DC IKUNGI AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

DC IKUNGI AFUNGUA MAFUNZO YA MGAMBO

August 05, 2016
IKU1
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akikagua vijana wa mafunzo ya Mgambo kutoka vijiji vitano vya Dung’unyi, Munkinya, Kipumbuiko, Samaka na Damankiya vinavyounda Kata ya Dung’unyi katika Tarafa ya Ikungi
IKU2
Kikosi cha  vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakionyesha umahiri wao katika mafunzo waliyoyapata mbele ya mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
IKU3
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Ikungi
IKU4
Kundi la vijana wa Mgambo kutoka Kijiji cha Ighombwe, Jerumani, na Mahonda wakimsikiliza mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo katika Tarafa ya Sepuka
IKU5
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya ikungi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturu akijadili jambo na Mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi Fortunatus Ndalama
IKU6
Mkuu wa Wilaya Miraji Jumanne Mtaturua akizungumza na watendaji Kata, na viongozi wa vijiji mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya mgambo yatakayodumu kwa wiki 16
……………………………………………………………………………………………..
Na Mathias Canal, Singida
Wiki 16, Miezi minne itatosha kuwakutanisha pamoja vijana wa kata mbalimbali Wilayani Ikungi kwa pamoja wakipatiwa mafunzo ya Mgambo hususani kujifunza uzalendo, Mbinu za medani za kupambana na uhalifu, Kuimarisha nidhamu na kujituma.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakati akifungua rasmi mafunzo hayo yatakayojikita pia katika kuimarisha utu na uadilifu.
Mtaturu amesema kuwa vijana wote walioamua kujitolea katika mafunzo hayo kwa ridhaa yao watapaswa kuwekwa katika kumbukumbu ya vijana ambao baada ya kumaliza mafunzo wataanzishiwa vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
“Tanzania ina wimbi la vijana wengi ambao wanajiamulia maisha wenyewe kutokana na wazazi wao kuyakimbia majukumu yao ya kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kumjua Mungu na nidhamu kwa kila mtu kwenye jamii hivyo sisi kama serikali ngazi ya Wilaya tutahakikisha Vijana hawa wanaimarika katika maadili mema” Alisema Mtaturu
Dc Mtaturu amesema kuwa mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo vijana hao watapaswa kuamua wanataka kujishughulisha na nini kati ya ufugaji na kilimo cha kisasa ambapo ofisi ya mkuu wa Wilaya itasimamia kuhakikisha wanafanikiwa katika malengo yao.
Sambamba na hayo amewaeleza vijana hao kuwa serikali ina mamlaka ya kuwasaidia watanzania kujikwamua katika wimbi kubwa la umasikini lakini pia vijana na watanzania kwa ujumla wanapaswa kutumia muda wao mwingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali kwa kufanya kazi sio kucheza bao, kujihusisha na vikundi ovu, kunywa pombe, Ngono zembe ama kucheza Pool Table wakati wa kazi.
Dc Mtaturu amewapongeza vijana hao kwa kujitolea kwa moyo mmoja kushiriki katika mafunzo hayo ambapo amesema kuwa mafunzo wanayoyapata sio mateso ila ni sehemu ya kuwaimarisha kimwili na kiakili, Kujifunza maadili mema, ili kuwa na uchungu na nchi yetu.
Mafunzo ya mgambo yaliyofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu yanahusisha Tarafa mbili ya Ikungi na Sepuka ambapo katika Tarafa ya Ikungi vijana wa kiume waliojitokeza ni 138 huku wanawake wakiwa 6.
Kwa upande wa Tarafa ya Sepuka kuna jumla ya vijana 210 ambapo vijana wa kiume ni 206 na wanawake ni wa 4.
Katika ufunguzi wa Mafunzo hayo katika Tarafa hizo mbili Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi aliambatana na Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya.
Dc Mtaturu amesisitiza kuwa mgambo wanajulikana kama jeshi la akiba ambapo wajibu wao Mkubwa ni kushirikiana na jeshi la polisi na Jamii katika kuimarisha ulinzi wa watu na Mali zao.
DIWANI WA CHADEMA ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAADHIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILANI IKUNGI

DIWANI WA CHADEMA ASWEKWA NDANI KWA KUKIUKA MAADHIMIO YA BARAZA LA MADIWANI WILANI IKUNGI

August 05, 2016
index
Kutoka Kushoto ni Eng Sadick Chakka Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga, na Kulia ni Abel Suri Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
…………………………………………………………………………………….
Na Mathias Canal, Singida
Jeshi la polisi Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida limemtia nguvuni Diwani wa Kata ya Iseke kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Emmanuely Njingu kwa kosa la kukwamisha shughuli za serikali kwa kuzuia watendaji wa serikali kufanya kazi yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato.
Njingu ambaye alikuwa mjumbe wa kamati ya fedha awali kabla ya kuwekwa nguvuni na jeshi la polisi alivuliwa ujumbe wa kamati hiyo kutokana na kukiuka taratibu na makubaliano ya baraza la madiwani jambo ambalo limepelekea kuhamishiwa katika kamati nyingine.
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambaye ni Diwani wa Kata ya Irisia Ally Juma Mwanga amesema kuwa Diwani huyo amekamatwa kwa mujibu wa sheria hivyo yeye kama mwenyekiti hawezi kuingilia taratibu, sheria,na kanuni za serikali.
Mwanga amesema kuwa tarehe 19 mwezi Julai moja ya maadhimio ya kamati ya fedha na vikao vya baraza ilikuwa ni kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri lakini diwani huyo amekiuka makubaliano hayo kwa kung’oa mageti ya vizuizi vya barabarani kwa ajili ya ukaguzi wa mazao jambo ambalo limepelekea kuzorota kwa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Ameongeza kuwa Mjumbe yeyote anayekiuka maazimio wanayokubaliana na kutoa siri za kamati adhabu yake kisheriani kupoteza sifa ya kuwa mjumbe wa kamati husika.
Amesema diwani huyo ameondoshwa katika nafasi hiyo baada ya maridhiano ya kamati hiyo na kukubaliana kumuhamishia katika kamati nyingine ya huduma za uchumi.
“Jambo mkishakubaliana kisheria tena kwenye vikao vya kisheria maana yake linakuwa ni sheria hivyo kwa kiongozi yeyote akikiuka taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake, kanuni za Halmashauri ni za watu wote hazichagui upande mmoja” Alisema Mwanga
Hapo jana Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alihutubia Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ikiwa ni mara yake ya mwanzo kabisa tangu alipochaguliwa na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambapo pamoja na kuzungumzia kuwepo kwa changemoto ya uhaba wa maabara, afya duni na miundombinu pia alizungumzia kuhusu ukusanyaji hafifu wa mapato jambo ambalo linairudisha nyuma Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Bajeti ya Wilaya ya Ikungi kwa Mwaka 2013/2014 ilikuwa na Shilingi 509,701,044 namakusanyoyakeyakawa ni 338,325,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kuwa na upungufuwa shilingi 171,376,044.
Mwaka 2014/2015 ilipangwa bajeti ya shilingi 631,455,000 lakini makusanyo yake yakawa ni shilingi 457,555,172 ambapo mwaka ulimalizika kwa kukusanya 173,899,828.
Mwaka wa bajeti 2015/2016 bajeti ya Halmashauri iliyopangwa ilikuwa ni shilingi 1,127,030,000 makusanyo yalikuwa ni 679,283,000 ambapo hata hivyo mwaka ulimalizika kwa kwa kuwa na upungufu wa shilingi 450,747,000 hivyo kwa miaka mitatu Halmashauri hiyo imeshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji.
Mwanga amesema kuwa Kutofikiwa malengo hayo kumesababishwa na kutopewa ushirikiano watendaji katika ukusanyaji wa mapato hii ikiwa ni kufuatia kauli za mazuio zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa.
Hata hivyo ametoa Mwito kwa viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi za dini na wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kufikia malengo ya kuifanya Ikungi kukua kiuchumi .

DAWASCO YAINGIA MITINI ZIARA YA NAIBU WAZIRI MPINA

August 05, 2016
   
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa katika ziara ya kukagua uharibifu wa mazingira.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akisikiliza kero za harufu kali za mabwawa ya maji taka kutoka kwa wana nchi yaliyopo Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira.

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara kukagua miundo mbinu ya Dawasco inayolalamikiwa na wana nchi kwa kutiririsha maji machafu sehemu za makazi, jijini Dare s salaam mapema hii leo.

                                      EVELYN MKOKOI
                                             AFISA HABARI
                              OFISI YA MAKAMU WA RAIS
                                            DAR ES SALAAM
Katika hali isiyo ya kawaida shirika la maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar Es Saaal na Pwani DAWASCO, limeingia mitini katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya kutembelea miondombinu  ya maji taka na maji safi Jinini dar Es Salaam na Pwani Leo.
Licha ya Shirika Hilo kupewa Taarifa ya Ziara ya Naibu waziri Mpina mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa kumuwasilisha mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.
Akiongea kwa ukali baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha maji taka kwenda baharini la Ocean road, Naibu Waziri Mpina amesema ubovu wa bomba la ocean road unatokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha dhahiri kuwa DAWASCO wana Jeuri kwa IKulu, kwa kutokulifanyia ukarabati kwa muda muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo hayo.
Alipotembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni, Mhe Mpina Alisema pamoja na kuwa miondombinu hiyo inaelemewa na wingi wa  wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husina zina wajibu wa kuyafanyia usafi mabwawa hayo lakini, hazijaonekana jitihada zozote za kufanya hivyo, na miondombinu hiyo inaonekana kutofanyiwa ukarabati kwa muda wa miezi sita.
Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa miundombinu hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.
Akiongea kwa Uchungu, Mkazi mmoja wa Mabibo aliyekataa kutaja jina lake alisema kuwa, ninanukuu“Mabwawa haya ni ya Dawasco na hata tukitaka kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao kuelekea kwenye mabwawa wana taka tuwalipe na tunafanya hivyo, wenye viwanda halikadhalika wanawalipa dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu ya dawasco, lakini najiuliza, kwa nini wanakuwa wagumu kuyafanyia ukarabati au hata kusafisha tuu?. Mwisho wa kunukuu.
Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundiombinu ya DAWASCO leo Jijini Dar Es Saalam ilihushisha maafisa kutoka DAWASA na BAraza la taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi yote inayosimamiwa na DAWASCO na kuon akama wanatenda haki katika kutoa huduma kwa wananchi.

VIONGOZI WA DINI WATEMBELEA UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM KUONA MAENDELEO YA UJENZI WA TERMINAL 3

August 05, 2016
 Viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, wakiomba dua kuombea ujenzi wa Uwanja wa  Jengo la Tatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walipofanya ziara ya siku moja kutembelea jengo hilo Dar es Salaam jana. 
Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Mohamed Milanga akitoa maelezo kwa viongozi hao wa dini waliotembelea uwanja huo Dar es Salaam jana.
 Mwonekano wa uwanja huo unaojengwa.
 Mwonekano wa chumba cha wasafiri katika jengo hilo.

Baadhi ya wakandarasi wa ujenzi huo.




 Askofu, Stephen Mang'ano wa Kanisa la Menonite (kushoto), akiongoza maombi ya kuombea ujenzi wa uwanja huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Ramadhan Maleta (wa pili kulia), akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo mbele ya viongozi wa dini wanaounda Kamati ya Amani.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Wolffgang Marschick akizungumza na viongozi hao wa dini.
Viongozi hao wa dini wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kukamilisha ziara yao.

Na Dotto Mwaibale

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) imesema inatarajia kujenga njia ya pili ya kurukia ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) baada ya kubainika uwanja njia ya sasa haitatosha ifikapo mwaka 2025.

Tayari mamlaka hiyo imeshaanza kufanya mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuanza kujenga njia ya pili ya kurukia ndege.

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam jana waliotembelea mradi huo, Kaimu Mkurugenzi wa TAA, Ramadhan Maleta alisema, wataalamu walifanya utafiti na kubaini kuwa kufikia 2025 njia moja inayotumika sasa haitatosha kwa kuwa mahitaji yatakuwa yameongezeka.

Maleta alisema, pia Serikali iko katika mchakato wa kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya maboresho ya jengo la abiria (terminal II), maboresho ambayo yatafanyika kuanzia mwakani.

“Maboresho ya jengo la terminal II yataanza mwakani, kwa sasa Serikali iko katika mchakato wa kutafuta pesa kwa ajili ya kufanya maboresho hayo ili tuweze kutoa huduma bora,” alisema Maleta.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema, mradi huo ni muhimu zaidi kwa kuwa utazidi kuimarisha heshima ya Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.

Pia alisema jengo hilo likikamilika kwa wakati litawasaidia Watanzania na pia litaongeza idadi ya ndege kubwa kutua nchini.

Alisema ujenzi wa jengo hilo ni ishara tosha kuwa Serikali inafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi wake maendeleo, na kwamba kamati hiyo itashirikiana na Serikali si tu katika kuhamasisha masuala ya amani bali hata maendeleo.

Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon alisema, kikubwa kilichowafanya kutembelea mradi huo ni kutaka kuona juhudi za Serikali kuhakikisha Tanzania inakuwa na uwanja mkubwa wa kisasa.

Mbali na ziara hiyo, kamati hiyo pia ilitumia nafasi hiyo kufanya maombi na duoa kwa ajili ya mradi huo ili uweze kukamilika salama bila kutokea kwa tatizo la aina yoyote ambalo linaweza kukwamisha.

Akitoa ufafanuzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Mradi huo, Mohammed Millanga alisema, ujenzi wa jengo hilo litakalohudumia abiria milioni sita kwa mwaka unatarajiwa kukamilika Desemba mwakani.

Alisema hadi sasa mradi huo ambao ulikuwa utekelezwe kwa awamu mbili kwa sasa awamu hizo zinatekelezwa kwa pamoja na umekamilika kwa asilimia 45.

CHAMA CHA WAFANYAKAZI COTWU (T) KANDA YA DAR ES SALAAM CHAFANYA MKUTANO WAKE MKUU HOTELI YA VILA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

August 05, 2016

Kaimu Mkurugenzi, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Shanes Nungu (katikati), akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mussa Mwakalinga na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine.


Wanawake waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanawake wajumbe wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mkutano huo.
Vigogo wa chama hicho wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine, Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Mussa Mwakalinga.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania COTWU (T), Kanda ya Dar es Salaam wakiimba wimbo wa mshikamano katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Wajumbe wakionesha mshikamano wao wakati wakiimba wimbo maalumu wa mshikamano.
Katibu wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, Elisa Luvigo akizungumza katika mkutano huo.
Makatibu wa matawi wa chama hicho wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Tanzania (CMA), Shanes Nungu (wa tatu kushoto).
Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Dar es Salaam, George Faustine (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha mgeni rasmi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA.

August 05, 2016
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya  Kanda ya Ziwa.
Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.

Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika.

Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa mwenyeji.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo kufufua kilimo cha pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo zikiwemo taasisi za serikali na wajasirimali, wamesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kutembelea maonyesho hayo tofauti na maonesho ya miaka iliyopita.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Damian Chang’a, amesema maonesho ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya Halmashauri 18 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyangana na Mara huku mikoa ya Simiyu na Kagera ikishindwa kushiriki.

Itakumbukwa kwamba, alieyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nae aliwahi kutoa ahadi kama aliyoitoa Mongela, katika Maonesho ya Nanenane miaka iliyopita.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (kushoto), akifuatilia jambo kwenye maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia).
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa.
Burudani ya asili kutoka kikundi cha ngoma za asili Bujora
Mchezo wa nyoka kutoka Bujora
Wapiga picha wakifuatilia wacheza ngoma kutoka Bujora
Taasisi ya Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Watoto Majumbani, Foundation Karibu Tanzania pia inatoa elimu kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

TPA YATAKIWA KUJENGA CHEREZO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

August 05, 2016


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kujenga chelezo (gereji ya kukarabati meli na vivuko), katika bandari ya Dar es Salaam ili kuokoa fedha nyingi zinazotumika kwa matengenezo nje ya nchi.

Waziri Prof. Mbarawa amesema hayo wilayani Kyela, wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa meli mbili mpya za mizigo zinazojengwa na Kampuni ya Songoro Marine katika bandari ya Itungi ambayo ni Bandari Kuu katika Ziwa Nyasa na kuelezea kuridhishwa kwake na hatua za ujenzi uliofikiwa.

“Tukijenga chelezo Dar es Salaam tutaokoa fedha nyingi tunazozipeleka nje kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa vivuko na meli zetu", amesema Waziri Prof. Mbarawa. Amesisitiza kuwa kujengwa kwa chelezo katika bandari hiyo kutaongeza ajira kwa wananchi na pato kwa mamlaka kwani vyombo vya Sekta binafsi vitaweza kufanyiwa ukarabati wa vyombo vyao vya majini.

Aidha katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda- Matema KM 34.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami na kumtaka Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kukamilisha kwa viwango na ubora unaotakiwa ili idumu kwa muda mrefu.

"Tunapotoa fedha tumedhamiria kuhakikisha kitu tunachofanya kiendane na thamani ya fedha hiyo hivyo hakikisha unatekeleza kazi hii kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa",amesisitiza Prof.Mbarawa.

Hata hivyo Prof. Mbarawa amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kwa haraka na kufungua uchumi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa amemuomba Waziri Mbarawa kuruhusu wahandisi wazalendo kuendelea kusimamia mradi huo ikiwa ni hatua ya kuwajengea uwezo watanzania kusimamia miradi mikubwa nchini.

Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kukagua miundombinu na kuongea na wafanyakazi waliopo chini ya wizara yake katika mkoa wa Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akielekea katika Bandari ya Itungi kukagua maendeleo ya ujenzi wa meli mbili mpya zinazojengwa katika bandari hiyo wilayani Kyela.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Eng. Salehe Songoro akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa meli mbili mpya mbili kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipotembelea bandari ya Itungi kuona maendeleo ya ujenzi huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Eng. Salehe Songoro wakati alipokagua moja ya mashine ya meli mpya inayojengwa katika bandari ya Itungi, wilayani Kyela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akikagua risiti za malipo na Mhasibu wa Bandari ya Itungi (wa pili kushoto), wilayani Kyela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akioneshwa risiti za mizigo inayosafirishwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) na Captain Thom Faya, wakati alipokagua utendaji wa kampuni hiyo katika Meli ya MV Songea, bandari ya Itungi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa, wakati alipotembelea eneo la mto ilipopita barabara ya kwenda Bandari ya Itungi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa (wa kwanza kulia) wakati alipokagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda- Matema KM 34.6 inayojengwa kwa kiwango cha Lami, Wilayani Kyela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo wa Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Teknolojia Stahiki ya Nguvu Kazi (ATTI- MBEYA) Bw. Mohamed Chamle (wa tatu kulia), mara baada ya kukagua miundombinu ya chuo hiko.

KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO CHA NIDA TEXTILES INDUSTIES CHATOZWA FAINI YA SHILINGI MILIONI THELATHINI, KWA UCHAFU NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

August 05, 2016
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akipata Maelezo kutoka kwa mmoja wa Maafisa wa kiwanda cha Urafiki Ttextile kilichopo jijini Dar es salaam mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho mapema hii leo.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akikagua mto kibangu ambao umechafuliwa na maji yanayotiririshwa na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo tabata jijini dare s salaam.      
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati)akitembezwa ndani ya kiwanda cha Urafiki Textile mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho mapema hii leo

                 EVELYN MKOKI AFISA HABARI
                    OFISI YA MAKAMU WA RAIS
                            DAR ES SALAAM
                                              4/8/2016

Kiwanda cha kutengeneza nguo cha Nida Textile Industries kilichopo Tabata Jijini Dar es Salaam kimetozwa faini ya shilingi milioni Thelathini kwa kosa la uchafuzi w a mazingira kwa kutiririsha maji taka na yenye sumu katika mto kibangu kuhatarisha maisha ya mazingira na viumbe hai  pamoja na kiwanda hicho kuwa na mazingira machafu na hivyo kuatarisha maisha ya wafanyakazi kiwandani hapo.

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku saba kwa Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi waMazingira NEMC imetokana na ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ya kukagua viwanda na mazingira nchini ambapo sambamba na adhabu hiyo kiwanda hicho kimetakiwa kufanya usafi mara moja katika mazingira kiwandani hapo, pamoja kupeleka repoti ya upimaji wa moshi, vumbi litokanalo na makaa ya mawe na maji yanayotoka kiwandani hapo ili serikali kujiridhisha kama si hatarishi kwa mazingira. 

‘’Ili kujiridhisha NEMC waje nao wachukue vipimo vya maji haya yanayotiririka ili tuone kama ni salama kwa mazingira na viumbe hai, na kiwanda kiwasilishe cheti cha utirishaji maji kwa Baraza.” Alisisitiza Naibu Waziri Mpina.

Kwa upande wake Meneja wa kiwanda hicho Bwana Mohamed Rajabu alipoulizwa kama ameikubali adhabu hiyo, alitupia lawama kwa NEMC na kusema kuwa wao ndo walitoa kibali cha athari ya tathimini ya mazingira kwa kiwanda hicho na ndiyo maana kinaendelea kufanya kazi na kuwa wangekuwa wanapita kwanza na kutoa onyo kwa wenye viwanda kabla ya kutoa adhabu kali ya mamilioni ya fedha, na kuongeza kuwa kukabiliana na faini kubwa hivyo kwa kiwanda hicho kunaweza kupelekea wafanyaki kupoteza ajira zao kwa kupunguzwa kazini.

Akiitimisha katika zoezi hilo Naibu waziri Mpina aliwataka wawekezaji na wenye viwanda nchini kutii sheria na kuthamini maisha ya wafanyakazi kwa kuyaweka mazingira safi na salama.