RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI DK. DAU PAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA MITATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA BALOZI DK. DAU PAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA MITATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

September 14, 2016
dr3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Ramadhani Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Tixon Nzunda kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala mkoa wa Songwe, Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Adoh Mapunda kuwa Katibu Tawala mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr10 dr11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Dkt. Ramadhani Dau na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw. Adoh Mapunda wa pili kutoka (kushoto), Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa Bw. Tixon Nzunda watatu kutoka (kushoto) , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba wapili kutoka (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Ntandu wakwanza (kulia) mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
dr14
Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Ramadhani Dau, Katibu Tawala mkoa wa Rukwa Tixon Nzunda, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe Eliya Ntandu pamoja na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Adoh Mapunda wakila kiapo cha Uadilifu  mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
WAZIRI WA AFYA AWAAGIZA MAKATIBU TAWALA KUTOA RUHUSA KWA MANESI KUFANYA UTAFITI WA AFYA

WAZIRI WA AFYA AWAAGIZA MAKATIBU TAWALA KUTOA RUHUSA KWA MANESI KUFANYA UTAFITI WA AFYA

September 14, 2016
ummy1
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia leo mkoani Dodoma katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi wapatao 187 watakaofanya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 unaotarajia kuanza nchi nzima kuanzia wiki ijayo. (Picha na Veronica Kazimoto)
ummy2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya kina kuhusu Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo unaotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia wiki ijayo. (Picha na Veronica Kazimoto)
ummy3
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumza leo mkoani Dodoma wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 unaotarajia kufanyika nchi nzima kuanzia wiki ijayo. (Picha na Veronica Kazimoto)
ummy4
Mratibu wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 Bi. Mariam Kitembe wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kiasi cha Shilingi milioni moja na laki sita (1,600,000) zilizochangwa na wadadisi wa Utafiti huo kwa ajili ya waathirika wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera hivi karibuni. Mhe. Ummy Mwalimu amekabidhiwa fedha hizo wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo mkoani Dodoma. (Picha na Veronica Kazimoto)
ummy5
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya utafiti huo iliyofanyika leo mkoani Dodoma. (Picha na Veronica Kazimoto)
ummy6
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar pamoja na wakufunzi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 mara baada ya kufunga mafunzo ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 leo mkoani Dodoma. (Picha na Veronica Kazimoto).
………………………………………………………………………………
Na. Emanuel Ghula- Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Makatibu Tawala wa mikoa yote nchini kutoa ruhusa kwa manesi ambao ni wadadisi wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016 ili kufanya utafiti huo.
Akizungumza leo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya wadadisi hao iliyofanyika mkoani Dodoma, Waziri Ummy amesema utafiti huu ni wa muhimu sana hivyo Makatibu Tawala hawana budi kuwaruhusu manesi hao waliopata mafunzo kufanya utafiti huo.
“Ninawaagiza Makatibu Tawala wote nchini kuhakikisha wanatoa ruhusa kwa manesi mliopo hapa leo ili muweze kulisaidia taifa letu kwa kutuletea takwimu sahihi zitakazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo hususani katika suala zima la afya”, ameagiza Mhe. Ummy Mwalimu.
Amefafanua kuwa, takwimu hizi zitasaidia kuboresha juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali za kusogeza huduma zinazohusiana na VVU kama vile huduma za upimaji wa VVU bure katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali, kutoa huduma ya kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) pamoja na utoaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU zijulikanazo kama ARV.
“Utafiti huu ni wa kipekee ukilinganisha na tafiti zingine zilizofanywa zinazohusu UKIMWI kutokana na kujumuisha upimaji wa homa ya ini ambao umekuwa tishio katika baadhi ya nchi barani Afrika”, amesisitiza Mhe. Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ametoa wito kwa wananchi wote nchini kutoa ushirikiano kwa wadadisi watakaopita katika kaya mbalimbali zilizochanguliwa kwa ajili ya kufanya utafiti huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huu utahusisha watu wote kwenye kaya zipatazo elfu kumi na sita (16,000) zilizochaguliwa kitaalam na kuwafikia watu wazima wapatao elfu arobaini (40,000) na watoto zaidi ya elfu nane (8,000).
Dkt. Chuwa ameeleza kuwa, takwimu hizi zitaisaidia Serikali katika kupanga na kusimamia utekelezaji wa sera mbalimbali zinazohusu sekta ya afya nchini hususani upatikanaji wa huduma za afya.
Wadadisi wapatao 187 ambao ni manesi kutoka hospitali mbalimbali nchini, wamemaliza mafunzo ya Utafiti wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI ambao unatarajia kuanza wiki ijayo.
Utafiti wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI utahusisha upimaji wa UKIMWI, maambukizi mapya na wingi wa VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU, wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count), kiwango cha usugu wa dawa za ARV, kiwango cha maambukizi ya kaswende pamoja na homa ya ini (Hepatitis B na C).

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA 6 WA ZAMBIA MHE EDGAR LUNGU MJINI LUSAKA

September 14, 2016


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akipungia mkono maelfu ya wananchi waliokuwa wakimshingilia wakati akiingia  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais Robert Mugabe akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt Kenneth Kaunda
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Botswana Luteni Jenerali Seretse Khama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Rutto,  Makamu wa Rais wa Namibia Mhe. Nickey Iyambo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe william Ruttona wageni wengine wakielekea jukwaani  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akipitia ratiba kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako kamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakiwa kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka ambako kamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwasili kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akipokea heshima ya mizinga 21  kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akiwa na mkewa Mama Esther Lungu kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Rais mteule wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu akila kiapo kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka kwenye sherehe za kuapishwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia leo Septemba 13, 2016
 Taswira ya Makamu wa Rais  wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina akila kiapo ikionekana kqwenye luninga kubwa kwenyeUwanja wa Taifa wa Mashujaa jijini Lusaka  leo Septemba 13, 2016
 Rais Robert Mugabe wa Zambia akizungumza kwa niaba ya viongozi waalikwa wote
 Ndege vita zikipita angani
 Rais Edgar C. Lungu akielekea kukagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo
 Rais Edgar C. Lungu akikagua gwaride la heshima baada ya kula kiapo
 Rais Edgar C. Lungu akielekea jukwa kuu baada ya kukagua gwaride la heshima 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi walikwa wengine kwenye  sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
 Ndege vita zikipamba sherehe angani
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Makamu wa Rais  wa Zambia Mama Inonge Mutukwa Wina kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakisimama na kushiriki dua kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium) jijini Lusaka baada ya shughuli za kuapishwa Rais Lungu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akinong'onezwa jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya watoto Mhe. Agnes Musunga baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiongea na mwandhi wa habari wa ZNBC baada ya sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya 6 wa Zambia Mhe Edgar C. Lungu leo Septemba 13, 2016. PICHA NA IKULU

MASHINDANO YA MGIMWA CUP YAMEZINDULIWA RASMI NA DC WA MUFINDI JUMHURI WILIAMU

September 14, 2016

mkuu wa wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi
 mkuu wa wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji
 mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.

  mkuu wa wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.


na fredy mgunda,iringa. 

MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.

Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri Wiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Wiliamu

Aidha Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.

 “ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Wiliamu
   
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.

“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la mufindi kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema nyimbo

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya mufindi.

“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema kaguo.

Mashindano ya mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

September 14, 2016


Baadhiya wabunge wakiingia katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria vikao vya bunge vinavyoendeleo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Mwigulu Nchemba akiwaeleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mijadala bungeni leo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili (2) katika mfuko wa mazingira kwa ajili ya zoezi ya upandaji miti ili kutunza mazingira.
Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu swali wakati wa kikao cha bunge kinachoendelea leo Mjini Dodoma ambapo alisema kuwa agizo la Rais Dkt. Magufuli la kuhakikisha viwanda vinavyobinafsishwa vinafanya kazi linaendelea kutekelezwa tangu Novemba 2015.
Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Azzan Musa Zungu akiendesha kikao cha bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Charles Tizeba akiwasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO