WAZIRI NAPE NNAUYE AKAGUA MAREKEBISHO YA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA UWANJA WA TAIFA.

WAZIRI NAPE NNAUYE AKAGUA MAREKEBISHO YA MIUNDOMBINU ILIYOHARIBIWA UWANJA WA TAIFA.

December 11, 2016

9
Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye jinsi Kamera za CCTV zinavyoweza kumnasa mtu akifanya jambo lolote baya ndani ya Uwanja wa Taifa wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
8
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye, Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya pamoja na Waandishi wa habari wakiangalia hatua iliyofikiwa ya urekebishaji wa viti na miundombinu mingine ya uwanjani hapo wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.
7
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya pamoja na Waandishi wa habari wakielekea kuangalia hatua iliyofikiwa ya urekebishaji wa viti na miundombinu mingine ya uwanjani hapo wakati alipotembelea kukagua marekebisho ya miundombinu ya uwanja huo leo 11 Desemba, 2016 Jijini Dar es Salaam.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM.

December 11, 2016


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU MGENI RASMI UZINDUZI WA MPANGO WA KUZUIA UNYAYASAJI KIJINSIA

December 11, 2016

Na Ally Daud -MAELEZO
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2017-22) wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Hayo yamesemwa jana  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto (Maendeleo ya Jamii) Bi. Siaba Nkinga katika mkutano na waandishi wa habari, ambapo alisema uzinduzi huo unatarajia kufanyika Desemba 13 mwaka huu Jijini Dar es Salaam
“Mpango huu jumuishi wa miaka mitano utakaouzinduliwa umezingatia nguzo kuu mbili, ambazo ni kuzuia na utoaji wa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia” alisema Bi. Nkinga
Alisema kuwa mpango kazi huo unatarajiwa kutoa msukumo mpya katika kuwezesha utekelezaji  majukumu ikiwemo kutetea, kushauri na kutoa elimu kwa umma ili kuongeza uelewa  kwa jamii kuhusu athari za ukatili kwa wanawake.
Kwa mujibu wa Nkinga alisema kuwa  utafiti uliofanywa na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF) wa mwaka 2015, unaonyesha kuwa Tanzania ina asilimia 3.5 ya watoto wa umri wa miaka  7 – 17 walio nje ya shule kutokana na sababu mbalimbali za ukatili.  
Alibainisha  Vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyoshamiri zaidi ni pamoja na vipigo, ubakaji, ulawiti, mauaji ya vikongwe, na watu wenye ualibino, usafirishaji haramu wa binadamu, kutelekeza familia, udhalilishaji, ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni.

Ufahamu Ugonjwa wa Canine Parvovirus Unaoweza kupoteza maisha ya Mbwa wako ndani ya muda mfupi.

December 11, 2016
Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine ambao huweza kupata magonjwa mbalimbali ambayo hupelekea kufa au kuwapa vilema vya maisha. Mbwa ni kama binadamu yoyote tu ambaye akishambuliwa na magonjwa basi anaweza kuwa dhaifu na kupelekea kupoteza maisha au kupona lakini pia ni wanyama kama binadamu tu wengine ambao hata wakipatwa na baadhi ya magonjwa basi wanaweza kustahimili na kupona kabisa.
Basi leo tutaangalia baadhi ya magonjwa yanayowapata viumbe hivi vinavyopendwa sana na rafiki mkubwa wa binadamu. Kama ilivyo kwa wanyama wengine na binadamu ugonjwa uanza kuonekana kutokana na dalili flani ambapo ndio zinakupa taarifa za kuhisi kuwa mnyama huyu ni mgonjwa. Lakini kuna baadhi ya magonjwa ukiona dalili zake basi unajua kabisa kuwa ishatafuna sehemu kubwa na kupona ni majaaliwa na hali ipo hivyo hivyo kwa wanyama kama Mbwa.
Tuanze na Huu leo
1:Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa mbwa huyo.
Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka sana.
Hizi ndio dalili kubwa sana za ugonjwa huu wa Parvo ni Kuharisha damu, Kutapika, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito ghafla. Mara umuonapo mbwa wako ana dalili hizi basi unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wako wa wanyama kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi ijapokuwa kama mbwa huyo hakuwahi kupatiwa chanjo ya Ugonjwa huo tokea utotoni basi asilimia ya kupona ni ndogo sana kwa maana unapoona dalili za ugonjwa huu basi ni dhahiri unakuwa ushamshambulia sana mbwa huyo.
Nini husababisha ugonjwa huu wa Parvo?
Mara nyingi ugonjwa huu usababishwa na mbwa aliyehathirika moja kwa moja na ugonjwa huu japokuwa kuna sababu nyingine kama endapo mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu anapojisaidia haja kubwa na mbwa mwingine akapita kunusa basi mbwa huyo anakuwa anaambukizwa moja kwa moja. Inasemekana virus vya ugonjwa huu vinauwezo wa kuishi kwenye udongo kwa takribani mwaka mmoja na ugonjwa huu unaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa mbwa mmoja kwenda kwa mbwa mwingine.
Vilevile Ugonjwa huu unaweza kuletwa na viatu endapo mtu amekanyanga kinyesi cha mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu basi anapoingia nyumbani au kwenye mazingira ya mbwa ni rahisi sana kuacha virusi hivyo na ikumbukwe kuwa virusi hivi huishi kwa takribani mwaka mzima kwenye udongo.
Unapohisi umekanyaga kinyesi au kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na virusi vya parvo basi unashauriwa kusafisha eneo hilo kwa kutumia madawa ya kuua virusi kwaajili ya kujirinda na ugonjwa huo hatari.
Vilevile Kutompa chanjo sahihi mbwa wako na kwa wakati kunaweza kupelekea kusababisha mbwa wako kupata ugonjwa huo, Kama unavyofahamu kuwa mbwa wanatabia ya kunusa kila sehemu endapo bahati mbaya kanusa sehemu ambayo tayari kuna virusi vya ugonjwa huo na hana chanjo basi ni rahisi kushambuliwa na virusi hivyo.
Tiba ni Ipi kwa Ugonjwa Huu?
Inavyosemekana mpaka sasa hakuna tiba sahihi ya ugonjwa huu lakini Mbwa anapozaliwa tu na kufikisha muda wa wiki moja hadi mwezi unashauriwa kumpatia chanjo mbalimbali kwaajili ya kumkinga na magonjwa kama haya na chanjo hio sio ya mara moja tu anapochomwa mwanzoni basi unatakiwa kufata ushauri wa mtaalamu wa wanyama kwa ratiba tena ya kurudia kumchoma chanjo katika kipindi kijacho.
Aina hizi za mbwa ndio aina rahisi sana kushambuliwa sana na ugonjwa huu RottweilersDoberman Pinschers, Pit Bulls, Labrador RetrieversGerman Shepherds.
Tukutane tena siku ijayo.
Je umeipenda makala hii?Basi unaweza kushare na Wenzako 
Tu follow instagram kwa jina la @lukazablog @lukazablog @lukazablog