KANISA LA SINZA CHRISTIAN CENTER LATUPIWA VYOMBO NJE

June 09, 2016
Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza Christian Center  latupiwa nje vyombo vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera , akizungumza na Dar es salaam yetu Blog  mke wa mmiliki  wa jingo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema; “huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa jengo letu." 
Alipotafutwa msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo, hakupatikana kuzungumzia sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.

Hili ni eneo la Kanisa Hilo
Viti  vyote vikiwa vimetolewa nje
 Vyombo vya Muziki vikiwa nje
 Magari yakiwa yanatolewa nje
 Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi
 Vikombe nje
 Wametoa vitu vyote
Magodoro na vitanda vyote nje  
 Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa
Kushoto kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya kuendelea kutoa vitu.
 Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com

Bayport yaendelea kutoa hati za viwanja kwa wateja wao

June 09, 2016

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria wa Bayport, Mrisho Mohamed.


TAASISI ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.


Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya Bayport.
Ibrahim Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema kusudio lao ni kugawa hati kwa wateja wao mapema iwezekanavyo ili kujitofautisha na wadau wengine wanaojihusisha na mambo ya uuzaji wa ardhi kwa njia mbalimbali.


Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme katikati akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desdery Selestine Mkenda. Kulia ni Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.


Alisema kwamba hati zinazotoka kwa mwaka huu ni zile zinazohusu wateja walionunua viwanja hivyo katika mradi wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mradi uliopokewa vizuri na Watanzania, jambo lililochangia Bayport kupanua wigo huo kwa kuanzisha miradi mingine ya Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani Ibrahim D Mahinya. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Mteja wa kiwanja cha Vikuruti vinavyotolewa na Bayport, Ibrahim D Mahinya akizungumza jambo.
Ibrahim Mahinya, akitia sahihi ya dole gumba kama njia ya kukamilisha utaratibu wa makabidhiano ya hati yake.

Thabit Mndeme katikati akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati za viwanja.
Mteja wa viwanja vya Vikuruti, Desdery Mkenda kushoto akishuhudia nyaraka zinazohusiana na mambo ya hati yake aliyokabidhiwa baada ya kuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katikati ni Meneja Biashara wa Bayport, Thabit Mndeme na Afisa Sheria wa taasisi hiyo Mrisho Mohamed.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kulia akipeana mkono wa na mteja wao Ibrahim Mahinya baada ya makabidhiano ya hati yake ya kiwanja cha Vikuruti kukamilika.


“Tumepania kuwa tofauti na wadau wengine wanaotoa huduma ya ardhi, kwa kuhakikisha mteja wetu anapata hati yake haraka na bila usumbufu wowote kwa ajili ya kumuondolea kero za ufuatiliaji wa hati.


“Tunawaomba Watanzania waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuchangamkia fursa za mikopo katika miradi yetu yote ukiwamo wa Chalinze, Kigamboni, Kilwa, Kibaha na Bagamoyo ambayo vinauzwa kwa mita moja ya mraba Sh 10,000 Bagamoyo, Chalinze Sh 4500, Kibaha Sh 9000, Kilwa Sh 2000 na Kigamboni Sh 10000,” Alisema Mndeme.

Naye Mahinya aliyekabidhiwa hati yake kutoka Bayport alisema kwamba amefurahishwa kupewa hati kwa haraka jambo ambalo ni tofauti na matarajio yake kutokana na suala hilo kuwa na mzunguuko mkubwa.

“Nimepata hati yangu kwa haraka mno, hii ni tofauti na matarajio yangu kwa sababu nafahamu suala la hati linavyokuwa na mkanganyiko mkubwa kwa sababu linashirikisha mikono ya watu wengi na lina mambo mengi pia, ila kwa Bayport kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo nalazimika kusema kuwa utaratibu wa kazi wa taasisi hii umenivutia,” Alisema.

Mteja mwingine Mkenda aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake, baada ya kuwa mmoja wa Watanzania aliyejipatia viwanja vya Vikuruti vilivyozinduliwa na taasisi hiyo mwaka jana mwezi wa tano, huku huduma hiyo ya viwanja ikipatikana katika ofisi zote za Bayport.


Mbali na mikopo ya viwanja, Bayport pia wanatoa huduma ya mikopo ya haraka ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa, huku mikopo hiyo ikiwa haina amana wala dhamana.

ZAIDI YA MILIONI 600 KUSHINDANIWA KUPITIA PROMOSHENI YA"KAMATA MPUNGA YA VODACOM"

June 09, 2016

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni hiyo,Saurabh Jaiswal na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh Jaiswal(kushoto)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,wakimsikiliza Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew Kampambe(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.

Vodacom Tanzania leo imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha wateja wake kujishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi Milioni 615 ndani ya siku 140.Promosheni hii inayojulikana kama ‘Kamata Mpunga’ ni mwendelezo wa moja ya malengo ya kampuni hiyo ya  kubadilisha maisha ya wateja wake kuwa bora.
Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali za kubadilisha maisha ya wateja na watanzania kwa ujumla kama vile Mwaka jana iliendesha promosheni kubwa ambayo haijawahi kutokea nchini iliyojulikana kama Jaymillions ambayo ilibadilisha maisha ya wateja mbalimbali walioibuka washindi na maisha yao kuwa murua. Vilevile miaka ya nyuma kampuni iliwahi kuendesha promosheni kabambe kama vile timka na bodaboda na kampeni ya Mahela iliyomfanya Mwanafunzi wa Chuo cha elimu mkoani Kigoma kuibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/=.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni hii inajulikana kama ‘Kamata Mpunga’ inawahusisha wateja wote wa kampuni yetu na itawawezesha wateja watakaobahatika kushinda kuwa mamilionea, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku,kila wiki,kila mwezi na pia itakuwepo zawadi kubwa mwishoni mwa promosheni hii ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Nkurlu alisema kuwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kutakuwepo na washindi 3 wa shilingi Milioni 1/= kila mmoja na kila siku ya Jumapili atakuwepo mshindi wa Milioni 5/= na tarehe ya mwisho wa mwezi katika kipindi cha promosheni atakuwepo mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ambaye atajinyakulia kitita cha Milioni 100/= ambazo zitatolewa katika kipindi cha mwisho cha promosheni.

Nkurlu amesema ushiriki wa promosheni hii utakuwa ni rahisi ambapo mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno “GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi  300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”. Alisema.

Nkurlu alifafanua kuwa maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi. Kila mteja  atakapokuwa  anajibu  atakuwa anafahamishwa iwapo amepata swali na ataweza kujipatia pointi. Aliongeza kuwa kila ujumbe utakaotumwa kwenda namba 15544 mshiriki atajipatia bonasi ya pointi 100 za kuanzia ambazo zitaongezeka kadri atakavyokuwa anajibu maswali.
Nkurlu alifafanua zaidi kuwa katika ushiriki wa kawaida kwenye promosheni hii mteja ataweza kujishindia pointi 20 kwa kila jibu la swali litakapokuwa sahihi na pointi 10 iwapo jibu lake sio sahihi. Pia kutakuwa na  bonasi  ambayo itatolewa kwa nusu saa hadi siku nzima kwa lengo la kuwawezesha wateja wengi kushiriki na kuwa na nafasi ya kujishindia zawadi ya mamilioni ya fedha. Alifafanua zaidi kuwa kutakuwa na nafasi ya  ushiriki kwa kujiunga moja kwa moja ambapo mteja atatakiwa kutuma neno “WIN” kwenda namba 15544 na atakakwa kiasi cha shilingi 200 tu.