SDL KUANZA OKTOBA 17

July 05, 2015

Kwa kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya Ligi Daraja la Pili (SDL) yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hivi karibuni, SDL kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Timu itakayoongoza kundi itacheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2016/2017 wakati ya mwisho katika kila kundi itarudi kucheza Ligi ya Mkoa wake kwa msimu wa 2016/2017.

Makundi ya SDL ni kama ifuatavyo; Kundi A ni Abajalo FC (Tabora), Singida United (Singida), Mvuvuma FC (Kigoma), Milambo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam) na Transit Camp (Dar es Salaam).

Timu zinazounda kundi B ni Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma (Mara), Pamba FC (Mwanza), AFC Arusha, Madini FC (Arusha) na Alliance Schools (Mwanza).

Kundi C ni Kariakoo (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).

Nazo African Wanderers (Iringa), Mkamba Rangers (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma), Wenda FC (Mbeya), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya) na Sabasaba United (Morogoro) zitakuwa kundi D.

Klabu nyingi bado hazijatuma jina la uwanja wa nyumbani, hivyo zinakumbushwa kufanya hivyo haraka ili kurahisisha upangaji wa ratiba.

Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016 inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



Best Regards,
 
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  
 

WATANZANIA WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA LA ACCESS BENKI LILILOPO SABASABA ILI WAJIPATIE MKOPO WA CHAP CHAP

July 05, 2015
Wafanyakazi wa Access Benki, Frida Moshi akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Access Benki, Catherine Gyumi akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Bi. Gyumi alisema kwa sasa benki yao imeanzisha huduma ya 'ACCESSBANK WAKALA' wanaomrahisishia mteja kutoa na kuweka pesa akiwa mtaani kwake hakuna haja ya kwenda benki. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON  BLOG.
Afisa Mikopo wa Access Benki, Mwajabu Mhone akielezea machache wakati akihojiwa na Channel 10 kuelezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ambapo Mhone aliwaomba watanzania kufika bandani kwao ili kujipatia mikopo ya chap chap inayotolewa kwa wajasiliamali wadogo na wakubwa.
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiwaomba watanzania wateja wa benki hiyo kuitumia kikamilifu huduma ya 'RAHISI' inayomsaidia mteja kuweza kutoa na kuweka pesa popote alipo kupitia simu yake ya mkononi... piga *150*43# wakati akihojiwa na Channel 10  ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Sijaona Simon.
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiwaomba watanzania wateja wa benki hiyo kuitumia kikamilifu huduma ya 'RAHISI' inayomsaidia mteja kuweza kutoa na kuweka pesa popote alipo kupitia simu yake ya mkononi... piga *150*43# wakati akihojiwa na Channel 10  ndani ya banda lao namba nne lililoko katika banda lao lililopo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Access Benki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelewa na Kamera ya Kajunason Blog.
Wafanyakazi wa Access Benki wakisuburi kuhudumia wateja.
Kila mmoja akiweka mambo sawa....
Afisa Masoko Msaidizi wa Access Benki, Humphrey Masudi akiulizwa swali na mmoja ya wateja aliyetembea bandani kwao.

UTT-PID YASHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA NDANI YA BANDA LA WIZARA YA FEDHA

July 05, 2015
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akiwasikiliza wateja waliotembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kushoto) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) wakiwa na nyuso za furaha na Bi. Beatrice Ngoda katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
 Afisa Masoko Bi. Mary Minja (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akimsikiliza mteja aliyetembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la Wizara ya Fedha.
Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) ipo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yananoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Banda la UTT PID lipo jirani na kuingia katika Banda la Wizara ya Fedha upande wa kulia… karibuni sana wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi mjipatie huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za uuzwaji wa viwanja katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo vile vya mradi wa katika Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT–PID) miji ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani.
Akielezea Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
Aidha Bi. Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi hiyo hapa nchini.
Kwa sasa UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma za ushauri katika maeneo ya upembuaji yakinifu wa miradi mbali mbali, uratibu wa fedha na huduma zinazohusian katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi y a zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''