Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli Atoa Mkono wa Krismas na Mwaka Mpya kwa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar.

December 23, 2015

Mlukulu wa Ikulu Zanzibar Ndg Ameir Ali Khatib akimkabidhi Mbuzi Sister Mary Gemma wa kituo cha Wazee Welezo, hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya Wazee hao Welezo Zanzibar, Vyakula hivyo vimetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wazee hao kujumuiika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. 
Mlukulu wa Ikulu Zanzibar Ndg Ameir Ali Khatib akimkabidhi Mafuta ya Kupikia Sister Mary Gemma wa kituo cha Wazee Welezo, hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya Wazee hao Welezo Zanzibar, Vyakula hivyo vimetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wazee hao kujumuiika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Ndg. Msham Abdalla akiozungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidha vyakula hivyo vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 
Wazee wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa Wazee hao. kuweza kushiriki kwa vizuri katika sikukuu hizo.
Viongozi wa Kijiji cha Wazee wa Wasiojiweza Welezo Zanzibar wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa JamiiVijana Wanawake na Watoto Ndg Msham Abdalla wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa Wazee wa Welezo Zanzibar.
Msimamizi wa Kijiji hicho cha Wazee Welezo Zanzibar Sister Mary Gemma akitowa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada huo umefika wakati muafa na kutowa shukrani zake kwa Nioba ya Uongozi wa Kituo hicho kinachohudumia Wazee wasiojiweza Zanzibar.
Mzee wa Kijiji cha Wazee Wasiojiweza Welezo Zanzibar Mzee Shein Kombo akitowa shukrani kwa niaba ya Wazee wa Kijiji hicho kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa msaada wake kwa Kuwakumbuka na kumtakia kazi njema katika uongozi wake na kumalizia.
Hapa Kazi Tu.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot 

Zanzinews.com

AKINA MAMA NA VIJANA NI NGUZO KUBWA YA KULETA MABADILIKO KATIKA VIJIJI.

December 23, 2015

 Bwana Bony Lukas akieleza jinsi anavyofanya uraghbishi hasa katika kuwasaidia vijana kujua haki zao na kujitambua.

Na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
Ni suala ambalo lipo wazi kuhusu tofauti za kimaisha baina ya wakazi wa mijini na vijijini, ila changamoto nyingi zaidi zinaonekana kuwakabili zaidi wale wanaoishi vijijini. Huko wananchi wanakosa huduma ambazo kimsingi ni haki zao na hivyo kutokuwa na usawa baina yao na wale wa mijini.
Picha kubwa inayojionesha vijijini kwa upande wa wanawake ni hasi kwa kiasi Fulani ukilinganisha na ile ya wanaume. Usawa wa kijinsia na kielimu baina yao na wanaume ni mkubwa sana, kesi za unyanyasaji kwao ni nyingi zaidi.  Pamoja na jihudi nyingi za kuwawezesha wanawake bado hawajapata nafasi ya kutoshwa kuweza kusikilizwa. Wanaume wameendelea kuwa watoa maamuzi na wanufaikaji wa kimfumo. 
 Mmoja wa waraghbishi akiwa anaonesha ripoti ya wanafunzi watoro katika shule ya msingi ya Nyandekwa .
Takwimu zinaonesha kuwa hata idadi ya ufauru kwa wasichana kwa Shule za msingi imeongezeka ambapo mwaka 2013 wasichana waliofaulu ni  281,460 sawa na asilimia 50.20 ya wanafunzi 560,706 wakati wavulana waliofaulu  ni 279,246 sawa na asilimia 49.80. Kabla ya ya matokeo wasichana waliofanya mtihani walikuwa 456,082 sawa na asilimia 52.68 na wavulana 409,745 sawa na asilimia 47.32. Mwaka 2014 jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi Tanzania wasajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83. Jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 walifanya mtihani, wasichana waliofauru ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana 224,909 sawa na asilimia 46.41. 
 Mraghishi Mariam Stephano (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao.
Katika nchi yetu ya Tanzania kuna makabila zaidi ya 100 na kila moja likiwa na mila na tamaduni zake. Ni vizuri ikaeleweka kwamba wazee wetu hawakuwa wakichangamana kimakabila hivyo ni watu wachache walikuwa wanahama toka sehemu moja kwenda nyingine. Aina hii ya maisha ilipelekea wengi wao kuoana wa kabila moja, tofauti ikiwa ni vijiji ama kata, ila wengi ilikuwa toka mkoa ama wilaya moja. 

Tofauti na sasa  ambapo watu wanachanganyikana kutokana na shughuli za kiuchumi na kijamii. Hali hii ya kuchanganyikana baina ya makabila ndani ya mkoa ama wilaya ama kijiji kimoja imeleta tamaduni tofauti na zile ambazo zilikuwa zimezoeleka kiuchumi na kijamii.

Pamoja na mchanganyiko huo bado kumekuwa na changamoto nyingi sana zinazowakabili wakazi wa vijijini. Bado wanaishi kwenye lindi la umaskini na ukosefu mkubwa wa huduma za kijamii. Changamoto hizi zinasababisha baadhi yao kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanadai na kusimamia haki za msingi za kijamii; hawa wanaitwa waraghbishi.

Waraghbishi ni mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu ambao wamevutika kufanya uraghbishi aidha kwa kufundishwa ama kwa kuona matokeo ya matendo wanayofanywa na wanajamii wenzao. Hususani wale ambao wanachukua hatua katika kustawisha au kulinda haki za binadamu na kuwakumbusha wenzao majukumu yao kwa maslahi ya kijamii, kiuchumi ama kisiasa.
 Matilda Peter(wa pili kushoto) aliyeanza Uraghbishi 2015 akieleza namna anavyofanya Uraghbishi kwa kuwapa elimu wasichana juu ya kujitambua, na kuepuka mimba za utotoni
Moja ya haki hizo ni zile za wanawake ambao kwa muda mrefu wameonekana kuwa nyuma zaidi. Hali hii imewaondelea kujiamini na kujiona wao ni wa daraja la pili na hivyo kutokuwa na sauti katika jamii zao.
Mmoja wa waraghbishi hao ni Bw. Bony Lukas toka kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga. Mraghbishi huyu ameweza kuelimisha watu wa kijiji chake. 

Akielezea jinsi anavyoraghbisha vijana katika kijiji chao, Lukasi anasema:
“Vijana ndio wenye nguvu za kuweza kuleta maendeleo na ndio wenye mchango mkubwa ndani ya jamii zetu. Kwa hiyo ni lazima wawe ni watu wenye kujitambua katika nyanja zote. Ili waweze kupata nafasi mbalimbali za kuweza kutoa mchango wa mawazo ili yaweze kufanyiwa kazi”
Hali inatokana na ukweli kwamba vijana wamekuwa nyuma kwa muda mrefu bila. Uraghbishi kwao ni mrejesho wa nafasi finyu ambazo vijana wa vijijini wamekuwa hawapewi nafasi ya kuweza kuchangia pindi wawapo  katika mikutano ya kimaendeleo ndani ya vijiji. Hii ilitoa nafasi ya mraghbishi kupokea  mawazo kutoka kwa vijana wa kike na wakiume kwani vijiji  vilivyo vingi hupuuza mchango wa mawazo ya mtoto wa kike na kumuona hana thamani. 

Kwa mantiki hiyo mraghbishi Lukasi aliweza kuwatia ujasiri kwa kutoogopa kwani watakavyo kuwa na roho ya uoga ndio itakayo wafanya wabaki nyuma kimaendeleo. Kuna msemo unasema “woga wako ndio umaskini wako”. Hivyo alihakikisha anawawezesha vijana kujiamini na kushirikiana vyema na uongozi  wa kijiji.  

Elimu ya jinsia pia ni tatizo katika vijiji vingi vya hapa Tanzania ambapo mraghbishi Miriam Stephano yeye aliweza kutumia nafasi hiyo kwa kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu elimu ya jinsia. Akilielezea hilo anasema:
“Hapa kijijini kuna vijana wa rika tofauti tofauti. Wapo wale ambao ndio wanabalehe na wale waliovuka hiyo ngazi ya kubalehe. Mabadiliko hayo ya kimaumbile hupelekea vijana wengi kuanza kuwa na muelekeo usio sahihi. Sababu ikiwa ni mihemko inayo wakumba  pindi wawapo katika shughuli za kila siku hasa kwa wale wanao soma.” 
Mraghbishi Bujika Adam Joseph  kutoka kijiji cha Guduba akitoa mchango wake wa namna alivyofanya uraghbishi kwa kuwahimiza vijana kuhudhuria mikutano ya vijiji ili nao wapate kushiriki katika kutoa mawazo na michango yao mbalimbali ya mawazo.
Vijana hawa katika kijiji hicho wanapata changamoto mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya kimaumbile. Hili linapeklekea kupata mimba za utotoni pamoja na maambukizi ya virusi vha Ukimwi. Hivyo kupitia waraghbishi vijana hawa wamekuwa wakipewa elimu ili waweze kujikinga na kujiepusha na hari zinakokuwa zikiendelea kuleta mabadiliko katika miili yao.
Changamoto hii ndio iliyomplekea mraghbishi huyu mwanamke toka kijiji cha Nyendekwa, wilayani Kahama Bi. Mariam Stephano kuraghbisha  kundi hili, kama anavyofafanua yeye mwenyewe:  
“Nikiwa kama mwanakijiji mraghbishi huwa ninapita katika mashule mbalimbali. Huko naomba ruhusa kwa mwalimu mkuu na kuweza kuzungumza na wanafunzi wa kike jinsi gani wanaweza kushughulika na mabadiliko ya miili yao. Nawaelekeza nini wafanye pindi wanapofikia umri wa kubalehe. Hapo ntawafundisha usafi wa mwili na namna ya kukwepa vishawishi vitakvyowapelekea aidha kupata maambukizi ya virusi vya Ukumwi ama mimba za utotoni”

Elimu hii ya jinsia inawasaidia watoto katika kijiji cha Nyandekwa, kwani wengi wao huanza kujitambua na kuwa na akili ya kutafakari yale yaliyo mema na mabaya. Na pia inawasaidia hata upande wa serikali katika dhana ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na magonjwa ya zinaa. 
Bi Anna  Zengu aliyepata uwenyekiti wa Kitongoji cha Busolwa kutokana na Uraghbishi akielezea kwa kina jinsi alivyo wasaidia akina mama wenzake kujitambua na kujua umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi bora wanaofaa kuongoza Taifa.
Kwa upande wa mraghbishi Wilbert Michael kutoka kijiji cha Kakebe wilayani Kahama yeye alifanya utafiti usio rasmi juu ya tabia za uongozi wa kijiji chao. Hapo aliweza kugundua mambo kadhaa yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wa kijiji hicho pasipo kuwashirikisha na wananchi. Na walifanya hivyo kwa maslahi binafsi.
Akielezea hali hiyo, Michael anasema:
“Kupitia uraghbishi nilionao niliweza kufuatilia mambo mbalimbali katika ofisi ya kijiji pamoja na ile ya kata. Lengo ikiwa ni kubaini tatizo lililokuwa linakabili kijiji. Kubwa likiwa ni viongozi kujali maslahi binafsi, hapakuwa na uwazi kwenye mikataba ya kimaendeleo ya kijiji,”
Swali la kujiuliza yeye mraghbishi alijuaje habari hizo, akijibu swali hilo ansema:
“Nililigundua kupitia mbao za matangazo ambapo walibandika tangazo la kuingia kwa mkataba na watu wanao sambaza vyandarua  vijijini na wao kuchukua kama ni mradi wa kujipatia kipato. Kupitia mradi vijana walitakiwa kugawa vyandarua hivyo, na hivyo ilikuwa ndio iwe ajira yao.”
Badala yake Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa kijiji wao wakawa wanawachangisha vijana fedha kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kwa kila mmoja.  Lengo lao likiwa ni kuwasajili kwa kuwa wasambazaji wa vyandarua hivyo kinyume cha dhana nzima ya kuleta maendeleo kijini. 

Na ndipo mraghbishi Michaeli  alitumia uraghbishi wake kwa kuweza kuwataarifu wananchi na ndipo wananchi walipoamua kumwajibisha mwenyekiti huyo. Walichoamua ni kupeleka malalamiko katika ngazi mbalimbali za kata na wilaya ili waweze kumvua madaraka yake na kupendekeza jina la mweenyekiti mpya wanayemtaka na atakayeshirikiana na wanakijiji.
Hii ni dhahiri kwamba bado wananchi wanaoishi vijijini wanahitaji elimu ya kiraia itakayowawezesha kuwasilisha matatizo yao kwenye ngazi husika. Ili nao waweze kuwasaidia wenzao wanapogundua yale yanayofanywa na viongozi wao hayaendani na dhana ya ukweli na uwazi.  Na piakuwa na ujasiri wa kuweza kuongea sehemu mbalimbali. 
Baadhi ya wakazi wa kata ya Nyandekwa wakiwa wanajadiliana jambo

Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com

Raia Waamirifu wilayani Kahama Wakerwa na Utoro.

December 23, 2015

 
Pichani nikiwa nazungumza na   Raia waamilifu kutoka kijiji cha Kilago  wilayani Kahama ambapo nilipata nafasi ya kujua mambo  mbalimbali ikwemo mchango wa uraghabishi  katika kijiji hicho katika sekta ya elimu 

Na Krantz Mwantepele , Kahama
Utoro ni tabia ya kuondoka au kutokufika mahali mara kwa mara bila ya kutoa taarifa. Tabia hii ipo kwenye maeneo ya makazini pamoja na shuleni. Katika baadhi ya kata za wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Tabia hii imekuwa kero kwa wanajamii wa kata za Nyandekwa na Kilago kwa kuwa inawarudisha nyuma kimaendeleo. Wakiwa kama sehemu ya wananchi wa kata hizo, waraghbishi wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watoto watoro wanahudhuria shuleni.

Ikiwa kama sehemu ya uraghbishi, kutambua changamoto zinazokabili jamii wanayoishi, waraghbishi walitambua kwamba hili ni tatizo na hivyo kuamua kulishughulikia.

“Nikiwa njiani kuelekea kwenye shughuli zangu, nikakuta watoto wamejibanza kwenye kichaka, na wengine walikuwa wakicheza mpira. Nikataka kujua kulikoni mbona hawapo shuleni, wakati ni muda wa masomo?”

Hili ni swali ambalo raia mwamilifu na mraghbishi Paul Izengo toka katika kijiji cha Nyandekwa kilichopo wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, alitaka kulipatia majibu yake. Udadisi huu ndio uliopelekea kwa yeye kuwasogelea watoto ambao kimsingi walitakiwa kuwa shuleni mda huo na kutaka kujua kulikoni.
Na jibu lilikuwa ni moja tu kwamba wametoroka shule na kwanini watoroke. Paul hakuishia tu kujiuliza maswali, alikwenda hatua moja mbele kwa kuwafuata watoto wale na kuwauliza,
“Nyinyi mnafanya nini hapa? Wakati huu ni muda wa kuwa darasani. Haya shuleni haraka, niliwakaripia, hao wakakimbia.”
Kukimbia wakati umeulizwa ni dalili ya kuogopa kutokana na kosa unalojua umefanya. Watoto wale walijua kwamba wamekosa, na kosa lilikuwa ni utoro shuleni. Hili si tatizo tu la kijiji cha Nyandekwa, hata Kilago pia ambapo baadhi ya wazazi wanatajwa kuwa chanzo cha tatizo hilo la utoro.
Akiwa kama raia mwamilifu na mraghbishi toka katika kijiji cha Kilago, wilayani Kahama Mathew Charles anasema:
“Wazazi ndio sababu ya utoro huu mashuleni, wanawapa watoto wao kazi muda ambao ni wa kwenda shule. HIvyo unapomwambia ukweli anachukia anaona kama vile unamwingilia maisha yake,”
Tabia hiyo ya baadhi wa wazazi kuunga mkono utoro wa watoto wao kwa visingizio vya kutaka kuwa huru na maisha, haviwatakatishi tamaa waraghbishi hao. Kwani hili ni jukumu lao katika kuhakikisha watoto wanapata haki zao.
Katika kusadia watoto hao wanarudi shuleni, waraghbishi kupitia mtandao wao wa wilaya ya Kahama, wamekuwa wakitoa elimu na kuwakishirikisha baadhi ya wazazi wa watoto hao kutambua umuhimu wa elimu na inapobidi kukamata watoto watoro na kuwapelekashule. Na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafuata na kuomba ushauri wanapoona mtoto ameanza kuwa na tabia ya utoro. Na mara nyingi wamekuwa wakiwashauri wazazi hawa kushirikiana na walimu ili kuweza kufuatilia maendeleo ya watoto wao. Akifafanua hilo Michael Mathew anasema:

“Kwa mfano katika kipindi cha mwezi wa 10 wazazi wawili wamekuja kuniomba niongee na watoto wao umuhimu wa kwenda shule. Na nafarijika kuona harakati zangu za uraghbishi zinatambuliwa kwenye kijiji change.




Raia Waamilifu, Mathew Charles (kushoto) wa kijiji cha Kilago na Alphonce Peter toka kijiji cha Ufala wilayani Kahama wakifurahia jambo walipkuwa wakijadili tatizo la utoro mashuleni

Tukiacha hili za wazazi kutowapeleka watoto wao shule kwa sababu mbalimbali, ambapo serikali imekuwa ikiwachulia hatua kali za kisheria wazazi hao, watoto wenyewe nao ni chanzo cha kingine cha utoro mashuleni. Wengine wanaaga wamekwenda shule lakini ukweli ni kwamba hawafiki shule na badala yake wanajificha wanapokujua hadi muda wa kurudi unapofika nao hurejea majumbani kana kwamba wanatoka shule.
Hivyo ni wajibu wa raia mwamilifu na aliye mraghbishi anapaswa kuhakikisha watoto wanapata haki yao hii ya msingi ya elimu. Na hivyo ikibidi hata kutumia nguvu, kama anavyosimulia Mathew Charles:
“Muda mwingine nawabeba kwa nguvu watoto hadi shuleni na kuwakabidhi kwa mwalimu. Nimeshafanya hivyo kwa watoto watano sasa. Tunajua kwamba wasiposoma sasa watakuwa mizigo kwenye jamii. Kuna siku watatukumbuka kwamba tulikuwa tunawasaidia,”
Ni dhahiri kwamba tatizo hili ni kubwa na si jukumu la walimu peke yao?
Nikiwa katika picha ya pamoja na waragahbishi na raia waamilifu wa kijiji cha Kilago wilayani Kahama siku za hivi karibuni 

Kila mwananchi pale alipo ana jukumu la kuhahakisha huduma bora za jamii zinapatikana kwa mustakabali wa maendeleo yao. Katika kufanikisha hili raia waamirifu ama waraghbishi toka katika vijiji vya kata ya Nyandekwa na Kilago wameonesha njia katika kuhakikisha wanafunzi watoro wanahudhuria shuleni.



Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini
                                                              
Akielezea jinsi alivyoamua kushughulikia tatizo hilo kijijini pao, Paul ambaye pia ni kiongozi wa waraghbishi wapya kutoka kijiji cha Nyandekwa anasema:

“Nililazimika kumpigia simu mwalimu mkuu na kuomba kuonana naye kwa lengo la kujadiliana naye kuhusu hili tatizo. Na pale ndipo nilipoweza kuelewa ukubwa wa tatizo la utoro. Hivyo nikakubaliana na mwalimu kuwa tutasaidiana katika kuhakikisha kwamba watoto watoro wanahudhuria shuleni.”
Kwa mujibu wa orodha aliyokabidhiwa mraghbishi Paul Izengo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandekwa, kuna wanafunzi 21 ambao wameripotiwa utoro kati ya 449 wa shule hiyo.
Kitendo hiki cha mraghbishi kuamua pasipo kulazimishwa na mtu kufuatilia suala la utoro wa wanafunzi katika shule yao ya msingi pale kijijini, ndicho ambacho raia mwamilifu anatakiwa kukifanya.
Raia mwamilifu ni yule ambaye anachukua hatua kwa kushirikiana na wanajamii wengine wa maeneo yake. Huyu ni yule anayetambua majukumu na haki zake kwa mujibu wa ibara ya 12 hadi 24 ya Katiba ya Muungano wa Tanzania. Huyu ni raia anayependa kuona mabadiliko chanya kwenye jamii yake. Huyu ni yule anayetenda pasipo kulazimishwa, bali kwa utashi na uelewa wake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. 
Katika kuhakikisha anaelewa vizuri chanzo cha tatizo hilo, ilimlazimu Paul kwenda kumtembelea mzazi ambaye mtoto wake yumo kwenye orodha wa watoro. Na huko alitaka kujua, nini hasa kinachosababisha tatizo hilo.
“Nilikwenda kwa mama mzazi wa mmoja wa wale watoto walioripotiwa kuwa watoro. Lengo langu nilitaka kujua nini hasa tatizo mpaka mtoto haendi shuleni. Ndipo nilipogundua kuna changamoto kubwa zaidi. Inahitajika elimu ya ziada kutolewa,” 
Mama mzazi huyo, alimweleza mraghbishi huyo kwamba michango kwa ajili ya kulipia mitihani ya watoto wake waliopo darasa la 4 na la 6 ni changamoto kubwa inayomkabili. Kushindwa huko kuwalipia watoto wake gharama hizo kumepelekea kwa watoto hao kurudihswa nyumbani.
Sababu nyingine anayoitaja mama huyo ni upungufu wa chakula hasa watoto wanapokwenda asubuhi na kurudi shule mchana. Hali hii inasababisha watoto wasiende shule na kujikita katika shughuli za kuzalisha kwa ajili ya familia.
Pamoja na changamoto hizo, bado raia huyu mwamilifu alimshauri mama huyo kwenda kuonana na mwalimu mkuu ili aangalie ni kwa jinsi gani anaweza kusaidiwa ili watoto wake wahudhurie shuleni.
Ushauri huu unatokana na ukweli kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo Ramadhani Masatu naye pia ni raia mwamilifu kwa nafasi yake. Uwamilifu huo unaelezewa na mraghbishi Elizabeth Ngayalina, toka kijiji cha Nyandekwa:
“Mwalimu mkuu ni muelewa na ndio maana amekubali kushirikiana nasi. Ametupatia kwanza idadi ya wanafunzi ambao ni watoro kwa kuwa anajua ni jukumu letu sote si la kwake na walimu wenzake”  
Nikiwa katika picha ya  pamoja na Waraghbishi na Raia Waamilifu toka katika kijiji cha Nyandekwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao hapo kijijini

Kwa hakika raia hawa waamilifu toka katika vijiji vya Nyandekwa na Kilago wanahitaji kuungwa mkono na wadau wote wa maendeleo. Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto na ndio maana sera ya serikali ni kutoa bure elimu ya msingi na ile ya sekondari. Njia pekee ya kumkomboa mtoto ni kumpatia elimu ambayo ndio dira ya maendeleo ya kila nchi, kuwa na wasomi wengi kadri iwezekanavyo. 

                  CHANZO; MWANAHARAKATI MZALENDO 

RAIS MAGUFULI AONANA NA MJUMBE MAALUMU WA RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA NA MABALOZI WA USWISI NA KUWAIT

December 23, 2015

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Al Najem baada ya kuwa na mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mjumbe Maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Louise Mushikwabo Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Mjumbe Maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Louise Mushikwabo Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Mjumbe Maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Louise Mushikwabo Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015. Nyuma yao ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Florence Tinguely baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Disemba 23, 2015.PICHA NA IKULU.

UDHAIFU WA USIMAMIZI WA MIRADI MBALIMBALI NI CHANGAMOTO KATIKA KULETA KASI YA MAENDELEO NDANI YA JAMII .

December 23, 2015


Waraghbishi toka kijiji cha Pandagichiza wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya tanki la maji, ambalo baadhi yao ndio wasimamizi wake kutokana uaminifu wao.
Tanzania ya leo, imepitia mabadiliko mengi yanayogusa kila sekta tangu ilipojikomboa na kuwa nchi huru baada miaka 53 ya utawala wa kikoloni. Kwa mfano, katika kipindi hicho hadi sasa, nchi imeshuhudia kuimarika kwa huduma mbalimbali za kijamii. Kwa uchache, huduma hizi ni pamoja na  afya, elimu, demokrasia, utalii, viwanda na miundombinu mbalimbali.  Katika sekta ya elimu, ongezeko kubwa la shule kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu limeshuhudiwa. Hii ni moja ya hatua kubwa kuwahi kufikiwa tangu nchi ilipoanza kujitawala. Katika sekta ya afya, hospitali, zahanati na vituo vya afya vimejengwa kwa wingi kutegeme mahitaji ya watu.

Miundombinu ya barabara imeimarika maradufu na kuifanya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kuwa na barabara zenye lami kwa kilomita nyingi. Lakini pamoja na mafanikio hayo, nchi imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali katika kila hatua ya kujaribu kuboresha huduma na mahitaji ya kijamii. Miongoni mwa changamoto hizo ni usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na ubora wa huduma zinazotolewa. Viwango vya ubora kwa huduma zinazotolewa, vimekuwa vikipungua kadri siku zinavyokwenda na sababu kubwa ni udhaifu wa usimamizi kutoka kwa mamlaka husika.

Udhaifu huu umesababisha wananchi ambao kimsingi ndiyo walipa kodi za serikali kulalamika kila siku. Ikumbukwe kuwa ukusanyaji mzuri wa kodi na kuweka matumizi wazi husaidia kuboresha huduma mbalimbali ndani ya jamii. Ili kuepukana na utawala mbovu usiojali wala kuheshimu misingi ya utawala bora, kuna haja ya wananchi kufanya kazi pamoja. Hapa ndipo tunapouona mpango wa Chukua Hatua kama mkombozi kupita uraghbishi, yaani kuwahuisha na kuwahamasisha watu walionyimwa haki kujiona kama watendaji wakuu na siyo kama watu wa chini mbele ya matabaka mengine.
 Mkurugenzi wa Shirika la CABUIPA Bw. David Rwegoshora akitoa ufafanuzi wa kina namna shirika lao linavyofanya kazi.
Ni sahihi, kuona wananchi wakisimama imara, kujithamini na kujenga uelewa wa misingi ya uchambuzi wa hali ya maisha yao. Lakini pia, kuwawezesha watu kuwa na utamaduni wa kuthubutu kujaribu mambo mbalimbali ya maendeleo. Watu hao tunawaita waraghbishi.Waraghbishi hawa wameanza uraghbishi tangu mwaka 2010 pale mpango wa Chukua Hatua ulipoanza katika wilaya za Bukombe, Kahama, Shinyanga Vijijini, Maswa, Kishapu na Bariadi.  Ziliongezeka wilaya mbili, Itilima na Mbogwe baada ya baadhi ya wilaya za Mkoa wa Shinyanga kuhamishiwa mikoa mipya ya Geita na Simiyu na wilaya ya Ngorongoro kwa mkoa wa Arusha.  Uraghbishi ulianza kwa kikundi cha watu wasiozidi 15 kupitia Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) katika mkutano wa kimkakati uliofanyika katika Chuo cha Ushirika tawi la Shinyanga, mwezi Septemba mwaka 2010. Miongoni mwao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa mtandao kwa Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Titus Ndugulile kutoka kijiji cha Mwamala.

“Ni vigumu kuamini kama mpango huu umekuwa mkubwa kiasi hiki. Tulianza watu 12 tu miaka mitano iliyopita, lakini leo tupo waraghbishi zaidi ya 400. Kwa hakika haya ni mafuriko ya waraghbishi, kwani sasa kila sehemu wanapatikana,” alisema Ndugulile.Baada ya kikao hicho, yalifuata mafunzo maalumu ya uraghbishi kwa siku tatu yakiendeshwa kila wilaya. Mafunzo hayo yalilenga kufundisha namna ya kutafuta na kupata taarifa na kutambua changamoto zinazoikabili jamii na njia za kuzitatua.

“Nilikwenda ofisi zetu za halmashauri kuulizia vyanzo vya mapato vya wilaya na kuelezwa kuwa Mgodi wa Mwadui hauchangii chochote pamoja na kuwa upo katika eneo hilo. Taarifa hii niliwashirikisha na wenzangu pia.”Hayo ni maneno ya mraghbishi Fredina Said kutoka kijiji cha Negezi, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Pamoja na kwamba hakuweza kulifikisha mbali suala hilo, angalau aliweza kufahamu kilichokuwa kikiendelea Pamoja na mambo hayo, walifundishwa pia namna ya kujiamini kupitia mafunzo ya uraghbishi waliyokuwa wakiyapata kwa mara ya kwanza.

Mafunzo haya yalitolewa kwa nadharia na vitendo ambapo waraghbishi baada ya kupatiwa mafunzo ya darasani walipewa kazi ya kutembelea ofisi za halmashauri za wilaya zao.  Lengo ni moja tu, kuwajengea uwezo wa kuongea na viongozi wa kitaifa kama mkuu wa wilaya au mkurugenzi baada ya awali kuonyesha hofu na kutojiamini. “Ilikuwa mara ya kwanza kuonana na mkuu wa wilaya na kumuulizia masuala ya pembejeo za kilimo. Nilikuwa na hofu, hata hivyo kinyume na matarajio yangu, maswali yote aliyajibu ingawa siyo kwa kiwango nilichotarajia,” alisema mraghbishi Fedson Yaida wa Kijiji cha Shenda, wilaya Mbogwe, mkoani Geita Matokeo ya kutembelea ofisi hizo yalionekana pale walipopatiwa majibu ya maswali yao. 

Kazi hii ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuwandaa waraghbishi na majukumu makubwa ya uraghbishi. Waraghbishi hawa walikuwa wakiwakilisha wananchi wa vijiji vyao, hivyo moja ya jukumu lao ilikuwa ni kuwashirikisha walichojifunza.  Jukumu hilo walilifanya vizuri na waliweza kutambuliwa kwa urahisi na viongozi wa vijiji pamoja na wananchi wenzao. Na kwa sababu walipatiwa mafunzo kupitia mradi wa Chukua Hatua, walijikuta wakiitwa kwa jina hilo hilo la Chukua Hatua. Mfano mzuri ni waraghbishi waliopo katika kijiji cha Mwime, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Hali hii ilisababisha wananchi wengi katika vijiji ambavyo mradi wa Chukua Hatua unaendeshwa kujitambulisha kama waraghbishi na kutaka na wao wapatiwe mafunzo. Na hapo ndipo lilipokuja wazo la kuwawezesha waraghbishi wa zamani na wapya kufanya kazi kwa pamojaAkielezea jinsi alivyowafundisha waraghbishi jinsi ya kufanya uraghbishi katika kijiji chake na vile vya jirani, mraghbishi kutoka Kijiji cha Ololosokwani, Kootu Tome, alisema: “Nimefundisha waraghbishi wa kijiji cha jirani. Niliwaeleza maana ya uraghbishi, kwamba hawatakiwi kujionyesha wazi kwa kila jambo, badala yake wanawashawishi watu kuchukua hatua katika kile anachokuwa amewafafanulia,”  
  
Viongozi wa mitandao ya wilaya za Bukombe na Mbogwe mkoani Geita wakiwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika kata ya Masumbwe hivi karibuni 
Mraghbishi mwingine ni Julius Katende kutoka Kijiji cha Ngarwa, wilayani Ngorongongo aliwafundisha waraghbishi wapya tofauti ya uraghbishi na uhamasishaji. Mraghbishi si mwamasishaji, bali ni mtu anayeibua hoja katika jamii na kuzitafutia majibu kwa kushirikiana na wenzake. Jumla ya waraghbishi wapya 762 wamefundishwa na waraghbishi 322 wa zamani, ikiwa ni ongezeko mara mbili katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai hadi Septemba na kufanya idadi yao kuwa 1,084. Kati yao, wanawake ni zaidi ya 400. Hili ni ongozeko kubwa ambalo ni wazi linatokana na juhudi za pamoja. “Tuliwafundisha kutoka katika maeneo mbalimbali ambayo wamekuwa na kawaida ya kukusanyika,” haya ni maneno ya mkurugenzi wa Tamasha, Richard Mabala, wakati akifafanua namna wanavyoendesha mafunzo hayo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Waraghbishi kwa upande mmoja wanawakilisha wananchi wa maeneo yao na wamekuwa mstari wa mbele kusimamia rasilimali zao na kuhakikisha huduma bora za jamii zinapatikana. Lakini ili kufanikisha, malengo ya mpango wa Chukua Hatua, viongozi wa vijiji, hasa wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wanafundishwa uraghbishi pia kulingana na nafasi zao.Jukumu la kuwafundisha viongozi hawa kwa upande wa mikoa ya kanda ya ziwa wamepewa CABUIPA, shirika mdau la mpango wa Chukua Hatua lilipo Kahama. Akifafanua wanachofanya, mkurugenzi wa shirika hilo, David Rwegoshora alisema:

“Katika kipindi cha miezi mitatu tumefundisha wenyeviti 167 na watendaji 33 ngazi ya kata. Kati yao, wanawake walikuwa sita.” Kwa upande wa Ngorongoro, wenyeviti 14, watendaji 14 wa vijiji na 6 wa kata walipatiwa mafunzo hayo. Kundi lingine ni Sungusungu, ambapo hadi sasa idadi yao ni 15 nao walipewa mafunzo hayo ya uraghbishi. Wote hawa ni waraghbishi kwa nafasi zao. Katika awamu iliyopita ilijumuisha na viongozi wa dini wakiwamo masheikh, maimamu, wachungaji na makatekista.

Katika kuhakikisha waraghbishi wanawafikia watu wengi zaidi na kuwafundisha uraghbishi, mitandao ya waraghbishi imeanzishwa katika wilaya za Mbogwe, Kahama, Maswa, Kishapu, Bariadi, Shinyanga Vijijini, Itilima na Bukombe. Mitandao hii ilianza rasmi mwaka 2014 na kuwaleta pamoja waraghbishi wa mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.  Hadi sasa, kuna wenyeviti pamoja na wasaidizi wao, ambao idadi yao imefikia 32, wanawake 16, sawa na asilimia 50. Wingi huu wa waraghbishi hauangalii itikadi za vyama, badala yake unaangalia kilicho bora kwa wanajamii kwa ujumla.
<!--[if gte mso 9]> Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail info@tonemg.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.tonemg.com

TIGO YAZINDUA DUKA JIPYA MUSOMA MJINI

December 23, 2015
    Mkuu   wa  Wilaya ya  Musoma  Mjini ,Mhe.Zelothe Stephen akikaribishwa   na    mwenyeji wake, Meneja  Beatrice Kinabo  kabla  ya uzinduzi wa  tawi  jipya la Tigo  Musoma  mjini. Wengine  pichani   Mkuu  wa   Polisi   Mkoa  wa Mara, Philip Kalangi  na    mwakilisi      wa RAC.

                                 Meneja wa   Mauzo  wa Tigo Mkoa    wa  Mara Edwin Kisamo  akitoa   utambulisho  kwa meza  kuu.

Meneja  wa   Mauzo Tigo  Kanda  ya   Ziwa, Edgar Mapande akiongea na wageni  waalikwa na wanahabari  kabla ya  uzinduzi wa  Duka la Tigo wilayani  Musoma   Mjini 

Mkuu  wa  Wilaya  ya MusomaMjini ,Mhe.Zelothe Stephen akikata  utepe kufungua  rasmi  duka la TigoMusomaMjini , anayeshuhudia  ni Meneja huduma kwa  Wateja wa  Tigo kanda ya  Ziwa Beatrice Kinabo.

   Meneja  wa  Mauzo Tigo  Kandayaziwa, Edgar Mapande  akimkabidhi  simu Mkuu wa  Wilaya  ya  Musoma  Mjini  Mhe.Zelothe Stephen, mara  baada  ya  uzinduzi wa   duka la Tigo Musoma   mjini.

      Mkuu  wa  Wilaya  ya  MusomaMjini , Mhe.Zelothe Stephen akiongea na waandishi wa habari na wadau  mbalimbali  wakati wa  ufunguzi  wa  duka la Tigo   Musomamjini, Wengine   kutoka  kulia Meneja wa Mauzo Tigo mkoa wa Mara, Edwin Kisamo, Meneja huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo  na   Katibu  wa   Mkuu  wa mkoa  Bw. Marwa

        Meneja  wa  Mauzo  Tigo  Kanda ya  ziwa, Edgar Mapande  akimkabidhi  simu   Mkuu  wa Polisi  Mkoa  wa Mara, Philip Kalangi  mara baada ya  uzinduzi wa  duka la Tigo  Musoma mjini.

     Baadhi  ya  wateja  wakiangalia  bidhaa  mbalimbali  mara  baada ya  ufunguzi wa duka la Tigo Musoma Mjini



    Wadau  mbalimbali  waliohudhuria uzinduzi

       Mkuu  wa  Wilaya  ya  Musoma  Mjini ,Mhe.Zelothe Stephen  akiwa  kwenye  picha ya  pamoja  na  wafanyakazi  wa Tigo  na  wadau  mbalimbali.

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"