MAKAMU WA RAIS Dk.MPANGO AKAGUA MRADI WA MAJI SAME - MWANGA - KOROGWE

June 14, 2024

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewapongeza viongozi wa Wizara ya Maji kwa kusimamia na kufanikisha vema utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Same -Mwanga – Korogwe.

Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo alipokagua Mradi huo na kushuhudia wananchi wakianza kunufaika na maji yanayotokana na Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe ambao umefikia asilimia 95. Aidha ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kufanikisha ujenzi wa Kituo cha kupoozea Umeme cha kuhudumia mradi huo.

Aidha Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Maji kuhakikisha vijiji vyote vinavyozunguka mradi huo vinanufaika na maji safi na salama yatokanayo na mradi ili waweze kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya mradi huo.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewasihi wananchi wa Same na Mwanga kuanza kutumia vema maji hayo kwa kuhifadhi mazingira ikiwemo kupanda miti katika maeneo yao. Aidha amewataka viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro kuandaa malambo kwaajili ya kunywesha mifugo ili kulinda mradi huo wa maji dhidi ya unyweshaji mifugo katika chanzo cha mradi huo.

Makamu wa Rais amewahimiza wananchi wanaozunguka mradi wa Same – Mwanga – Korogwe kuhakikisha wanakuwa walinzi wa mradi huo ili uweze kudumu na kuwanufaisha kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watendaji wa sekta ya Maji kuhakikisha wanawaunganisha wananchi wa Mwanga na Same huduma ya maji kwa wakati. Pia amewasihi watendaji katika sekta hiyo kuzingatia utoaji wa ankara sahihi kwa wananchi wakati Wizara ikiendelea na utaratibu wa kufanikisha mita za maji za malipo ya kabla.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimsaidia kubeba ndoo kichwani Bi. Halima Mbaga mara baada ya kuchota maji ya bomba yanayotokana na na Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati akikagua mradi huo akiwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifungua maji katika moja ya bomba iliyopo Kijiji cha Mkizingo Wilaya ya Mwanga maji yanayotokana na Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati akikagua mradi huo akiwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiongeza nguvu ya kusukuma maji katika moja ya mtambo uliyopo eneo la kuchuja maji wakati akikagua Maendeleo ya Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe akiwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikagua Maendeleo ya Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe akiwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.





















Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuhusu maendeleo ya Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe uliyofikia asilimia 95 wakati akikagua mradi huo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Maji, Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na watumishi mbalimbali mara baada ya kukagua Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe akiwa Wilaya Mwanga Mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mkizingo Wilaya ya Mwanga walioanza kunufaika na Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe wakati akikagua mradi huo akiwa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro tarehe 14 Juni 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso mara baada ya kuwasili katika eneo la Nyumba ya Mungu Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwaajili ya kukagua Maendeleo ya Mradi wa Maji wa Same – Mwanga – Korogwe tarehe 14 Juni 2024.

MAJALIWA AMKARIBISHA ZUHURA YUNUS OFISI YA WAZIRI MKUU

June 14, 2024

  

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Zuhura Yunus, mara baada ya Zuhura kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo jana, Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Zuhura amepandishwa cheo kutoka nafasi yake ya awali ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais.