WATANZANIA WATANO WACHAGULIWA KUWA MABALOZI WA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI DUNIANI

January 13, 2017
“BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.

Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.

Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.

Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. 

Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.


https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

MAWAZIRI WA SMT NA SMZ WAKUTANA ZANZIBAR LEO, KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

January 13, 2017
Wa pili kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. January Makamba, akiongea katika kikao cha ngazi ya Mawaziri kinachohusisha Mawaziri Kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kinachojadili changamoto za Muungano, Mjini Unguja, wa Pili kutoka Kushoto ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa (SMZ) Mhe. Mohamed Aboud Mohamed. Kulia kwake ni Bwana Joseph Abdallah Meza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (SMZ) na wa kwanza Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Profesa Faustin Kamuzora.
Katika Picha Sehemu wa viongozi wa Serikali ya (SMZ) katika kikao cha ngazi ya Mawaziri kinachojadili changamoto cha Muungano Mjini Zanzibar Leo.

 (Picha na Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa wa OMR)