HUONI HAFIFU HUCHANGIA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI DARASANI

October 12, 2017
 Mwalimu wa shule ya Msingi Nguvumali Jijini Tanga akichukua maelezo ya wanafunzi kabla ya kuanza zoezi la upimaji wa huduma ya macho wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,
 Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Tanga,Dkt Frida Kassiane akiwapima macho mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Nguvumali Jijini Tanga wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo siku hiyo iliendana na sambamba na upimaji macho ulioendeshwa na Duka la Miwani la Noor Optics kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji hilo kwa wanafunzi wa shule za msingi za mabokweni,kwanjeka na nguvumali,

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima

 Amina Nasoro ambaye Mratibu wa Huduma ya Afya ya Macho katika kampuni ya kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga akichukua maeleza ya wanafunzi kabla ya kuwapima


 Zoezi la Uandikishaji wa majina wanafunzi wa shule ya Msingi Nguvumali kwa ajili ya upimaji wa macho likiendelea
Zoezi la kuwapima wanafunzi likiendelea
SABABU kubwa za wanafunzi wa shule za msingi  kutokufanya vizuri darasani imeelezwa inatokana  na uoni hafifi kwa baadhi yao na sio kwamba hawana akili .

Lakini pia imebainishwa pia kati ya watu 100 kati ya 15 wana kabi liwa na tatizo la macho ambalo limekuwa likiwaathiri kwa asilimia na kushindwa kufikia malengo yao.

Hayo yalibainishwa juzi na Mratibu wa Huduma za Macho Mkoani Tanga Dkt Frida Kassiane wakati wa siku ya afya ya macho duniani ambapo yalienda sambamba na upimaji wa macho uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya Noor Optics inayojishughulisha na matibabu ya macho na utoaji wa miwani Jijini Tanga.

Alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi kuumwa macho huku wakiwa hawajitambui kutokana na kutokuwepo kwa utaratibu za utoaji wa huduma za upimaji machi kwao hususani mashuleni.

“Ukiangalia leo hii baadhi ya wanafunzi utakuwa walikuwa wakifanya vizuri katika mitihani yao lakini ghafla wanaanza kushuka kiwango na hili unaweza kukuta linasababishwea na tatizo la macho kama lilivyogundulika kwa wanafunzi wachache kwenye shule tulizopita “Alisema.

Alisema suala hilo linasababishwa pia na lishe dunia kwa asilimia kubwa ya watoto wengi ikiwemo kukosa kupata vyakula vilivyokuwa na virutubisho vinavyoweza kuongeza nguvu na kinga ya macho.

Alisema zoezi hilo ambalo limeanza siku nne zilizopita limewafikia zaidi ya wanafunzi 1500 katika shule za Msingi,Kwanjeka,Mabokweni na Nguvumali ambapo baadhi yao walibainika kuna matatizo hayo na kusaidia matitabu zaidi na kampuni hiyo.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Noor Optics, Raouf Nasser alisema lengo kubwa ni kutoa huduma hiyo katika shule zote za msingi ili kusaidia kubaini changamoto za macho zinazowakabili na namna ya kupatiwa ufumbuzi.

Alisema alisema kampuni hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Tanga wameamua kuendesha zoezi hilo kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto ambao watabainika wanakabiliwa na matatizo hayo ili waweze kufikishwa kwa wataalamu kwa matibabu zaidi.

“Asilimia kubwa ya wazazi hawana uwezo wa kuwapeleka watoto wao katika hospitali kufanyiwa vipimo vya matatizo hayo hivyo sisi tumeamua kwa nia moja kusaidia jamii ikiwa ni kurudisha faida kwao kutokana na huduma tunazotoa “Alisema.

Aidha alisema msingi mzuri wa kuyatunza macho ni lazima kuwepo utaratibu wa kuyafanyia vipimo mara kwa mara hasa wanapokuwa kwenye hatua ya ukuaji kabla ya kufikia umri mkubwa ambapo tatizo hilo linaweza kuwa kubwa zaidi.

Nivo afunguka ya moyoni kuhusu wasanii wachanga

October 12, 2017
Msanii chipukizi kwenye muziki wa Bongo fleva, Vicent Petro ambaye kwa jina la sanaa anatambulika kama ‘Nivo’ aliyewahi kuachia ngoma yake moja ambayo inaitwa ‘Idea’ amefungukia yake kutoka moyoni kuhusu wasanii  Wachanga,  kutokana na jinsi ambavyo huwawanakosea mashariti  katika Muziki ikiwa ni pamoja na utovu wa nidhamu.

Nivo akiwa kwenye interview  Super News TV katika kipindi kizuri cha ‘New Talents Tanzania’ kinacho wapa fursa wasanii wachanga kuonyesha uwezo wa vipaji vyao, Nivo alifafanua pia baadhi ya mambo yanayo wakabili wasanii wachanga kiasi kwamba Muziki wao unashindwa kukua na kuweza kutimiza malengo yao.  Tumia dakika zako kadhaa kutazama Mahojiano yake hapa.

SHAKA AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIET YA BARAZA KUU UVCCM TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

October 12, 2017
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiongoza kikao cha Secretariet ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa kwa  maandalizi ya vikao vya kikanuni vya Umoja wa Vijana wa CCM vitakavyofanyika Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine vitajadili waombaji wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa nafasi za Mkoa na Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa CCM kabla kuwasilisha katika vikao vya Chama Cha Mapinduzi kwa uteuzi wa mwisho.(picha na Fahadi Siraji wa UVCCM )

NG’OMBE WALIOINGIZWA KATIKA WILAYA YA MWANGA KUTOKA NCHINI KENYA KINYUME NA SHERIA WAPIGWE MNADA – MPINA

October 12, 2017
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Baadhi wa wafugaji na Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro hawapo katika Picha, alipofanya ziara ya dharula katika kijiji cha Kyara wilayani Mwanga ambapo umetokea uingizwaji wa mifugo kinyume cha sheria na wafugaji wanaosadikika kutoka nchi jirani ya Kenya.

Katika Picha Waziri Mpina akiwa katika kikao na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro alipofana ziara ya Dharula. Baada kuwepo kwa uvamizi wa mifugo kutoka Kenya.

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kushoto na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo walipokuwa katika kikao na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro.


NA MWANDISHI MAALUM -MWANGA
Ikiwa ni siku ya nne baada ya kupewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Luhaga Mpina amefanya ziara ya dharula katika Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo, na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kupitia mwanasheria wa serikali wa mkoa, ndani ya siku saba kuzipiga mnada ng’ombe zote zilizoingizwa katika kijiji cha Kyerwa kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Mpina ameagiza Idadi ya Ng’ombe hao  1325 kupigwa mnada katika zoezi ambalo litasimamiwa na mwanasheria wa serikali, na kusema kuwa vyombo vya dola viendee kuhakikisha kuwa hakuna ng’ombe atakayepita wala kutoroshwa katika hali yoyote ile.
Aidha Mpina amevitaka vyombo vya dola kuendelea kuwasaka ng’ombe zaidi ya 4000 wanaosadikiwa kutoroshwa na kuwakama pamoja na kuchukua hatua stahiki, na amemtaka mhifadhi mkuu (TANAPA) asaidie kutoa vifaa ikiwa ni pamoja na helicopter na drown ili kuweza kusaidia oparesheni za kusaka mifugo iliyotoroshwa na mingine inayoendelea kuingia kinyemela nchini.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira, alieleza kuwa uvamizi huo wa Mifugo unasababisha tishio la kuambukizwa  kwa magonjwa kwa mifuko ambayo mkoa inayo pamoja na uharibifu wa mazingira hali inayopelekea mkoa kushindwa kufikia malengo ya kujitengea maeneo ya ufugaji, pamoja, uhaba mkubwa wa malisho na uhaba wa maziwa ambapo mwanga pekee ina ng’ombe zaidi ya 18,000.
Akiongea katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kutoka sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo alisema kwa kuwa ng’ombe hao wanatakiwa kuchukuliwa vipimo ili kujua kama wameathirika na magonjwa ya mifugo kwa na aliafiki wazo la kuteketeza kabisa ng’ombe hao endapo watapatikana na magonjwa yasiyotibika.
Madhara mengine yaliyoelezwa kutokana na uvamizi wa mifugo hiyo ni pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji, misitu na ongozeko la migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
RAIS DKT MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA SIKU TATU

RAIS DKT MAGUFULI AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA SIKU TATU

October 12, 2017

z (9)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari wa ziara ya siku tatu visiwani humo ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere..
z (2)
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
z (3)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
z (4)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
z (5)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
z (6)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama janet Magufulki wakisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 
z (7)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kuwasili katika uwanja  wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kwa ziara ya siku tatu visiwani humo  ambapo pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Siku ya Mwalimu Nyerere. 

WASHINDI WA SHINDANO LA FIKA NA FINCA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO LEO

October 12, 2017
Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba  Akimkabidhi zawadi ya Tiketi ya basi  Bw.Hussein Bashe (katikati) ambaye ni mshindi wa Bahati nasibu inayoendeshwa na Benki hiyo inayoitwa Fika Na FInca anayeshuhudia ni Afisa Usafirishaji wa mabasi ya kampuni ya New Force Masumbuko Masuke mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Finca Jijini Dar es salaam.

WAZIRI KALEMAN ATAKA MADENI YA BILI ZA UMEME KULIPWA KWA WAKATI TANESCO

October 12, 2017
 WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na uongozi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco na wadau wa mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha nishati hiyo inapatikana kwa uhakika ikiwemo kuwahudumia wateja kwa wakati na kuwepo kwa uhakika wa vifaa vyenye ubora ili kuwezesha
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati,Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo akiongea katika kikao hicho kushoto ni WAZIRI wa Nishati,Dkt Medard Kalemani
 Wajumbe na wadau mbalimbali wa nishati wakifuatilia kikao hicho leo

 Baadhi ya wajumbe wa uongozi wa shirika kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uzalishaji Umeme Mhandisi Abdallah Ikwasa na kushoto ni Meneja wa Mwandamizi wa Tehama Dudu
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tanesco nchini  Dkt Tito Mwinuka kushoto  na Mkurugenzi wa REA Mhandisi Gisima Nyamuhanga wakifuatilia kikao hicho
 Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wakimsikiliza kwa umakini Waziri Nishati,Dkt Medard Kalemani katika kikao hicho


Waziri wa Nishati Dkt Medard Kaleman akiambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Subira Mgalu wamefanya kikao na uongozi wa shirika la Umeme nchini (Tanesco) na wadau mbalimbali wa umeme ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha nishati ya umeme wa uhakika inapatikana.

Aliyasema hayo leo katika kikao cha pamoja baina yake na uongozi wa shirika hilo wakiwemo wadau ambapo alisema  watahakikisha wanawahudumia wateja kwa wakati ikiwemo uhakika wa vifaa vyenye bora ili kuwawezesha wananchi kupatiwa umeme kwa haraka zaidi .

Licha ya hivyo lakini pia Waziri huyo alitilia mkazo suala la madeni yote ya bili za umeme kulipwa kwa wakati kwenye shirika hilo ili kuweza kuwezesha ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi .

Akizungumza na wazabuni mbalimbali wa miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo,nyaya na mita,Waziri Kaleman alisema kuanzia sasa vifaa vya umeme vitanunuliwa ndani ya nchi kwani kufanya hivyo itapunguza gharama kubwa na kasi ya kuwahudumia wateja.

"Kwani kufanya hivyo vifaa hivyo vitakuwa karibu kupatikana ndani ya nchi na kutaongeza mapato ndani ya nchi na uzalendo "Alisema.

Hata hivyo alilipongeza shirika la Umeme nchini Tanesco kwa kufanya kazi kwa bidii na kutoa taarifa kwa wateja juu ya huduma mbalimbali ikiwemo kuwataka kuwajibika kwa kufanya kazi kwa waledi mkubwa

Aidha alisema kuwa mkakati wa shirika hilo ni kuhakikisha mpaka ifikapo 2020 madeni yote shirika hilo wanayoyadaiwa kwa wateja mbalimbali nchini yatakuwa yamekwisha kulipwa.

Sambamba na hayo alikema vitendo vya wizi wa umeme na kuwataka wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja na ambao watabainika watachukua hatua.