TANAPA KUANZISHA MIRADI YA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI VYA MAENEO YANAYOZUNGUKA HIFADHI HIZO.

September 02, 2013
NA AMINA OMARI,PANGANI

Hifadhi ya Taifa TANAPA inatarajia kuanzisha miradi ya vivitio vya asili vilivyoko kwenye vijijini vya maeneo yanayozunguka hifadhi hizo ili kuimarisha uchumi wa maeneo hayo na jamii inayozunguka hifadhi hizo nchini.

Hayo yameelezwa na Meneja Ujirani mwema Taifa Ahmed Mbagi wakati akiongea na  waandishi wa habari za mazingira Mkoani Tanga TARUJA walipotembelea hifadhi ya saadani ikiwa ni sehemu ya mafunzo yaliyoandaliwa na TANAPA .

Amesema miradi huyo ni sehemu ya mipango waliyokuwapo nayo ya kuhakikisha vijiji vinavyopakana na hifadhi za taifa kunufaika na wageni waoingia kwa njia ya vivutio vilivyoko kwenye maeneo yao kwa lengo la kujiongeza kipato.

“Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali walizokuwapo nazo kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na tamaduni zilizoko sehemu husika “.AlisemaMbagi.

Nae Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo amesema kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivituo vilivyoko kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.

“Hapa kijijini tuna vivutio kama soko la watumwa,mbuyo nyonga ambao ulitumika kuwanyonga watumwa pamoja na makaburi ya wajerumani wakwanza kurika saadani lakini kutoka na kukosa uwelewa wa kuvitangaza vivutio hivyo tunakosa fedha kutoka kwa watalii”alisema Mselo.

Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi  wa maeneo ya jirani yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze kuiongezea kipato kitakacho saidia kijiji na wananchi wake.

Hifadhi ya Saadani licha ya kuwa na mbuga za wanyama ni moja ya eneo la kwanza kuanzishwa kwa biashara ya soko la watumwa na waarabu waliowahi kuishi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki karne ya 14 iliyopita.

PANGANI YAHITAJI MIL 200 ILI KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA.

September 02, 2013
Na Oscar Assenga,Pangani
JUMLA ya shilingi milioni 200 zinahitajika kila mwaka ili kuweza kutekeleza miradi ya maendeleo katika Idara ya Afya wilayani Pangani mkoani Tanga  iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi mzuri.

Kaimu Mganga wa wilaya ya Pangani,Dr.Frank Makunde aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari za vijijini mkoa wa Tanga (Taruja)walioitembelea halmashauri ya wilaya hiyo kwa lengo la kuzungumza na waataalamu kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.

Waandishi hao walikuwa wilayani Pangani kwenye semina ya wandishi wa habari za mazingira ambayo iliratibiwa na chama hicho na kufadhiliwa na shirika la hifadhi ya Taifa ya Tanzania (Tanapa) yenye lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya umuhimu na uhifadhi wa mazingira.

Makunde amesema idara hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti hali ambayo inapelekea kukwamisha baadhi ya miradi yao muhimu kwa jamii zinazowazunguka na kushindwa kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Aliongeza kuwa mfumo manunuzi uliowekwa na serikali unakwamisha sana watendaji mbalimbali kwenye halmashauri hasa katika idara ya afya na kupelekea kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo.

   "Mfumo wa kuwalazimisha kununua vitu MSD wanapeleka maombi ya vitu wanaambiwa havipo hali ambayo inawapa usumbufu mkubwa wa kusubiri wakati uhitaji wetu ni kwa wakati huo hivyo kupelekea kukwambisha shughuli zetu za kila siku ....tunaiomba serikali iangalie mfumo wa MSD usiwe mmoja uwe zaidia ya mmoja ili kuleta ushindani "Alisema Makunde.

Aidha alisema idara hiyo pia inakabiliwa na uhaba wa watumishi hali ambayo inapalekea watumishi wengine kufanya kazi za ziada na kueleza suala lengine linalowapa wakati mgumu sana ni kutokuwepo wa nyumba za kutosha za watumishi kitendo ambacho kinachangia watumishi wengine kutopenda kufanya kazi wilayani
humo.

Alieleza changamoto nyengine wanayokabiliana nayo ni uhaba wa vitendea kazi hasa kwenye wodi ya wakina mama wajawazito ikiwemo uchangia mdogo wa wananchi katika mfuko wa afya ya Jamii (CHF).

HENRY JOSEPH AITWA TAIFA STARS

September 02, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
 Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars ambayo iko chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, na leo jioni itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho (Septemba 3 mwaka huu) itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Karume.

Wakati huo huo, kesho (Septemba 3 mwaka huu) saa 6 kamili mchana Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari.

LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI CL

September 02, 2013
NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Coton Sport ya Cameroon na Esperance ya Tunisia.

Mechi hiyo ya kundi B itachezwa Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Omnisport Roumdeadjia mjini Garoua, Cameroon. Kamishna atakuwa Bema Doumbia wa Ivory Coast.

Waamuzi wanatoka Madagascar wakiongozwa na Hamada Nampiandraza. Wasaidizi wake ni Jean Eric Pierre Andrivoavonjy, Ferdinand Velomanana Linoro na Bruno Marie Andrimiharisia.