TUMUUNGE MKONO DK.MAGUFULI NDIO CHAGUO LA CCM- CATHERINE MAGIGE

July 26, 2015

SAM_4396 
Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha ,Catherine Magige  akizungumza jana katika mkutano wa wagombea Ubunge 12 kupitia chama cha mapinduzi waliofanya ziara ya kujinadi kwa wananchama pamoja na wananchi kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho jana katika mtaa wa kati(CCM Mkoa),ambapo hivi karibuni Catherine aliibuka ushindi wa kishindo kwa kura 409 kati ya kura 560 huku anayemfwatia akipata kura 248.
Habari picha na Pamela Mollel
SAM_4403 
Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha,  Catherine Magige  akisalimiana na wanachama wa chama hicho jana jijini Arusha,Aliwatoa rai kwa wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi kumuunga mkono mgombea Urais Dk.John Pombe Magufuli kwani ndio chaguo la CCM,huku pia akisisitiza wanaccm kuchagua kiongozi kwanzia ngazi ya udiwani,ubunge anayekubalika ndani ya CCMna nje ya CCM.
SAM_4391 
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha, Mayasa Kimbau ambaye pia ni mratibu wa Mkoa akiteta jambo na Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha jana katika mtaa wa kati (CCM Mkoa) wakati wa ziara ya watia nia wa chama cha mapinduzi wakijitambulisha na kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kupitishwa na chama hicho katika nafasi ya Ubunge.
SAM_4404 
Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT)Catherine Magige Mkoa wa Arusha akifurahia jambo na mwenyekiti wa wilaya ya Arusha katika ofisi za chama cha mapinduzi jijini Arusha jana wakati watia nia ubunge 12 kupitia chama hicho walipata nafasi ya kujinadi kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.
SAM_4289 
Mbunge viti maalum kundi la wananwake (UWT) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige  akizungumza na waandishi wa habari siku alipotangazwa kuwa mshindi.

PHIDESIA MBUNGE VITI MAALUM AWATAKA WANANCHI WASIRUBUNIWE

July 26, 2015


SAM_4394 
Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima aliyeshinda katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).akizungumza katika mkutano wa chama cha mapinduzi jana mtaa wa kati (CCM MKOA)wakati wagombea 12 wa chama hicho walipofanya ziara ya kutembelea kila kata na kujinadi kwa wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi wasirubuniwe na kama walipewa rushwa na mgombea yeyote wasimchague bali wamchague kiongozi sahihi wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  katika jimbo la Arusha.
 …………………………….
Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog
SAM_4366 
Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalimaambaye alishinda katika  kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple “A”,Mkurugenzi wa Phide entertainment akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM katika ofisi za (CCM Mkoa) jijini Arusha jana
SAM_4398 
Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi mtaa wa kati jijini Arusha ambapo aliwataka wapambe wawagombea watulize mung’ari zao na kuacha tabia ya kukebihana huku akisisitiza wananchi kuchagua kiongozi bora.
SAM_4363 
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia  ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge akiteta jambo na Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple “A” na Mkurugenzi wa Phide entertainment kabla ya mkutano wao wa kujinadi kuanza.
SAM_4368Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple “A”na Mkurugenzi wa Phide entertainment akibadilishana mawazo na wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge
SAM_4374Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple “A” na Mkurugenzi wa Phide entertainment akiwa katika picha ya pamoja na watia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM.
SAM_4372Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple “A” akisalimiana na wadau ambao ni watia nia Ubunge na Udiwani,kushoto ni Simba Salum anayeomba chama cha mapinduzi kumpitisha kuwania nafasi ya udiwani mtaa wa kati bondeni na kulia wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge

Makundi 5 yang'ara ndani ya Temeke kwenye usaili wa kwanza Dance 100% 2015 Temeke

July 26, 2015
Usili wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.

Makundi haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.

Akizungumza baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki usajili unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda, ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande wa dansi zaidi.

Majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie Vampire.

Majaji pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo wanavyovitumia kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia ushindi.

Usajili wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka huu.

Usikose kujionea kwa urefu yote yaliyojiri  pale TCC Chang'ombe katika mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.

East Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu na mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance 100% (2015).

PICHANI JUU: Kati ya makundi matano yaliyopita kwenye usaili wa kwanza wa Dance 100% (2015) - Temeke. Kundi linaitwa 'The Best Boys Kaka Zao'
 Kutoka kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100%  ni Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka Temeke.
 Shabiki wa kundi la 'Noma Sana' akiwa anajitayarisha kushangilia timu yake kwenye usaili wa kwanza Temeke kwenye Dance 100% (2015)
 Washiriki wa kundi la 'Noma Sana' mwaka huu kwenye Dance 100% wakiwa wanafanya yao viwanja vya TCC Changombe.
Watangazaji rasmi wa Dance 100%, TBway 360 na Maggie Vampire wakiwa wanasherehesha kikamilifu huku burudani mbalimbali zikijiri TCC Changombe.
KAWAIDA
RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KUADHIMISHA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

July 26, 2015


1
Brass Bendi ya Jeshi ikiingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuanza Maadhimisho.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO
2 3
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa (JWTZ) , Luteni Jenerali Samweli Ndomba akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli baada ya kuwasili viwanja vya mnazi mmoja.
4
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akiwasili.
5
Spika wa Bunge la Jamhuri Anne Makinda akiwasili.
6
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Idd.
7
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwasili.
8
Rais Jakaya Kikwete akiwasili.
9
Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kuimba wimbo wa Taifa.
10
Rais akiweka mkuki na ngao kwenye mnara wa Uhuru.
11
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akirejea kwenye sehemu yake baada ya kuweka sime kwenye mnara.
12
Kiongozi wa Mabalozi akiweka shada la amaua.
13
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi akiwa ameweka upinde na mshale kwenye mnara.
14
Mwenyekiti wa Tanzania Legion akiweka shoka kwenye mnara.
15
Baadhi ya wazee walioipigania Tanzania, viongozi wa dini na wageni waalikwa waliohudhuria.
16 17
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam sheikh Alhad Musa Salum akisoma dua.
18
Mchungaji Theophil Bolampete wa Kanisa Katoliki akiomba.
19
Mchungaji John Komoyo, akiomba.
20
Rais Jakaya Kikwete akiongoza viongozi mbalimbali kuimba wimbo wa Taifa baada ya Maadhimisho kukamilika.
22
Rais Jakaya Kikwete, akiwaaga baadhi ya Mashujaa waliopigana vita kuikomboa Tanzania.
23
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Iddi na Spika wa Bunge Anne Makinda wakiondoka kwenye viwanja vya mnazi mmoja.
24 25 26
Baadhi ya askari wa JWTZ waliopigana vita ya kuikomboa Tanzania.
27
Baadhi ya wananchi waliofika nje ya viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia Maadhimisho.

Mahojiano na Charles Magali ndani ya Washington DMV

July 26, 2015
Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi
Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio