DKT KIGWANGALLA AWATAKA WANAFUNZI KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

DKT KIGWANGALLA AWATAKA WANAFUNZI KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI

May 17, 2016

Wanafunzi Nchini hususani wale wa wa kike wameshahuriwa kujikita zaidia katika kupenda masomo ya Sayansi kwa bidii zote ili kuifanya Tanzania kufikia kwa haraka malengo yake ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Hii ni pamoja na Ukuaji wa viwanda vya ndani ambavyo vingi vitategemea ujuzi wa Sayansi na teknolojia.

Rai hiyo ametolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa mgeni rasmi wa Mahafali ya 19 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekodari ya St. Mary’s Mazinde Juu iliyopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Shule hiyo ambayo ni ya Wasichana watupu, jumla ya wanafunzi 136 wanaomaliza kidato cha sita walitunukiwa vyeti vyao vya kumaliza shule.
Dk. Kigwangalla amewapongeza wanafunzi hao 136 ambapo kati yao wanafunzi 80, ni wa mchepuo wa Sayansi ambapo amewataka kuto kata tamaa na baadala yake waongeze juhudi hadi elimu ya juu Zaidi ya ngazi ya Chuo huku pia akiwataka wanafunzi wengine hapa nchini kujikita katika masomo hayo ya Sayansi katika zama za sasa ambayo Tanzania inaelekea katika mapinduzi ya viwanda na uchumi wa Kati.

RUSHWA YA NGONO HUCHANGIA KURUDISHA NYUMA KASI YA MAENDELEO

May 17, 2016

 Mratibu wa Asasi ya kuinua maendeleo ya Jamii na Kuhifadhi Mazingira (Ececo)Ndosho Hamisi akisisitiza jambo wakati akitoa mada juu ya madhara ya rushwa ya ngono iliyofanyika kijiji cha Duga wilayani Mkinga iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa jamii ya wasichana wa wafuigaji wa kimasaia iliyofanyika

 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Duga Maforoni wakifuatilia mada mbalimbalio zilizokuwa zikiwasilishwa
 Katibu wa Asasi ya Kuinua Jamii na Kuhifadhi Mazingira (ECECO TANZANIA),Said Kamba akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina hiyo
 Diwani wa Kata ya Duga Maforoni Ally Ally akizungumza katika semina hiyo

IMEELEZWA kuwa rushwa ya ngono imekuwa ni tishio hapa nchini hali inayochangia kurudisha nyuma kasi ya maendeleo kwani imekuwa ikipunguza demokrasia na utawala bora kwa watanzania jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa vitendo.

Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Asasi ya Kuinua Maendeleo ya Jamii na Kuhifadhi Mazingira (Ececo), Ndosho Hamisi wakati wa semina ya rushwa ya ngono iliyofanyika Kijiji cha Maforoni Kata ya Duga wilayani hapa na kufadhiliwa na Women Fund Tanzania  (WTF)iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu mambo hayo kwa wasichana na wanawake hasa wa jamii ya wafugaji wa kimasai.

Alisema kuwa tatizo hilo limekuwa likichukua kasi kwenye sekta nyingi na kusababisha kukandamiza haki za wanaostahili kuweza kupata fursa za kuweza kupata nafasi za kukuza uchumi wao na hivyo wengi wao kuishia katika hali duni.

  “Ukiangalia leo hii unaweza kutaka kitu Fulani mahali lakini kwa sababu hauna sifa ambazo zinapaswa kukipata basi yanaweza kutumika mazingira ambayo sio sahihi ili uweze kukipata kutokana na kumtimizia mahitaji yake mlengwa na hili limekuwa tatizo kubwa “Alisema.

 “Ni kosa kisheria mtu mwenye mamlaka kumpandisha cheo mfanyakazi wake kutokana na kuwepo kwa mazingira ya rushwa ya ngono kwa sababu inasababisha kupunguza ufanisi kazini na hivyo kushindwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.

Alisema jambo hilo limekuwa na madhara mengi kwa jamii ikiwemo kupata magonjwa makubwa ikiwemo ukimwi lakini pia uzalilishaji kitendo ambacho kinapelekea kushusha utendaji na kuchangia kurudisha nyuma maendeleo.

Awali akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Diwani wa Kata ya Duga, Ally Mohamed aliipongeza asasi hiyo kwa kuona umuhimu kuwapatia mafunzo hayo ambayo yataweza kuwapa uelewa juu ya madhara ya rushwa ya ngono na kubadilika

“Unaweza kukuta wakati mwengine watoto wadogo wanazalilika kutokana na kutokujua madhara ya rushwa ya ngono hivyo semina hii itawafungua macho kuona namna ya kuweza kupiga vita vitendo hivyo “Alisema
SERENGETI BOYS YATAKATA INDIA

SERENGETI BOYS YATAKATA INDIA

May 17, 2016
Timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ leo Mei 17, 2016 imechanua vema baada ya kuilaza India mabao 3-1 katika mchezo wake wa pili wa michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka India katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Tilak, Maidan mjini Goa, India.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Maziku Amani katika dakika ya 21 wakati lile la pili India walijifunga baada ya beki wake kuhangaika kuokoa krosi ya Nickson Kibabage katika dakika ya 28 wakati lile la tatu lilifungwa na Asad Juma katika dakika ya 48 huku lile la India likifungwa na Komal Thatal katika dakika ya 38.


Kwa ushindi huo, Serengeti Boys sasa wanasubiri angalau sare au ushindi wa mchezo mmoja kati ya miwili, dhidi ya Korea Kusini utakaopigwa Alhamisi Mei 19, 2016 na Malaysia Mei 21, 2016 ili icheze nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Mei 12 kabla ya kufikia fainali zake Mei 26, mwaka huu. Katika mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoka sare ya Marekani ya bao 1-1.  

Katika mchezo huo, Serengeti Boys iliwakilishwa na Ramadhani Kabwili, Ally Nganzi, Ally Msengi, Asad Juma, Dickson Job, Issa Makamba, Maziku Amani, Nickson Kibabage, Shaaban Ada, Syprian Mtesigwa na Mohammed Abdallah.

India: Mohammed  Nawaz, Reamsochung Aimol, Boris Singh, Mohammed Khan, Juendra Singh, Suresh Wangjam, Amarjit Kiyam, Khumanthem Meetei, Sandjev Staldi, Aniket Jadhav na Komal Thatal.

Matokeo haya yanapatikana pia kupitia link za:
Indian Football Team Official FB page: https://www.facebook.com/TheIndianFootballTeam/

AIFF Youtube channel:  https://www.youtube.com/channel/UCiZ7OnWhEiPMA3II0VgLA6A
DK. MENGI ATOA DARASA KWA WASHIRIKI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA

DK. MENGI ATOA DARASA KWA WASHIRIKI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA

May 17, 2016
Dk. Reginald Mengi saini
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016 kwa ajili ya kutoa muhadhara kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika chuo hicho.(Picha zote na Modewjiblog)
IMELEZWA jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblog ofisini kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama chuoni hapo.
“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni kwao watazingatia usalama.
“Wote wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,” aliongeza Meja Jenerali Mohamed.
Wataalamu walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.
Akielezea ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa washirika.
Alisema chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.
“Chuo chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo masomoni.
“Dk. Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.
Dk Mengi na Meja Jenerali Yacoub Mohamed
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akisalimiana Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada ya kuwasili chuoni hapo kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama Mei 16, 2016 jijini Dar es Salaam.
Alisema chuo hicho hupokea washiriki ambao ni viongozi katika ofisi wanazofanyia kazi na hupokea washiriki kutoka nchi mbalimbali ambapo hupatiwa elimu kuhusu usalama ili wanapotoka chuoni hapo wakafanye kazi kwa umakini ili wasiweze kuwa sababu ya kupoteza usalama katika maeneo yanayowazunguka.
Katika mada yake iliyozungumza kuhusu wajibu wa vyombo vya habari binafsi katika usalama wa Taifa, Dk. Mengi alisema vyombo visipokuwa makini vikawajibika kitaaluma vinaweza kusababisha migogoro itakayohatarisha usalama wa taifa.
Akielezea uzoefu wake kama mmiliki wa vyombo vya habari binafsi alisema usalama ni jambo la muhimu kwa kila mtu bila kujali ana nafasi gani katika nchi hivyo ni wajibu wa kila mtu kushiriki katika kuimarisha usalama.
Alisema vyombo vya habari wanahakikisha habari zinazotolewa zinakuwa hazina madhara ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa amani lakini kusimamia misingi na maadili ya uandishi wa habari.
Brigadia Jenerali Yohana Mabongo
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Brigadia Jenerali Yohano Mabongo mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
“Kama kuna utulivu, mshikamano na usalama wa taifa kuna faida kwa taifa na hilo linaweza kusaidia kukuza kwa uchumi wa nchi ambao pia utakuwa na faida kwa kila mwananchi,
“Vyombo vya habari vinatakiwa kufuata maadili ya kazi yake kuupasha umma habari na kutoa elimu bila kuathiri hali ya amani na utulivu kwa sababu tunaelewa kuwa pamoja na kutoa habari lakini pia ni wajibu wetu kuhakikisha kuna usalama nchini,” alisema Dk. Mengi.
Yacoub Mohamed NDC
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama chuoni hapo.
Dk. Reginald Mengi 1
Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016.
Reginald Mengi NDC
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Meja Jenerali Yacoub Mohamed
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa historia fupi ya chuo hicho kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Dk. Reginald Mengi akiaga
Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akiagana na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed (kulia) mara baada ya kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika chuo hicho kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
National Defence College
Muonekano wa mbele wa Jengo la Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, DKT. ASHA- ROSE MIGIRO

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, DKT. ASHA- ROSE MIGIRO

May 17, 2016

1 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Balozi wa Tanzania  nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose  Migiro kabla ya mazungumzo yao  Ofisini kwake jijini Dar es salaam  Mei 17, 2016.
2 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha – Rose Migiro  ofisini kwake jijini Dar es salaam Mei 17, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASIKINI AFRIKA NA KUKABIDHI HUNDI ZA MADAWATI

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASIKINI AFRIKA NA KUKABIDHI HUNDI ZA MADAWATI

May 17, 2016

sm1 
Washiriki wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.                           
sm2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya Masikini kwa Nchi Jumuiya za Afrika uliofunguliwa leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
sm01 
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kufungua Mkutano wa kwanza wa Mifuko ya Maendeleo ya Jamii TASAF kuhusu mpango wa Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokua akifungua mkutano leo Mei 16, 2016 katika Hoteli ya Ngurudoto Mjini Arusha.
sm4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anaeshuhulikia Nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bibi. Bella Bird walipokutana katika ukumbi wa Mikutano wa Ngurudoto Mjini Arusha leo Mei 16, 2016, ambapo Makamu wa Rais alifungua mkutano wa kwanza wa TASAF kuhusu Uhawilishaji wa Fedha na kunusuru kaya masikini kwa Nchi Jumuiya ya Afrika.
sm5 
Makamu wa Rais wa Jamhuri uya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya  Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mkoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha.katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe.       sm6 
Makamu wa Rais wa Jamhuri uya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Hundi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela  kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa Madawati. Jumla ya Madawati Elfu 16.5 yenye thamani ya Tshs. 1 Bilioni moja zilikabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa inayozunguka Mbuga ya Hifadhi ya Taifa kwa ajili yakukabiliana na tatizo la Madawati kwenye Shule zote zilizomo katika Wilaya za Mkoa hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 16,2016 katika ukumbi wa Ngurudoto mjini Arusha. Katikati waziri wa Maliasili Utalii Profesa Jumanne Magembe (Picha na OMR)

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO,JAMES MBATIA AANDAA JIMBO LAKE KUKABILIANA NA MAJANGA (NDENGA).

May 17, 2016
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akichokoza mada wakati wa kongamano la Elimu juu ya maafa katika jimbo hilo baada ya kukumbwa na mafuriko ,Kongamano lililofanyika katika shule maalum ya Viziwi na kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa,Vijiji na Vitongoji,Maofisa watendaji,Madiwani,wakuu wa idara mbalimbali katika jimbo hilo.
Baaadhi ya washiriki wa kongamano hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akichangia mada katika kongamano hilo ambalo alikuwa mgeni rasmi pia,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia na kulia Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akichangia mada katika kongamano hilo lililotumika pia kuondoa itikadi za kisiasa huku akitoa wito kwa viongozi wote katika jimbo hilo kufanya kazi za maenedeleo bila ya kujali itikadi za kisiasa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akichangia mada katika kongamano hilo lililoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akielea namna ambavyo Wilaya hiyo ilivyopata athari kutokana na mvua zilizonyesha Aprily 24 na 25 mwaka huu.
Mwenyekiti wa mji mdogo wa Himbo ,Hussein Jamal akichangia mada katika kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga,(kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila wakiteta jambo wakati kongamano hilo.
Baadhi wa wachangiaji katika kongamano hilo wakitoa michango yao.
Mbunge Mbatia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga.
Washiriki wa kongamano hilo wakiwa wamejigawa kulingana na kata wanazotoka ambazo zinafikia 16 katika jimbo la Vunjo wakijadili maafa yaliyozikumba kata hizo na namna ya kukabiliana nayo kabla ya mkutano huo kutoa maazimio.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO,SAID MECKY SADICKY AFANYA ZIARA KATIKA MAGHALA NA MADUKA YA MARENGA INVESTMENT KUJIONEA HALI YA TATIZO LA SUKARI

May 17, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwasili katika ghala la kuhifadhia bidhaa la Kampuni ya Marenga Investment alipofanya ziara ya ghafla kwa lengo la kujionea hali ya upungufu wa sukari pamoja na kufanya ukaguzi mwingine.aliiongozana nao ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwa katika ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali la kampuni ya Marenga Investment.kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Wilbroad Mutafungwa.
Mifuko ya Sukari iliyopo katika ghala hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiwana Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa wakimngojea mmiliki wa Ghala hilo .
Sehemu ya Sukari inayozalishwa na kampuni ya sukari ya TPC ikiwa katika mifuko ya kilogramu 2.
Sehemu ya bidhaa ya unga ikiwa katika Ghala hilo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya Novatus Makunga na Kamanda wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa wakati wakimngojea mmiliki wa ghala hilo.
Mmilikiwa ghala la kuihifadhia bidhaa za kampuni ya Marenga Investment,Joseph Kimosso (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa Saidi Mecky Sadicky mara baada ya kuwasili katika ghala hilo.
Sehemu ya Mchele ukiwa katika gunia .
Mmiliki wa Ghala la kuhifadhia bidhaa mbalimbali za kampuni ya Marenga Investment,Joseph Kimosso akiumuongoza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky kutembelea maeneo zilipohifadhiwa bidhaa mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akitembelea kukagua ghala la kampuni ya Marenga.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akikagua moja ya bidhaa ili kujua endapo muda wake wa matumizi umemalizika ama la.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akikagua sukari ilifungwa katika mfuko maalum ya uzito wa Kg 2 alipotembelea Super Market ya Marenga iliyopo Kiboriloni mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akizungumza na wateja waliofika katika duka la Marenga kwa ajili ya kununua Sukari.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akitoka katika Duka la Marenga Investment.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadicky akiagana na mmiliki wa kampuni ya Marenga Investment ,Joseph Kimosso baada ya kutembelea Maduka ya kampuni hiyo pamoja na kufanya ukaguzi katika maghara ya kampuni hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.