo kwani wanaweza kupata madhara makubwa zaidi.

Kauli ya Daktari hiyo imekuja siku chache baada ya kuwepo kwa wimbi la Ugonjwa wa Macho maarufu kama Red Eyes likiendelea kuwatesa watanzania katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Dkt Hussein ambaye pia ni Mratibu wa Macho Mkoa wa Tanga aliyasema hayo leo wakati akizungumzia kuhusu ugonjwa huo kwa mkoa ambapo alisema mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 90 wameugua huku asilimia kubwa wakitokea kwenye Jiji la Tanga

Alisema kwamba badala yake wananchi wanapougua ugonjwa huo wafike kwenye Vituo vya Afya au Hospitali kwa ajili ya kuwaona madaktari ili kuweza kupatiwa matibabu ikiwemo kupewa ushauri nini wafanye.

“Lakini niwaambie kwamba watu waache kutumia mitishamba,kuweka mkojo kwenye macho na maji ya chumvi kwani kufanya hivyo kunaweza kunaweza kusababishia matatizo makubwa sana huku akishauri wafike kwa daktari ili waweze kupata tiba sahihi”Alisema

Aidha Daktari huyo aliwataka pia wale wanaopata maambukizi ya ugonjwa huo wasitumie dawa za mwenzake maana wakitumia dawa vibaya wanaweza kupata matatizo makubwa kwani kila mtu anakuwa na kipimo chake cha matumizi.

Dkt Hussein alisema kwamba mtu mmoja akipata ugonjwa huo anaweza kumuambukiza mwenzake huku akitoa tahadhari wananchi waache kushirikiana kwenye vitu kama vile Taulo,Vitambaa(leso) ya mwenzake ikiwemo maji ya choo.

Hata hivyo Dkt Hussein pia alisema kwamba hivi sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi ikiwemo maeneo mbalimbali ili kuweza kujikinga na ugonjwa huo na hatua za kukabiliana nazo wanapokumbana na hali hiyo.

"Lakini mtu akiumwa na ugonjwa huo ikiwemo wanafunzi,watumishi wanashauriwa kupumzika nyumbani angalau siku mbili tatu ili asiendelee kusambaza kwa watu wengine "Alisema Dkt Hussein
MAKONDA AWASILIANA  WAZIRI BASHUNGWA AKIMTAKA KUONGEZA NGUVU UJENZI WA BARABARA YA KAKONKO

MAKONDA AWASILIANA WAZIRI BASHUNGWA AKIMTAKA KUONGEZA NGUVU UJENZI WA BARABARA YA KAKONKO

February 02, 2024



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amempigia simu Waziri wa Ujenzi Ndugu. Innocent Bashungwa na kumtaka kuongeza nguvu katika kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kakonko kuelekea Halmashauri ya Kakonko yenye urefu wa Kilomita 3 kwa kiwango cha lami ambapo Waziri Bashungwa ameahidi kutekeleza ili wananchi kuondokana na changamoto hiyo ya mawasiliano.

Akiwa Wilayani Kakonko, Mwenezi Makonda amepokea changamoto hiyo ambapo aliwataka TANROADS na TARURA kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kuzingatia muda ilikusudi Watanzania kunufaika na urahisi wa mawasiliano ya barabara kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka.

Pia, Amewasihi watendaji kuongeza nguvu ya ushawishi ili kupata fedha za kutekeleza miradi kwa haraka.

“Ahadi za Rais ni ahadi ya upendeleo na sio maana kwamba mipango iliyopo inaachwa..Hapana, ndio maana tunatekeleza Bajeti kwa kutekeleza Ilani ya CCM na maelekezo ya Viongozi wakuu” Alisema Mwenezi Makonda.
“Kwenye Maendeleo kazi kubwa tuliyonayo ni uwezo wa ushawishi, Keki inaweza kuwa ndogo lakini ni nyinyi namna gani ya kuipambania, Wataalam ongezeni namna ya ushawishi kutekeleza na kukamilisha miradi ya maendeleo Nchini” Amesema Makonda. 

    

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA MAFIA

February 02, 2024

 

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (katikati) akikabidhi vifaa Kinga vya maabara kwa Kaimu Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (kulia) baada ya kutoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa shule ya Sekondari Kitomondo katika Wilaya ya Mafia Februari 1, 2024

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo, Ayen Mathias, akiuliza swali kwa wawezeshaji katika mafunzo ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali shuleni hapo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo wakifuatilia mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani kutoka kwa wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (hawapo pichani).
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki, Stanford Mwasilonda, akiwasilisha mada kuhusu madhara ya Kemikali kwa washiriki wa mafunzo ya matumizi salama ya kemikali.

Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Elice Omary (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na alama mbalimbali za tahadhari za kemikali.

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (kushoto) akiongea na walimu wa shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kutembelea maabara ya Shule hiyo iliyopo wilayani Mafia.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitomondo wilayani Mafia, Ramadhani Janabi (aliyesimama) akiwakaribisha timu ya wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika Mafunzo ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo yaliyofanyika katika shule hiyo Februari 01 2024.


Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (aliyekaa kulia), na Walimu wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara.

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (aliyekaa kulia), na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara katika shule hiyo.


************

Na Mwanaheri Jazza 


Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Imetoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti salama wa kemikali pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya kazi za Maabara kwa wanafunzi na walimu wa sayansi katika shule ya Sekondari Kitomondo wilayani Mafia Mkoa wa Pwani.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Elice Omary, amesema utoaji wa vifaa hivyo utasaidia kuwakinga wanafunzi hao na athari mbalimbali zinazoweza kijitokeza wakati wakifanya mafunzo Kwa vitendo wawapo maabara.

"Tumepata fursa ya kuwapa elimu walimu na wanafunzi wa shule hii ya Kitomondo juu ya madhara yanayopatikana na matumizi mabaya ya kemikali na jinsi ambavyo wanaweza kujikinga, pia tumetoa baadhi ya vifaa Kinga Ili watakapokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo waweze kujikinga na athari mbalimbali zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya kemikali" alisema Elice.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitomondo Ramadhan Janabi amesema vifaa Kinga hivyo vitasaidia walimu na wanafunzi kujikinga wakiwa katika mafunzo ya vitendo Kwa kuwa Maabara Kuna kemikali Hatarishi.

"Kwetu sisi huu msaada utasaidia sana Kwa kuwa tunafahamu maabara Kuna kemikali ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu, hivyo wanafunzi na walimu wanaofundisha watavaa na kuwa salama" alisema Mwalimu Mohamed.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, Amina Athumani na Ayen Mathias wameishukuru Mamlaka kwa kuwapatia vifaa vya kujikinga wakati wakifanya mafunzo kwa vitendo".

"Tunaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutuletea vifaa hivi kwani ni msaada mkubwa kwetu tutajikinga na kemikali hatarishi tukiwa maabara" walisema wanafunzi hao.

RAIS DKT SAMIA SULUHU AMUAPISHA KATIBU TAWALA WA MKOA WA IRINGA IKULU CHAMWINO LEO

February 02, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Doris Ntuli Kalasa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino tarehe 2 Februari, 2024 .
Ndugu Doris Ntuli Kalasa akila kiapo cha  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino tarehe 2 Februari, 2024 .




DKT. MOLLEL AOMBA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA HAMASA YA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

DKT. MOLLEL AOMBA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA HAMASA YA KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

February 02, 2024



Na WAF – Dodoma

Serikali imetoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa kisiasa, kidini na kimila kuungana na Serikali katika kuhamasisha umma kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pale mchakato utakapoanza rasmi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali namba 56 kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge wa Jimbo la Kinondoni aliyeuliza Je, nini kauli ya Serikali juu ya Bima ya Afya kwa Watoto?

Dkt. Mollel amesema kuwa nchini kuna watoto Milioni 31, milioni 1.5 wako kwenye mfumo wa Bima ya afya ya sasa na milioni 30.7 wako kwenye mifumo ya bima za afya nyingine zilizopo nchini.

“Niwahakikishie wananchi kuwa ujio wa bima ya afya kwa wote utakuwa suluhisho la changamoto ya matibabu kwa wananchi wote bila kujali hali ya kiuchumi na kikwazo cha fedha, hivyo naomba mchakato utakapoanza wananchi mjitokeze kujiunga na skimu za zitakazobainishwa ambazo zitakua kwa rika zote”. Ameeleza Dkt. Mollel.

  

CHUJIO LA MAJI KABANGA LAKAMILIKA NEEMA KWA WAKAZI WA KASULU.

CHUJIO LA MAJI KABANGA LAKAMILIKA NEEMA KWA WAKAZI WA KASULU.

February 02, 2024



NAIBU Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema ili kutatua changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya kusafisha na kutibu maji katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, Serikali tayari imekamilisha ukarabati wa chujio la maji la Kabanga ambalo limeanza kufanya kazi.

Mhandisi Mahundi ameyasema hayo leo Februari 1 2024, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Josephine Gezabuke aliyeuliza ni lini Halmashauri ya Mji wa Kasulu itaondokana na matumizi ya maji machafu kutokana na ukosefu wa chujio.

Mhandisi Mahundi amesema Chujio hilo la maji la Kabanga lina uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 1,000,000 kwa siku.

“Ujenzi wa machujio ya maji kutoka vyanzo vya Mto Chai na Miseno umeanza na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mwezi Aprili, 2024, Machujio haya yatakuwa na uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 3,000,000 kwa siku.

“Kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 15. Serikali kupitia mradi wa Miji 28 imeanza ujenzi wa chujio la maji kutoka Chanzo cha Maji cha Mto Ruchugi na kwa sasa mradi huo utekelezaji wake umefikia asilimia 5 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili, 2025 ambapo Chujio hilo litakuwa na uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 15,000,000 kwa siku”amesema
WAZIRI MKUU BUNGENI LEO FEBRUARI 02,2024

WAZIRI MKUU BUNGENI LEO FEBRUARI 02,2024

February 02, 2024

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kushoto) na Mbunge wa Mchinga Salma Kikwete, Bungeni jijini Dodoma, Februari 02, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Bungeni jijini Dodoma, Februari 02, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Jumanne Mtaturu, Bungeni jijini Dodoma, Februari 02, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VIWANDA 7 VYA KUCHAKATA MAZAO YA ASALI VYAJENGWA

VIWANDA 7 VYA KUCHAKATA MAZAO YA ASALI VYAJENGWA

February 02, 2024





Na. Anangisye Mwateba- Dodoma

Serikali imewezesha ujenzi wa viwanda saba (7) vya kuchakata na kufungasha asali katika Wilaya za Sikonge, Mlele, Nzega, Tabora, Manyoni, Kibondo na Bukombe vitakavyotumika kuongezea thamani asali inayozalishwa na kuuzwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Haya yamebainika wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) akijibu swali la Mhe. Athuman Almas Maige Mbuge wa Tabora Kaskazini katika kikao cha cha tatu cha Mkutano wa 14 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaondelea jijini Dodoma aliyetaka kujua Je Serikali ina mpango gani wa kufanya asali kuwa moja ya zao la kimkakati?

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa ufugaji nyuki ni moja ya shughuli muhimu za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa makabila mengi hapa nchini, Afrika na katika maeneo mengi duniani.
- Advertisement -


Aidha, ufugaji nyuki una mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula kupitia uchavushaji. Ufugaji Nyuki ni miongoni mwa shughuli za kiuchumi hasa kwa jamii inayoishi kando kando na maeneo yaliyohifadhiwa.

‘Kwa kutambua umuhimu wa shughuli hii, Serikali imechukua hatua kadhaa za kufanya asali kuwa zao la kimkakati. Hatua hizo ni pamoja na: Kuimarisha mifumo ya usimamizi pamoja na kutunga na kutoa miongozo mbalimbali inayohusu ufugaji nyuki; kuwezesha wafugaji nyuki kwa kuwapatia mizinga ya kisasa. Mathalan katika kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita zaidi ya mizinga ya kisasa 64,593 imetolewa kwa vikundi vya wafugaji nyuki kutoka katika mikoa mbalimbali”. Mhe. Kitandula alisema.

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa Serikali inatekeleza programu na miradi mbalimbali ya kuwezesha kuongeza uzalishaji wa asali sambamba na kutafuta masoko mapya ya asali katika nchi za Umoja wa Ulaya na Asia.

Pia aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo inatekeleza mradi wa kuwezesha ufugaji nyuki katika mikoa mitano (Tabora, Singida, Katavi, Kigoma na Shinyanga) kwa upande wa Tanzania Bara na Kisiwa cha Pemba kwa upande wa Zanzibar.

Vilevile, Serikali inakamilisha Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki ambao utachochea uzalishaji, mauzo ya asali nje ya nchi pamoja na ajira hasa kwavijana na wanawake.