COASTAL Union yawatimua wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.
Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umetimua rasmi
wajumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo ambao walichaguliwa katika uchaguzi
mkuu mwaka uliopita kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Akitangaza uamuzi wa kuwafukuza katika mkutano mkuu wa
wanachama mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Hemed Aurora alisema
hatua hiyo inatokana na wajumbe hao kuwa mzigo katika nafasi zao ikiwemo
kushindwa kuhudhuria vikao vya kamati tendaji tokea walipochaguliwa.
Kauli ya Aurora inafuatia na swali aliliulizwa na Mwanachama
wa Klabu hiyo, Miraji Wandi aliyetaka kujua uongozi wa timu hiyo umewachukuliwa
hatua gani viongozi ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao hali ambayo
inapelekea kuwa mzigo kwa klabu hiyo?
Aurora alisema tayari wameandaa utaratibu wa kuandika barua
kwa ajili ya kuwatimua rasmi katika nafasi zao hizo pamoja na kutangaza nafasi
za hizo katika uchaguzi mdogo ambao utafanyika hivi karibuni kuziba mapengo
hayo.
Aidha mwenyekiti huyo aliwataka viongozi waliopo katika klabu
hiyo na wanachama kila mmoja kutimiza majukumu yake ili kuweza kusukuma
gurudumu la maendeleo ya timu hiyo ambayo imedhamiria msimu ujao kuchukua
ubingwa.
Mwenyekiti huyo aliwataja wajumbe wa kamati ya utendaji ambao
wamewatimuliwa ni Julius Benjamini na Nashoni Kweli ambao tokea wachaguliwe
katika nafasi zao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao.
Mwisho.
Coastal haina mpango wa kumsajili mlinda mlango mwengine-Binslum
Na Oscar Assenga,Tanga.
MKURUGENZI wa Ufundi wa Klabu ya Coastal Union ya
Tanga,Nassoro Hemed “Binslum amesema timu hiyo haina mpango wa kumsajili mlinda
mlango mwengine isipokuwa waliopo wakishirikiana na Shabani Kado.
Kauli hiyo ya Binslum inafuatia taarifa ambazo zimekuwa
zikieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo wana mpango wa kumsajili aliyekuwa mlinda
mlango wa Simba Juma Kaseja katika kipindi hiki na kusema taarifa hizo hazina
ukweli wowote ule.
Binsulum alisema wanachokifanya hivi sasa ni kuangalia wachezaji
wenye uwezo wa kuweza kuiletea mafanikio timu hiyo na sio majina kwani wapo
wachezaji wa aina hiyo ambao hawaweze kuwa msaada katika timu.
Alisema kuelekea msimu mpya wameimarisha safu ya walinda
milango ambapo Shabani Kado atasaidiana na Said Rubawa aliyesajiliwa kutoka
Oljoro JKT na Mansour A.Mansour ambaye walimpandisha kutoka katika kikosi chao
cha pili chini ya umri wa miaka 20.
Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza kuwa hawajafanya
mazungumzo yoyote na Juma Kaseja pia hawana mpango nae ambapo wao wanasajili
kwa mipango lengo lao likiwa ni kupata mafanikio kwenye msimu mpya wa Ligi kuu
Tanzania bara.
Alisema kabla ya kufanya usajili huo walimu walitoa mipango
yao nao kama uongozi wakaona watekeleze na kueleza kuwa katika kikosi chao
mchezaji huyo hana nafasi kutokana na kuwa na walinda milango mahiri.
Wakati
huo huo uongozi klabu hiyo umemteua Hafidhi Kido kuwa mwandishi wa
klabu hiyo ambaye atakuwa na jumuku la kuhakikisha taarifa za klabu hiyo
zinafika kwa wakati katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini
nafasi ambayo aliteuliwa leo(jana).
Subscribe to:
Posts (Atom)