RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64 PIA AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MATUNDA CHA SAYONA CHALINZE MKOANI PWANI

June 22, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa  Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya barabara ya Bagamoyo-Makofia –Msata kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WAASWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

June 22, 2017
tar1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akifafanua jambo kwa watumishi wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma yenye kauli mbiu “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe kuleta Mabadiliko Barani Afrika” Waliyoadhimishi Dodoma Juni 22, 2017 kulia aliyekaa ni Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi.
tar2
Baadhi ya watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika Ukumbi wa Mikutano ofisi hiyo Dodoma ili kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea Barani Afrika.
tar3
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akieleza kanuni za maadili kiutendaji kwa watumishi wa ofisi hiyo wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma walipokutana na watumishi wote Dodoma ili kujadili masuala ya kiutumishi Juni 22, 2017.
tar4
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akisoma Kanuni za Maadili ya Utendaji Katika Utumishi wa Umma wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo ofisi hiyo imeadhimisha kwa kukutana na watumishi wake kujadili masuala ya msingi ya kiutumishi Juni 22, 2017.
tar5
Msaidizi wa Waziri Mkuu (Hotuba) Bw. Abdalah Mtibora akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa mkutano (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 22Juni, 2017.
tar7
Mhasibu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Kissa Mwakipesile akieleza hoja yake kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu ofisi hiyo Bw.Issa Nchansi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Juni 22, 2017 Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
tar8
Afisa Tehama Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Innocent Mboya akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Juni 22, 2017 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
tar9
Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akifunga mkutano wa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 Juni Barani Afrika.
 (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)
……………………………………………………………………………
Na. Mwandishi Wetu
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameaswa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maadili na utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Dkt. Hamisi Mwinyimvua alipokutana na wafanyakazi wa ofisi yake Dodoma kwa lengo la kuiadhimisha Wiki hiyo inayofanyika kila mwaka kuanzia Juni 16-23 Barani Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe kuleta Mabadiliko Barani Afrika”.
“Kila mtumishi wa umma anapaswa kuwa mwadilifu na mchapakazi hivyo niwaombe watumishi wote muwe mfano kwa kuwa waadilifu katika utendaji wenu kwa kuzingatia sheria zote za utumishi wa umma ili kuisaidia Serikali na kuwafikia wananchi kiujumla.”alieleza Dkt.Mwinyimvua
Katika kuiadhimisha wiki hii ya utumishi wa Umma ni wakati pekee wa kujitathimini eneo la kiutendaji na kuona maeneo yenye mapungufu ili yafanyiwe maboresho kwa haraka lengo likiwa kuondokana na mazoea yaliyokuwepo na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Issa Nchansi amewataka watumishi  kuzingatia mambo nane muhimu yaliyoainishwa katika Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ikiwemo; Utoaji wa huduma bora, Utii kwa Serikali, bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, uwajibikaji kwa umma,kuheshimu sheria, matumizi sahihi ya taarifa na uadilifu sehemu ya kazi.
Naye, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi aliwaomba watumishi wote kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu kwa kuwawezesha vijana kielimu, kiuchumi na kijamii ili waweze kuzalisha na kuwa tegemeo la taifa.
“Niwaombe watumishi wote kuiangalia hili kundi la vijana wanaoajiriwa na Serikali kwa kuwatia moyo na kuwaunga mkono katika utekelezaji wa kazi zao” alisisitiza Tarishi
Sambamba na hili, Katibu Mkuu, Tarishi alisema  kuwa ili kuwe na utendaji wenye matokeo lazima kuitumia wiki hii kukumbushana majukumu na nafasi zetu katika kuitumikia serikali.
“Tuwe na utendaji wenye matokeo na si kuhesabu siku, miezi hadi mwaka bali tuwajibike kwa uadilifu kila muda tuwapo Serikalini.”
MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ,IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA ZANZIBAR

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI ,IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA ZANZIBAR

June 22, 2017
unnamed
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza na maafisa wakuu wa Jeshi la Polisi alipofanya kikao na maafisa hao akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kabla ya kwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Ali Mohamed Shein. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani makame. Picha na Hassan Mndeme.
1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Hassan Mndeme.
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Hassan Mndeme.

CRDB BANK tawi la Azikiwe Premier yaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwa Kuwakumbuka Watoto Waishio Katika Mazingira Magumu

June 22, 2017
Benki ya CRDB ndio benki yenye huduma bora Tanzania kuliko benki nyingine yoyote, imeendeleo kuonyesha kuwajali Watanzania ambapo Menejmenti na Wafanyakazi wa CRDB Bank Tawi la Azikiwe Premier, la jijini Dar es Salaam, wameadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kwa kuwatembelea watoto wanaotunzwa katika kituo cha Jeshi la Wokovu kwa kuwapelekea zawadi mbalimbali za mahitaji muhimu, na kuwadhamini baadhi yao kwa kuwafungulia akaunti, kuwachangia, kugharimia elimu zao, na kugharimia mahitaji yao.


CRDB Azikiwe Premier Photo 8.JPG 
Wafanyakazi wa CRDB BANK, tawi la Azikiwe Premier, wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaotunzwa katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 7.JPG 
Mfanyakazi wa CRDB BANK, tawi la Azikiwe Premier, akikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaotunzwa katika kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 17.JPG 
Mkurugenzi na wafanyakazi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, kwenye picha ya pamoja na mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 19.JPG 
Mkurugenzi na wafanyakazi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, wakiwa na keki ya mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 5.JPG 
Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Musula, na wafanyakazi wa tawi hilo, na wateja, wakionyesha fedha walizomchangia mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 18.JPG 
Mkurugenzi na wafanyakazi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, wakikata keki na mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 20.JPG 
Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Musula, akimlisha keki mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.
CRDB Azikiwe Premier Photo 11.JPG 
Mkurugenzi wa CRDB Bank, Tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Musula, akimlisha keki mtoto Mariam Stephen Jackson, aliyekuwa akiishi katika mazingira magumu. Marriam pia amefunguliwa akauti maalum ya watoto ya benki hiyo iitwayo Junior Jumbo,ambayo wafanyakazi wa Tawi hilo la Azikiwe Premier, wananchangia kugharimia elimu yake. Sherehe hiyo imefanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Africa ilioadhimishwa na benki hiyo kwa wiki nzima sasa.

DTB BENKI KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZAO MKOANI TANGA

June 22, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa ajili ya wateja wao mkoani Tanga  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
 MKUU wa wilaya ya Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari hiyo
 Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
 Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa habari
 Wageni waalikw
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto akisalimiana na Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Kassim Kisauji wakati wa hafla ya futari hiyo
 sehemu ya wageni waalikwa wakipata futari

BENKI ya Diamond Trust(DTB) Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wa huduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza namba ya wahudumu ikiwa ni mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi wakati futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu dhuiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.

Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigo mpana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa Tanga ambao unatarajiwa kufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .

“Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amana kubwa za wateja hivyo tumeona kuwaandalia futari hiyo ni namna bora ya kuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.

“Unajua wateja wetu wamekuwa wakitusapoti hivyo ndio maana tumeona vizuri kuwaandalia futari lakini pia niwaambie kuwa  wanaweza kutuma na  kusafirisha fedha kwa haraka kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi”Alisema

Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkuu  wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliwataka wakazi wa mkoa huu kuendelea kumuombea Rais John Magufuli aweze kuendelea kupigania haki za watanzania wanyonge ambazo zimekuwa zikipotea.

Alisema kuwa kiongozi huyo mkuu wa nchi amekuwa akifanya mambo makubwa ya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo haraka na kukuza uchumi ambao utatufikisha kwenye mafanikio.

“Ndugu zangu waislamu tuendelee kuombea nchi yetu na Rais wetu ili yeye na viongozi wote waendelee kutenda yaliyomema na yanayompendeza mwenyezi mungu”Alisema RC Shigella.

“Lakini pia niendelee kuwashukuru kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano kwa mkoa huu kwa kipindi cha tokea mwezi ulipoanza mpaka sasa  hivyo muendelee kuwa na upendo kwa watu wote.

Awali akizungumza katika futari hiyo,Shehe wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu  aliwataka waislamu mkoano hapa kuendelea mshikamano waliokuwa nao kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuendelea kutenda yaliyo mema.

“Tuendelee kushikamana tupendane lakini kubwa zaidi tuhakikisha tunazingati kufanya ibada mara kwa mara na sio kipindi cha mwezi huutu hata baada ya kumalizika kwake “Alisema.

TIGO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA

June 22, 2017
. Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Nyanda za juu kusini Bwana Jackson Kiswaga akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kugawa msaada katika kituo cha watoto Dairlybread kilichopo kata ya Nzihi, akiwa na baadhi ya viongozi wa kata hiyo.

Mwenyekiti wa kata ya Nzihi akifafanua jambo mbele ya wananchi na watoto wa kituo cha Dairlbread kilichopo kata ya Nzihi mkoani Iringa.

Baadhi ya watumishi wa kituo cha kulea watoto cha Dairlbread cha kata ya Nzihi  wakijitambulisha wao na watoto mbele ya mkurugenzo wa kampuni ya Tigo nyanda za juu kusini Bw. Jackson Kiswaga hayupo pichani. 
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya nyanda za juu kusini, Jackson Kiswaga akikabidhi misaada ya vyakula na mahitaji mengine  kwa vituo vya watoto wenye uhitaji  vya Daily Bread Ahsante Sana na Kipera Disabled  mkoani Iringa juzi.

FANYA YAFUATAYO KUNOGESHA SIKUKUU YA EID-AL-FITR

June 22, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Ni siku chache zimebakia kabla ya waumini wa dini ya kiislamu nchini na duniani kote kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Zipo namna tofauti za kusherehekea sikukuu hii kulingana na sehemu watu walipo.

Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuifanya sikukuu hii kuwa ya tofauti na kipekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka.   
 
Fanya maandalizi pamoja na familia. Katika kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia sikukuu basi ni vema ukawashirikisha kwenye maandalizi yake. Kama baba au mama wa familia na una watoto au ndugu unaishi nao litakuwa ni jambo zuri kama mtafanya hata kikao kidogo na kujadili. Kwa mfano, shughuli zote zitakazofanyika kipindi cha sikukuu, chakula kitakachopikwa, vinywaji, zawadi, wapi kwa kusherehekea, wageni gani wa kuwaalika, kupamba nyumba nakadhalika. Hii itasaidia siku hiyo ikifika kila mtu anafurahia na sio kufanya mambo ambayo yatakufurahisha wewe tu kuwaacha baadhi ya wengine kunung’unika.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA BAGAMOYO-- MSATA KM 64 PIA AWEKA JIWE LA MSINGI KIWANDA CHA MATUNDA CHA SAYONA CHALINZE MKOANI PWANI

June 22, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Mama Salma Kikwete (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete , Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wa Kiserikali na Wabunge, akivuta kitambaa kuashiria jiwe la ufunguzi wa  Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuweka jiwe la ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya barabara ya Bagamoyo-Makofia –Msata kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Pwani na Dar es Salaam mara baada ya kufungua barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo, Mama Salama Kikwete, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Norman Sigala, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Hamphrey Polepole pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kufungua Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akielezea hatua za ujenzi wa Madaraja katika barabara ya Bagamoyo-Msata huku Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha Viuadudu cha Kibaha mkoani Pwani.
Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akisalimia kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akizungumza kabla ya ufunguzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia Msata yenye urefu wa kilometa 64 katika eneo la Daraja la Ruvu chini, Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Prof. Norman Sigala wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya ufunguzi wa barabara hiyo ya Bagamoyo-Msata.