MKUTANO WA WADAU WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI WAFANYIKA JIJINI DAR

January 30, 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto ) na Meneja Mradi wa Benki ya Dunia (WB) katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Oliver Braedt (kulia) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava akifungua warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Dk. Lutengano Mwakahesya akifungua warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Meneja Mradi wa Benki ya Dunia (WB) katika nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Oliver Braedt akichangia jambo katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Wadau mbalimbali wa warsha hiyo wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (hayupo pichani) katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
Baadhi ya wadau kutoka kampuni zinazojihusisha na usambazaji wa umeme vijijini wakifuatilia mada kwa makini zilizokuwa zinawasilishwa na watoa mada (hawapo pichani) kwa nyakati tofauti katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana
Baadhi ya wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa mstari wa mbele) wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wadau mbalimbali (hawapo pichani) katika warsha iliyokutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme vijijini iliyofanyika jijini Dar es salaam kujadili mpango mkakati katika usambazaji wa umeme vijijini. Pia ilihusisha wadau wengine kutoka nchi za Peru, Vietnam, Brazil, Tunisia na Ghana.
MATUKIO YA BUNGENI-MJINI DODOMA

MATUKIO YA BUNGENI-MJINI DODOMA

January 30, 2015

 2
MwanasheriaMkuu wa Serikali George Masaju akizungumza Bugeni Mjini Dodoma Januari 29, 2015.
(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
3
Waziri wa Mambo ya Ndani,Mathias Chikawe akiwasilisha taarifa ya serikali Bungeni Mjini Dodoma.
4
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu Maswali Bungeni Mjini Dodoma.
5
Waziri mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Maofisa wa Juu wa Benki ya NMB kwenye makazi yake mjini Dodoma Januari 29,2015. Kutoka kushoto ni Tom, Borghols, Richard Makungwa na Joseline Kamuhanda.
1
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob Mameo kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

MKUTANO MKUBWA WA KIMATAIFA WA TAASISI YA USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI TANZANIA (CILT) KUFANYIKA MACHI, 3 JIJINI ARUSHA

January 30, 2015

 Balozi wa Heshima wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania (CILT), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia), akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya kukusanya fedha kwa ajili ya mkutano wa kimataifa utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 4 hadi 5 ulioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajengea weredi wadau wa usafirishaji kutoka nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
 Mwenyekiti wa CILT, George Makuke (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mipango wa MOT, Migire Gabriel, Balozi wa Heshima wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania (CILT), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
Mkurugenzi wa Mipango wa MOT, Migire Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
…………………………………..
Dotto Mwaibale
 
IMEELEZWA kuwa ukosefu wa weledi na utaalam wa masuala mbalimbali ya usafirishaji ndio chanzo cha kutokea kwa ajili nyingi nchini.
Hayo aliyasema jana Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa Usafirishaji na Uchukuzi nchini(FCILT), George Makuke wataki wakizungumzia maandalizi ya mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu Mkoani Arusha.
Mkutano huo utahusisha nchi mbalimbali Duniani ukiwa na lengo la kujenga weledi katika masuala ya usafirishaji na uchukuzi.
Akizungumzia mkutano huo alisema kuna mambo mengi yanafanyika katika usafirishai ambayo si sahihi hivyo mkutano huo utasaidia wahusika kutoa huduma kihalali.
“Ukiangalia kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika masuala ya usafirishai kwa kuzidisha bei lakini hata watoa huduma wenyewe wamekuwa hawana weledi hivyo mkutano huo utajadili namna ya kuondia changamoto zote hizi”alisema 
Kwa Upande wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kuwa mkutano huo ni mkubwa hivyo atahamasisha taasisi mbalimbali kutoa michango yao kwani unahitaji fedha nyingi kwaajili ya kuwahudumia wageni.
“Hasa nitaangalia namna gani taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii wamechangia kiasi gani maana wao ndio watakaofaidika kwani watu watatoka nchi mbalimbali hivyo itasaidia kuitangaza nchi”alisema 
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo,Zakaria Hans pope, alisema mkutano huo utasaidia kukuza uchumi kwani kama kukiwepo njia sahihi za usafirishaji mapato lazima yaongezeke.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
MAONESHO YA KIMATIFA YANAYOFANYIKA MASCUT-OMAN

MAONESHO YA KIMATIFA YANAYOFANYIKA MASCUT-OMAN

January 30, 2015


1
Wageni mbalimbali wakiingia na kutoka Katika Banda la Watanzania kujione bidhaa za Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Picha zote na Faki Mjaka-Mascut Oman
2
Msanii wa kuchora Fred Halla akifanya sanaa yake ya Uchoraji katika Katika Banda la Watanzania.Fred ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
3
Msanii wa Uchongaji Iddy Amana akiwahudumia wateja katika Banda la Watanzania. Iddy ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
4
Mpishi wa Vyakula mbali mbali Haji Omar akiwahudumia wateja wake wanaopenda vyakula vya Kitanzania.Haji ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
5
Baadhi ya Wateja wa Vyakula vya kitanzania wakila chakula chenye Asili ya Tanzania,Zanzibar (Urojo) katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
6
Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman Bi Khadija Bhatashy akiulizia bei ya bidhaa katika Banda la Iran. Iran ni moja ya nchi washiriki wa Maonesho hayo.
……………………………………………………………………………………………….
Na Faki Mjaka-Mascut Oman,
Kukosekana kwa Semina ya pamoja na uelewa mdogo wa lugha ya Kiarabu ni miongoni mwa Changamoto zinazowakabili Wajasiriamali wa Kitanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Omani. Hayo yameelezwa na Watanzania wanaoshiriki Maonesho hayo yanayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja na kushirikisha Mataifa mbalimbali. Mmoja ya Wajasiriamali hao Kulthum Mohamed amesema uelewa mdogo wa lugha ya Kiarabu ni changamoto kwake inayomkabili katika kutoa ufafanuzi wa baadhi ya Bidhaa alizokuwa nazo. Mjasiri Amali huyo wa Viungo (spices) amedai kuwa licha ya baadhi ya Waarabu kujua Lugha ya Kiswahili amebaini hawapendi kuzungumza jambo ambalo linawapa shida. “Licha ya hawa WaomanI kukijua Kiswahili lakini wengi wao wanavyofika hapa wanajifanya hawakijui jambo ambalo linatukwaza kidogo katika kutoa ufafanuzi wa Bidhaa zetu kwa Lugha ya Kiarabu” Alisema Kulthum. Aidha K amebaini kuwa hakukuwa na Semina ya Pamoja ya Washiriki kujua mambo mbalimbali na Vipaumbele vya Waarabu jambo ambalo lingeweza kuwajengea uelewa mpana wa Waoman nakujua Bidhaa muhimu zaidi za kuja nazo katika Maonesho hayo. Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo wa Watazania katika Maonesho hayo ya Utamaduni na Sanaa Bi Khadija Battashy amesema kuna baadhi ya Bidhaa ambazo haziendani sana na Utamaduni wa Omani kama vile nguo za kike zenye Mikono Mifupi. “Kwa mfano utakuta baadhi ya Nguo tulizokuja za kike nyingi zao zimetengenezwa zikiwa na Mikono mifupi tena zimepasuliwa sasa kwa Utamaduni wao hawa hawazipendelei sana,nadhani tungetengeneza za Mikono mifupi Wangezipenda zaidi” Alisema Bi Khadija Battashy. Hata hivyo anaamini Tanzania itafanya vyema katika Monesho hayo na hata kuibuka Mshindi wa mwanzo ikiwa kutatokea kutangazwa mshindi. Kwa upande wake Mjasiriamali wa Bidhaa za Nguo Bi Anna Matinde amesema ana matumaini makubwa kuwa Bidhaa za Tanzania zitapata Wateja kutoka na ubora wake. “Mi naamini Bidhaa zetu ni bora na zitapata Wateja maana hata hiyo Mishahara ya Waarabu bado tunaamini ikitoka watazidi kununua bidhaa zetu” Aliongeza Bi Anna. Kwa Upande wao Wageni wanaolitembelea Banda la Tanzania wamelisifia kutokana na kuwa na bidhaa bora na za upekee zikiwemo za Viungo kama vile Karafuu na Mavazi ya Kimasai. Maonesho hayo ya Muda wamwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika katika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 jioni na kufungwa saa nne usiku kwa Majira ya Oman ambapo Nchi mbalimbali Washiriki huonesha Bidhaa zilizotengenezwa kwa Mikono zinazowakilisha Utamaduni wao na Watu hununua Bidhaa hizo.