*RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA ALGERIA ALIYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI

January 15, 2015

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kisha kuagana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel,  Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumanne jioni January 13, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Wakiagana baada ya mazungumzo yao. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE NA MKEWE WAMJULIA HALI MBUNGE WA NAMTUMBO MHE VITA KAWAWA ALIYELAZWA HOSPITALI YA AMI JIJINI DAR ES SALAAM

January 15, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mbunge wa Namtumbo Mhe. Vita Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu ya tumbo. Katikati yao ni Mhe Adam Malima, nai bu Waziri wa Fedha na kushoto ni Daktari katika wodi hiyo. Picha na IKULU

*WANAFUNZI 84 WA UDOM WATIWA MBARONI KWA KUHAMASISHA MAANDAMANO MJINI DODOMA

January 15, 2015
 Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya kutiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.
Baadhi ya Wanafunzi 84 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani Chuoni hapo na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo mjini Dodoma leo.