TAMKO LA JESHI LA POLISI

TAMKO LA JESHI LA POLISI

September 03, 2014

01 
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.02Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014  Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
“Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.
 “Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
 Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
 Alisema oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.
 Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
“Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.
 Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.
 Pia aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.

MTANANGE WA NGAO YA JAMII BAINA YA YANGA NA AZAM FC WASOGEZWA MBELE

September 03, 2014



MECHI ya Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 baina ya mabingwa Azam fc na makamu bingwa, Dar Young Africans sasa utapigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam septemba 14 badala ya septemba 13 mwaka huu kama ilivyopanga.
Shirikisho la soka Tanzania limeamua kuusogeza kwa siku moja mchezo huo uliotakiwa kupigwa jumamosi na sasa kupigwa jumapili kwa lengo la kuwapa fursa mashabiki wengi kuuona.
TFF  imesema jumapili ni siku tulivu kuliko jumamosi na mchezo wa mwaka huu utaambatana na shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu.
Pia sehemu ya mapato ya mchezo huo yatapelekwa katika shughuli ya kijamii iliyochaguliwa.
Mechi hiyo itapigwa ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa ligi kuu septemba 20 mwaka huu ambapo Yanga wataanzia ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar katika dimba la Jamhuri mkoani Morogoro.
Mnyama Simba atakuwa uwanja wa Taifa siku moja baada ya kufunguliwa kwa ligi kuu (septemba 21 mwaka huuu) dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.

Azam fc watakuwa nyumbani Azam Conmplex kuchuana na Polisi Morogoro.
 JAJA AMFUNIKA COUTINHO, AIFUNGIA YANGA IKIICHAPA THIKA UNITED 1-0

JAJA AMFUNIKA COUTINHO, AIFUNGIA YANGA IKIICHAPA THIKA UNITED 1-0

September 03, 2014
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mechi ya leo. (Picha na Frank Momanyi)

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MBRAZIL Geilson Santos Santana ‘Jaja’ kwa mara ya kwanza akicheza katika uwanja wa kisasa wa Taifa jijini Dar es salaam amefanikiwa kuifungia Yanga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Thika United ya Kenya.
Katika mechi hii iliyoanza saa 11:00 jioni, Jaja aliandika bao hilo katika dakika ya 60 ya mchezo.
Jaja ameweza kumfunika Mbrazil mwenzake, Andrey Coutinho aliyoonekana kuwa moto wa kuotea mbali katika mechi tatu zilizopita.
Coutinho aliifungia Yanga mabao 2 katika mechi tatu alizocheza Zanzibar wakati Jaja alifunga moja dhidi ya Chipukizi FC uwanja wa Gombani Pemba.
Cuutinho aliitungua Shangani na KMKM, Yanga ikishindi mabao 2-0 kwa kila mechi.
Lakini leo Jaja alitulia na kumzidi kete Coutinho aliyetarajia kuwavutia mashabiki wengi wa Yanga.
Maximo aliwaanzisha pamoja Jaja, Saimon Msuva na Coutinho katika safu ya ushambuliaji, wakati Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite walianza katikati.
Winga ya kulia alianza Hassan Dilunga. Safu ya ulinzi walianza Juma Abdul, kulia, Oscar Joshua, kushoto na mabeki wa kati walianza Nadir Haroub na Kelvin Yondani.

AYSHA CHEYO NDIYE MISS TANZANIA USA PAGEANT 2014

September 03, 2014

Miss Tanzania USA Pageant wa 2013 Joy Kalemera akimvisha taji miss Tanzania USA pageant 2014 Aysha Cheyo siku ya Jumamosi Aug 31, 2014 Baada ya kunyakua taji hilo kwenye mashindano ya umiss yaliyofanyika Slvr Spring, Maryland nchini Marekani.
Miss Tanzania USA pageant 2013 Joy Kalemera akipigia makofi mshindi mpya wa taji hilo Aysha Cheyo mara tu baada ya kumaliza kumvika taji hilo.
Mshindi wa taji la miss Tanzania USA Pageant Aysha Cheyo akiwa na furaha ya kunyakua taji hilo.
Aysha Cheyo na Joy Kalemera wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA Pageant Ma Winny Casey.
Mshindi wa Miss Tanzania USA Pageant Aysha Cheyo akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Kupewa Mushala (kushoto) na mshindi wa tatu Jessica Lavius na miss Congeniality ni Grace Mlingi

SILVER ATAKA KAZI ZA WASANII ZILINDWE.

September 03, 2014
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MSANII wa mziki wa Bongofleva mkoani Tanga,Sophia Patrick
“Silver”ameitaka wizara ya Habari Utamaduni na Michezo iweke sheria kali zitakazowezesha kulindwa kwa kazi zai ili wasanii wa mziki huo kupata mafanikio kutokana na kazi hizo.

Silver alitoa ushauri huo wakati akizungumza na Blog hii

ambapo alisema kuwa wasanii wamekuwa wakifanya kazi ngumu sana lakini mafanikio yanakuwa ni madogo sana kutokana na kuwepo kwa mianya ya kutokulindwa kazi hizo.

Alisema kuwa wakati umefika kwa mamlaka hizo husika kuhakikisha
  wanalivalia nyuga suala hilo kwa kuweka mpango kabambe ambao utawezesha kuondoa tatizo hilo hasa kwa wasanii chipukizi hapa nchini.

Akizungumzia changamoto ambazo wanakumbana nazo,Silver ambaye pia ni
  mwanafunzi wa Chuo Kikuu mkoani hapa akichukua masomo ya sanaa, alisema kuwa changamoto kubwa ni upande wa vyombo vya habari hususani watangazaji na madj ambao wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwao jambo ambalo lisipochukuliwa hatua huenda mziki huu ukatoweka .
Hata hivyo aliwataka wasanii wengine chipukizi kuhakikisha wanafanya  kazi zao kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kufikia malengo ya kuhakikisha wanautangaza vilivyo mziki huo ndani na nje ya nchi.

Msanii huyo hivi sasa anatamba na nyimbo zake mbili ambazo ni

“Univeristy  na Ingara ambazo ameziimba katika mahadhi tofauti tofauti chini ya Mtayarishaji wa mziki huo mkoani hapa Danny Toucher kupitia studio za Akili Music.